WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere

Tuesday, July 16, 2013

Lowassa awaingilia CHADEMA

Waziri  Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa

WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiri kuwa minyukano ya kuwania tiketi ya urais ndani yake imeleta hofu kwa baadhi ya wananchi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameendelea na harakati za kuendesha harambee kwa makundi mbalimbali na sasa kawageukia wafanyabiashara ndogo ndogo, wamachinga jijini Mwanza.

Mkoa wa Mwanza umekuwa na ugeni kwa nyakati tofauti mwezi huu wa viongozi wa juu wa CCM, wiki jana mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Januari Makamba alifungua semina ya viongozi na watendaji wa CCM ngazi ya kata wilayani Ilemela.
Katika hotuba yake, alisema; “Nchi yetu ipo katika hofu, wananchi wanahofu kuhusu hatima ya uongozi wa nchi yetu. Wote tunafahamu kuna minyukano inaendelea kuhusu nani ni nani katika urais. Na minyukano hii ndiyo inayoleta hofu kwa wanachama na wananchi.”

“Afya ya chama chetu ndiyo afya ya nchi yetu. Kama viongozi ni wajibu wetu kujua kwa nini wananchi wana hofu. Tubaini upungufu uliopo na tuushughulikie ili kuwatoa hofu wananchi.’
Wakati Makamba akitoa tahadhari hiyo, Lowassa ameingia kwenye siasa za Mwanza kufanyia kazi makosa ya CCM ya mwaka 2010 ya kuwapuuza wamachinga.

Ni jambo dhahiri sasa, siasa za Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla upo ukweli mpya unaojidhirisha wazi kwamba siasa zake zinabadili mwelekeo, zikichagizwa zaidi na wamachinga.
Wamachinga kwa sasa ni kama ndiyo chachu ya mafanikio ya 

kisiasa kwa CHADEMA, na hasa ushindi wa ubunge kwa chama hicho katika majimbo ya Nyamagana na Ilemela.

Lowassa aliyejiuzulu baada ya kuzongwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, alifanya ziara eneo la Makoroboi ambalo ni eneo maarufu kwa wamachinga na kuwapa msaada wa Sh milioni 20, na kuwaahidi kuwafanyia harambee ili kuwachangishia Sh bilioni moja, kwa ajili ya wamachinga wote wa jiji la Mwanza.

Ni kama vile sasa Lowassa anaingilia mbinu za kisiasa za CHADEMA, hususan za Mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje, ambaye kwa muda sasa, kati ya nguzo za nguvu zake za kisiasa ni wamachinga.

Ingawa Lowassa amekuwa na malengo yanayoaminika ya kutaka kuwania urais, japo makovu ya tuhuma za ufisadi ni vigumu kufutika kwake, lakini ni kama vile anapandikiza mwelekeo mpya wa siasa za CCM, jijini Mwanza.

Hata hivyo, hatua hiyo ya Lowassa inadaiwa kudhihirisha kufanikisha malengo yake binafsi zaidi, kwani angeweza kuongeza nguvu mfuko wa wamachinga uliopata kuchangiwa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa Mwanza mwaka jana.

Katika kuwasaidia wamachinga, Kikwete alitoa shilingi milioni 10 kuwasaidia katika mafunzo lakini kwa sasa, ni kama Lowassa ameamua kutwaa mtazamo huo wa Kikwete na chama chake kusaidia wamachinga, akiuweka katika mwelekeo binafsi zaidi.

"Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimeandika kuwa nimekuja na Naibu Katibu Mkuu CCM – Bara, Mwigulu Nchemba ili kubomoa ngome ya chama fulani hapa Mwanza, hilo siyo kweli, hayo yapuuzeni. Nimekuja na rafiki zangu ili kuwasikiliza kama mlivyoniita," alisema Lowassa akiwaeleza wamachinga wa Makoroboi huku akiwataja marafiki zake wa Mwanza kuwa ni Rapahel Chegeni, Mjumbe wa NEC CCM Wilaya ya Busega, Christopher Gachuma mjumbe wa NEC - Tarime, Shanif Mansoor Mbunge wa  Kwimba CCM na Altaf Mansoor maarufu kama 'dogo' Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Mafuta ya Mansoor Oil (MOIL), ambayo wanaiongoza na kaka yake, Mbunge wa Kwimba.

Wakati hayo yakiendelea jijini Mwanza, jijini Arusha, mbivu na mbichi kati ya CHADEMA na CCM zitajulikana mwishoni mwa juma hili, pale wananchi wa kata nne watakapopiga kura ya kuchagua madiwani, uchaguzi ambao umekuwa na mvuto wa aina yake, ikiamika CHADEMA ndicho chama chenye ushawishi Arusha, lakini pia CCM kikijizatiti kubomoa CHADEMA kisiasa kupitia sanduku la kura, kwa madai CHADEMA kimegeuza Arusha kuwa mkoa wa fujo, badala ya kuendelea kuwa mkoa tulivu kwa biashara ya utalii na shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Wagombea  wanaochuana kwa karibu na vyama vyao kwenye mabano ni Kata ya Themi; Melance Kinabo maarufu kama Kaburu (CHADEMA), Victor Mkolwe (CCM) na Labora Peter Ndarpoi (CUF), Kata ya Kaloleni, Emmanuel Kessy (CHADEMA), Emmanuel Meleari (CCM) na Abbas Darwesh (CUF).

Kata Elerai ni Jeremiah Mpinga (CHADEMA), Emmanuel Laizer (CCM), John Bayo (CUF) na Kata ya Kimandolu ni Rayson Ngowi (CHADEMA) na Edna Jonathan Sauli (CCM). Uchaguzi huo ulioahirishwa baada ya mlipuko wa bomu siku kuamkia kupiga kura, mjini Arusha katika viwanja vya Soweto, unatarajiwa 
kufanyika Julai 14, mwaka huu.

http://www.raiamwema.co.tz
Lowassa awaingilia CHADEMA
Mwandishi Wetu
Toleo la 302
10 Jul 2013
Waziri  Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa
WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiri kuwa minyukano ya kuwania tiketi ya urais ndani yake imeleta hofu kwa baadhi ya wananchi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameendelea na harakati za kuendesha harambee kwa makundi mbalimbali na sasa kawageukia wafanyabiashara ndogo ndogo, wamachinga jijini Mwanza.
Mkoa wa Mwanza umekuwa na ugeni kwa nyakati tofauti mwezi huu wa viongozi wa juu wa CCM, wiki jana mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Januari Makamba alifungua semina ya viongozi na watendaji wa CCM ngazi ya kata wilayani Ilemela.
Katika hotuba yake, alisema; “Nchi yetu ipo katika hofu, wananchi wanahofu kuhusu hatima ya uongozi wa nchi yetu. Wote tunafahamu kuna minyukano inaendelea kuhusu nani ni nani katika urais. Na minyukano hii ndiyo inayoleta hofu kwa wanachama na wananchi.”
“Afya ya chama chetu ndiyo afya ya nchi yetu. Kama viongozi ni wajibu wetu kujua kwa nini wananchi wana hofu. Tubaini upungufu uliopo na tuushughulikie ili kuwatoa hofu wananchi.’
Wakati Makamba akitoa tahadhari hiyo, Lowassa ameingia kwenye siasa za Mwanza kufanyia kazi makosa ya CCM ya mwaka 2010 ya kuwapuuza wamachinga.
Ni jambo dhahiri sasa, siasa za Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla upo ukweli mpya unaojidhirisha wazi kwamba siasa zake zinabadili mwelekeo, zikichagizwa zaidi na wamachinga.
Wamachinga kwa sasa ni kama ndiyo chachu ya mafanikio ya kisiasa kwa CHADEMA, na hasa ushindi wa ubunge kwa chama hicho katika majimbo ya Nyamagana na Ilemela.
Lowassa aliyejiuzulu baada ya kuzongwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, alifanya ziara eneo la Makoroboi ambalo ni eneo maarufu kwa wamachinga na kuwapa msaada wa Sh milioni 20, na kuwaahidi kuwafanyia harambee ili kuwachangishia Sh bilioni moja, kwa ajili ya wamachinga wote wa jiji la Mwanza.
Ni kama vile sasa Lowassa anaingilia mbinu za kisiasa za CHADEMA, hususan za Mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje, ambaye kwa muda sasa, kati ya nguzo za nguvu zake za kisiasa ni wamachinga.
Ingawa Lowassa amekuwa na malengo yanayoaminika ya kutaka kuwania urais, japo makovu ya tuhuma za ufisadi ni vigumu kufutika kwake, lakini ni kama vile anapandikiza mwelekeo mpya wa siasa za CCM, jijini Mwanza.
Hata hivyo, hatua hiyo ya Lowassa inadaiwa kudhihirisha kufanikisha malengo yake binafsi zaidi, kwani angeweza kuongeza nguvu mfuko wa wamachinga uliopata kuchangiwa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa Mwanza mwaka jana.
Katika kuwasaidia wamachinga, Kikwete alitoa shilingi milioni 10 kuwasaidia katika mafunzo lakini kwa sasa, ni kama Lowassa ameamua kutwaa mtazamo huo wa Kikwete na chama chake kusaidia wamachinga, akiuweka katika mwelekeo binafsi zaidi.
"Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimeandika kuwa nimekuja na Naibu Katibu Mkuu CCM – Bara, Mwigulu Nchemba ili kubomoa ngome ya chama fulani hapa Mwanza, hilo siyo kweli, hayo yapuuzeni. Nimekuja na rafiki zangu ili kuwasikiliza kama mlivyoniita," alisema Lowassa akiwaeleza wamachinga wa Makoroboi huku akiwataja marafiki zake wa Mwanza kuwa ni Rapahel Chegeni, Mjumbe wa NEC CCM Wilaya ya Busega, Christopher Gachuma mjumbe wa NEC - Tarime, Shanif Mansoor Mbunge wa  Kwimba CCM na Altaf Mansoor maarufu kama 'dogo' Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Mafuta ya Mansoor Oil (MOIL), ambayo wanaiongoza na kaka yake, Mbunge wa Kwimba.
Wakati hayo yakiendelea jijini Mwanza, jijini Arusha, mbivu na mbichi kati ya CHADEMA na CCM zitajulikana mwishoni mwa juma hili, pale wananchi wa kata nne watakapopiga kura ya kuchagua madiwani, uchaguzi ambao umekuwa na mvuto wa aina yake, ikiamika CHADEMA ndicho chama chenye ushawishi Arusha, lakini pia CCM kikijizatiti kubomoa CHADEMA kisiasa kupitia sanduku la kura, kwa madai CHADEMA kimegeuza Arusha kuwa mkoa wa fujo, badala ya kuendelea kuwa mkoa tulivu kwa biashara ya utalii na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Wagombea  wanaochuana kwa karibu na vyama vyao kwenye mabano ni Kata ya Themi; Melance Kinabo maarufu kama Kaburu (CHADEMA), Victor Mkolwe (CCM) na Labora Peter Ndarpoi (CUF), Kata ya Kaloleni, Emmanuel Kessy (CHADEMA), Emmanuel Meleari (CCM) na Abbas Darwesh (CUF).
Kata Elerai ni Jeremiah Mpinga (CHADEMA), Emmanuel Laizer (CCM), John Bayo (CUF) na Kata ya Kimandolu ni Rayson Ngowi (CHADEMA) na Edna Jonathan Sauli (CCM). Uchaguzi huo ulioahirishwa baada ya mlipuko wa bomu siku kuamkia kupiga kura, mjini Arusha katika viwanja vya Soweto, unatarajiwa kufanyika Julai 14, mwaka huu.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/lowassa-awaingilia-chadema#sthash.WZINXggn.dpuf

No comments:

Post a Comment