Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais
wa Marekani Mama Michelle Obama pamoja na Mama Laura Bush, mke wa Rais
Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush kwenye hoteli ya Serena
tarehe 2.7.2013.
---
Na Anna Nkinda - Maelezo
Mke wa Rais wa Marekani
Mama Michelle Obama amempongeza Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutoa
elimu bure kwa watoto Wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi .
Mama Obama alizitoa pongezi hizo leo
wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa
wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi
kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia wanawake na watoto hasa katika
upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.
"Jana nilitembelea makumbusho ya taifa,
nilikutana na watoto ambao baadhi yao walikuwa ni wale
wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure
elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri
anayoifanya", alisema Mama Obama.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama
Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha
wanawake wa Afrika
ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya,
elimu na ujasiriamali.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa katika mkutano huo
washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi na kutembelea
hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako
watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii
inayowazunguka.
Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo
anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na
Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili
kuimarisha bara la Afrika.
Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na
Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya
wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie
Blair.
Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika
lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya kwa wanawake, upatikanaji
Wa elimu na uchumi katika Afrika.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akihojiwa na Mtangazaji, Adesewa Josh kutoka
Channels TV ya nchini Nigeria wakati wa mkutano wa wake wa Marais wa
nchi zaa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam
tarehe 3.7.2013.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika wakisikiliza hotuba
ya Rais Jakaya Kikwete alipohutubia mkutano huo tarehe 3.7.2013.Picha na John Lukuwi
source: Haki Ngowi
No comments:
Post a Comment