BABA WA MAREHEMU KUINGIA MAREKANI LEO
Familia ya mwanafunzi mtanzania
aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia
nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo
vyetu faimilia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na
baba mkubwa wake bwana Ilyasa Sykes.
Marehemu ambaye alikuwa na miaka 22,
ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili
sykes na pia ni wa msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.
Omar aliuawa kwa shambulio la risasi
karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa
alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North
West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC) na Polisi wa chuo hicho
(HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika
bado hawajatiwa mbaroni.
LM
Kwa mujibu wa habari za ndani za
jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilichaanza
upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza
Swahili TV*, licha ya upepelezi wanaoendelea nao pia wanaomba
ushirikiano wa wananchi kwajili ya kufanikisha uchunguzi wao. zawadi ya
dola 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji
hao.
Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa
kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University
Polisi pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes, kwa mujibu wa maelezo
yao mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na
swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi
huu.
stay tuned kwa exclusive story
:tembelea http://swahilitv.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment