Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza la Sajent Shaibu Shehe Othman aliyeuawa
Daafur katika harakati za kulinda amani chini ya Kikosi cha Umoja wa
Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar
hdg
Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma,
wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha
Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la
ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya
askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele
ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13,
2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka
heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa
Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya
kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini
Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla
Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo. hdg
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment