WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, May 16, 2014

Ukawa wailipua CCM


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umehoji sababu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kug’ang’ania muundo wa serikali mbili wakati muundo huo umeshindwa kuleta maendeleo kkwa miaka 50.

Kauli hizo zilitolewa jana na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa ibrahim Lipumba,katika mikutano ya hadhara kwenye mikoa ya Manyara na Iringa.

Akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Babati, mkoani Manyara jana, Dk. Slaa aalidai kuwa CCM kinang’ang’ania muundo wa serikali mbili uendelee ili kuendeleza vitendo vya ufisadi ambavyo vimekuwa vikiongezeka nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Kwaraha mjini Babati, ulioandaliwa na Ukawa, Dk. Slaa alisema ufisadi umekuwa ukiongezeka nchini kutokana na Tanzania kuvaa koti la Tanganyika ili viongozi waendelee kulinda maslahi yao.

Dk. Slaa alisema  jambo la katiba halihitaji, porojo, udanyanyifu sababu katiba inahusu maisha ya watu, hivyo CCM wasitoe sababu dhaifu za kukataa serikali tatu kwa sababu wananchi wanafahamu ndani ya miaka 50 ya muundo wa serikali mbili kero zimekuwa zikiongezeka badala ya kupungua.

Alisema mwasisi wa taifa hili, Hayati mwalimu Julius Nyerere, katika hotuba zake alishawahi kusisitiza kuwa itakuwa ni upumbavu kama viongozi watakuwa na mawazo kwamba katiba haibadiliki na kwamba viongozi wa serikali wawe makini na suala la katiba ili wasije wakaharibu heshima ya nchi.

“Inashangaza CCM inataka kupora katiba na kuifanya ya kwake wakati muasisi wa nchi hii Nyerere katika hotuba zake alishawashi kusisitiza katiba ni mali ya wananchi,” alisema.

Alisema muundo wa serikali tatu hauwezi kuongeza gharama kama inavyodaiwa na CCM kwani ndani ya miaka ya 50, wananchi wameendelea kukabiliwa na kero mbalimbali ikiwamo ukosefu wa maji ndani ya muundo wa serikali mbili.

Aidha, Dk. Slaa alihoji suala la Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwamba amepata wapi mamlaka ya kuzindua miradi ambayo serikali imechangia fedha katika kuijenga.

 “Kinana anazindua miradi mbalimbali katika ziara zake anazofanya za kichama, je, nani amempa haki ya kuzindua miradi ya serikali?” alihoji.

Dk. Slaa alisema CCM ieleze imechangia kiasi gani katika kukamilisha miradi hiyo inayozindukiwa na Kinana kwa sababu utaratibu uliopo ni kwamba miradi yote inayojengwa inajengwa kwa fedha za serikali na siyo chama cha siasa.

Alisema hatua ya viongozi wa CCM kuzindua miradi iliyogharamiwa na serikali ni kuweka matabaka ndani ya nchi kwa sababu miradi hiyo inayengwa kwa fedha za Watanzania wote bila kujali anatoka chama fulani cha siasa.

“Kinana anatengeneza matabaka,sababu miradi yote inayengwa kwa fedha ambazo zimetokana na kodi ya wananchi wote, afafanue fedha hizo CCM wamechangia kiasi gani bila hivyo tutamtangaza kama janga la taifa,”alisema.

Alisema kumekuwa na propaganda kwamba Chadema na Ukawa wana mpango wa kupindua nchi kwa madai kuna fedha wanazopata kutoka kwa wafadhili wa nje.

Alisema Chadema kinatumia pesa zake na ikiishiwa huwa inakopa kwa Ndesamburo na Mbowe ambao ni viongozi na wafanyabiashara wakubwa.


“Kama tutapindua nchi kwa kutumia pesa za Mbowe, Ndesamburo hiyo ni hatari na serikali ya CCM inatakiwa kujiuzulu, hawa ni wanafanyabisahara halali na hata Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wanafahamu hivyo,” alisema. 

Aidha, alimtaka Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, kuwaelimisha wakuu wa polisi wa wilaya kwa nini wanazuia maandamano ya Ukawa.

LIPUMBA
Kwa upande wake, Profesa Lipumba alisema CCM wanaogopa kwamba Katiba ya sasa ikipitishwa itadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma ambayo yamekuwa yakifanywa na baadhi ya viongozi.

Katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Mwembe Togwa, Manispaa ya Iringa, Profesa Lipumba, alisema badala ya kujadili Rasimu ya Katiba ilitolewa na Tume ya Jaji warioba, lakini CCM wamekiuka na kujaribu kupenyeza maoni ya chama chao.

Alisema CCM wanatafuta njia yoyote kuzuia Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na ya Tume ya Jaji warioba baada ya kupata maoni ya wananchi isipitishwe kwa maelezo kuwa wanaogopa kuwa itawabana.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment