|
Wananchi wakishangilia na kuonesha vidole kuunga mkono serikali mbili za Muungano wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM leo kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.Mkutano huo uliudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana |
Mama
Fatma Karume akihutubia katika mkutano huo na kukemea Ukawa wanaotaka
kuuvunja Muungano kwa kutaka Serikali Tatu katika mabadiliko ya Katiba
mpya.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhman Kinana akimpongeza Mjane wa Hayati Abeid Amani Karume, kwa hotuba yake nzuri katika mkutano huo.
Wananchi
wakishangilia katika mkutano huo hasa baada ya Mjumbe wa NEC, Mohamed
Seif Khatib kumuelezea Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuwa na
tabia ya kinyonga kuhusu suala la Muungano, ambapo awali alikuwa
muuminji Muungano wa Serikali tatu, mara wa mkataba na sasa anataka
Serikali tau
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Idd akihutubia katika
mkutano huo na kupendekeza UKAWA kufutwa kwa vile haina uhalali wowote
akidai kuwa si chama kwani haina usajili. Alisema kuwa Ukawa imeundwa
kwa lengo la kuuvunja Muungano uliodumu kwa miaka 50 na kudumisha amani
na umoja kwa Tanzania.
Kinana na
viongozi wengine wakiuombea dua muungano wa Tanzania pamoja viongozi
waanzilishi wa muungano huo ambao ni Julius Nyerere na Abeid Karume.
Mjumbe wa
Bunge la Katiba,Asha Bakari Makame akimchana chana Katibu Mkuu wa CUF,
Seif Sharif Hamad kwa tabia yake ya kinyonga kuhusu muundo wa Muungano.
Mamboo poa .(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG) (FS)
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment