- · REFA AJIBU MPAMBANO NDANI YA SIKU 60
- · UKAWA SISI NI – 3
- · CCM SISI NI – 2
- · UWANJA WA MAPAMBANO WAGEUKIA UNGUJA NA PEMBA
Niliwahi andika huko nyuma kuwa safari ya
upatikaji wa katiba mpya katika taifa lolote sio rahisi kama mara nyingi
tunavyofikiria. Ni safari inayohitaji hekima busara na utashi wa hali ya juu na
sio mbwembwe ambazo zinatawaliwa na siasa na wanasiasa wetu.kwa upande wetu
kama taifa ilikuwa ni safari nzuri ambayo ilianzishwa na Mheshimiwa Raisi wetu Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana kwa karibu sana na Rais wa serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein.
Nia hii nzuri ilianza kukutana na vikwazona na kutofautiana
kwa wanasiasa tokea mwanzo wake;wakati wa maandalizi ya sheria ya rasimu ya katiba
mpya tofauti hizo zilitoka kwenye vyama vya upinzani na CCM bahati nzuri busara
za waheshimiwa maraisi wetu amabo wanafanya kazi kwa kushauriana ziliweza kuleta
mariadhiano na mswaada wa sheria ya mabadiliko ya katiba kakamilika na
baadae tume ya rasimu ya katiba mpya ikaundwa china ya uenyekiti wa Jaji
na waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba.
Mheshimiwa Warioba pamoja na tume yake baada ya
kukamilika kwa Uandaaji wa Rasimu maraisi wetu walipitia majina ya wajumbe waliopendekezwa
na kuwateua wajumbe 601 ili kuunda bunge maalum la katiba na vikao vyao
vilianza Febuari 18 2014 wakipewa miezi mitatu kukamilsha mchakato wa upatikaji
wa katiba mpya.
Amakweli kwa sisi wananchi mienzi hii mitatu
kwetu imekuwa ni kalakabao na bao la kisigino ambalo limetunyima ushindi wa maisha
yetu bora ambayo yangetokana na katiba hii mpya ambayo imekuwa ni kilio Taifa cha
muda mrefu.
Mwanzo huu mbaya ulianza na wawakilishi wetu
kuangalia masilahi yao binafsi: ombi la kuongezewa posho ya kujikimu wakipinga
ile ambayo walikuwa wamepangiwa na serikali. Kwa sisi wananchi wengi ilikuwa
haituingii akilini kwani hawa wawakilishi wetu ambao wanajua matatizo na
umasikini wetu baada ya kwenda Dodoma wakajadili mazuri ya katiba ili ituweze
kutukwamua sisi wananchi wa kawaida wao wanahangaika na matumbo yao. Kwa kweli
kwa tuliowengi hili likuwa na pigo la kushindwa kwa bunge hilo maalumu.
Tunaishukuru serikali kwani ilitupilia mbali ombi lao na wakaendelea na vikao
vyao.
Ni ukweli ambao haufichiki kwani siasa kama
itikadi ambayo inaongozwa na kikundi au chama Fulani ni itikadi ambayo
imefichika sana katika unafiki na hasa ukiwapata wanasiasa ambao wameficha
masilahi yao katika migongo ya watu wengine.
Miezi hii mitatu kama taifa imekuwa ni pigo
kubwa sana kwetu wananchi kwani tuliyoyaona na kusikia kwa upande mmoja ilikuwa
ni aibu na kwa upande mwingine wanasiasa wetu sio wavumilivu na walishindwa
kuvumiliana katika hoja zao ambazo zilikuwa zikitofautiana na itikadi zao. Tuliendelea
kushuhudia sio mjadala wenye tija kwa Taifa bali hisia binafsi za wajumbe wa
bunge la katiba na matusi na mipasho inayoishia kupakana matope na kutukanana.
Pengine hiyo ndio kazi ya siasa lakini kwa
upande wa pili wa wananchi mipasho na matusi hayatusaidia kutukwamua sisi hapa
tulipo leo; kama Taifa bado tunaogelea kwenye dimbwi umasikini tunatamani
tuishi katika maisha bora lakini kwa mwendo huu wa UKAWA na CCM kutupiana mpira
hawawezi kutuvusha sisi salama katika nchi ambayo itakuwa imejaa asali na
maziwa.
Tunaelewa kuwa hakuna hata sehemu moja
mabadiliko yakafanyika kwa urahisi; mabadiliko yeyote yale ni ushindani wa hoja
na yanahitaji uvumilivu na ushawishi; lakini kama tunataka hoja zetu zikubaliwe
mara moja hapo hakuna ushindani wa ndani ya siasa; nafikiri wajumbe wa Bunge
maalum ambalo limetawaliwa na wanazuoni, wanasiasa wakongwe na wataalumu
wengine kutoka asasi tofauti wanatakiwa kutumia Zaidi busara katika kutekeleza
majukumu yao mapya katika awamu ya pili ambapo refa ameshaamua mpambano ni siku
60 tu.
Katika awamu ya pili ya mjadala tunawaomba
wajumbe wa bunge maalumu kuzingatia amani na umoja wa Taifa letu na wanatakiwa watimize ndoto za taifa la kesho na sio kufikiria
tamaa zao je kama waasisi wa Taifa hili wasinge jitoa muhanga kwa ajili
yetu tungekuwa hapa ambapo tupo leo? Tusikubali kutumiwa kama daraja la
kuwavusha wengine ili kufurahia asali na maziwa ya taifa hili peke yao na sio
kwa faida ya Taifa nzaima.
Tunawaomba sana wajumbe wa Bunge maalumu kuepuka nguvu yeyote ile ambayo mwisho wake itakuwa ni nguvu ya
fujo kwani haitakuacha wewe mwenyewe salama. Na kama itakuacha salama utakuwa
mkimbizi katika nchi ya ugenini. Kama Taifa tutafurahi sana kama
majadiliano haya ambayo yameanza yakiweza kuendelea ili taifa lipatiwe Katiba
Bora ambayo itakuwa na misingi ya kuheshima mali ya umma ambao ndio msingi wa
maisha bora ya wananchi wa Taifa hili. Tukumbuke kuwa wajumbe wote ambao
wanaunda Bunge hili la katiba hatutaki watupatie katiba mpya kwa haki za
bunduki. Kwa kufanya hivyo watarudisha nyuma maendeleo ya Taifa letu.
Nafikiri itakuwa ni busara kama UKAWA watarudi
kwenye Bunge la katiba mkabadilishane hoja mfikie maamuzi na kama sisi wananchi
tutaona jinsi ambavyo haki haijetendeka hapo ni wakati mzuri wa kuwaunga mkono;
hebu tepuke Nguvu ya Umma kwa hivi sasa kwani mtawauruza wananchi; kwani
wananchi bado wananafasi yao nzuri tu ya kukubaliana nanyi au hapana katika
kura ya maoni.
Plato na Aristotle waliwahi sema kuwa “Yatupasa
kufahamu kwamba katika siasa ndiko liliko chimbuko na suluhisho la mambo yote
yanayowagusa watu na haki zao kuanzia uchumi, sayansi, uhunzi, ujenzi, ulezi,
uuguzi, sheria na hukumu zake, ulinzi wa taifa, mahusiano ya kimataifa n.k. Kwa
kuwa siasa ni uongozi, basi viongozi shuruti wawe watu waadilifu, wazalendo,
wakweli na waaminifu wenye moyo wa huruma na imani, wanaoguswa na shida za watu
na kuzitafutia dawa mujarabu, na wawe ni wakali kwa wale wasio waadilifu, wasio
wazalendo, wasio wakweli na wasio waaminifu”.
Mwanazuoni mmoja aliandika kuwa “Kumbe
wanaofanya kazi ya siasa kwa uadilifu wanakuwa wanaifanya kazi ya Mungu ya
kuwatumikia watu wake na malipo yake ni makubwa katika dunia hii na akhera.
Lakini wanaoifanya kazi ya siasa kwa kuieguza kuwa ni pango la wizi, rushwa,
uonevu, uuwaji, unyonyaji na kila ubaya ujulikanao, basi Mwenyezi Mungu Mfalme
wa Wafalme huwa anawadhalilisha katika dunia hii na kesho akhera ipo adhabu
kubwa inawasubiri. Na wasio na dini je wasemeje? Nao wana miongozo yao mfano
serikali yetu haina dini lakini inazo sheria za kukataza dhuluma na uonevu”.
Kutokana na dhuluma ya haki ya kutupatia katiba
mpya kwa katika kipindi cha siku Tisini ambazo walipangiwa; hoja zao zilitoka moyoni kumbe ni unafiki mtupu; katika
macho yao wanapoongea na kuwaongelea wananchi walala hoi utafikiri kweli
wanawajali, wakikupa kisogo tu wameshakusahau kabisa kalakabao.
Katika kipindi hiki nimejifunza kuwa Wanasiasa
wengi wanaangalia sana masilahi yao na kundi wanaloliongoza na sio masilahi ya
jamii inayowazunguka. Kwa maneno mengine wanasiasa wengi hawapo kwa ajili ya
manufaa ya nchi. Uwakilishi wao ili wafanikiwe kutimiza malengo yao umejikita
katika uongo, hila, wizi na ufisaidi kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Mimi
naamini kabisa siasa za ukweli zinawezekana, japo muhimili mkubwa wa siasa
wakati mwingine ni kupakana na kutukanana ili kushushiana hadhi mbele ya jamii
inayowapa dhamana wanasiasa watawale.
Kwa vile uongo hauwezi kuendelea kuwa utamaduni
wetu, na kwa kuwa uongo haupendezi hata mbele ya Macho ya Mungu (Kwa wanao
amini uwepo wake), sisi kama jamii, bado hatujachelewa, tubadilike, tujifunze
kusema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu, na jitihada hizo, zianzie ngazi
ya familia.
lakini najiuliza hao waongo wametokea wapi?,je
sio sehemu ya jamii yetu?,
mimi naamini kuwa kama Mheshimiwa raisi
alivyosema kuwa amekubali kuongeza siku 60 ili kukamilisha upatikaji wa katiba
mpya ama sio ambayo amabyo tumekuwa nayo kwa miaka 50 na imetufikisha hapa
tulipo tukiendelea kuwa wamoja na kufurahia Amani ambayo tunayo itaendelea
kutumika.
Mabadiliko huletwa na watu waliokusudia. lakini
anayetawala anachokifuata ni nani anasema nini ili amfurahishe au amfadhaishe
na huo ndio unakuwa mwanzo wa ufisadi na hakika fisadi ni nduguye na rushwa. Tukubaliane
kuleta maendeleo sote kwa pamoja bila kuzingatia tofauti zetu za kidini,
kiitikadi na hata kimtazamo na hakika kwa mantiki hiyo kila kitu kinawezekana,
maana hakuna mtu asiye na kipaji sote tuna
vipaji tofauti na sote tuna ndoto ya maisha mazuri. Lakini katika kufikia hatua hii sisi kama jamii
ya watanzania ni vizuri tukatahadhalisha
na wanasiasa wanaojalibu kubadili ukweli na kutoa lugha nyepesi nyepesi kwa
kuwalaghai wananchi. wanasiasa feki wanadhani watanzania wanaakili kama zao za
udanganyifu. Watanzania inabidi tuseme sasa basi. tunaitaji vitendo na si
siasa.
“Tupo
hapa sio kwa ajili ya kujadili masuala ya vyama vyetu vya siasa au kutetea
maslahi ya vyama vyetu bali kwa ajili ya kujadili mambo ya msingi ya kikatiba
ambayo yana manufaa kwa watanzania,” ila kupigania haki za wanyonge, kama walivyo fanya waasisi wetu, la kushangaza
wajumbe wetu mmekuwa watu wa vituko, majigambo na visasi kuliko kuwaletea
maendeleo ya kweli na amani wananchi waliowachagua.
Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa wale
waliochaguliwa kuingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba hawawezi kuwa na historia
ya kidunia kama ambavyo wengi waliofanikiwa kupigania haki na misingi ya nchi
zao wataendelea kusifika milele na milele kwa matusi, kususa na mipasho.
Na sisi kama Taifa tunakila sababu ya kuwashukuru
waanzilishi wa Muungano wetu ambao unatupa nguvu leo hii ya kuongea utakavyo na
umepata elimu ndani ya Muungano huu ambayo imekupa mtazamo wa kuona na kujenga
hoja: hivyo hatuna sababu ya kuwatusi na kuwabeza waasisi wa Taifa hili Hayati
Mwalimu Julius Nyerere na Marehemu Abeid Karume. Wao kama Binadamu wamelitoa
taifa mbali. Na wao kama binadamu wanamapungufu yao ya kiutendaji; Je wewe ni
safi sana na huna mapungufu yeyoye na uko tayari kurusha jiwe ukijijua kuwa
wewe ni mwanasiasa bora ndani ya chama chako na kwa jamii ya Tanzania.
Ni wakati wa kujitathimini kwa wajumbe wa bunge
maalumu ili watupatie katiba mpya na sio kuendelea kutuletea mipasho na matusi;
Tuendelee kumwomba Mungu kuwapa hekima na busara wanasiasa wetu waweze kuona
kama viongozi waliotangulia mbele ya haki, walivyokuwa wakiona mbele zaidi lakini
sasa wanabezwa sana kwa kuwa wamekufa.
MUNGU
IBARIKI AWAMU YA PILI YA SAFARI HII YA KATIBA MPYA- TANZANIA
No comments:
Post a Comment