Asisitiza ikishindakana basi
Rais Jakaya Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa
mshikamano daima pamoja na wafanyakazi wakati wa sherehe za Siku ya
Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudencia Kabaka, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(Tucta), Notibuka Maskini na Katibu Mkuu wa Tucta,Nicholaus Mgaya.
PICHA:KHALFAN SAID
Rais Jakaya Kikwete, amesema iwapo siku 60 za
nyongeza zitakwisha bila wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kufikia
maridhiano na kupata Katiba mpya, hakutakuwa na nyongeza nyingine ya
muda.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati akihutubia maelfu ya wafanyakazi katika sikuku ya Mei Mosi ambazo Kitaifa zilifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alisema hadi sasa mwenendo wa Bunge hilo haumtishi kwa kuwa kila mjumbe ana mawazo na mtazamo wake.
Rais alisema kwamba wanajadiliana kwa kina, bali kinachokera ni matumzi ya lugha za matusi na zisizo na staha.
“Waliomba nyongeza ya muda nikawapa siku 60, ni matumani ya ngu ndani ya siku hizo watafikia maridhiano na kutuletea Katiba bora, hakutakuwa na muda wa nyongeza, tukiongeza zaidi ya hapo itakuwa ni mwaka mzima tunafanya jambo hilo hilo,” alisema Rais Kikwete, ambaye aliongeza siku 60 baada ya bunge hilo kusuasua kutokana na kutawaliwa na malumbano na mabishano, hivyo kushindwa kufikia makubaliano katika masuala kadhaa kabla ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Rais Kikwete alisema wananchi watachoka kusikia na kuangalia jambo hilo hilo, wakati kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo ni vyema wajumbe wa Bunge hilo wakajikita katika kuvumiliana na kufikia maridhiano.
“Tukiongeza zaidi ya hapo ni kazi, itakuwa mwaka mzima tunazungumzie jambo moja watu watachoka kuona jambo hilo hilo, tunataka kuona na kufanya mambo mengine,” alibainisha.
Alisema iwapo Katiba mpya itashindwa kupatikana kwa kipindi hicho, Katiba ya sasa itaendelea kutumika na mchakato huo utaanza upya mbele ya safari.
“Wakishindwa kutupa katiba inayopemndekezwa, itabidi tusitishe mchakato hadi mbeleni,” alisema bila kufafanua zaidi.
Hata hivyo, kauli ya Rais Kikwete inaweza kutasfiriwa kwamba kama katiba itashindikana katika muda wa nyongeza ya siku 60 zitakazoanza Agosti 5, mwaka huu, huenda mchakato mwingine ukaanza baada ya yeye (Kikwete) kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2015.
Alisema pamoja na mvutano na hali inayoonekana ndani ya Bunge hilo, maridhiano ndiyo njia pakee ya kuweza kusonga mbele, hivyo alisema ni vyema wajumbe wakaingia katika maridhiano ili kupata Katiba Bora.
Alisema anatarajia wajumbe hao watatumia vyema kipindi cha mapumziko na majadala utakaportejea upya watafikia maamuzi mazuri kwa kutumia utaratibu uliowekwa kwa kupiga kura ya theluthi mbili kutoka Bara na Visiwani.
“Kuna wakati unaona wajumbe wanatukanana wenyewe kwa wenyewe…matuamani yangu hawataishia pale watarudi kujadili masuala ya msingi na kuwaletea wananchi Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupigiwa kura,” alisema Rais Kikwete akimaanisha kura ya maoni itakayopigwa na wananchi kuikubali au kuikataa katiba itakayopendekezwa.
Hata hivyo, alilitaka Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), kuwaeleza wajumbe wao walio ndani ya Bunge la Katiba masuala ya kuyazungumzia ambayo ni maslahi ya wafanyakazi.
“Wapeni kazi juu ya maeneo wanayopaswa kuyazungumzia ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi, mkiwaacha wafanye kwa vichwa na utashi wao, wataacha ya wafanyakazi na kuzungumza ya wengine ikiwamo kumezwa na makundi yenye ajenda zao,” alifafanua Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema ndani ya Bunge hilo wawakilishi kutoka Tucta ni 12, lakini wajumbe wengi ni wafanyakazi, hivyo watazungumzia maslahi yao.

“Sisemi wasijuhishe na mambo mengine yenye maslahi kwa Taifa, bali
waangalie ya maslahi ya wafanyakazi na wayazungumzie,” alifafanua
Kikwete.
Bunge Maalum la Katiba linaloundwa na wajumbe 639, ikiwa 201 ni wa kuteuliwa na Rais na wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, lilipewa siku 70 na nyongeza ya siku 20 kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Bunge hilo lililoanza Februari 18 ,mwaka huu lilitumia takribani siku 21 za mwanzo kujadili na kupitisha Kanuni za kuliongoza, ikiwamo kuunda kamati 16 ikiwamo 12 za kujadili sura za Rasimu Katiba.
Kamati hizo zilijichimbia katika kumbi mbalimbali mjini Dodoma na kujadili sura ya kwanza na ya sita, huku mjadala mzito na uliosababisha Bunge kuingia kwenye mvutano mkubwa ni sura ya sita inayozungumzia muundo wa Muungano.
Kundi la wajumbe wengi wakiongozwa na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatetea muundo wa sasa wa serikali mbili uendelee kwa kwa maelezo kuwa ndio utakaodumisha Muungano huku kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) linaloundwa na vyama vya upinzani vikiwamo Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na baadhi ya vyama vidogo wakisimamia serikali tatu kwa hoja kwamba Rasimu ilipendekeza serikali tatu kutokana na maoni ya wananchi.
Aidha, baada ya Kamati hizo kumaliza kazi na kurudi kama Bunge maalum, wenyeviti wa kamati hizo waliwasilsuha taarifa ya wengi huku wengine wakiwasilisha ya wachache.
Mjadala huo ulijikita katika kurushiana vijembe, maneno yasiyo na staha, matusi, kudhihaki waasisi, kumshambulia Jaji Warioba kwamba alichakachua takwimu na kupendekeza serikali tatu kwa maslahi yake binafsi.
Hata hivyo, wakati mjadala wa sura hizo ukiwa katikati kundi la wajumbe wanaounda Ukawa walitoka nje ya ukumbi Aprili 16, mwaka huu kususia mchakato huo kwa madai kwamba CCM imeliteka bunge na mjadala huo kutokana na kufuta mapendekezo ya tume ya sura hizo mbili na kupenyeza rasimu yake.
Hadi Bunge hilo linahairisha ngwe yake ya kwanza Aprili 25, mwaka huu wajumbe wa Ukawa walikuwa nje ya Bunge kwa takribani siku tisa huku wakianza kuzunguka maeneo kadhaa ya nchi kuwaeleza wananchi juu ya mwenendo wa Bunge kupitia mikutano ya hadhara.
Bunge hilo limehairishwa kupisha Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza Jumanne ijayo na B litaendelea tena Agosti 5, mwaka huu kwa siku 60 alizoziongeza rais Kikwete, baada ya kuombwa na Mwenyekiti wake, Samuel Sitta, baada ya kuona kwamba siku 70 zingemalizika kwa kujadili sura mbili tu bila hata kufikia makubaliano.
TUCTA YAKEMEA WAJUMBE
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, alisema wanakemea na kulaani matumizi ya lugha za kejeli, kashfa, matusi, vurugu na kutojiheshimu kulikoonyeshwa na wajumbe wa Bunge hilo.
Alisema wananchi wengi wamesikitishwa na hali hiyo hadi kukata tamaa ya kupatikana kwa katiba mpya.
“Tucta tunashauri namna pekee ya kufuta machungu na murejesha matumaini ya wananchi kwa Bunge hilo ni kwa wale wanaohusika, kutambua makosa yao na kujirekebisha,” alisema Mgaya.
Aidha, shirikisho hilo lilipendekeza kuwapo kwa semina za wajumbe wa Bunge hilo kwa nia ya kujadiliana, kuchambua na kuafikiana juu ya mfumo bora wa Muungano na upatikane nje ya Bunge utasaidia kuharakisha shughuli za Bunge hilo.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment