Dar es Salaam. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili nchini, Gilbert Buberwa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa dengue.
Kifo cha Dk Buberwa kinafanya idadi ya
watumishi wa afya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo kufikia
wawili baada ya muuguzi Hamida Likoti kufariki dunia wiki iliyopita. (J M)
Ugonjwa huo uliolipuka mkoani Dar es
Salaam, umezua taharuki kwa wakazi wake kwa sababu hauna tiba na
unasababishwa na mbu, Aedes Egyptae, anayeuma mchana na anayeweza
kuzaliana katika majisafi yaliyotuama.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania
(MAT), Dk Primus Saidia alisema jana kuwa Dk Buberwa alifariki dunia saa
saba usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH).
Dk Buberwa alianza kuumwa ugonjwa huo
akiwa kazini katika Hospitali ya Temeke na kulazwa na hali yake
ilipobadilika, alihamishiwa MNH kwa matibabu zaidi.
"Kadiri siku zilivyozidi kwenda
alibainika kwamba viungo vyake muhimu, yaani ini na figo vimeharibika,
hivyo alisafishwa figo huku akiwa amelezwa Chumba cha Uangalizi Maalumu
(ICU).
Dk Saidia alikumbusha kuwa virusi vya
dengue havina tiba isipokuwa dalili zake ambazo ni homa, kuumwa kichwa
na viungo vya mwili – ndizo zenye tiba.
Dk Buberwa alianza kuugua Mei 3, mwaka
huu na siku iliyofuata alipelekwa hospitali na mkewe ambako alilazwa
ili kupata uangalizi wa karibu wa madaktari wenzake.
Kaka wa marehemu, Wakili Nickson
Ludovick alisema: "Tunasubiri ndugu kutoka Bukoba na Musoma kwa mazishi
yatakayofanyika hapa Dar es Salaam katika makaburi ya Kinyerezi
keshokutwa."
Madaktari, wauguzi walazwa
Dk Malima alisema hadi jana, wafanyakazi tisa wa Hospitali ya Temeke walikuwa wamelazwa kutokana na homa hiyo.
Alisema wafanyakazi hao ni madaktari
watano, wauguzi watatu na mtaalamu mmoja wa maabara. "Kwa kipindi cha
wiki mbili zilizopita tumepokea wagonjwa wa dengue waliothibitika 15,"
alieleza Dk Malima.
chanzo Mwananchi
No comments:
Post a Comment