Papa Francis na Rais Mahmud Abbas wa Wapalestina (kushoto) na Rais Shimon Peres wa Israel (kulia) katika bustani za Vatican.
Papa
Francis ametowa wito mzito Jumapili (09.06.2014)kwa Rais Shimon Peres wa
Israel na mwenzake Mahmoud Abbas wa Wapalestina mwishoni mwa misa ya
jioni ya saa mbili iliofanyika katika bustani za Vatican, mjumuiko ambao
papa anataraji utauanzisha tena mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati.(Martha Magessa)
Amesema
juhudi za kutafuta amani zinahitaji ushujaa kuliko hata ule wa vita,
unahitaji kusema ndio kwa kukutana na hapana kwa mzozo,ndio kwa kwa na
mazungumzo na hapana kwa uhasama.
Papa
alikuwa akizungumza baada ya marabi wa Kiyahudi, makadinali wa Kikristo
na maimamu wa Kiislamu kukariri aya kutoka Agano la kale,agano jipya na
Quran kwa lugha ya Kitaliana,Kingereza,Kiyahudi na Kiarabu katika tukio
la kwanza lenye kujumuisha dini tafauti.
Katika
hotuba yake nzito kwa lugha ya Kitaliana Papa Francis ametowa wito wa
kuheshimiwa kwa makubaliano na kupinga vitendo vya uchokozi.Amesema yote
hayo yanahitaji ushujaa, nguvu na un'gan'ganizi.
Papa
Francis ambaye alitowa mwaliko wa ghafla kwa viongozi hao wawili wakati
wa ziara yake katika Ardhi Takatifu mwezi uliopita yaani Israel na
Maeneo ya Wapalestina amesema kwamba juhudi za kutafuta amani ni hatua
ya uwajibikaji mkubwa mbele ya ufahamu wetu na mbele ya watu wetu na
kueleza kwamba mamilioni ya watu duniani kote wa imani za dini tafauti
wanaiombea amani pamoja nao.
Huo
ulikuwa mkutano wa kwanza wa hadhara kati ya marais hao wawili kufanyika
baada ya zaidi ya mwaka mmoja na umefanyika ikiwa ni zaidi ya mwezi
mmoja baada ya mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Marekani
kusambaratika huku kila upande ukiilamu mwenzake.
Peres
ambaye anatimiza miaka 90 na muda wake unamalizika mwezi ujao aliachana
na hotuba aliyokuwa ameiandaa kwa Kingereza na Kihebrew kusema kwamba
yeye ni mtu mzima aliayeshuhudia vita na kuonja amani na kwamba viongozi
wote wanastahiki kuwapatia watoto mustakbali mwema.
Abbas
ameomba Mungu awaletee amani ya haki na kamili kwa nchi yao na eneo hilo
zima ili kwamba watu wa Mashariki ya Kati na dunia kwa jumla wafurahie
matunda ya amani,utulivu na kuishi pamoja kwa maelewano.
Wakati
huo huo Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso
ameuambia mkutano wa usalama wa Israel makubaliano ya muungano wa
Wapalestina na kundi la Hamas lazima yaungwe mkono.
Tamko
lake hilo la jana limekuja siku chache tu baada serikali ya muungano ya
Wapalestina yenye kuundwa na wataalmu huru wa kisiasa lakini inayoungwa
mkono na Hamas kuapishwa hatua ambayo imekaribishwa na jumuiya ya
kimataifa lakini imepingwa na Israel kama ni kikwazo kikuu cha amani.
Barroso
amewaambia wajumbe katika mkutano huo unaofanyika kwenye mji wa mwambao
wa Israel wa Herzliya kwamba kwa maslahi ya mustakbali wa makubaliano ya
amani na uwakilishi halali wa serikali makubaliano ya usuluhishi baina
ya Wapalestina yanapaswa kuungwa mkono.
CHANZO:DW
No comments:
Post a Comment