- MBUNGE JOSHUA NASSARI NA ANANDE NNKO WAMEREMETA KWENYE KANISA LA PENTEKOSTE KILINGA,MERU
Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete mkewe Anande Nnko. |
Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda mfupi baada ya kuvishana. |
Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na hapa maharusi wakitia saini katika vyeti vyao. |
Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete mumewe Joshua Nassari. |
Hatimaye Bw Harusi Joshua Nassari anateremka katika usafiri wake aina ya Range Rover muda mfupi baada ya kufika katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu kama kwa Mchungaji Babu. |
Wageni mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ya ndoa mmoja wapo ni huyu ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai(katikati) |
Bibi Harusi Anande Nnko alikuwa ni mwenye furaha kila wakati ,"Full Tabasamu." |
Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu walikuwa wamevalia mavazi nadhifu aina ya suti wakingojea ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la Kilinga. |
Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi Anande Nko. |
Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX. |
Kisha Maharusi wakapongezana. |
Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT) David Batenzi. |
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada hiyo (hawapo pichani) |
Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa kwanza) |
"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa. |
Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo. |
Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko. |
Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka zao katika kapu la sadaka. |
Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei. |
Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment