MZEE SMALL
Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku huu akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha Mzee Small
HISTORIA YA MAREHEMU MZEE SMALL
Marehemu Mzee Small akiwa na mkewe Bi. Fatuma.
Jina lake ni Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (58). Amezaliwa mwaka 1955. Alikuwa msanii mkongwe wa vichekesho na maigizo hapa Bongo.
Mzee Small (kushoto) akiwavunja mbavu JB, Mzee Mbizo na Richie.
Mzee Small alipata elimu ya msingi katika Shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, Mzee Small kila ulipozungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.
Mzee Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 30 iliyopita na alipata kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono’ (kwa sasa na yeye ni marehemu).
Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small ametumika katika vikundi vya…
source: global publisher
No comments:
Post a Comment