- ILETEENI TAIFA KATIBA MPYA
- MSIPOFANYA HIVYO DHAMBI HII ITAWATAFUNA MPAKA MNAINGIA KABURINI;
LAKINI: BADO
TUNAHITAJI BUSARA ZAIDI KUTOKA KWA WAJUMBE HASA WALE WANAOTOKANA NA VYAMA;
- Tukumbuke kuwa “Siasa si mchezo mchafu, ila wachezaji wake ndiyo wachafu.”
- Je wajumbe wa bunge la katiba wanapofanya maaumuzi kuhusu katiba mpya wanaangalia, dhana ya “wao” na “sisi”
- Ni kweli kuwa Siasa hutafasiriwa kuwa ni fikra, busara na mipango ya kuendesha nchi au ya kujinufaisha wao wenyewe?
- Litakuwa ni jambo la kuheshimiwa ka viongozi wetu kama Waheshimiwa wajumbe wa bunge la katiba watakuwa wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya mioyo kwa faida ya wananchi wao.
- Confucius aliwahi sema kuwa ‘Utajiri na vyeo ndivyo vitu ambavyo kila bianadamu anavitamani; lakini ikiwa njia ya kuvipata ni kwa kwenda kinyume na misingi yake, anapaswa ajiepushe navyo.’
- Rudolph Giuliani aliwahi sema kuwa ‘Kiongozi huchaguliwa kwa kuwa yeyote anayemuweka pale huwa anaamini maamuzi, tabia na uwezo wa maarifa yake – siyo ujuzi wa kufuata maoni. Ni wajibu wa kiongozi kuchukua hatua kufuatana na sifa hizo.’
- “kiongozi ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu za kuwafurahisha viongozi wengine”
- Tamaa ya kujilimbikizia mali huo ni udhaifu wa mwanadamu ambao hapaswi kuupa nafasi iwapo unazingatia uadilifu wa uongozi kama wajumbe wetu hizo ndizo fikra zao hawatufai hao.
Demokrasia kama falsafa ya
Plato ambayo inahusiana na uendeshaji wa shughuli za kisiasa inalenga zaidi
katika utumishi kwa umma na uendeshaji
wa jamii na taifa. Wananchi wote hawawezi ongoza nchi kwa mara moja; Katika
msingi huu wananchi kutokana na wingi wao waliridhika itakuwa sio rahisi kwa
wao wote kukutana, kufanya maamuzi na kuyasimamia moja kwa moja maamuzi hayo
yanayowahusu wao kama jamii; dhana ya kuwachagua viongozi wachache huzaliwa kwa
chimbuko hili na kuruhusiwa kuunda serikali. Ambayo huendesha kulingana na
katiba ya nchi ambayo imetokana na wananchi.
Tatizo kubwa tulilonalo
kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio
katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Kwani inatupasa kutambua
kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu. Lakini ridhaa hiyo
haitolewi hivi hivi tu, inaambatana na amana, kwamba waongozi watatekeleza
dhamana na wajibu wao kwa makubaliano na maelewano ya kufuata
barabara na kuheshimu ipasavyo kanuni na maadili fulani yanayoitambulisha
na kuiongoza jamii husika.
Kwa kauli zinazotofautiana
na misimamo inayotofautiana kuhusu ukamilishaji wa uandikaji wa katiba mpya
kufuatia mgomgano wa mawazo na itikadi; zoezi la uandikaji wa katiba mpya
unaishia kwenye fursa na ushawishi kwa
malengo ya chama au itikadi Fulani ndio iwe kinara wa katiba mpya. ikumbukwe
kuwa kiongozi muadilifu hakubali kufuata au kutoa maamuzi bila kufanya ukadirifu wa
hoja na hali husika.
Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya
wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu
John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa. Tuchague
viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza,
kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama
wanavyojinadi.
Serikali ni watu, inaundwa
na watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya
kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa
kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa
matakwa na utashi wa Wananchi wake.
- Kuna amani gani na utulivu gani katika nchi yetu wakati mioyo yetu sisi kama wananchi imevimba kwa kujaa hasira za ubinafsi wa hoja na matusi ya wajumbe waliopewa dhamana ya kutuwakilisha?
Uadilifu wa wajumbe wa
bunge la katiba umeporwa na wachache kwa manufaa binafsi nap engine kujiwekea
matumaini makubwa ya utajiri kwa baadae. Je mijadala ya hivi sasa kuhusu katiba
mpya nje ya bunge yataimarisha hoja za ufanisi wa katiba mpya au kuleta zaidi
mgawanyo? Je kuhusu amani yetu?
Kama ilivyo kwa umoja wa
kitaifa, kiongozi muadilifu pia hufanya kila bidii kuhakikisha amani na utulivu
wa kweli katika nchi vinapatikana. Amani na utulivu ni chachu ya wananchi kwa
kushirikiana na Serikali yao kujiletea maendeleo. Maendeleo hayaji mahala penye
magomvi na hasama. Lakini na amani na utulivu pia haviji mahala pasipo na haki
na uadilifu. Uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi hupelekea hasara ya maisha na
mali ya watu na hayo hayawi malengo ya uongozi muadilifu katika nchi
Uadilifu wa uongozi unadai
kuheshimu nguvu ya hoja na fikra bora na hayo yanaweza kupatikana tu iwapo nchi
inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia. Hivyo, katika kutoa uongozi sahihi, kwa
kuzingatia maslahi bora ya nchi na watu wake, haki, uadilifu, umoja, amani na
utulivu, hapana budi kwa kiongozi kuiamini, kuiheshimu na kuifuata barabara
misingi ya kidemokrasia.
Bado binadamu si mkamilifu
na kwa vyovyote vile hufikia mahala akafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kama
yalifanywa kwa nia njema na kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana wakati
maamuzi hayo yanafanywa. Hayo yanaeleweka na kiongozi muadilifu anapaswa
kuyakubali na kuliomba radhi Taifa. Hiki ndiyo kilele na kigezo kikuu cha
uadilifu wa uongozi katika siasa. Kukubali kubeba dhamana kwa madhara
yaliyotokana na maamuzi yako au yaliyofanywa kwa jina lako.
Maamuzi ya kiongozi wa
kisiasa huathiri taifa zima, busara na hekima huzaa maamuzi yanayotokana na
tafakuri ya kina, yanayozingatia hali halisi ya mambo na maslahi na manufaa ya
muda mrefu. Kiongozi muadilifu anatakiwa ayaone haya na ayazigatie kwa kila
hatua anayochukua.
Je kama baadhi ya wajumbe
wa bunge la katiba watasusia kikao ambacho kinatarajia kuanza mwezi wa Nane je
watakuwa wame kurupuka katika kufanya
maamuzi hayo bila kuyafanyia kazi vizuri na kukiuka msingi mkubwa sana wa
demokrasia? Tukubali tu kuwa njia ya kusonga mbele ni kukubali kutofautiana
katika fikra lakini tubaki kuwa wamoja katika hoja na maridhiano.
Wajumbe wa bunge la katika
2014 mnapaswa kujitafakari wenyewe na kuona mzigo mzito ambao uko mbele yenu
leo hii kwa faida ya Taifa na sio kundeleza matusi, vijembe, ubabe shindaneni
kwa hoja na hatimaye mkubaliane kwa maridhiano.
Wananchi tunasubiri
kilicho bora bila kuathiri amani na umoja wetu wa kitaifa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
No comments:
Post a Comment