Kuna hii nukuu kuhusu aina tatu za marafiki najaribu kuioanisha na viongozi wetu wa siasa Tanzania; Je wanasiasa wetu wanafanana na nukuu hii?
“Kuna aina tatu za marafiki, wale wanaolinganishwa na chakula kwani bila chakula hatuwezi ishi; wale kama dawa ambao tunawahitaji wakati Fulani tu na wale kama ugonjwa ambao hauwahitajia kabisa”.
Maisha katika medali za siasa katika dhama hizi je tunaweza kuwalinganisha au kuwatenga wanasiasa wetu katika makundi matatu kulingana na nukuu ya hapo juu? Kama ni ndio, swali la msingi hapa la kufungulia mjadala wetu wa leo Je tafsiri ya nukuu hii iweje sasa?. Na namna gani tunaweza kudurufu ukweli wa msemo huu;
Hebu tuwangalie Wanasiasa ambao tunaweza kuwalinganisha na
“chakula”;
kundi hili ni lile la wanasiasa ambao wana busara, hekima uadilifu, waaminifu, wakweli wastaarabu wacha Mungu na wawajibikaji wa kweli; utendaji wao wa kazi unaongozwa na maadili na woga kulingana na imani zao na zinazoangalia sana matendo mema. (Hayati Edward M.Sokoine )
Kundi hili wao wanaona kuwa nafasi ambazo wanazo kama wanasiasa au cheo ni dhamana isipotumiwa vizuri kwa manufaa ya wote mtoaji anahaki ya kukichua cheo hicho na kumpa mtu mwingene ambaye ni mwadilifu, na mwaminifu.
Tunajua kuwa chakula ni uhai, na ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu, kwani mwili wa binadanu unahitaji chakula, bila chakula mwili utadhoofika na hatimaye kushindwa kufanya kazi na pengine kusababisha umauti kwa kiumbe husika;
Hili ni kundi ambalo kwa sababu ya ukweli wao uwajibikaji wao wakipata nafasi nzuri ya kuwatumikia wananchi wanatekeleza ahadi kwa matendo, na ikitokea kunatatizo la utekelezaji wa ahadi hizo anakuwa tayari kusema ukweli na wananchi wanakubaliana naye kwa tabia yake ya iliyotukuka.
Hawa ni wale ambao wanaweka masilahi ya taifa mbele kwa faida ya watanzania, ambao wao huridhia muafaka wa sera nzuri za maendeleo ya nchi. Hawa ni wale ambao wanajenga daraja la uaminifu kati yao na wananchi waliowapa nafasi ya kuwatukimia. Hawa sio wanafiki wachoyo, wezi wala rushwa; ni viongozi ambao wanaridhika na kile kidogo ambacho wanapata; ( Mwalimu Nyerere)
Wanasiasa kama dawa
Hawa ni wanasiasa ambao wana vipaji vya kuweza kujenga hoja nzuri na wanajitahidi katika utekelezaji wa sera nzuri kwa wananchi; lakini wanashindwa kutimiza malengo yao kwani mara nyingi wanakosa nyezo nzuri za utandaji au kukubalika ndani ya serikali kwani. Ni kundi ambalo ni nzuri na tegemeo katika uhai wa siasa na uongozi wan chi, lakini hawahitajiki sana wanatumika tu kwa sababu Fulani kwa muda mfupi hataji likikamilika husaauliwa mara mpaka kuwe na hitaji tene; hawa ni madorate wazuri wajenga hoja nzuri hata wakati mwingine wapatanishi wazuri; tatizo hawahitajiki wakati wote kwani wanaonekana kama vikwazo na wakati mwingine wanakuwa hawana nguvu sana na wakiweza kufanya kazi pamoja na wanasiasa wa kundi la kwanza kuna kuwa na msukumo mzuri sana wa maendeleo ya nchi;
Hawa ni wafichuaji wa uozo wa serikali
Wanansiasa kama ugonjwa
Kundi hilli la wanasiasa hatuwahitaji kabisa kwani ndio wale mangunguli wa kula rushwa ambao wanaishia kuliingiza taifa katika hasara kubwa sana;
Kundi hili linatawaliwa na ubinafsi zaidi; kundi la umimi ni watu
wasiojali maendeleo ya wananchi kwa jumla wao hukumbuka tu raha zao hawakumbuki wengine. Hawa ni wanasiasa ambao wanazungumza mno kuhusu siasa na sio sera. Kwao siasa ni kila kitu; Wanasiasa wabaya daima huweka matumaini yao mbele na kuua matumaini ya maendeleo ya taifa; kwa kuwalagai wananchi kwa siasa uchara zenye faida ya muda mfupi na huwa kama kiini macho kwaJamii.
Kundi hili lina pesa nyingi ambazo upatikanaji wake unatia mashaka; daima ni pesa chafu na zinaendelea kutumika katika mchezo mchafu. Hawa ni wanasiasa ambao ni wala rushwa, rusha wanapata kutokana na kujihusisha na rushwa; ni makini na ni werevu sana na wanafahamiana na watu wengi wapenda rushwa; kwao siasa ni rushwa na bila kujiingiza kwenye siasa hakuna rushwa.
Je tutauondoaje ugonjwa huu Mkubwa?
Tunawahitaji tuwe na wafanyakazi wa serikali ambao ni waaminifu ambao wataweza kuwazuia wanasiasa walafi katika mipango yao ya ufisadi.
tunahitaji serikal ambayo ni safi; tunahitaji watendaji wasafi ambao ni sehemu kubwa ya serikali. Serikali ambayo haitakuwa tayari kuwakaribisha mafisadi hao katika utendaji wake; serikali ambayo itakuwa tayari kuishi kwa matendo bora na kuamini kuwa “ Ikulu ni Mahali Patakatifu” na sio sehemu ya kuwaruhusu mafisadi kuchafua utakatifu wake.
Ni ukweli kuwa hatuwezi kupata wanasiasa wakamilifu kwa asilimia mia moja; bali tunawihitaji wanasiasa ambao ni watendaji na waadilifu kwa asilikia kubwa ambao watajitoa mhanga kwa ajili ya maendeleo ya watu wao na sio kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.( sakata la Umeme Tanzania nani wa kulaumiwa ni siasa chafu iliyochafua hali ya mwanga na kuleta giza nene)
Tunahitaji viongozi wanaoweza kukemea hali hii ili kuwanyima nafasi mafisadi kuuza nchi kwa faida binafsi. Ni ukweli kuwa Uongo na maigizo ya ulaghai yakirudiwa sana bila kukemewa yanaweza kuonekana kama ukweli; na wao kuonekana kuwa ni waleta maendeleo kumbe wamevaa ngozi ya kondoo wakati ndani ni chui wabaya sana.
No comments:
Post a Comment