WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, July 16, 2011

BUNGE LETU NA MWELEKEKEO WAKE WA UTENDAJI (POSHO)

WAHESHIMIWA WABUNGE TUMIENI POSHO ZENU KATIKA KUPATA USHAURI WA KITAALAMU KWA FAIDA YA MAJIMBO YENU.

Bunge letu la 10 katika mikutano yake iliyofanyika na tangu kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka jana, limeonekana mbele ya jumuia ya kitanzania ni bunge ambalo limetawaliwa na mambo mengi ya vituko ambayo pengine kwa wananchi wengi ni kama bunge ambalo halijadili sana matatizo ya wananchi bali linaishia katika mambo ya aibu kwa chombo kikubwa cha kutunga sheria na kusimamia uendeshaji wa mambo ya Serikali.

Wengi wanaona kinachoendelea Dodoma kila wakikutana ni kama uhuru ambao umepita mipaka ya kujadiliana kwa lugha ya kistaarabu, ni uhuru unaofanana na ule wa kijiweni au katika vikao vya moja baridi moja moto; au ni mijaddala ambayo inaendelea katika mazingira ambayo maelewano yanakuwa hayana usimamizi kila mtu anasema, na kama vile hakuna kiongozi wa kusimamia;
Bunge la 10 sio tu linajadili mambo ya manufaa kwa nchi yetu pekee, na kutoa michango yenye tija, bali huwa tunashuhudia vituko vya wabunge na kejeli wanazozitoa,

Pamoja na kuwa Mheshimiwa Spika amewaruhusu kuwa “Wewe kama una shida yako sema hapa… hata Mbunge akienda na vituko vyake bungeni, wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge wanaendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakanywe chai pamoja, waendelee na kazi”.  

Je Kauli hii inaashiria nini? Kwamba wabunge wanaruhusiwa kuongea chochote na kufanya chochote bila kujali maadili au Ethics za uongozi? Je Wabunge wanatawaliwa na maadili gani? Na kama ni hivyo kauli kama, “mlango ufungwe tupigane” ni sahihi? Kama ndivyo kwa nini basi mbunge alitolewa kwa kuvaa tofauti na maadili ya Kibunge? Je kauli yeyote iwe nzuri au mbayo ambayo haikizi utendaji wa bunge zinakubaliwa?

Je masilahi ya nchi yatatetewa vipi? Kama hakuna utaratibu wa kuzibiti nini kinasemwa  nafikiri kauli kama hizi zitakuwa ngumu kutekelezwa, mheshimiwa Spika aliendelea kusahuri kuwa:

“Nawaomba tuweke maslahi ya Watanzania na taifa mbele,tudumishe amani na utulivu, tupuuze sera zozote za kudhoofisha utaifa wetu kama Watanzania na kutugawa kwa misingi yoyote ile, iwe ya kikabila, imani za dini, rangi au kwa itikadi za kisiasa”

“Jamani tuendelee kukua, tusiendelee kuwa kero kwa watu. Walikuwa wanapenda sana kuangalia sana kipindi hiki, lakini sasa wengine wanakereka sana kwa tabia zetu. Kwa hiyo tubadilike, muwe watu waheshimiwa kama tunavyoheshimiwa na watu waliotuchagua.”

Nafikiri hakuna demokrasia ambayo haiana mipaka lazima kuna mipaka ya kila kitu: Je faida ya Mwongozo na kanuni za bunge zinafaida gani kwa wabunge na taif a kwa ujumla wake?


Kama Spika alivyodsema “Kuhusu hili la ‘Utaratibu na Mwongozo’, kwa kweli sasa tunatia aibu. Waheshimiwa mnajidharau, yaani imekuwa kelele, huku Mwongozo, mara kuhusu Utaratibu, tumegeuka kama watu wa Kariakoo!..... “Kariakoo ni sokoni kila mtu anazungumza anavyotaka na hakuna wa kuwazuia, lakini hapa ndani kuna utaratibu si sokoni,”

Kwa kweli nafikiri Posho ya Ubunge ya kila mwezi ambayo ni Sh5 milioni ambayo ni kwa ajili ya mafuta, matengenezo ya gari, malipo ya dereva na wasaidizi wa mbunge. Kama waheshimiwa wabunge wataweza kuitumia vizuri kuwaweka karibu na wataalamu kama wana sheria, wanauchumi na wataalamu wa jamii itawasaidia sana hawa waheshimiwa kwani hata wakiwa wanakwenda bungeni watajuu nini wanatakiwa kusema au hata wanapotoa hoja kuhusu mahitaji ya majimbo yao zinakuwa na uzito wa vielelezo; na hata uchangiaji wa hoja utakuwa ni wa uzito zaidi, kama wabunge  wengine wanavyofanya duniani? Hoja nzuri huvuta hisia za wabunge wengine bila kuangalia ni chama gani mbunge yuko; huu ndio mwelekeo ambao wananchi tunahitaji sasa;

Je wabunge wetu wana waataalamu wowote? Kwa vile posho zao kwa hivi sasa ziko kisheria basi watumie posho hizo kwa faida ya wananchi walipa kodi kwa kuwaletea maendeleo sio kugeuza bunge kuwa sehemu ya vituko  maudhi na vichekesho;
Kwa kweli Inatia aibu sana kwa watu kama wabunge kuzozana na kuoneshana umwamba ndani ya bunge, kauli za mwongozo kila wakati ni upevu wa demokrasia au kupevuka kisiasa bali inakuwa ni kero kwa wafuatiliaji makini wa mambo ya bunge kwa maendeleo ya wananchi.

Sio vyema Kulinganisha bunge letu na sehemu kama kariakoo kwani kwa mlinganishoi huu tunalivunjia heshima Bunge na  waheshimiwa wabunge kama moja ya muhimili mkuu wa serikali.
tabia ya kuropoka ovyo bungeni inayofanywa na baadhi ya wabunge mithili ya mkusanyiko ambao hauna nidhamu pasipomsimamizi.

“Hapa bungeni kuna utaratibu wa kuzungumza, mtu akiwa anazungumza wengine mnapaswa kumsikiliza, lakini jana (Juzi) mtu mmoja anachangia na wengine wanazungumza utadhani mko Kariakoo.”

Bunge si sehemu ya kuendeleza tabia za uropokaji, Bunge ni chombo cha kukusanya fikra ambazo zinasaidia serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake. Ni ukweli kuwa bunge litabaki kuwa ni sehemu ya kupambanisha fikra zinazogusa mustakabali wa umma

Waheshimiwa wabunge tumieni posho ambazo mnaendelea kuzipata kwa kuboresha hoja kwa kupata ushauri wa kitaalamu katika utendaji wenu;

Tunaweza kuzichapa kama huko Russia, waheshimiwa wakionyeshana ubabe
India je tatizo hapa lilikuwa nini hapa.

No comments:

Post a Comment