SHERIA AU MAZOEA AMBAYO YANAENDESHA WIZARA ZETU?
“Don't ever take a fence down until you know why it was put up”.
"Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana,"
"Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (jana), nitamuarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua."
KISHERIA hakuna mtu aliye juu ya sheria. Iwe kiongozi wa umma, serikali, taasisi yoyote au mwananchi wa kawaida anatakiwa kuheshimu kanuni na misingi ya sheria.Watu wote wanapaswa kutii,
kuheshimu na kuzifuata kwa mujibu wa Katiba ya nchi husika.
Sheria zinapaswa kufuatwa bila kujali au kubagua mhusika kwa namna yoyote uwe wa rangi, kabila, dini, itikadi au kitu kingine cha namna hiyo; kwa msingi huo Kuvunja sheria yoyote ya nchi ni uhalifu. Bila kujali cheo au hadhi ya mhusika, itikadi yake, utajiri au umaskini kiasi gani, wala haihusiani na rangi hata kabila ni jambo ambalo haliruhusiwi. Kwa msingi huu ukiukwaji ukifanywa kunakuwa na karipio linaloendana na adhabu, kwa msingi huu hata matukio ya watu kujichukulia sheria mikononi kwa kuadhibu wenzao ni kosa kisheria japo kiutamaduni wetu wa kila siku inaonekana ni haki mbadala.
Viongozi wetu wanaposhindwa kufuata sheria na kuvunja sheria hupelekea wananchi kuishi maisha ya wasiwasi kwani hupoteza imani na kuua mfumo mzima wa sheria na uaminifu;
Tukio la hivi karibuni la Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini la kuamurisha idara zote ambazo ziko chini yake kuchangia mchakato wa Bajeti ya Wizara hiyo, kimsingi ni ukiukaji wa sheria ya Matumizi sahii ya fedha za walipa kodi;
Watu wamejiuliza maswali mengi sana hizo pesa zote kwa nini zitumike katika mchakato wa kupitisha bajeti husika? Bajeti hiyo ilikuwa na siri gani kubwa hata wizara itafute pesa zaidi kutoka katika idara zake?
Pesa hizo walikuwa wanapelekewa akina nani? Walikuwa wanalipwa akina nani? Na kwa kiwango na kigezo gani?
Je kunauwezekano mkubwa sana kwamba kuna pesa nyingi sana katika wizara na idara zake ambazo ziko ziko tu (idle) na waataalamu kwa kushirikiana na wanasiasa wanazitafutia njia za kuzitafuna kwa kigeuzo cha uandaaji na upitishaji wa bajeti?
Je katibu Mkuu husika huyo ametolewa kafara safari hii kwani inasomeka kuwa ni mazoea yao kila mwaka utaratibu huu hufanyika?
Sasa kama katibu mkuu ni kinara wa kuashiria rushwa ndani ya utendaji wa kazi zake je kuna haki ambayo itatendeka kwani tunafahamu kuwa makatibu wakuu ndio wataalaum ndani ya wizara ambao wanatumiwa kama wataalamu (professional /professionalism).
Katika hali kama hii je tunaweza kumuhukumu mara moja au inatulazimu tusubiri na kutoa hukumu mpaka tupate vielelzo vya uhakika kama Katibu Mkuu Kiongozi alivyosema?
Kama ndivyo je utaratibu wa serikali wa kulishughulikia swala hili ni sahihi? Kwa nini aendelee kulipwa (likizo) ya malipo wakati ni mtuhumiwa katika kesi hii?, kwanini stahili zake zote zisimamishwe na kama hatakuwa na hatia ndipo arudishiwe hizo stahili?
Kwa staili hii Je serikali haioni kuwa unaongeza wasiwasi katika uchunguzi wake na pengine kuwapa wananchi mawsali mengi ya kujiuliza kuwa serikali yetu sio makini?
Si vyema kuhukumu au kuondoa uzio bila kuelewa nini kiko nyuma ya huo uzio? Kwa nini katibu huyo aliytoa agizo hili kwa kujiamini kimandishi?
Je ni utaratibu huu ni wa wizara hii tu au ni wizara zote hutumia utaratibu huu katika uchakachuaji wa bajeti zao?
Sheria daima zinawekwa kama uzio ili kuzuia wavunjaji wa sheria wasipate njia rahisi katika kutekeleza adhima yao; sehemu ikiwekwa uzio tayari inakuwa imejijengea utaratibu wa watu kufuata kana wanataka kuingia ndani wapiti katika mlango ulio salama; endapo mtu ataruka uzio huo huyo ni mharifu na anastahili adhabu; kwa hiyo uzio hujengwa kwa ajili ya kumzuia mtu yeyote kukiuka sheria zilizopo; Je katibu huyu hajekiuka taratibu kwa kuruka uzio alioujenga yeye mwenyewe?
Kama ndio hivyo kwa nini tujenge uzio ambao mwisho wa siku na wajengaji wenyewe ndio wanao vunja?
Tunaiomba serikali iwaadhibu watendaji wote wa juu wa serikali kulingana na matendo yao kitendo cha Katibu Mkuu kuagiza uchangiji wa pesa hizo na kuwa na matumizi ambayo hayajeidhinishwa kisheria ni kosa kubwa la kuhujumu uchumi wanchi;
Nakumbuka mheshimiwa Rais aliwahi kusema kuwa;
kila mara zingatieni nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, kanuni, taratibu za fehda, na taratibu za manunuzi.
Wabadhirifu na wezi wa fedha za umma wachukuliwe hatua za kisheria.
Je katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini wakati anaandaa utaratibu huu alishauriana na nani? Kuna Kiongozi wa juu pengine alimpa uhakika kuwa achangishe tu atamlinda au utaratibu ambao ameukuta katika wizara hiyo na amekuwa akiuendeleza tu?
Mheshimiwa Rais sasa anatakiwa waonea haya au kuwavumilia viongozi hawawa namna hii wanaotumia nafasi zao katiaka kufanya ubadhirifu ambao unakoleza ufujaji wa mali ya umma na kudidimiza maendeleo ya nchi. Ni viongozi hawa ambao wanasukuma guruduma la maendeleo nyuma wakati wenzao tunajitahidi kulibingirisha kwenda mbele!
Tunaihimiza serikali kuchukua hatua zinazofaa ambazo zitakuwa ni mfano kwa wengine ambao wanatabia kama ya Katibu Mkuu mhusika.
No comments:
Post a Comment