Huyu ndie KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye;
Je nafasi hiyo ambayo chama chake imemkabidhi inamfaa au hapana?
Je staili zake za utendaji zitasaidia kurudisha imani ya wananchama wake hasa wale ambao wamehama au wako wako tu ?
Je kujichanganya kwake na ndani ya maisha ya wanachama wake na wapenda siasa kutasaidia kukiimarisha na kukijengea chama chake imani? kama ndio je anahitaji watendaji kama yeye amabao ni vijana ambao wana hitaji nguvu ya hoja na sio porojo;
Nape Nnauye kweli ataweza kuokoa Chama kilichofanya vibaya wakati wa uchaguzi kwa kupata kura ambazo hazikutarajiwa; Kijana anayedhani anaweza kuokoa CCM kwa kubadilishana hoja dhidi ya upinzani.
Kabla ya kupata nafasi hiyo alishawahi sema, “Wenzetu wamepiga hatua sana katika ‘accountability’, uongozi si jambo watu wanapigania, maana tunahitaji maadili makubwa na mara nyingi ku-sacrifice kwa mengi, hivyo anayekwenda hata kama si wote, anakuwa kaamua kweli kuwatumikia watu... Tulikuwa nayo hii kwenye Azimio la Arusha na nadhani sasa ni muhimu sana kuliko mwaka 1967 lilipoanzishwa,” alisema Nnauye.
Alisema kwa siasa za Tanzania, bado kuna safari ndefu ya kwenda tunakotaka japo kuwa yapo mazuri, lakini pia yapo mapungufu yanayopaswa kufanyiwa kazi na vyama vya siasa ili kuweza kujenga demokrasia ya kweli.
Je kauli zake hizi ndizo anazozifanyia kazi sasa au naye anarudi kule kule nyuma akifuata mapigo ya Gitaa ambalo pengine ni bovu au nyuzi zake zimelegea, au mpigaji hajui au hana uzoefu au tatizo la uelewa au ni woga hajelizoea hilo gitaa, au anaogopa vitisho vya wasikilizaji.
Kila la kheri Bwana Nape wana CCM wameonyesha kukusikiliza
No comments:
Post a Comment