MZEE MAKAMBA INATOSHA NA INAFAA UPUMZIKE
SEHEMU YA KWANZA
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mheshimiwa Rais JK alivunja kamati Kuu ya CCM huko Dodoma tarehe 9/4/2011 tukio ambalo lilihusisha kustaafishwa kwa Katibu wake Mkuu mzee wetu Bwana Yusufu Makamba;
Utendaji wa kusua sua wa Mzee makamba umekuwa kilio cha siku nyingi cha wanachama wa CCM; wengi walikuwa hawaridhishwi na utendaji wake wa kazi hasa katika maswalal yote ambayo yanahusu kumshauri Mheshimiwa Rais kama kiongozi wa serikali na kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi;
Pamoja na mapungufu Mengi ya Mzee wetu Makamba lakini Mheshimiwa Rais ataendelea kubeba lawama kwa kuchelewa kuliona tatizo hili pamoja na kilio kirefu cha wana CCM kuwa Makamba alikuwa mzigo kwa Chama katika ufanisi;
Pamoja na uamuzi huu Mzuri na mzito swali la msingi hapa ni hili Kwa nini imemchukua Mwenyekiti wa Chama nuda mrefu kusafisha utendaji ndani ya chama?
kama Kweli kamati yake kuu ya chama chake ilikuwa haifanyi kazi vizuri, na imemwangusha kwa kiasi kikubwa, kwa nini alikubali kuendelea kuibeba?, "ni sawa kama kuendesha gari ambalo halina balance nzuri ya upepo unaotakiwa kwenye matairi yake, kwani kabla ya ajali utalazimika kutumia nguvu zaidi katika kuhakikisha kuwa gari hilo inakwenda vizuri na haliachi barabara", kitu ambacho kimekuwa sicho, kwani katika hali tofauti tofauti Mwenyekiti amejikuta akishindwa kuhimili mikiki mikiki ya barabarani ambayo imekuwa ikisababishwa na ubovu wa matairi( watendaji) kwa au kujali masilai yao binafsi, na kupoteza mwelekeo wa sera na dira za Chama;

Sijui nini kimemtokea Dereva Wetu(mheshimiwa Rais Na Mwenyekiti wa CCM) mpaka ameamua kulitosa gari hilo amabalo fundi wake Mkuu alikuwa Mzee Makamba; na kuamua kuchukua gari nyingine;
Kwa tafakari yangu na kama nilivyowahi kuandika katika blog hii huko nyuma kuwa kuwa Mzee Makamba alishindwa kutekeleza yafuatayo;
Kwa tafakari yangu na kama nilivyowahi kuandika katika blog hii huko nyuma kuwa kuwa Mzee Makamba alishindwa kutekeleza yafuatayo;
- · Kutoa ushauri sahii kwa wakati sahihi
- · Kutumia sana sera za ubabe wakati hakuna haja ya sera hizo
- · Kutumia lugha ambazo zilikuwa hazivuti ushawishi kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla
- · Kushindwa kutoa ushauri mzuri kwa Mwenyekiti wake wakati yeye ndio mtendaji mkuu wa chama;
Tukumbuke siasa yenye msingi wa utawala Bora sio ubabe na ukitumika sana huondoa busara na hekima; uongozi bora unatawaliwa na uongozi hekima, ambayo itazaa uadilifu, uwajibikaji na umoja.
Wakati umefika kama saa izungukavyo, saa yako imefika kwa wewe mzee wetu Makamba uweze pumzika, inatosha hapo ulipomfikisha Mwenyekiti panatosha, tuwaachie na wengine nao tuone watamsaidiaje Mwenyekiti katika kuitengeneza Tanzania yetu na kuleta neema kwa watanzania wote.
Mungu Ibariki Tanzania na Afrika
No comments:
Post a Comment