WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, March 31, 2011

UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA SERIKALI

KAULI ZINAZOTOFAUTIANA MIONGONI MWA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI NI WAJIBIKAJI WA PAMOJA?


Uwajibika wa pamoja kati ya watendaji wakuu wa serikali ni dhana muhimu katika utekelezaji wa majukumu na sera za serikali;
Kila kiongozi anamchango ambao unaweza kusaidia kuleta  mabadiliko katika jamii, la msingi katika kufanikisha hilo kunahitajika kuwepo kwa njia makini, kufuata taratibu na kuwa na mawasiliano ya hali ya juu (effective Communication) miongoni mwao. Ni muhimu kuhakikisha kuwa hoja zao na utekelezaji wao unachambuliwa katka vikao muhimu vya pamoja (in Camera) na kama unafaa  utumike  katika kutekeleza majukumu yao ( ministry Responsibility) katika wizara na idara zao husika katika kuwaleta maendeleo wananchi wake.

SERIKALI yoyote yenye mafanikio ya uwajibikaji wa pamoja ni ile ambayo inaheshimu misingi ya utawala bora, ambayo moja ya nguzo zake kubwa ni nidhamu ya utendaji wa kazi na mahusiano mazuri ya kazi kati ya watumishi, wakiwamo viongozi wa kada mbalimbali.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa JK katika moja ya mikutano yake pamoja na watendaji wake wakuu, amewakumbusha wateule wake kuhusu uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) katika kuongoza nchi, akisisitiza kuwa uwajibikaji huo unaelezwa kwa ufasaha katika Hati Maalum (Instrument) ya Majukumu ya kila Wizara. Katka msisitizo Rais Kikwete alisema kuwa
·        Uzoefu unaonyesha kuwa Mawaziri wengi ni wazito kufanya mawasiliano na wananchi hata pale ambako Wizara imefanya mambo mengi mazuri. Hivyo, Mawaziri muwe mstari wa mbele kuelezea mafanikio ya utendaji wa Serikali katika Wizara zetu,” ameelekeza Rais Kikwete na kuongeza: 
·        Lazima ujengwe utamaduni wa kudumu wa kuwasiliana na wananchi wote ambao ndio waajiri wetu kupitia kura zao. Mawaziri wote tumieni Vitengo vyenu vya Mawasiliano na vyombo vya habari kwa ustadi ipasavyo,
·        Ni rahisi kunyoosha vidole, na kuwabandikia  watu wengine lawama za matatizo haya.


JE KUWEPO KWA TOFAUTI ZA KAULI KATIKA SIKU ZA KARIBUNI MIONGONI MWA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI INAONDOA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA AU INAIMARISHA UWAJIBIKAJI;

Katika siku hizi za karibuni kumekuwako sana na kutofautiana kwa kauli miongoni mwa watendaji wakuu wa serikala huhusa mawaziri kuhusu hoja moja ambazo zinaishia kuwa na mielekeo miwili tofauti  na misimamo tofauti;

kuhusu swala la loliondo waziri mwenye dhamana ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Haji Mponda ilimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kusitisha kwa muda utoaji wa huduma hiyo hadi itakapojiridhisha kwamba dawa inakidhi ubora na inatolewa katika mazingira safi; agizo hilo likiwa mbioni kutekelezwa jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Serikali haina tena mpango wa kuzuia huduma hiyo kwa kuwa inahusisha imani za watu

kuhusu bomoa bomoa waziri mwenye dhaman  Dr John Pombe Magufuli  alijikuta akipigwa stop na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akihutubia mkutano wa hadhara alipomuagiza, waziri  John Magufuli kuwa asitishe mara moja ubomoaji wa majengo yaliyo katika hifadhi ya barabara hadi Baraza la Mawaziri litakapoamua vinginevyo. Kama haitoshi Mheshimiwa Rais JK alipotembelea wizara ya Ujenzi alimuagiza Waziri Magufuli kuzingatia kile alichokiita “utu” na “ubinadamu”

kwa nini Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda waliona vyema kumkaripia Waziri Magufuli hadharani, tena kwa kauli za kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi na wapigakura wake ili aonekane kama mtu katili asiye na utu wala ubinadamu? Kwa nini hoja na kauli zao hazikupelekwa kwanza katika Baraza la Mawaziri kama kweli walikuwa na nia ya kufanya hivyo? Na kama wanaona kuwa sheria inayosimamia hifadhi za barabara haifai kwa nini wasizungumzie haja ya kupeleka muswada bungeni ili sheria hiyo iwekewe “utu” na “ubinadamu” badala ya kumsingizia waziri huyo kwamba anatumia ubabe”?


HIVI SERIKALI HAINA MGAWANYO WA MAJUKUMU KWA MAWAZIRI WAKE
 Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, alisema ni kosa kwa mawaziri kupingana hadharani na kuongeza kuwa kama kuna mwenye dukuduku kuna namna ya kuwasilisha maoni yao. Kwa mujibu wa Chikawe, taratibu hizo ni kwa mawaziri husika kuwasiliana na kushauriana na inapotokea anayeshauriwa haelewi, upo utaratibu wa kupeleka maoni hayo kwa Waziri Mkuu.

maswali ya kujiuliza sasa  je na pale ambapo Waziri Mkuu na hatimaye Mheshimiwa Rais hawaoni umuhimu wa kutumia vikao vya Baraza la mawaziri katika kurekebisha jambo lolote na kumkosoa waziri mwenye dhaman mbele ya watu bila waziri kujua nini kinaendelea;
Je kuna umuhimu gani wa wale ambao wako chini yao kutekeleza huo uwajibikaji wa pamoja?  Kama waandishi wengi walivyo hoji, Je Kwa nini hoja na kauli zao  hazikupelekwa kwanza katika Baraza la Mawaziri kama kweli walikuwa na nia ya kufanya hivyo? Na kama wanaona kuwa sheria inayosimamia hifadhi za barabara haifai kwa nini wasizungumzie haja ya kupeleka muswada bungeni ili sheria hiyo iwekewe “utu” na “ubinadamu” badala ya kumsingizia waziri huyo kwamba anatumia ubabe”?  je  kumkaripia Waziri Magufuli hadharani, tena kwa kauli za kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi na wapigakura wake ili aonekane kama mtu katili asiye na utu wala ubinadamu inaimarisha uwajibikaji wa pamoja au inabomoa?
Nafikiri viongozi wetu wengi wanatakiwa watumie muda wa kutosha kujifunza faida za” effective communications” na wapi wanastahili kusema hoja gani kwa faida ya nani?

Kama taifa tutuweza sana kusonga mbele pale tutakapo weza kuondoa kabisa hulka za kisiasa katika kutekeleza maendeleo ya wananchi, busara na hekima ni silaha ya uwajibikaji wa pamoja 

No comments:

Post a Comment