JE MATATIZO YANAYOENDELEA KUTOKEA TANZANIA LEO: JE RAIS WETU AMEKOSA WASHAURI WAZURI?
Sehemu ya Kwanza
Tanzania tumebarikiwa kuwa na uchaguzi mkuu ambao ulifanyika kwa amani bila vurugu zozote za umwagaji wa damu, pamoja na kasoro hapa na pale, ambazo zilijitokeza kabla na baada ya upigaji kura;ambazo zilipelekea Chama cha Maendeleo na Demokrasia kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi na hatimaye kususia matokea kwa msingi kuwa uchaguzi hakuwa huru na matokeo ya urais YALICHAKACHULIWA ili kumsaidia mgombea wa CCM kushinda uchaguzi huu mwezi October 2010;
Maswali ya Msingi hapa Je washauri wa rais wa siasa , uchumi na huduma za jamii, na kadhalika wanamshauri Rais wetu nini katika kushughulikia kero za wananchi na katika kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni? Au wanakuwa kama bendera wakiogopa kusema ukweli kwa msingi wa kuogopa kupoteza ajira zao na wakijua kuwa kazi zao ni za msimu mfupi?
Baada ya uchaguzi tumeoona vyama vya upinzani vikiongozwa na CUF na CHADEMA wakiwahamasiha wafuasi wao katika madai ya kuandika Katiba upya , kilio hicho cha madai ya katiba mpya kilipata majibu kutoka kwa msheshimiwa Rais JK kuwa serikali yake iko tayari kuridhia mabadiliko hayo.
Tatizo nyingine ambalo bado limeendelea kuliweka taifa mahali pabaya ni pamoja na kukidhiri kwa vitendo vya rushwa (ufisadi uliobebea) ambao bado unaendelea kufanya na viongozi na washirika wao ndani ya serikali; tatizo hilo kwa hivi sasa linahusishwa na tatizo sugu la kukosekana kwa umeme na wananchi kupinga kwa sauti moja malipo ya kampuni ya kufua umeme wa generator Dowans. Kama kweli huu ni mradi wa wazito ndani chama na serikali basi itafika mahali ambapo wananchi watalazimika kufuata msimamo wa Karl Marx (1818 – 1883) na Friedrich ENGELS (1820 – 1895) wanasema kwamba matajiri na wanaoshikilia vyombo vya utajiri mara nyingi hutumia nguvu kwa kukuza na kulinda mali zao. Ila, ungandamizaji wao unapofikia kilele, masikini wana haki ya kuleta uasi mkubwa kwa mageuzi ya kiuchumi na ya kisiasa. Ndio maana leo tunaona kuwa wananchi wengi wameanza kusimama kiume na kuanza kudai haki zao; wakiitumia kauli mbiu kuwa “hutulipi Dowans” hata kama serikali itaishia kulipa kwa siri lakini kilio cha wananchi kimeshasikika; washauri mpo na umeshauri nini katika utata huu wa zabuni za mitambo hii?
Mauaji wa raia kadhaa huko Arusha ambayo yalitokea baada ya wafuasi wa CHADEMA kufanya maandamano yaliyokuwa yakipinga matokeo ya ushindi wa Meya wa arusha kwa tiketi ya CCM. Mauaji hayo katika msingi wowote ule yameendelea kuchafua historia nzuri ya nchi yetu na kutukumbusha kile kilichofanyika Zanzibar miaka kadhaa iliyopita; katika hili, je washauri wa rais waliishauri serikali kutumia nguvu kuzima maandamano hayo? Kama ndio je walifuata msimamo wa Mwanafalsafa Machiavel (1462 – 1527) katika maamdishi yake alishauri kwamba viongozi watumie nguvu ili wabaki madarakani na kulinda heshima za nchi zao. Pia anaomba viongozi wawe wenye busara na itakapohitajika, wawe wakali kama simba. Je huu ndio ni msimamo wa serikali yetu? Au ilikuwa bahati mbaya kwa kukosekana kwa mawasiliano mazuri miongoni mwa Taasisi husuka? Je taratibu za gani zifuatwe ili kuepusha hali hii siku za usoni? Hili ni jukumu la washauri wa Mweshimiwa Rais pamoja na busara na uvumilivu wa viongozi wetu;
Kumekuwako pia na uharibifu uliotokana na mabomu yaiyolipuka Gongo la Mboto ambayo yamesababisha wananchi zaidi ya 20 kupoteza maisha na mali pia, swali la msingi hapa je taasisi zetu zinazoshughulikia usalama zinawajibika vipi katika ukaguzi wa vifaa vyao na wanatumia utaratibu gani wa uhifadhi wa vifaa ambavyo vinaweza kuleta madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa (Joto au baridi);je wanautaratibu wa kukagua vifaa hivyo kutokana na ukaji wa siku nyingi? Je washauri wetu wanamshauri Mheshimiwa Rais nini kuhusu uwajibikaji katika mazingira ya namna hii: Je katika kuhakisha kuwa hali hii haitokei tena je washauri wa mheshimiwa Rais watamsaidiaje kwa faida ya watanzania wote?
No comments:
Post a Comment