WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, March 22, 2011

JE SERIKALI YETU TANZANIA INAYO WASHAURI WAZURI?

JE MATATIZO YANAYOENDELEA KUTOKEA TANZANIA LEO: JE RAIS WETU AMEKOSA WASHAURI WAZURI?


Sehemu ya Pili



katika hizi siku za karibuni kumeanza kujitokeza maandamano yenye “sura ya amani” yakiwa na kibwagizo cha kudai maisha bora kwa watanzania, ambayo yanaendeshwa na CDM yakishinikiza serikali ya CCM kutatua kero za wananchi kwa haraka iwezekanavyo. Ikumbukwe kuwa Tangu 1989, mapambano ya raia yasiyotumia nguvu yamesababisha kuvunjika kwa utawala wa kikomunisti wa chama kimoja cha Urusi, vyama Ulaya ya mashariki, Jamuhuri ya Baltes na Mongolie na muungano kwa amani wa Ujeremani na kukomesha utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika kusini. Ijapokuwa mapambano hayo, pengine yalikuwa na vifo (Birmanie 1988, Chine 1989), kuna tofauti kabisa na mapinduzi ya kale kama yale ya Amerika ,Ufaransa, Urusi, Uchina yaliyogupikwa na mauaji mengi zaidi. Pembeni ya maandamano makubwa yanayoonekana wazi ya kutafuta mabadiliko ya utawala, kuna vyama vya kisiasa ambavyo vinatumia mwanya wa kuuza sera zao kwa wananchi dhidi ya chama kilicho madarakani kwa msingi wa kuwa kimeshindwa kuatatua kero za wananchi. Je chama ambacho kipo madarakani kinatakiwa kujipanga vipi? Ni ukweli ambao haufichiki kuwa Rais kama kiongozi wa juu kabisa katika nchi anatawala kwa msaada mkubwa wa washauri wake; Je kama washauri wameiona hali hii wanamshauri nini?

Swali nyingine ninalojiuliza ni kitu gani kitapelekea uwepo wa maandamano haya yenye kibwagizo cha amani (sauti ya umma)? je yanakuja kwa sura ya kudai nini? ni uhuru wa watu, usawa , maendeleo mazuri ya kwa wananchi wote?, au ni sehemu tu ya kuanzisha uvunjaji wa amani miongoni mwa watanzania? ama kuna alama gani za ki-historia au za nyakati hizi za siasa, uchumi, jamii, utamanduni, zinazo onyesha kuwa jamii ya kitanzania imefikia mwenendo wa maisha ya kutojali na kutotii serikali yake iliyochaguliwa kihalali? Hapa namnukuu mwanafalsafa Jean Jacques ROUSSEAU (1712 – 1778) alivyoandika kwamba “wanainchi ni lazima waheshimu viongozi wao walio na majukumu ya kutoa amri kwa ajili ya wote. Serikali inayo haki ya kupiga vita watu wote wasiotii amri zake na kuwahukumu kifo. Pia, serikali inayo mamlaka ya kuamru watu wajitoe muhanga kwa ajili yake.”

Pengine tuwaulize washauri wa Mheshimiwa Rais kuwa je mabadiliko gani yametokea ndani ya jamii iliyokuwa imetulia bila msisimko wa kisiasa, na leo hii imekuwa tayari kuungana na vyama vya siasa katika maandamano yanayoendelea sehemu mbalimbali hata wengine wakiwa tayari kuyapoteza maisha yao, kwanini?
·        Kujitokeza kwa wingi katika maandamano haya ya amani ni kielelezo hali halisi kuwa wananchi wamechoshwa na:
·        Ugumu wa maisha na wakati huo huo kundi la watu wachache wanafaidi rasilimali za nchi na watoto wao wakifaidi elimu bora nje ya nchi
·        Wananchi wanasikitika kuona kuwa taifa lenye rasilimali nyingi na za pekee dunia linaendelea kuwa masikini na watoto wa taifa hili wakiendelea kuwa wapumbavu kwa kukosa haki ya msingi ya elimu

 Ni ukweli siopingika kuwa wananchi wanachoshwa na hali hii ndio maana kiongozi mwinigine yeyyote anayejitokeza  na kuwagusa katika kuboresha maisha yao, wanakuwa tayari kumkimbilia na kuamaini kuwa ataleta khali nzuri ya maisha hata kama hali haitabadilika; Inasikitisha miaka 49 ya uhuru Tanzania bado  haina umeme wa uhakika; maji safi na barabara, na kadhalika; wananchi wamechoshwa na umasikini katika nchi yao tajiri; Matatizo yote ambayo yanajitokeza leo wananchi wanona  in kazi ya mikono Serikali na chama kilicho madarakani;

Rai yangu washauri wa Mheshimiwa Rais wetu wawajibike ipasavyo kwa faida ya taifa na sio kwa masilahi ya kikundi kidogo cha watu; na mheshimiwa rais akiona ushauri wao hauna tija kwa wananchi basi awawajibishe kwani taifa hili lina rasilimali kubwa sana ya wataalamu ambao wako tayari kuifikisha nchi mahali pazuri sana kwa manufaa ya wote.


Mungu Ibariki Tanzania na utuepushe na fikra zozote za kuvunyika kwa amani 

No comments:

Post a Comment