MWENENDO HUU WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UTATUFIKISHA WAPI?
Ilikuwa ni shangwe kubwa pale Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Mheshimiwa JK alipotoa taarifa rasmi kuwa serikali yake iko tayari kushughukikia mapendekezo ya kuandaa katiba mpya
Watanzania wengi kwa ujumla walikuwa wamejawa na shauku na hamu ya mabadiliko ya katiba wakijua kuwa wakati sasa umefika kwa wananchi wa Tanzania kuwa na katiba mpya ambayo itajumuisha misingi ya taifa itakayokuwa imelinda maslahi ya wananchi kwa ustawi na maendeleo yao.
Kwa msingi huu toka kongamano la kwanza ambalo lilifanyika chuo kikuu cha dar es salaam chini ya wenyekiti wa Prof Issa Shivji na Jenarali Uliwengu wananchi wengi walijitokeza wasomi, wanasiasa wananchi wa kawaidi na vikundi mbalimbali vya jamii; ili kushauri katiba mpya iwe na sura gani, na zoezi nzima la upatikanaji wa maoni uwe vipi.
Kama Makamu wa Kwnza wa serikali ya umoja wa kitaifa Maalim Seif alivyo wahi sema“hali inavyokwenda wananchi wengi wamehamasika kutaka kutoa maoni juu ya kuwa na katiba mpya hivyo ni vizuri wananchi wakapata nafasi ya kutoa maoni yao kwa kuwa katiba inayowashirikisha wananchi ndio katiba madhubuti nchini”.
Msisitizo hu unatokana na dhana kuwa iwapo Wananchi wataweza kushiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kuandaa Katiba mpya itasaidia katika kuepusha dhana kuwa suala la kuandika Katiba sio la kikundi Fulani, chama fulani au ni la Wanasheria, kwa vile wao wamebobea katika sheria hasa za masuala ya Katiba.
Wengi walipendekeza kuwa ni muhimu wananchi wote, washirikishwe ikiwa ni pamoja na wale wasiojua kusoma wala kuandika na wanajamii mbalimbali mijini na vijijini watakavyowezeshwa kuweza kushiriki katika kuweka misingi ya uandikaji Katiba, kutoa maoni katika mijadala ya awali na kwa Tume ya kuratibu maoni, pamoja na kuchagua wawakilishi kutoka miongoni mwao kushiriki katika vyombo muhimu vya kujadili mapendekezo na rasimu za Katiba ikiwemo wajumbe wa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba na mara nyingi mjadala unaishia kwenye kikao cha Bunge Maalum la Katiba.
Nchi inapoamua kuandika katiba mpya ukweli wake ni kuwa ni upanuzi wa demokrasia na maendeleo ya nchi kwa kuwa na katiba ya nchi inayoonyesha utashi wa wananchi.
Kazi ambayo iko mbele yetu ni kubwa sana sisi kama Watanzania ni lazima tuhakikishe kuwa mchakato wa kufikia katiba mpya unakuwa huru, yenye uwigo mpana sio wa kulindana bali ni wa uwazi na ambao una uhalali wa kutosha kuweza kufikia kusema kuwa Katiba itakayopatikana kweli imetokana na watu na mazingira yetu.
Mchakato wa kufikia Katiba Mpya usipoweka misingi ambayo utahakikisha wananchi wote wana nafasi sawa ya kuchangia mawazo yao ya dhati bila kuogopa au kununuliwa tutakuwa tumefanikiwa kuifikisha katiba mahali pazuri kwa usalama wan chi bali kama kutakuwa na mchakato mbovu tutakuwa tumeiharibu kabisa nchi yetu na maendeleo yake kidogo ambayo tunayo hivi sasa.
Lengo la kila mtanzania tunatamani kuandika Katiba Mpya ili kuweza kukiachia kizazi kijacho mfumo mzuri wa utawala ambao utawapa nafasi ya kufanikiwa katika maisha na mipango yao na ambao utawahakikishia mtiririko mzuri wa mahusiano na kuwajibishana kati yao na watawala wao.
Nini kinatokea sasa?
1. Wengi wamepinga rasimu hiyo ya katiba kwa sababu tofauti mojawapo ikiwa inafanyika katika kipindi kifupi na pengine wananchi wengi hawatapata nafasi ya kutoa maoni yao.
2. Mikutano iliyofanyika Dodoma na Dar es salaam imeonyesha mapungufu makubwa katika siku za awali tu; je kamati au wizara inayoshughulikia rasimu ya kuratibu maoni ya utayarishaji wa katiba mpya kweli wamejiandaa kwa katiba mpya au ni ubabaishaji tu?
3. Je Kamati waliangalia mahitaji halisi ya wananchi na kiu ya wananchi kutoa mawazo yao?
4. Hebu angalia mambo yalivyokuwa Dar es salaam, ilikuwa ni tatizo kubwa pale ukumbi ulipojaa wananchi wengi ambao kwa sababu moja au nyingine waliishia kulala tu , nini kilikuwa kunaendelea, je wapi tutapata hiyo rasimu bora ambayo inakizi haja wakati hatuna ushindani katika uchangiaji hoja wakati wananchi waliopokelewa au kuletwa katika ukumbi huu kwa sababu moja au nyingine waliishia kulala tu?
5. Kule Zanzibar kwa kulitokea tukio la kuchana Rasimu hiyo wananchi na wachangiaji wakiwa wamejawa na hasira ya utaratibu mzima wa uandaji na mwonekano wa rasimu hiyo; Je ni kweli kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hakuhusishwa kikamilifu? Je Rasimu unaelezaje swala la Muungano? Je linakizi haja kwa pande zote? Je wale wanaona wanamezwa wamepewa kinga gani ili wasipatwe na janga hilo?
6. Je kama zoezi hili halitakwenda vizuri kwa kigezo cha muda nani atawajibishwa kulipa gharama halisi ambayo imetumika katika maandalizi hayo? Ikumbukwe kuwa bado pesa hiyo ni ya mlala hoi.
HITIMISHO
Lazima tukubali kuwa Mheshimiwa Rais amebariki utaratibu mzima wa uandikaji wa katiba upya, hili ni jambo la kihistoria na ambalo halitakiwi kufanyiwa mzaha na watendaji wachache kwa masilahi yao binafsi au chama chochote, hebu tulifanye jambo hili kwa masilahi ya wananchi wa Tanzania na sio kwa manufaa ya wana siasa na vyama vyao;
Mungu ibariki Tanzania na watu wake
No comments:
Post a Comment