Kwa nini sheria hazifuatwi katika maisha ya kila siku ya mtanzania tatizo liko wapi? Sheria hazieleweki au sheria zimejaa mianya mingi inayoruhusu kutofuatwa katika utekeleji wake?
Tunapaswa kufanya nini ili kuhakikisha kuwa harakati za kutetea na kuona kuwa sheria zinafuatwa, zinafanikiwa bila kuvunja misingi ya utawala bora na wa sheria?
Je "Watu wote ni sawa mbele ya sheria, au wengine wanayo haki zaidi kutokana na umaarufu wao?.
Je utekelezaji wa sheria unafanyika bila ubaguzi wowote, na kumwezesha kila raia keheshimiwa na kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria"?
Ni kwa namna gani tunaweza kujenga mfumo wa utawala wa sheria usioipa nafasi dola kutumia kiujanja mianya ya kisheria na kupata nafasi ya kutotekeleza kanuni za sheria na kama itatekelezwa kuchukua muda mrefu ili kupunguza nguvu ya kosa katika kuleta haki inayotakiwa kwa jamii?
Je Migomo, maandamano, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali unaofanywa kutoka na matukio haya ni sababu ya kwisha kwa uvumilivu kutoka na uzembeaji katika kutekeleza sheria au ni mazoea tu yaliyojengeka mbele ya raia au jamii?
Ni ukweli ambao haufichiki kuwa miaka takribani 50 ya uhuru wa nchi hii wananchi wameweza kuona ni kwa jinsi gani matatizo yanayoikumba nchi Tanzania yanazidi kuongeza licha ya kuwepo utawala wa sheria. Na wakati huo huo kuna vyombo na taasisi mbalimbali za kisheria zenye nguvu na mamlaka ya kushughulikia zikiwa zimepewa nyenzo na nguvu za kisheria katika kutekeleza majukumu yao, cha kushangaza ni kuwa taasisi au idara hizo zipo na pengine zinaangalia tu bila kuwajibika.
- Je zinaogopa au hazioni umuhimu wa kuwajibika kwa sababu za masilahi zaidi?
Je hii inatokana na ukweli kuwa pengine sheria pamoja na kupitishwa na vyombo husika lakini utekelezaji wake lazima ubarikiwe na kikundi kidogo cha wenye mali Mafisadi ili itekelezwe kwa matakwa yao.
- Kama ni hivyo basi sheria iko kwa ajili na kwa manufaa ya nani?
- Je sheria zinatungwa na matajiri kuwazuia maskini kuwasogelea matajiri na kuhakikisha matajiri wanaendelea kutumia utekelezaji wa sheria kuwakandamiza maskini;
- je sheria zinatungwa kuwafurahisha matajiri na kuwaridhisha maskini lakini wakati wote kuwanufaisha watawala!
Ni aibu kama vyombo vya dola vinaweza kumfunga Mmachinga katika siku mbili kwa kosa na kuuza vitu katika sehemu ambayo haijeruhusiwa na wakati huo huo inashindwa kumfunga Fisadi aliyethibitika kuliibia taifa mabilioni ya shilling kwa vile tu eti kwa sababu ya pesa zake anaweza kushinda kesi na kuisababishia serikali hasara zaidi; lo hii ni hatari.
Swali la msingi hapa sheria zetu ni kwa ajili na manufaa ya nani? Kwa nini utekelezaji wake unakuwa na kigugumizi. Nafikiri uzaifu huu wa sheria zetu ndio unaotuletea kila ambacho wananchi kuhukumu na kuchukua hatua ambazo wakati mwingine zinakiuka utaratibu wa utawala bora;
- je ni busara haki hata kama iko ndani ya sheria haitatekelezwa mpaka kwa maandamano na migomo;
Haki ya ya matibabu bora haitapatikana mpaka kwa utoaji rushwa;
Haki yangu ya kosa lolote la barabarani haitaeleweka mbele ya askari wa usalama wa barabarani bila ya hongo;
Wananchi wanatakiwa kuelimisha kwa upole na upendo pale wanapokosea na ikibidi adhabu ifanywe kulingana na sheria; mkosa alipe faini yake kihalali ili iwe ni fundisho na pesa hiyo isadie maendeleo ya nchi;
Kwa kufanya hivyo taifa litaweza kuimarisha utawala bora, amabao ni utawala wa sheria, na hapo itakuwa rahisi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa, dawa za kulevya, matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma. Mhalifu anaweza na anapaswa kuadhibiwa kwa sababu amehalifu sheria kwa matakwa/ridhaa yake.
kwani inamaanisha kuwa mara mtu anapotiwa hatiani na kuonekana kuwa alitenda kwa ridhaa yake na akijua anachotenda hapo hapo uhuru wake unabadilishana na faini halali ambayo inampasa kulipa. tukiweza kujenga mazingira ya kulipa faini halali kwa makosa halali;tutafanikiwa vile vile kwashinda wale ambao wanatumia mamlaka au madaraka waliyopewa vibaya kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi.
kwani inamaanisha kuwa mara mtu anapotiwa hatiani na kuonekana kuwa alitenda kwa ridhaa yake na akijua anachotenda hapo hapo uhuru wake unabadilishana na faini halali ambayo inampasa kulipa. tukiweza kujenga mazingira ya kulipa faini halali kwa makosa halali;tutafanikiwa vile vile kwashinda wale ambao wanatumia mamlaka au madaraka waliyopewa vibaya kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi.
Nafikiri itakuwa ni busara kama wasimamizi wa sheria watakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao katika kupinga matumizi mabaya ya sheria hizo kwa mtu yeyote bila kujali cheo chake na pesa zake na anamfahamu nani;
Hilo likiwezekana tutaondoa dhana ya kukimbilia kuhukumu wakati hatuna vithibitisho “Prejudice” ni ukweli ambao haupingiki kuwa watu hawajezaliwa na hali ya kupinga kutotaka kutekeleza sheria bali tatizo na utaratibu mzima wa usimamiaji wa sheria ndio unaopelekea watu kuvunja sheria.
Wazo la leo nini kifanyike kuondoa hali hii ambayo imetawala vichwa vyetu kwa muda mrefu sasa?
· Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu haki zao za msingi za sheria na wanatakiwa wasiinunue haki yao kwa rushwa.
· Tunahitaji wasimamiaji wa sheria ambao watakuwa tayari kutekeleza majukumu yao bila kuogopa na vile vile kuwaelimisha jamii kuhusu haki yao ya msingi.
· Inatupasa kujenga uhusiano mzuri kati ya raia na watekelezaji wote wa sheria mfano polisi wawe ni msaada mzuri kwa madereva pale madereva wanapokosea na wawaadhibu bila ya kuwaonea haya hata kidogo na hii itatusaidia kupunguza ajali nyingi;
· Viongozi wetu wakuu waonyeshe mfano mzuri katika kutekeleza majukumu yao bila upendeleo wowote ule;
Tukifanya hivyo huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuirudisha nchi yetu katika dira ya utawala bora na wa sheria.
Pamoja tukisimama hatutashindwa jambo lolote
No comments:
Post a Comment