KUFUATIA AJALI YA MELI YA “MV SPICE ISALANDER “SISI
KAMA TAIFA TUFANYE NINI KUEPUSHA HALI HII ISITOKEE TENA?
Mwishoni mwa
wiki kulitokea ajali mbaya ya kupinduka kwa Meli na kuzama, ajali ambayo imesababisha
vifo vya watanzania wenzetu zaidi ya 200 wengi wao wakiwa wananwake na watoto,
ajali ambayo ilitokea katika bahari ya Hindi katika eneo lenye mkondo mkali wa
Nungwi ikiwa inaelekea Pemba;
Msiba huo ni
mkubwa kitaifa kwani umekatisha maisha ya watanzania wenzetu ambao ni nguvu
kazi yetu kwa maendeleo yetu; wengi wa aliofariki ni wazazi wa familia zetu na
watoto ambao walikuwa wanaandaliwa kwa ajili ya maendeleo yetu ya kesho.
Kwa mara
nyingine nachukua nafasi hii kutoa pole kwa kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa wazazi kwa msiba
huu mkubwa. Na kwa viongozi wetu wakuu wa taifa letu Raisi wa Serikali ya
Mapinduzi Ya Zanzibar pamoja na timu yake yote ya uongozi; Raisi wa Jamuhuri wa
Muungano wa Tanzania na timu yake vile vile;
Swali ambalo
limenigusa sana siku hii ya leo ni hili kwa nini ajali hii ilitokea?
Ni kweli
imekuwa ajali kama ajali ambayo imekuja bila hodi na haikuwezekana kabisa
kuepukwa?
Je ni ajali
ambayo imechangiwa na uzembe wa usimamizi wa wajibu wetu kama watendaji?
Je ni tatizo
la uwajibikaji na kuweka rehani ya maisha ya watanzania kwa kuendekeza “ muhali” na kushindwa
kusimamia na kukemea sheria katika atendaji pale panapohitaji kufanya hivyo?
Je ni tatizo
la tamaa ya wamiliki wa vyombo na wasimamizi wa miradi hivyo kushindwa kufuata
taratibu zinazoongoza biashaya zao?
Mwananchi wa kawaida atajiuliza lakini serikali zetu ziko wapi
katika kuwajibika?
Au zinasubiri kuwajibika baada ya tatizo kutokea au hufanya kazi
vipi ( management in crisis or management after crisis or crisis management)?
Leo naungana
na kauli ya Waziri katika Afisi ya Makamo wa pili wa Rais, Mhe Mohamed Aboud
Mohamed
“amesema,kuwa kamati maalum itaundwa ili
kuchunguza juu ya ajali hiyo na ikibainika kuwa uzembe umepatikana sheria
itachukua mkondo wake”. ..
”kuwa tatizo
kubwa la wazanzibari ni muhali, na amesema ili utendaji mzuri uwepo, lazima
suala hili la muhali liwekwe upande ili nchi ipige hatua za maendeleo, na
ikibainika kuna watu wanafanya uzembe wa kikazi lazima hatua za sheria
zichukuliwe”
Tunaipongeza
kauli hii ya awali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa itawachukulia hatua
za kisheria wale wote watakaobainiika kufanya uzembe uliosababisha kuzama kwa
meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi na kusababisha vifo vya
watu watanzania wenzetu zaidi ya 200.
Wasiwasi wangu
ni huu kuwa, pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuangalia na kukagua kila mara
vyombo vya usafiri ili kunusuru ajali ambazo zinaweza kuepukika.
Je wakibainika kwa uzembe huu watachukuliwa hatua za kweli ambazo zitakuwa fundisho kwa wamiliki na watendaji wengine?
Je wakibainika kwa uzembe huu watachukuliwa hatua za kweli ambazo zitakuwa fundisho kwa wamiliki na watendaji wengine?
Tatizo letu
kama taifa siku zote tume zinazoundwa zinaishia kuwa ni viini macho tu na
hakuna msukumo wa kweli wa adhabu ambazo zinakidhi haja na haki kwa wafiwa;
Kwa nini meli
hiyo ilipakia kupita uwezo wake? Kwa nini captain alikubali kuendelea na
safari? Kama yuko hai inapasa awajibishwe kulingana na uzito wa madhara ambayo
yametokea tusimwonee muhari;
Je tunaweza
kuthubutu kama serikali ya China inavyothubutu kwa raia wake ambao
wanasababisha hasara kwa taifa? Wao hawana mchezo;
Kama tukiweza
kuthubutu kwa wavunjaji sheria, uwajibishaji huu tutaweza kuzilinda na
kuzitekeleza sheria na kanuni ambazo
zimewekwa kwa ajili ya vyombo vya usafiri ili kudhibiti na kuzuia ajali
zisitokee, kwa bahati mbaya sana baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo huacha
kufuata kanuni hizo ama kwa makusudi na masilahi binafsi.
Ni kweli kuwa
ajali haziepukiki, lakini ajali nyingine husababishwa na uzembe wa wamiliki
pamoja nawatendaji wake na hili ndilo lilitokea wiki iliyopita huko Nungwi.
Natoa wito kwa
wadau wote kushikamana katika kuhakikisha vifo vinavyosababishwa na ajali
vinapungua kama si kumalizika kabisa kama tukisimama pamoja na kukataa
kuburuzwa na wenye mali na kuweza kuwakatalia wengine kupanda kwenye ambacho kimejaa kulingana na uwezo wake tutakuwa tumeweza kuthubutu kwa masilahi ya taifa.
udhaifu wa usimamiaji wa sheria na muhali umetupa wakati mgumu wa kujua meli hiyo ilikuwa na abiria wangapi? Kwa nini kunakuwa na taarifa ya idadi inayotofautiana? Huu ni
uzembe ambao kwa kweli hautakiwi kuendelea kuvumiliwa;
Mwisho tunaiomba Serikali yetu ambayo ndio muhimili wa maisha bora ya raia wake na usalama wao kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa sheria zake; serikali lazima ithubutu katika kuwawajibisha wote waliohusika na
kuwachukulia adhabu kali na kuacha MUHALI
No comments:
Post a Comment