Igunga imegeuka fitina
ugomvi na mbaya zaidi sio ugomvi wa hoja ni ugomvi wa misuri ambao hauna tija
kwa Taifa letu.
Tunaendelea kujiuliza kwa
nini wakati kampeni za hicho kiti kimoja tu zikiwa zinakaribia kufikia
ukingoni tunaendelea kushuhudia matukio
yanayotishia uvunjaji wa amani, yanazidi kuongezeka.
Kama vile, Kudhalilishwa
kwa watendaji serikali na vyama na serikali
Kujihami kwa baadhi ya
viongozi hadharani, kama ndugu yetu Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
(CCM), akiwa na bastola kiunoni akiwa akihutubia katika mkutano wa kampeni.
Kama magazeti mengi yalivyoonyesha kuwa”
Bastola ya Rage ilionekana wakati mbunge huyo akijiandaa kupanda jukwaani kwa
ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa CCM kwenye moja ya mikutano ya kampeni
jimboni humo”.
Kama Mwandishi wa makala hiyo alipouliza”Kwa sababu hiyo,
tunajiuliza, Rage alikuwa akikabiliwa na hatari gani hadi kulazimika kupanda
jukwaani ni bastola? Hivi kila mwenye silaha ya moto Igunga akisema atembee na silaha
yake hali itakuwaje?Na kwa wasio na silaha za moto, wakiamua kutoka na silaha
za jadi kama mishale, visu, mapanga na zinginezo, Igunga patakalika? Sisi
hatuungi mkono kitendo hicho na tunalitaka jeshi la Polisi kuchukua hatua ili
kuhakikisha kampeni za uchaguzi Igunga na hatimaye uchaguzi wake, unafanyika
katika mazingira ya utulivu na amani.”
Nakubaliana kabisa na
mwandishi wa makala hii kuwa huu ni udhaifu mkubwa kabisa kwa wasimamizi wetu
wa maswala ya amani na utulivu; Mheshimiwa Mbunge hakuwa na sababu yeyote ile
ya kuja kwenye kampeni na silaha, kama alikuwa na uhakika kuwa usalama wake
ulikuwa mashakani kulikuwa hakuna sababu yeyote kwa yeye kujumuika katika
kampeni kwa siku na wakati kama huo.
Tunafahamu kuwa vikosi vyetu vya ulinzi
na usalama jamani viko na vinaendelea kuwa makini katika kulinda amani ya
wakaazi wa Igunga na taifa kwa ujumla katika wakati huu wote wa kampeni;
Tukio nyingine ambalo nalo
limepigiwa sana kelele ni kitendo alichofanyiwa DC; kwa wahusika wote wale katika sakata hili la kumdhalilisha Mama huyu; kumekuwa na matumizi ya nguvu zaidi kuliko busara;hata kama wahusika wanakana na kuona waliyofanya ni sawa, ukweli ni kuwa kosa lilifanyika watake wasitake; Busara busara jamani tunahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote huko nyuma.
Bado ni ukweli ambao
haufichiki kuwa Heshima kwa viongozi wetu
na hata kwa mtanzania yeyote na
mtu yeyote ni muhimu. Nafikiri tulitakiwa kuangalia sheria na hatua zake
na sio kumdhalisha kama alivyofanyiwa huko igunga katika eneo lake la kazi. Ni
busara kujaribu kuepuka kujichukulia sheria mkononi;
Tukikumbuka sana wosia
wa Baba wa Taifa kuwa watanzania wote ni
ndugu. Ni vema basi sote kama taifa tukafuata sheria tulizojiwekea bila kujali
itikadi za vyama; na wabunge wetu wakawa mstari wa mbele katika kuishi kwa
matendo yale wanayoyapitisha bungeni na sio kuwa vinara wa kuongoza fujo na
uvunjaji wa sheria hizo. Sisi kama taifa tujitahidi kwa pamoja kudumisha amani!
“Inawezekana timiza wajibu wako”
Hakuna umaskini mbaya kama
umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya
sana' Mwalimu J. K. Nyerere,
Kama Taifa tusimame imara katika kupigania "umoja,
amani na upendo miongoni mwetu" hii ni kati ya zawadi kubwa sana ambayo waasisi wa taifa letu Mwalimu Nyeyere na Mzee
Abeid Karume walituachia
Tuache kuburuzwa na upepo
wa siasa na wanasiasa; ambao wanapigania zaidi masilahi binafsi na sio masilahi ya taifa, tufunguke sasa.
Nawatakieni Kampeni za mwisho mwisho zenye
amani na nguvu ya Hoja na sio matumizi
ya Misuri
No comments:
Post a Comment