POLISI WANAPOSHINDWA KUSIMAMIA SHERIA NA WAJIBU WAO; FIKRA YAKO NI IPI?
Polisi ni chombo cha serikali chenye nguvu ya kisheria ya
kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa, na usalama wa raia na mali zao unakuwepo.
Maswali ambayo sisi raia tunajiuliza leo kama polisi wanalindwa
na sheria ya kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kubaki salama;
Je Polisi wanaposhindwa kuwajibika kinyume na kiapo cha utii wa
sheria zilizowaweka kazini kwa kushindwa kuitumikia nchi na wananchi wake kwa
uadilifu nini kifanyike? Kuyahamisha majukumu yao kwa chombo kingine cha ulinzi
au kuwawajibisha?
Je tuwafanye nini baadhi ya polisi wanaotumia lugha za ubabe,
vitisho na kutumia nguvu hata wakati hakuna sababu ya kutumia nguvu kutatua
katika utendaji wake.
Je polisi wetu
wanatumiaje mafunzo yao katika kuwaelimisha
raia kuhusu makosa mbalimbali yanayofanyika, kwa sababu sio makosa yote
yanapelekwa mahakamani?
Je askari wetu
wanauhusiano wa namna gani na jamii inayowazunguka?
Je polisi wetu wanatumia sheria zaidi au ubabe katika kushughulikia kero za
raia wake?
"Je polisi anapomiliki
biashara kama daladala anaweza kusimamia
sheria vizuri ambayo inahusiana na biashara yake hiyo ya daladala pale uvunjaji
wa sheria ukitokea?"
Je
polisi wetu ni msaada kwa raia wenye shida kama inavyofanyika katika nchi
nyingine au ndo wanakuwa chanzo cha kero?
je ni jakumu la askari yeyote ambaye anayefanya doria dhidi ya
majambazi ni lipi au anaruhusiwa pia kufukazana
na wakosaji wangine kama “daladala” kwa wakati mmoja?
Je ni sahihi kwa polisi kusindikiza magari ambayo yanabeba magendo kama
swala la sukari hivi sasa? “ escot ya Mzigo”? Kilio cha waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo
Pinda katika ziara yake huko Mara jinsi polisi wanavyoshiriki kuhujumu uchumi
wa nchi.
Nafikiri itakuwa vyema kama polisi wetu wataendelea kuwa rafiki wa raia wema ili kuwawezesha kupata ushirikiano katika kubaini wahalifu. Tunazidi kuwaomba waendelea kufanya kazi zao kwa kufuata sheria na kiapo chao.UWEZO kuchapa kazi vizuri wanao, SABABU wanayo kuendelea kulinda amani; tatizo tu NIA inachechemea pengine kwa sabau ya uduni wa masilahi basi tunaiomba na serikali yetu iliangalie hili la masilahi bora kwa polisi wetu.
No comments:
Post a Comment