Kauli ya Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO"
Inatufundisha nini katika maendeleo ya taifa
hili na viongozi ambao wanashindwa kuchukua uamuzi mara moja?
Ili tuweze kuendelea
tunahitaji, pamoja na mambo mengine yote swala la uongozi bora ni muhimu sana;
Je viongozi wetu wako
tayari kutoa maamuzi magumu kwa faida ya watanzania bila woga?
Je Viongozi wetu bado wana Utamaduni
wa kuogapa kuwajibika katika utoaji maamuzi kwa ajili ya kikundi fulani cha watu?
Je Viongozi wetu wanaweza
kuthubutu wakati wanapo takiwa kuwajibika kufanya mambo kwa kuangalia masilahi
watanzania walio wengi hata kama yatawauzi na kuwakwera wachache wenye nguvu kama alivyokuwa
akifanya Hayati Edward Moringe Sokoine?
Ni ukweli ambao
haupingiki tukiangalia maelekezo ya Wanafalsafa kuwa “kukaa kimya bila kutolea
msimamo wako katika jambo fulani maana yake ni kwamba unakubali au unapinga ila
unao woga wa uwazi”. Na kama viongozi
wetu wana tabia hii ni kasoro kubwa; kama wahenga walivyotuambia kuwa; “ngoja
ngoja huumiza matumbo” tukingoja kufanya maamuzi tunaruhusu mawazo mabaya toka
kwa wamanchi wenye hasira pale ambapo kuna kuwa na tatizo.
Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi sema "Hatuwezi tukawa kweli chama cha watu
ikiwa hatujishughulishi na shida
za kawaida za watu wetu".Tujiulize,Je viongozi
tulionao ambao hawajishughulishi na shida zetu, wapo kwa ajili ya nani?
Ni ukweli kuwa “Hekima
na busara huzaa mafanikio ya uongozi bora, lakini machafuko ni udhaifu wa
uongozi”
Mkongwe wa siasa Mahatma Ghandi, aliwahi sema, “tufikirie
kesho lakini tutende kwa ajili ya leo.Hivyo mustakbali wa maisha yetu ya kesho
yatategemea maamuzi sahihi ya leo”.
Kama taifa nini tunahitaji?
· vyama vya siasa vyenye nguvu na vyenye kuheshimu
demokrasia,
· Bunge lenye nguvu za hoja lisilitawaliwa na
itikadi ya chama chochote!
·
Viongozi wenye
kufikiri kwa faida ya wananchi
·
Viongozi wanaweza
kusimamia sheria
Rais Mstaafu awa awamu
ya tatu, Benjamin Mkapa aliwahi kutamka hili kuwa sisi watanzania ni wagumu wa
kufikiri;
Swali langu hapa
Mheshimiwa Mkapa kama Rais mtaafu nini kilimsukuma yeye kutoa kauli hii?
Je ni ugumu wa
kuyakabili matatizo ya maisha au kama ndugu yetu Juvenalis Ngowi alivyowahi andika kuwa “Bahati mbaya ni kwamba inawezekana uvivu wetu huu wa kusoma
mambo magumu ndio unatuingiza “mkenge” hata kwenye mambo muhimu ya kitaifa kama
mikataba. Inafika mahali tunaingia mikataba ya kusikitisha kiasi cha kujiuliza
hivi Mwenyezi Mungu aliwapa watu hao ubongo wa nini? Maana uti wa mgongo pekee
ungewatosha watu hao”.
Ndipo tunapoukumbuka
wosia wa baba wa taifa’ "TUMUACHE BADO
AKUWE KIDOGO"
Kama wananchi ambao
ni sehemu ya kuwachagua hawa viongozi nafikiri inatupasa tuondoe uvivu wetu wa
kufikiri, tuamke sasa na tuache itikadi za kuwaacha kuwapa madaraka mtu yeyote
ambaye inaonekana wazi kuwa bado hajapata utashi wa kuwa kiongozi bora wa
kuwatumikia wananchi wake.
Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema - Ukiweka
dodoki kwenye maji safi litanyonya maji safi! Ukiliweka kwenye maji taka,
kadhalika litanyonya maji taka! Hapo ndipo tulipo! Uvivu wetu wa kufikiri
pengine huleta tatizo hili.
Sisi wadau wa kuwaweka madarakani tukisimamam
imara tutawafanya viongozi wetu kuweza kuthubutu au kuchukua maamuzi ambayo watawasaidia
na kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi na kulinda mali ya umma kwa nguvu
zote, bila kujali kitu chochote.
Nafikiri viongozi wetu wa sasa wanatakiwa kufuata busara na umakini ambao
marehemu Sokoine alikuwa nao katika uongozi wake Kwanini, wasikubali kujifunza
kwake waone matokeo yake? Kama kuna maamuzi magumu inatakiwa wayafanye; mbona
Sokoine alifanya na kuwafanya wahujumu uchumi kuiogopa serikali na kusalimu
amri?
Viongozi wetu wanaweza
kwani tunaimani kuwa kwa sasa wameshakuwa kifikra na utendaji unaozingatia misingi ya haki na kujali maendeleo ya watanzania wanyonge ndio maana tumewakabidhi nchi;
No comments:
Post a Comment