JE NI MAZINGIRA GANI YANAANDALIWA NA VYAMA KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO IGUNGA- TABORA?
Oscar Ameringer aliwahi sema kuwa "Politics is the gentle art of getting votes from the poor and campaign funds from the rich, by promising to protect each from the other" -
Hiki ndicho kinachotokea Igunga kwa sasa vyama kupitia wanasiasa wao wanajitahidi kuvuna kura kutoka kwa wananchi wa kawaida “ wenye kipato cha chini au kwa ufupi masikini; kwa msingi huu wanasiasa huwapumbaza masikini walala hoi kwa kuwanunua ili wawapigie kura bila wao wenyewe kujua kwa kutumia sera na mapenzi yao kwa chama husika na wakati mwingine kuwapatia pesa ambazo wanazipata kwa matajiri wenye malengo binafsi mara ushindi ukipatikana.
Pesa au rushwa ambayo inatolewa na wanasiasa ni mfumo wa utendaji wa kufikisha ujumbe kwa wanachama wao ili wahakikishe kwa naman yeyote ile ushindi unapatikana, kwa kauli mbio tofauti tofauti zinazoashiria maendeleo; kwa msingi huu wa kampeni ni wakati wa neema au mavuno kwa wafuasi wao na wananchi wanyanja.
Siasa ni ushindani na ni utaalau wa juu kabisa wa kupangilia mikakati hata kama ni ya uwongo, ili mradi lengo la kushika dola litimie. Kutokana na falfasa hii Ifahamike kuwa sio kila mtu au kila chama kinanafasi sawa katika aina hii ya kushiriki katika kuufikisha ujembe; uzoefu hutumika vitisho nya kuwatisha wanyonge hutmika pia; pesa ndo usiseme; Nguvu hii ya pesa huviondoa vyama vidogo ambavyo haviwezi kushindana na kuviacha vyama vyenye nguvu kama inavyotokea Igunga wakati huu wa kampeni ya nafasi ya Ubunge.
Wanasiasa akisimama ulingoni kauli zao ni namana ya kutatua kero za wananchi katika kuondoa kero zao; sikiliza kiini chote cha kampeni huko Igunga kwa sasa ni kutatua kero za wananchi wa Igunga kwa kunadi sera mbalimbali za maendeleo tutafanya hili na lile;
Tatizo kubwa la wanansiasa sio wakweli na hawajali hasa wakisha pata au wakishachaguliwa; wanakuwa na sababu nyingi tu za kujitetea, lakini ukweli hawajali tena kwani walichotaka si wamepata kushika dola.
Kama semi hizi tatu za kiingereza zinavyosema:.
l When the ruler himself is 'right,' then the people naturally follow him in his right course."
l “Whatever the best man does, others do that also. The world follows the standard he sets for himself”.
l "If a ruler himself is upright, all will go well even though he does not give orders. But if he himself is not upright, even though he gives orders, they will not be obeyed."
Semi hizi zinajumuisha tabia za wanasiasa wetu namna wanavyotakiwa wawe ili kujenga imani kwa wananchi na maendeleo ya taifa letu.
Turudi Igunga; Kilio kikubwa kwa hivi sasa huko Igunga ni matumizi mabaya ya pesa, pengine rushwa na tukumbuke kuwa rushwa ni jiko ambao zambi zote hupikwa huko; kwani watu hawa hutaka kuwa viongozi ili wajitengenezee faida binafsi, ni sawa na mwanaume ambaye sio mkweli anavyoweza kumdanganya mwanamke ili aweze kuutumia mwili wa mwanamke huyo katika kutimiza kujifurahisha yeye mwenyewe; baada ya kufanikisha haja yake humdharau na kumwona sio kitu tena hata kama walikubaliana katika kusaidiana ahadi hizo zote huyeyuka na kumwacha mwnamke huyo akisononeka kwa uaminifu wake na kujitoa kwake.
Je fujo zinazoendelea huko igunga je zinatokana na wananchi hasa vijana kuelewa haki zao na nia yao na kutaka kiongozi atayechaguliwa awe kweli mtatuzi wa shida zao? Au ni vurugu tu ambazo zinachochewa na wanasiasa kwa kutumia pesa ili iwe ni sababu ya kuvuruga amani ambayo ilitakiwa itawale uchaguzi huu mdogo? Au vyama vinaandaa sababu mapema ili hata vikishindwa katika uchaguzi viweza kuhalalisha matokea kuwa wameshindwa kwa sababu hii au ile;
Tatizo langu leo hii ni hili, aina hii ya kampeni inaharibu moja ya msingi wetu mkubwa san asana ambao ulijengwa na waasisi wa taifa hili utamaduni wa uvumilivu unavyobomoka hivi sasa. Tukumbuke kuwa taifa hili linafahamika ni miongoni mwa taifa ambalo lilikuwa limetulia na wananchi wake wamekuwa wakivumiliana sana. Je kwani nini leo hii wanasiasa wanatupeleka katika hali ya kuvunja umoja wetu? Wanatutakia nini hawa wanasiasa na vizazi vyetu? Wanatamani nchi hii isitawalike kwa faida yao? Kwa nini wanaingiza roho ya ukatili kwa vijana wadogo?
Nafikiri bado kuna kila sababu ya wanansiasa kutambua kuwa ni dhambi sana kuchezea amani ya nchi kwa masilahi binafsi na ya muda mfupi na kuliacha taifa katika janga kubwa la uvunjaji wa amani.
Pamoja na ushindani wa siasa huko Igunga lakini uchaguzi huu mdogo usiwe sababu ya kuvunja amani; tunawaomba wasimamizi wa sheria zihusuzo uchaguzi wawe makini kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa bila kumwogopa mtu, au kikundi chochote au chama chochote kile.
Muhimu ni kwamba tuzike tofauti zetu kwa faida ya taifa letu na vizazi vyake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA