WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, April 30, 2011

REFLECTING BACK- POLITICAL CORNER;



Why opposition parties failed in the 2010 General Election in Tanzania?


1.  The ruling party CCM has very strong bases in various villages around the country where there is large number of voters while


2.  Opposition parties have strong holds in urban centers were the number of voters is low but the euphoria is huge


3.  The president has too much power to appoint and disappoint, this leads to a large number of senior government officials to be presidential appointees hence obedient to the president; 



4.  Power mongering, the big opposition parties of CUF, CHADEMA, NCCR were competing against each other instead of joining hands to present one candidate for the opposition, this lead to spread of votes and creation of weakness against opposition




Friday, April 22, 2011

MSHIKE MSHIKE BUNGENI



Kauli ya Spika wa Bunge Anne Makinda:  Wabunge wanafanya mambo ya KIJINGA ina maana gani kwa jamii
·        Tufunge mlango tupigane”
·        "Mmezowea kutuburuza"
·        "Naomba mjiheshimu hapa si sokoni, Watanzania wengi wanawaangalia mnavyofanya mambo ya kijinga na kupiga kelele,"

Tusiwalaumu tuu wabunge, tujiulize wameingiaje bungeni? Tatizo la ujinga kama uko ambao unatokea Bungeni kama alivyosema mheshimiwa Spika linatoka na sisi tunaowachagua; je tunatumia vigezo gani kujua kweli kama WABUNGE TUNAOWACHAGUA wanaweza kujenga hoja za kweli na sio itikadi tu ya chama atokacho mbunge? Kama bunge halifanyi kazi yake vizuri lawama ni kwetu wananchi tuliowachagua.

Kwa watanzania wengi ambao walibahatika kufuatilia nini kilikuwa kinajili bungeni Dodoma wiki chache zilizopita watakubaliana nami kuwa tuliweza kupata kioja cha kuhitimisha mijadala ya bunge katika kikao chake cha 10.

Ilimlazimu Mheshimiwa Spika kutamka maneno ambayo nafikiri yalikuwa hayastahili kutamkwa bungeni kwa heshima na majukumu makubwa ya kazi ya bunge kama chombo muhimu sana katika kusaidia kuendesha shughuli za serikali; katika majukumu ya Kiuwakilishi (representational),utungaji wa sheria (legislative), upitishaji wa bajeti, mapato na matumizi ya nchi (budgetary and resource approval) pamoja na uwajibishaji wa serikali iliyoko madarakani (accountability). Bunge pia ni chombo cha kutathmini mwenendo wa jumla wa kisera unaopendekezwa na serikali ili kubaini kama mwelekeo wake unasawiri matakwa ya wananchi walio wengi nchini. Aidha ni kazi ya Bunge katika mfumo wa kidemokrasia kuhakikisha kuwa matendo ya serikali iliyopo yanakidhi matakwa ya jamii wanayoiwakilisha, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono hoja nzuri na kupinga zile zinazoonekana kukinzana na maslahi ya jumla ya kitaifa.

 Je Bunge letu linatekeleza kwa umakini majukumu haya au bunge kwa sasa limekuwa ni chombo kikuu cha ushauri tu kwa serikali bila kuwa na meno ya kuiwajibisha serikali pale ambapo inakosea?
Kwa maneno mengine wabunge wamechaguliwa na wananchi ili wawakilishe katika kuisimamia serikali. Hivyo wabunge hawatakiwi kabisa kupeleka mawazo na mitazamo yao wenyewe. Wanatakiwa wanapozungumza Bungeni au kupiga kura ni lazima wafikirie wapiga kura wao wamewatuma kufanya nini. 
Je tuliwatuma waende kupigana bungeni? Au kugeuza bunge kuwa ni soko kama mheshimmiwa makinda alivyowakemea wabunge wenzake;

Je wabunge wetu ambao tumewachagua  wanao uwezo wa kutawala katika kuchangia hoja bila kupigana na kutishana? Au ni wale ambao wanapenda sana kutawala hata kama hawana uwezo wa kutawala.”

Je wabunge wanafahamu kuwa Bunge letu la sasa bado lina nguvu kubwa ambayo halijaweza kuitumia vyema. 
Nafikiri tatizo la wabunge wengi wanatumia muda wao mwingi kulalamika na kushangaa mapungufu.  Wanatakiwa wawe na uwezo wa kupangua na kupanga upya mambo wanavyoona wao inafaa bila kujali maneno na minong’ono ya wanafiki wachache na wasio jali maslai ya wengi au kuwa na muono wa mbali.
Je wabunge wetu wengi ni kundi gani?

Je tunao wabunge wenye uwezo wa uongozi na wito wa uongozi kwa kuweka maslahi ya taifa mbele kwa manufaa ya watu.

Wabunge wetu wameingia bungeni kama moja ya njia sahihi za kujipatia neema, ubinafsi na maslahi binafsi;  
 
Je abunge wetu ni wale wenye uwezo mkubwa wa kushawishi kutokana na uwezo wao wa  kiuchumi, haautegemei mshahara wala marupurupu ya ubunge; Hawana muda wa kuchangia mijadala ya bungeni, wala hawana maswali, ila kwa sababu wana nguvu kubwa kiuchumi na jeuri ya pesa, wanao uwezo wa kuwabuluza wabunge wengine na kuhakikisha kuwa wanalolitaka liwe, ndilo linakuwa. Kwa maneno mengine aina hii ya wabunge ndio viongozi wenye nchi.

Friday, April 15, 2011

RASIMU YA KATIBA MPYA ISIYO KIDHI HAJA YA WATANZANIA WENGI

MWENENDO HUU WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UTATUFIKISHA WAPI?

Ilikuwa ni shangwe kubwa pale Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Mheshimiwa JK alipotoa  taarifa rasmi kuwa serikali yake iko tayari kushughukikia mapendekezo ya kuandaa katiba mpya

Watanzania wengi kwa ujumla walikuwa wamejawa na shauku na hamu ya mabadiliko ya katiba wakijua kuwa wakati sasa umefika kwa wananchi wa Tanzania kuwa na katiba mpya ambayo itajumuisha misingi ya taifa itakayokuwa imelinda maslahi ya wananchi  kwa ustawi na maendeleo yao. 

Kwa msingi huu toka kongamano la kwanza ambalo lilifanyika chuo kikuu cha dar es salaam chini ya wenyekiti wa Prof Issa Shivji na Jenarali Uliwengu wananchi wengi walijitokeza wasomi, wanasiasa wananchi wa kawaidi na vikundi mbalimbali vya jamii; ili kushauri katiba mpya iwe na sura gani, na zoezi nzima la upatikanaji wa maoni uwe vipi.

Kama Makamu wa Kwnza wa serikali ya umoja wa kitaifa  Maalim Seif alivyo wahi sema“hali inavyokwenda wananchi wengi wamehamasika kutaka kutoa maoni juu ya kuwa na katiba mpya hivyo ni vizuri wananchi wakapata nafasi ya kutoa maoni yao kwa kuwa katiba inayowashirikisha wananchi ndio katiba madhubuti nchini”.

Msisitizo hu unatokana na dhana kuwa iwapo Wananchi wataweza kushiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kuandaa Katiba mpya  itasaidia katika kuepusha  dhana kuwa suala la kuandika Katiba sio la kikundi Fulani, chama fulani au ni la Wanasheria,  kwa vile wao wamebobea katika sheria hasa za masuala ya Katiba.  

Wengi walipendekeza kuwa ni muhimu  wananchi wote, washirikishwe ikiwa ni pamoja na wale wasiojua kusoma wala kuandika na wanajamii mbalimbali mijini na vijijini watakavyowezeshwa kuweza kushiriki katika kuweka misingi ya uandikaji Katiba, kutoa maoni katika mijadala ya awali na kwa Tume ya kuratibu maoni, pamoja na kuchagua wawakilishi kutoka miongoni mwao kushiriki katika vyombo muhimu vya kujadili mapendekezo na rasimu za Katiba ikiwemo wajumbe wa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba na mara nyingi mjadala unaishia kwenye kikao cha  Bunge Maalum la Katiba.

Nchi inapoamua kuandika katiba mpya ukweli wake ni kuwa ni  upanuzi wa demokrasia na maendeleo ya nchi kwa kuwa na katiba ya nchi inayoonyesha utashi wa wananchi.

Kazi ambayo iko mbele yetu ni kubwa sana sisi kama  Watanzania ni lazima tuhakikishe kuwa mchakato wa kufikia katiba mpya unakuwa huru, yenye uwigo mpana sio wa kulindana bali ni wa uwazi na ambao una uhalali wa kutosha kuweza kufikia kusema kuwa Katiba itakayopatikana kweli imetokana na watu na mazingira yetu.

Mchakato wa kufikia Katiba Mpya usipoweka misingi ambayo utahakikisha wananchi wote wana nafasi sawa ya kuchangia mawazo yao ya dhati  bila kuogopa au kununuliwa tutakuwa tumefanikiwa kuifikisha katiba mahali pazuri kwa usalama wan chi bali  kama kutakuwa na mchakato mbovu tutakuwa tumeiharibu kabisa nchi yetu na maendeleo yake kidogo ambayo tunayo hivi sasa.
Lengo la kila mtanzania tunatamani kuandika Katiba Mpya ili kuweza kukiachia kizazi kijacho mfumo mzuri wa utawala ambao utawapa nafasi ya kufanikiwa katika maisha na mipango yao na ambao utawahakikishia mtiririko mzuri wa mahusiano na kuwajibishana kati yao na watawala wao.

Nini kinatokea sasa?

1.  Wengi wamepinga rasimu hiyo ya katiba kwa sababu tofauti mojawapo ikiwa inafanyika katika kipindi kifupi na pengine wananchi wengi hawatapata nafasi ya kutoa maoni yao.

2.  Mikutano iliyofanyika Dodoma na Dar es salaam imeonyesha mapungufu makubwa katika siku za awali tu; je kamati au wizara inayoshughulikia rasimu ya kuratibu maoni ya utayarishaji wa katiba mpya kweli wamejiandaa kwa katiba mpya au ni ubabaishaji tu?

3.  Je Kamati waliangalia mahitaji halisi ya wananchi na kiu ya wananchi kutoa mawazo yao?

4.  Hebu angalia mambo yalivyokuwa Dar es salaam, ilikuwa ni tatizo kubwa pale ukumbi ulipojaa wananchi wengi ambao kwa sababu moja au nyingine waliishia kulala tu , nini kilikuwa kunaendelea, je wapi tutapata hiyo rasimu bora ambayo inakizi haja wakati hatuna ushindani katika uchangiaji hoja wakati wananchi waliopokelewa au kuletwa katika ukumbi huu kwa sababu moja au nyingine waliishia kulala tu?

5.  Kule Zanzibar kwa kulitokea tukio la kuchana Rasimu hiyo wananchi na wachangiaji wakiwa wamejawa na hasira ya utaratibu mzima wa uandaji na mwonekano wa rasimu hiyo; Je ni kweli kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hakuhusishwa kikamilifu? Je Rasimu unaelezaje swala la Muungano? Je linakizi haja kwa pande zote? Je wale wanaona wanamezwa wamepewa kinga gani ili wasipatwe na janga hilo?

6.  Je kama zoezi hili halitakwenda vizuri kwa kigezo cha muda nani atawajibishwa kulipa gharama halisi ambayo imetumika  katika maandalizi hayo? Ikumbukwe kuwa bado pesa hiyo ni ya mlala hoi.

HITIMISHO

Lazima tukubali kuwa Mheshimiwa Rais amebariki utaratibu mzima wa uandikaji wa katiba upya, hili ni jambo la kihistoria na ambalo halitakiwi kufanyiwa mzaha na watendaji wachache kwa masilahi yao binafsi au chama chochote,  hebu tulifanye jambo hili kwa masilahi ya wananchi wa Tanzania na sio kwa manufaa ya wana siasa na vyama vyao;
Mungu ibariki Tanzania na watu wake

Tuesday, April 12, 2011

KIKWETE NA MCHAKATO NDANI YA CCM

MZEE MAKAMBA INATOSHA  NA INAFAA UPUMZIKE
                          SEHEMU YA KWANZA


Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mheshimiwa Rais JK alivunja kamati Kuu ya CCM  huko   Dodoma tarehe 9/4/2011 tukio ambalo lilihusisha kustaafishwa kwa  Katibu wake Mkuu mzee wetu  Bwana Yusufu Makamba;

Utendaji wa kusua sua wa Mzee makamba umekuwa kilio cha siku nyingi cha wanachama wa CCM; wengi walikuwa hawaridhishwi na utendaji wake wa kazi hasa katika maswalal yote ambayo yanahusu kumshauri Mheshimiwa Rais kama kiongozi wa serikali na kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi;

Pamoja na mapungufu Mengi ya Mzee wetu Makamba lakini Mheshimiwa Rais ataendelea kubeba lawama kwa kuchelewa kuliona tatizo hili pamoja na kilio kirefu cha wana CCM kuwa Makamba alikuwa mzigo kwa Chama katika ufanisi;


Pamoja na uamuzi huu Mzuri na mzito swali la msingi hapa ni hili Kwa nini imemchukua Mwenyekiti wa Chama nuda mrefu kusafisha utendaji ndani ya chama?


kama Kweli  kamati yake kuu ya chama chake ilikuwa haifanyi kazi vizuri, na imemwangusha kwa kiasi kikubwa, kwa nini alikubali  kuendelea kuibeba?, "ni sawa kama kuendesha gari ambalo halina balance nzuri ya upepo unaotakiwa  kwenye matairi yake, kwani kabla ya ajali utalazimika kutumia  nguvu zaidi katika kuhakikisha kuwa gari hilo inakwenda vizuri na haliachi barabara", kitu ambacho kimekuwa sicho, kwani katika hali tofauti tofauti Mwenyekiti amejikuta akishindwa kuhimili mikiki mikiki ya barabarani ambayo imekuwa ikisababishwa na ubovu wa matairi( watendaji) kwa au kujali masilai yao binafsi, na kupoteza mwelekeo wa sera na dira za Chama;

Sijui nini kimemtokea Dereva Wetu(mheshimiwa Rais Na Mwenyekiti wa CCM) mpaka ameamua kulitosa gari hilo amabalo  fundi wake Mkuu alikuwa Mzee Makamba; na kuamua kuchukua gari nyingine; 


Kwa tafakari yangu na kama nilivyowahi kuandika katika blog hii huko nyuma kuwa  kuwa Mzee Makamba alishindwa kutekeleza yafuatayo;

  • ·        Kutoa ushauri sahii kwa wakati sahihi



  • ·        Kutumia sana sera za ubabe wakati hakuna haja ya sera hizo
  • ·        Kutumia lugha ambazo zilikuwa hazivuti ushawishi kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla
  • ·        Kushindwa kutoa ushauri mzuri kwa Mwenyekiti wake wakati yeye ndio mtendaji mkuu wa chama;

Tukumbuke siasa yenye msingi wa utawala Bora sio ubabe na ukitumika sana huondoa busara na hekima; uongozi bora unatawaliwa na uongozi hekima, ambayo itazaa uadilifu, uwajibikaji na umoja.

Wakati umefika kama saa izungukavyo, saa yako imefika kwa wewe mzee wetu Makamba  uweze pumzika,  inatosha hapo ulipomfikisha Mwenyekiti panatosha, tuwaachie na wengine nao tuone watamsaidiaje Mwenyekiti katika kuitengeneza Tanzania yetu na kuleta neema kwa watanzania wote.




Mungu Ibariki Tanzania na Afrika