Mheshimiwa Anna Makinda amechaguliwa kuliongoza Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha Mapinduzi; kwa maneno MENGINE mheshimiwa Anna Makinda ni SPIKA wetu na hilo halina ubishi kwani amechaguliwa kulingana na taratibu na kanuni ya Katiba yetu.
Nachukua fursa hii kukupngeza kwa ushindi huu, mimi siangalii uwingi wa kura ambazo zilikupa ushindi mimi nataka kuangalia wajibu wako kama Spika utakuwa ni upi na utalisaidiaje taifa hili ambalo lina makundi mawili ya watu:
Kundi la kwanza ni lile ambalo linaishi katika maisha bora na ya uhakika hawa ni matajiri (Privileged) na kundi nyingine ambalo ni kubwa katika nchi yetu ni WALALA HOI MASIKINI ambao hawaijui hata kesho yao itakuwaje wamezungukwa na umasikini uliokidhiri na hao ndio wengi (underprivileged). Cha ajabu hawa ndio waliokuchagua wewe Mheshimiwa “Spika”. Swali la msingi je kundi hili linakugusa vipi wewe katika utendaji wako wa kazi? Utalisadiaje katika kipindi chako cha uongozi?
Wewe umefanikiwa kuwa Spika wa kwanza mwanamke katika historia ya Jamuhuri wa Tanzania, na kikubwa zaidi katika tafsiri nyingi za wataalamu Mwanamke ni muhimiri mkubwa sana wa maendeleo katika ngazi yeyote ile kama akipatiwa nafasi na akiaminiwa; katika kila jambo nzuri la maendeleo ukiangalia nyuma yake kuna msukumo wa mwamamke;
Wengi wetu tumekulia vijijini na kwenda shule ambazo zilikuwa katika umbali mkubwa, je bado tunakumbuka jinsi wazazi wetu walivyotusaidia hasa MAMA zetu? walikuwa wakiamka alfajiri kutuandalia chakula cha kubeba shule, na kutusindikiza hata kama ni hatua kumi na kututakia masomo mema pengine wakati huo huo Baba alikuwa amelala na hajui hata kama ana wajibu wa kusaidiaana na Mama katika kufanikisha adhima ya elimu ya mtoto wao. Mimi binafsi Siwezi sahau hii "loving commitment" ambayo imejengwa katika mioyo ya akina mama.
Mheshimiwa Spika Je tutarajie hii loving commitment amabyo umejaliwa na Mwenyezi Mungu toka kwako katika kulisaidia hili kundi la underprivileged (walalahoi masikini)? Au kwa vile uko Kileleni tusikuhesabu tena kuwa si Mwenzetu hutaweza tena kuhimili vishindo kutoka upande wa privileged (matajiri) ambao ndio wanao tumia uwezo wao kuongoza shughuli za serikali na kukuongoza wewe nini ufanye?
Ninafahamu fika kuwa unayo elimu (knowledge) na uzoefu wa kutosha (experience) kwa kuliongoza Bunge letu Tukufu. Jukumu ambalo unalo ni sawa na kuendesha gari katika makutano ya barabara inahitaji uelewa wa kutosha kuhusu kuyajua magari mengine yanaelekea wapi; lakini kwa kurahisisha uendeshaji na kuepusha ajali zitokanazo na uzembe na kutokuwa na subira hutumika taa za kuongozea magari ambazo hufanya kazi kwa usahihi mkubwa.
Na shughuli za Bunge nazo zinahitaji umakini mkubwa zaidi ya taa ya kuongozea magari. Sio sehemu ya majaribio ya uongozi (trial and error). Kwa misingi misingi hiyo Chama chako kimekuchagua kikijua kuwa una siza za utendaji na sio majaribio:
Kwa msingi huu itapendeza sana kwa jamii ya watanzania kama utakuwa:
- Spika ambaye utaaminiwa na kutegemewa wa watu wote
- Spika ambaye utaweza kujichanganya na tayari kujifunza kutoka kwa wengine ( ndani ya chama chako na Nje ya chama chako (wapinzani)
- Spika ambaye utaweza kutumia elimu yako na uzoefu katika katabiri usahihi wa majadiliano yatakayo iletea tija mbadala Taifa letu kwa ustawi wa watu wake na demokrasia yake.
- Kutoa uamuzi ambao utakuwa unafuata kanuni za uendeshaji wa Bunge bila upendeleo au kuwafurahisha wachache,
- Kufanya maamuzi mazito kwa faida ya wengi ambao ni masikini bila kujali kuwa unapoteza umaarufu ndani ya chama chako au vyama vya upinzani.
Yakumbuke sana maneno haya: “God grant me the serenity to accept the things I cannot change; courage to change the things I can; and wisdom to know the difference”.
Nakupongeza sana kwa kuchaguliwa, Mwenyezi Mungu akujalie Afya njema na Busara katika kutenda kazi yako kwa uadilifu, upendo na kwa Kumwogopa Muumba wako ili kujijengea uadilifu AMIN
“A warrior must learn to make every act count, since he is going to be here in this world for only a short while, in fact, too short for witnessing all the marvels of it.” By Carlos Castaneda –
“The challenges of change are always hard. It is important that we begin to unpack those challenges that confront this nation and realize that we each have a role that requires us to change and become more responsible for shaping our own future”. By Hillary Rodham Clinton
No comments:
Post a Comment