WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 28, 2010

Dr. JOHN POMBE MAGUFULI NA WIZARA MUHIMU KATIKA MAENDELEO YA TANZANIA.






Mhehimiwa Raisi  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika siku chache zilizopita alimchagua Mbunge wa Chato (CCM) mheshimiwa Dr. John P. Magufuli kushika wizara muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. Dr Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wa muda mrefu kuanzia wakati wa awamu ya tatu katka nafasi mbalimbali kabla ya kuwa waziri kamili;

Dr Magufuli mwansiasa na msomi aliyebobea katika siasa na uongozi, anao uzoefu wa kutosha katika shughuli za serikali; lakini kubwa kupita yote ni mchapakazi wa kuigiwa mfano, ni kiongozi ambaye hakati tamaa, ni mkweli kwa nchi yake, mwajibikaji, na ni msimamizi mzuri wa wizara yake, ni hodari vile vile kwa kuwawajibisha watendaji walio chini yake katika kutekeleza majukumu ya  serikali.

Mimi ninamwita kiongozi wa namna hii kuwa ni mzalendo ambaye anaitakia mema nchi yake, ana mapenzi na nchi yake, yuko tayari kuifia nchi yake, na ni mkweli kwa nchi yake. Mara nyingi kiongozi wa aina sio mwoga sio mwoga na anafanya maamuzi yake kwa kuwa na facts; na yuko tayari kusimamia utekelezaji wa uamuzi wake kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa anatekeleza wajibu wake kwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa na nchi (serikali) ambaye yeye ni mwajiri wake au kwa taratibu ambazo zimewekwa na chama chake (sera) kwa manufaa ya nchi.
Dr. Magufuli ni shupavu wa kusimamia maamuzi ya serikali yake bila kumwonea aibu kiongozi mwingine yeyote ambaye atataka kufanya tofauti hali halisi ndani ya mamlaka ambayo amekabidhiwa.

Je wizara hii Mpya ina maana gani kwetu? Dr. Magufuli anamchango gani kwa wananchi?

Katika vigezo kadhaa vya maendeleo ya nchi hutegemea sana ukuaji wa uchumi, na kukua kwa uchumi kunategemea vitu vingi ambavyo hurandana: mawasiliano ya barabara na anga ni kati ya vipao mbele muhimu sana vya maendeleo. Kwa mfano mawasiliano kama barabara hustawisha afya,ustawi wa jamii,ukuaji wa uchumi utokanao na mazao, ukuaji wa uchumi utakanao na fedha za kigeni viwanja vya ndege, ni muhimu kwa maendeleo  ya taifa kwa ujumla. tunahitaji  barabara nzuri  na imara kwa mawasiliano (connectivity) na viwanja  vya ndege  vya kisasa kwa kuongeza pata la taifa( Fedha za Kigeni) ni vitu muhimu kwa kukuza uchumi;

Ili kufanikisha maendeleo ya nchi yetu tunahitaji kiongozi kama Dr. Magufuli, mkweli, mwadilifu, machapa kazi, asiyetetereka kisera na kiusimamizi na ambaye yuko tayari kupambana na ushindani kwa hoja au kwa matendo na zaidi hasa anayo elimu na uzoefu wa kutosha: na isitoshe Dr Magufuli anafanya kazi na kiongozi mwingine mahili kama Naibu waziri wake Dr. H. Mwakyembe; kiongozi ambaye ni mkweli na ni mwadilifu kama Bosi wake. kwa mantiki hii wizara hii imekamilika na tunatarajia mambo makubwa sana ya kiwango cha juu.

Hongera Dr. John Pombe Magufuli tunasubiri mwendelezo wa uwajibikaji na mabadiliko makubwa ya sura za barabara zetu na viwanja vyetu vya ndege na kadhalika

4 comments:

  1. This is very interesting, You are a very
    skilled blogger. I've joined your rss feed and look forward to
    seeking more of your great post. Also, I've shared your website in my social networks!


    Feel free to surf to my web page :: runescape 2007 money making

    ReplyDelete
  2. I’m not that much of a internet reader to be
    honest but your blogs really nice, keep it up!
    I'll go ahead and bookmark your site to come back later. Cheers

    My web blog ... browse around this website

    ReplyDelete
  3. I like it when people get together and share views.
    Great site, stick with it!

    Feel free to visit my webpage clash of clans hack (http://mp-united.com/guestbook)

    ReplyDelete
  4. Hi there, I found your site by way of Google while looking for a comparable subject,
    your site came up, it looks good. I've bookmarked it in my google bookmarks.

    Hello there, just turned into alert to your weblog via Google, and located that
    it is truly informative. I'm going to be careful for brussels.
    I will be grateful in case you continue this in future.
    Many other people shall be benefited from your writing.
    Cheers!

    Also visit my web page :: top eleven hack (http://my.Opencrypt.com)

    ReplyDelete