WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, November 24, 2010

JE NCHI YETU NZURI SANA "TANZANIA" INAYO DEMOKRASIA YA KWELI?

                                                            


Kulingana na tafsiri nyingi za neno democrasia inahusisha zaidi ushirikishwaji ( uwakilishi) wa wananchi katika maamuzi yao ya maendeleo kwa kukabidhi majukumu kwa serikali iliyochaguliwa na watu/wananchi; kwa tafsiri ya haraka demokrasia ni utawala wa watu, unaofanywa na watu kwa manufaa ya watu.
Mara nyingi tumesikia viongozi wetu wakituambia kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia kwa  msingi huu kwamba kuna mfumo wa vyama vingi ambao unatoa fursa ya kuchagua viongozi kila baadaya miaka mitano na kuweza kuunda serikali ambayo itawasidia wananchi katika kujiletea maendeleo yao.
Lakini ikumbukwe kuwa demokrasia sio mfumo ambao unajiendesha wenyewe, unaendeshwa na watu kulingana na mazingira ya mahali, uwezo wa kimaendeleo ni kipimo kizuri sana cha demokrasia. Kwa msingi huu ni rahisi kabisa kwa wale ambao wamepata dhaman ya kuendesha nchi kuibadilisha kulingana na matakwa yoa kwa mgongo wa wanachi.
Tujipime kwa maswali haya machache ili tuweze kujua kama nchi yetu in demokrasia ya kweli:
1.      Ni kweli kuwa wawakilishi ambao tunawachagua kupitia vyama vyao wanawakilisha mawazo yetu au wana wakilisha mawazo ya chama kichowapitisha kugombea nafasi hizo?

2.      Je viongozi wetu wa juu kabisa wa serikali wakisha chaguliwa na wanannchi kuongoza nchi wanawatumikia nani wanannchi walala hoi au wafanyabishara wakumwa ikiwa ni sehemu ya kulipa fadhili na kuwafurahisha baada ya wao kutumia pesa zao kuwasaidia kupata uongozi (paymasters) na kuto wajali wananchi ambo ni sehemu kubwa ya demokrasia?

3.      Ni Kweli tunapiga kura kwa uhalisia wa kuwapata wawakilishi wa kutusaidia kuondoa kero za maisha yetu au tunapiga kura kwa ushabiki na kununuliwa tu?

4.      Je tuna uhuru wa kujieleza na kusikilizwa na viongozi tulio wachagua?

5.      Je tunauhuru wa kuwachagua wawakilishi tuwapendao kupitia utaratibu wowote ule uliowekwa na chama au inatubidi kuwapigia kura wale wawakilishi ambao wamechaguliwa na uongozi wa juu was chama husika?

6.       Je tunaweza kuikosoa serikali yetu na tukasikilizwa bila kutishwa?

7.      Je demokrasia yetu imetawalia na pesa au maoni na matakwa ya kweli ya wanaichi?
8.      Je serikali inatoa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa wanaichi kujua nini maana ya democrasia?

9.      Je tunaouvumilivu wa kutosha wa kisiasa hata pale tunaposhindwa kupata nafasi za uongozi wanchi  na kuwa na busara ya kutafuta njia mbadala ambayo itakuza demokrasia?

10.  Je vyama vilivyo katika kushiriki ushindani wa kisiasa vinapata nafasi sawa na vyama vile ambavyo vimejiimarisha kwa muda mrefu na vina nguvu na  uwezo mkubwa wa kipesa, ukilinganisha na vyama ambavyo bado ni vichanga na havina pesa ya kujitangaza?
Kama zaidi yanusu ya  majibu ya maswali haya yataonyesha positive basi tuna elekea kwenye demokrasia ya kweli ikumbukwe kuwa demokrasia ya kweli ni process ambayo itachukua muda mrefu kuimarika sio kitu cha mara moja. Na hii itafanikiwa tu kama level yetu ya uchumi, uvumilivu wa kisiasa,  uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji utayari wa kurekebisha  katiba  iliyoko ili iwe a true living organism hii inaweza kuharakisha democrasia yetu.
"If a door is shut, attempts should be made to open it; if it is ajar, it should be pushed until it is wide open. In neither case should the door be blown up at the expense of those inside."
Julius Kambarage Nyerere, from his Stability and Change in Africa speech given to the University of Toronto, Canada, 2 October 1969.
“It has been said that has been said that democracy is the worst form of government except all the others that have been tried”. 
Winston Churchill 
“Without God, democracy will not and cannot long endure”. 
Ronald Reagan 
“Democracy cannot succeed unless those who express their choice are prepared to choose wisely. The real safeguard of democracy, therefore, is education”. 
Franklin D. Roosevelt 

“Let us never forget that government is ourselves and not an alien power over us. The ultimate rulers of our democracy are not a President and senators and congressmen and government officials, but the voters of this country”. 
Franklin D. Roosevelt 

No comments:

Post a Comment