Sanaa ni taaluma ambayo ni muhimu sana katika ukuaji wa maisha yate binadamu. Wasanii ni nguzo muhimu katika kudumisha na kupeleka ujumbe kwa njia mbalimbali. Sanaa na wasanii ni dhana ya ushirikishwaji ambayo inatuondoa katika utaratibu wetu wa maisha ya kila siku iwe katika biashara , uongozi na kazi zingine za kila siku ambazo zinatulazimu kutumia akili zetu:
Kama tunavyofahamu katika utaratibu wa kazi akili zetu hufanya kazi sana na zinahitaji uwepo wa kitu mbadala ambacho kitasaidia kuipumzisha, na kwa akili kupumzika kutoka katika uwigo wa watu wanaoluzunguka kwa masaa nane; matumizi ya teknolojia ambayo huitaji umakini kubwa, kutokuwa na uhakika wa kazi kutokana na kuyumba kwa uchumi, tunahitaji kitulizo burudani ambayo ni sahihi; wengi tunaishia kusikiliza na kucheza muziki, kuangalia movies, pengine kwenda camping na kadhalika. Kwa kweli burudani hutupa mapumziko kwa ustawi wa maisha yetu. Bila sanaa maisha yetu yangefanana na usemi huu “all work and no play make Jack a dully Boy”
Kwa upande mwingine Sanaa wasanii na burudani ni kioo cha jamii, kwani huelimisha, huonya, hufundisha na kutuliwaza kama itatumika katika misingi ya kuonyesha ukweli na uhalisia wa maisha yetu wasanii na sanaa zao zitatufanya tucheke, tubadilishane mawzo, zitachangamsha akili zetu na kutuondoa na unyonge unaotokana na akili na mwili kuchoka;
Mathalani kwa ufupi ukiangalia kazi kama ya Msanii Afande Sele (Darubini Kali), au kazi ya Prof. J na MwaFa “ Jukumu Letu” au kazi za wasanii wa Filamu kama Kanumba Ray Kigosi, Pastor Emmanuel Myamba; Johari au Aunt Ezekiel, JB, Irene Uwoya, Lady Jay Dee; Chopa; Bishanga; Hadija Kopa bi Kidude, Ali Kiba na wengine wote; kwa kweli “we are proud of you” tunajivunia uwezo wenu na faraja ambayo tunaipata.
Tatizo langu kubwa ni hili kwenu wasanii wa Kitanzania?
Je nyinyi kama wasanii mmenjiandaaje kuyakabili maisha yenu wenyewe?
Je pamoja na kufanya kazi kwa bidii ya ubunifu wa mawazo, utungaji wa nyimbo muda mnaotumia, kazi zenu zinalingana na mapato? Najua jibu ni hapana sasa tuanzie wapi? Tuanzie kwa wanunuaji wa haki za kazi zenu? Au ni tatizo ka ushawishi wa kibiashara na soko kubwa la wahindi ambao wanamiliki kazi zenu, kwa vile wanafahamu kuwa mna njaa wanawalalia kwa malipo? Au tatizo ni ubora wa kazi zenu haziko katika kiwango kinachotakiwa? Au mnahitaji tu umaarufu ndani ya jamii? Serikali yetu imeanza kuchukua hatua ya kuwasaidieni? Maswali ni mengi ambayo yakipata ufumbuzi uzito wa kazi zenu utalingana na malipo yenu.
Nina fahamu safari ni hatua, nawapongeza sana wasania wa muziki ambao wamefanikiwa kuanzisha bendi zao , Banana Zoro, TID, Lady Jay Dee na wengine wengi na wanafanya vizuri kimuziki na kimaisha swali langu la msingi wamefanikiwaje kufika hapo walipo fika? vipi, je wanaweza kuwaeleza wenzao siri ya mafanikio na kuwapa mwongozo? Hongera sana endelea kupambana ukifahamu kuwa hakuna mafanikio yasiyokosa matatiozo kama alivyosema mtaalamu Napoleon Hill “No man ever achieved worthwhile success who did not, at one time or other, find himself with at least one foot hanging well over the brink of failure”
Ray
Kwa upande wa wasanii wa filamu nawapongeza wale wote ambao wamejitahidi kufungua studio zao ili kujikwamua kimapato wasanii kama Kanumba, Pastor Myamba JB na wengine, hii ni hatua muhimu kwa maendeleo yenu, tunakila sababu ya kuwapongeza, hatua ya pili ni kujaribu kushirikiana na wasanii wengine waanze kuleta kazi zao kwenu nanyi msio wachoyo wa mwongozo wa kuwasaidia nao kuweza kujinasua kimaisha. Hongera Ray Kigosi kwa safari yako yenye mafanikio huko Singapore kwa ajili ya kuhimarisha utawi wa kazi zako na za wengine.
.
Pastor Myamba
Inasikitisha sana wakati Sisi tunaburudika na ubunifu wenu, tunafarajika na kazi zenu tunaondoa stress zetu, performance/uwajibikaji wetu unapanda na tunapandishwa vyeo makazini na kadhalika. Wakati katika upande wa pili wa shilingi wasanii wetu mnafaidika kidogo sana na mnaridhika kwa kiasi kidogo mnachokipata na kujikita zaidi katika starehe. Ni vyema kama mtaweza kubadilika na kwani pengine katika miaka 10 uwezo wenu utakuwa umeshuka na umaarufuuaanza kupotea suluhu ni kujiimarisha kwa kujiandaa kuanzia sasa. Tukumbuke Age is very important in the entertainment industry. Rajendra Prasad
Important quotes:
1. The big secret in life is that there is no big secret. Whatever your goal, you can get there if you're willing to work. Oprah
The key to realizing a dream is to focus not on success but significance - and then even the small steps and little victories along your path will take on greater meaning. Oprah
3. Good people are good because they've come to wisdom through failure. We get very little wisdom from success, you know. - William Saroyan
4. For everyone of us that succeeds, it's because there's somebody there to show you the way out. The light doesn't always necessarily have to be in your family; for me it was teachers and school. Oprah
No comments:
Post a Comment