WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 28, 2010

Dr. JOHN POMBE MAGUFULI NA WIZARA MUHIMU KATIKA MAENDELEO YA TANZANIA.






Mhehimiwa Raisi  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika siku chache zilizopita alimchagua Mbunge wa Chato (CCM) mheshimiwa Dr. John P. Magufuli kushika wizara muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. Dr Magufuli ni miongoni mwa mawaziri wa muda mrefu kuanzia wakati wa awamu ya tatu katka nafasi mbalimbali kabla ya kuwa waziri kamili;

Dr Magufuli mwansiasa na msomi aliyebobea katika siasa na uongozi, anao uzoefu wa kutosha katika shughuli za serikali; lakini kubwa kupita yote ni mchapakazi wa kuigiwa mfano, ni kiongozi ambaye hakati tamaa, ni mkweli kwa nchi yake, mwajibikaji, na ni msimamizi mzuri wa wizara yake, ni hodari vile vile kwa kuwawajibisha watendaji walio chini yake katika kutekeleza majukumu ya  serikali.

Mimi ninamwita kiongozi wa namna hii kuwa ni mzalendo ambaye anaitakia mema nchi yake, ana mapenzi na nchi yake, yuko tayari kuifia nchi yake, na ni mkweli kwa nchi yake. Mara nyingi kiongozi wa aina sio mwoga sio mwoga na anafanya maamuzi yake kwa kuwa na facts; na yuko tayari kusimamia utekelezaji wa uamuzi wake kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa anatekeleza wajibu wake kwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa na nchi (serikali) ambaye yeye ni mwajiri wake au kwa taratibu ambazo zimewekwa na chama chake (sera) kwa manufaa ya nchi.
Dr. Magufuli ni shupavu wa kusimamia maamuzi ya serikali yake bila kumwonea aibu kiongozi mwingine yeyote ambaye atataka kufanya tofauti hali halisi ndani ya mamlaka ambayo amekabidhiwa.

Je wizara hii Mpya ina maana gani kwetu? Dr. Magufuli anamchango gani kwa wananchi?

Katika vigezo kadhaa vya maendeleo ya nchi hutegemea sana ukuaji wa uchumi, na kukua kwa uchumi kunategemea vitu vingi ambavyo hurandana: mawasiliano ya barabara na anga ni kati ya vipao mbele muhimu sana vya maendeleo. Kwa mfano mawasiliano kama barabara hustawisha afya,ustawi wa jamii,ukuaji wa uchumi utokanao na mazao, ukuaji wa uchumi utakanao na fedha za kigeni viwanja vya ndege, ni muhimu kwa maendeleo  ya taifa kwa ujumla. tunahitaji  barabara nzuri  na imara kwa mawasiliano (connectivity) na viwanja  vya ndege  vya kisasa kwa kuongeza pata la taifa( Fedha za Kigeni) ni vitu muhimu kwa kukuza uchumi;

Ili kufanikisha maendeleo ya nchi yetu tunahitaji kiongozi kama Dr. Magufuli, mkweli, mwadilifu, machapa kazi, asiyetetereka kisera na kiusimamizi na ambaye yuko tayari kupambana na ushindani kwa hoja au kwa matendo na zaidi hasa anayo elimu na uzoefu wa kutosha: na isitoshe Dr Magufuli anafanya kazi na kiongozi mwingine mahili kama Naibu waziri wake Dr. H. Mwakyembe; kiongozi ambaye ni mkweli na ni mwadilifu kama Bosi wake. kwa mantiki hii wizara hii imekamilika na tunatarajia mambo makubwa sana ya kiwango cha juu.

Hongera Dr. John Pombe Magufuli tunasubiri mwendelezo wa uwajibikaji na mabadiliko makubwa ya sura za barabara zetu na viwanja vyetu vya ndege na kadhalika

Friday, November 26, 2010

WHAT IS CHEMISTRY?

CHEMISTRY IS EVERYWHERE!
God kept chemistry above
               Wondering till when found,
Be used and known all around.

Making of harmful things was now the deal,
           Making money out of dangerous mix,
And people use chemistry to get what they want.

Christians with faith came in between,
               Saying that it`s God we are dealing with,
With handle and care they made beautiful things,
              And let the world know that chemistry is within.

                                         God revealed it for us to make use of it!

Rose turuka!

Thursday, November 25, 2010

NINI MWELEKEO WA WASANII WA TANZANIA KATIKA KUENDELEZA MAISHA YAO?

                                                                       Kanumba


Sanaa ni taaluma ambayo ni muhimu sana katika ukuaji wa maisha yate  binadamu. Wasanii ni nguzo muhimu katika kudumisha na kupeleka ujumbe kwa njia mbalimbali. Sanaa na wasanii  ni dhana ya ushirikishwaji ambayo inatuondoa katika utaratibu wetu wa maisha ya kila siku iwe katika biashara ,  uongozi  na kazi zingine za kila siku ambazo zinatulazimu kutumia akili zetu:

Kama tunavyofahamu katika utaratibu wa kazi akili zetu hufanya kazi sana na zinahitaji uwepo wa kitu mbadala ambacho kitasaidia kuipumzisha, na kwa akili kupumzika kutoka katika uwigo wa watu wanaoluzunguka kwa masaa nane; matumizi ya teknolojia ambayo huitaji umakini kubwa, kutokuwa na uhakika wa kazi kutokana na kuyumba kwa uchumi, tunahitaji kitulizo burudani ambayo ni sahihi; wengi tunaishia kusikiliza na kucheza muziki, kuangalia movies, pengine kwenda camping na kadhalika. Kwa kweli burudani hutupa mapumziko kwa ustawi wa maisha yetu. Bila sanaa maisha yetu yangefanana na usemi huu “all work and no play make Jack a dully Boy”



Kwa upande mwingine Sanaa wasanii na burudani ni kioo cha jamii, kwani huelimisha, huonya, hufundisha na kutuliwaza kama itatumika katika misingi ya kuonyesha ukweli na uhalisia wa maisha yetu wasanii na sanaa zao zitatufanya tucheke, tubadilishane mawzo, zitachangamsha akili zetu na kutuondoa na unyonge unaotokana na akili na mwili kuchoka;

Mathalani kwa ufupi ukiangalia kazi kama ya Msanii Afande Sele (Darubini Kali), au kazi ya Prof. J na MwaFa “ Jukumu Letu” au kazi za wasanii wa Filamu kama Kanumba Ray Kigosi, Pastor Emmanuel Myamba; Johari au Aunt Ezekiel, JB, Irene Uwoya, Lady Jay Dee; Chopa; Bishanga; Hadija Kopa bi Kidude, Ali Kiba  na wengine wote; kwa kweli “we are proud of you”  tunajivunia uwezo wenu na faraja ambayo tunaipata.







Tatizo langu kubwa ni hili kwenu wasanii wa Kitanzania?

Je nyinyi kama wasanii mmenjiandaaje kuyakabili maisha yenu wenyewe?
Je pamoja na kufanya kazi kwa bidii ya ubunifu wa mawazo, utungaji wa nyimbo muda mnaotumia, kazi zenu zinalingana na mapato? Najua jibu ni hapana sasa tuanzie wapi? Tuanzie kwa wanunuaji wa haki za kazi zenu? Au ni tatizo ka ushawishi wa kibiashara na soko kubwa la wahindi ambao wanamiliki kazi zenu, kwa vile wanafahamu kuwa mna njaa wanawalalia kwa malipo? Au tatizo ni ubora wa kazi zenu haziko katika kiwango kinachotakiwa? Au mnahitaji tu umaarufu ndani ya jamii? Serikali yetu imeanza kuchukua hatua ya kuwasaidieni? Maswali ni mengi ambayo yakipata ufumbuzi uzito wa kazi zenu utalingana na malipo yenu.

Nina fahamu safari ni hatua, nawapongeza sana wasania wa muziki ambao wamefanikiwa kuanzisha bendi zao , Banana Zoro, TID, Lady Jay Dee  na wengine wengi na wanafanya vizuri kimuziki na kimaisha swali langu la msingi wamefanikiwaje kufika hapo walipo fika?  vipi, je wanaweza kuwaeleza wenzao siri ya mafanikio na  kuwapa mwongozo? Hongera sana endelea kupambana ukifahamu kuwa hakuna mafanikio yasiyokosa matatiozo kama alivyosema mtaalamu Napoleon Hill  “No man ever achieved worthwhile success who did not, at one time or other, find himself with at least one foot hanging well over the brink of failure” 




                                                                Ray
Kwa upande wa wasanii wa filamu nawapongeza wale wote ambao wamejitahidi kufungua studio zao ili kujikwamua kimapato wasanii kama Kanumba, Pastor Myamba JB na wengine,  hii ni hatua muhimu kwa maendeleo yenu, tunakila sababu ya kuwapongeza, hatua ya pili ni kujaribu kushirikiana na wasanii wengine waanze kuleta kazi zao kwenu nanyi msio wachoyo wa mwongozo wa kuwasaidia  nao kuweza kujinasua kimaisha. Hongera Ray Kigosi kwa safari yako yenye mafanikio huko Singapore kwa ajili ya kuhimarisha utawi wa kazi zako na za wengine. 

.



                                                            Pastor Myamba

Inasikitisha sana wakati Sisi tunaburudika na ubunifu wenu, tunafarajika na kazi zenu tunaondoa stress zetu, performance/uwajibikaji wetu unapanda na tunapandishwa vyeo makazini na kadhalika. Wakati katika upande wa pili wa shilingi wasanii wetu mnafaidika kidogo sana na mnaridhika kwa kiasi kidogo mnachokipata na kujikita zaidi katika starehe. Ni vyema kama mtaweza kubadilika na kwani pengine  katika miaka 10 uwezo wenu utakuwa umeshuka na umaarufuuaanza kupotea suluhu ni kujiimarisha kwa kujiandaa kuanzia sasa. Tukumbuke Age is very important in the entertainment industry. Rajendra Prasad

Important quotes:

1.      The big secret in life is that there is no big secret. Whatever your goal, you can get there if you're willing to work. Oprah


The key to realizing a dream is to focus not on success but significance - and then even the small steps and little victories along your path will take on greater meaning. Oprah



3.      Good people are good because they've come to wisdom through failure. We get very little wisdom from success, you know. - William Saroyan

4.      For everyone of us that succeeds, it's because there's somebody there to show you the way out. The light doesn't always necessarily have to be in your family; for me it was teachers and school. Oprah






Wednesday, November 24, 2010

JE NCHI YETU NZURI SANA "TANZANIA" INAYO DEMOKRASIA YA KWELI?

                                                            


Kulingana na tafsiri nyingi za neno democrasia inahusisha zaidi ushirikishwaji ( uwakilishi) wa wananchi katika maamuzi yao ya maendeleo kwa kukabidhi majukumu kwa serikali iliyochaguliwa na watu/wananchi; kwa tafsiri ya haraka demokrasia ni utawala wa watu, unaofanywa na watu kwa manufaa ya watu.
Mara nyingi tumesikia viongozi wetu wakituambia kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia kwa  msingi huu kwamba kuna mfumo wa vyama vingi ambao unatoa fursa ya kuchagua viongozi kila baadaya miaka mitano na kuweza kuunda serikali ambayo itawasidia wananchi katika kujiletea maendeleo yao.
Lakini ikumbukwe kuwa demokrasia sio mfumo ambao unajiendesha wenyewe, unaendeshwa na watu kulingana na mazingira ya mahali, uwezo wa kimaendeleo ni kipimo kizuri sana cha demokrasia. Kwa msingi huu ni rahisi kabisa kwa wale ambao wamepata dhaman ya kuendesha nchi kuibadilisha kulingana na matakwa yoa kwa mgongo wa wanachi.
Tujipime kwa maswali haya machache ili tuweze kujua kama nchi yetu in demokrasia ya kweli:
1.      Ni kweli kuwa wawakilishi ambao tunawachagua kupitia vyama vyao wanawakilisha mawazo yetu au wana wakilisha mawazo ya chama kichowapitisha kugombea nafasi hizo?

2.      Je viongozi wetu wa juu kabisa wa serikali wakisha chaguliwa na wanannchi kuongoza nchi wanawatumikia nani wanannchi walala hoi au wafanyabishara wakumwa ikiwa ni sehemu ya kulipa fadhili na kuwafurahisha baada ya wao kutumia pesa zao kuwasaidia kupata uongozi (paymasters) na kuto wajali wananchi ambo ni sehemu kubwa ya demokrasia?

3.      Ni Kweli tunapiga kura kwa uhalisia wa kuwapata wawakilishi wa kutusaidia kuondoa kero za maisha yetu au tunapiga kura kwa ushabiki na kununuliwa tu?

4.      Je tuna uhuru wa kujieleza na kusikilizwa na viongozi tulio wachagua?

5.      Je tunauhuru wa kuwachagua wawakilishi tuwapendao kupitia utaratibu wowote ule uliowekwa na chama au inatubidi kuwapigia kura wale wawakilishi ambao wamechaguliwa na uongozi wa juu was chama husika?

6.       Je tunaweza kuikosoa serikali yetu na tukasikilizwa bila kutishwa?

7.      Je demokrasia yetu imetawalia na pesa au maoni na matakwa ya kweli ya wanaichi?
8.      Je serikali inatoa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa wanaichi kujua nini maana ya democrasia?

9.      Je tunaouvumilivu wa kutosha wa kisiasa hata pale tunaposhindwa kupata nafasi za uongozi wanchi  na kuwa na busara ya kutafuta njia mbadala ambayo itakuza demokrasia?

10.  Je vyama vilivyo katika kushiriki ushindani wa kisiasa vinapata nafasi sawa na vyama vile ambavyo vimejiimarisha kwa muda mrefu na vina nguvu na  uwezo mkubwa wa kipesa, ukilinganisha na vyama ambavyo bado ni vichanga na havina pesa ya kujitangaza?
Kama zaidi yanusu ya  majibu ya maswali haya yataonyesha positive basi tuna elekea kwenye demokrasia ya kweli ikumbukwe kuwa demokrasia ya kweli ni process ambayo itachukua muda mrefu kuimarika sio kitu cha mara moja. Na hii itafanikiwa tu kama level yetu ya uchumi, uvumilivu wa kisiasa,  uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji utayari wa kurekebisha  katiba  iliyoko ili iwe a true living organism hii inaweza kuharakisha democrasia yetu.
"If a door is shut, attempts should be made to open it; if it is ajar, it should be pushed until it is wide open. In neither case should the door be blown up at the expense of those inside."
Julius Kambarage Nyerere, from his Stability and Change in Africa speech given to the University of Toronto, Canada, 2 October 1969.
“It has been said that has been said that democracy is the worst form of government except all the others that have been tried”. 
Winston Churchill 
“Without God, democracy will not and cannot long endure”. 
Ronald Reagan 
“Democracy cannot succeed unless those who express their choice are prepared to choose wisely. The real safeguard of democracy, therefore, is education”. 
Franklin D. Roosevelt 

“Let us never forget that government is ourselves and not an alien power over us. The ultimate rulers of our democracy are not a President and senators and congressmen and government officials, but the voters of this country”. 
Franklin D. Roosevelt 

Tuesday, November 23, 2010

SALAMU ZA PONGEZI KWA SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMA ANNA MAKINDA


Mheshimiwa Anna Makinda amechaguliwa kuliongoza Bunge la  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha Mapinduzi; kwa maneno MENGINE mheshimiwa Anna Makinda ni SPIKA wetu na hilo halina ubishi kwani amechaguliwa kulingana na taratibu na kanuni ya Katiba yetu.
Nachukua fursa hii kukupngeza kwa ushindi huu, mimi siangalii uwingi wa kura ambazo zilikupa ushindi mimi nataka kuangalia wajibu wako kama Spika utakuwa ni upi na utalisaidiaje taifa hili ambalo lina makundi mawili ya watu:

Kundi la kwanza ni lile ambalo linaishi katika maisha bora na ya uhakika hawa ni matajiri (Privileged) na kundi nyingine ambalo ni kubwa katika nchi yetu ni WALALA HOI MASIKINI ambao hawaijui hata kesho yao itakuwaje wamezungukwa na umasikini uliokidhiri na hao ndio wengi (underprivileged). Cha ajabu hawa ndio waliokuchagua wewe Mheshimiwa “Spika”. Swali la msingi je kundi hili linakugusa vipi wewe katika utendaji wako wa kazi? Utalisadiaje katika kipindi chako cha uongozi?

Wewe umefanikiwa kuwa Spika wa kwanza mwanamke katika historia ya Jamuhuri wa  Tanzania, na kikubwa zaidi katika tafsiri nyingi za wataalamu Mwanamke ni muhimiri mkubwa sana wa maendeleo katika ngazi yeyote ile kama akipatiwa nafasi na akiaminiwa; katika kila jambo nzuri la maendeleo ukiangalia nyuma yake kuna msukumo wa mwamamke;

Wengi wetu tumekulia vijijini na kwenda shule ambazo zilikuwa katika umbali mkubwa, je bado tunakumbuka jinsi wazazi wetu walivyotusaidia hasa MAMA zetu? walikuwa wakiamka alfajiri  kutuandalia chakula cha kubeba shule, na kutusindikiza hata kama ni hatua kumi na kututakia masomo mema pengine wakati huo huo Baba alikuwa amelala na hajui hata kama ana wajibu wa kusaidiaana na Mama katika kufanikisha adhima ya elimu ya mtoto wao. Mimi binafsi Siwezi sahau hii "loving  commitment" ambayo imejengwa katika mioyo ya akina mama.

Mheshimiwa Spika Je tutarajie hii loving commitment amabyo umejaliwa na Mwenyezi Mungu toka kwako katika kulisaidia hili kundi la underprivileged (walalahoi masikini)? Au kwa vile uko Kileleni tusikuhesabu tena kuwa si Mwenzetu hutaweza tena kuhimili vishindo kutoka upande wa privileged (matajiri) ambao ndio wanao tumia uwezo wao kuongoza shughuli za serikali na kukuongoza wewe nini ufanye?

Ninafahamu fika kuwa unayo elimu (knowledge) na uzoefu wa kutosha (experience) kwa kuliongoza Bunge letu Tukufu. Jukumu ambalo unalo ni sawa na kuendesha gari katika makutano ya barabara inahitaji uelewa wa kutosha kuhusu kuyajua magari mengine yanaelekea wapi; lakini kwa kurahisisha uendeshaji na kuepusha ajali zitokanazo na uzembe na kutokuwa na subira hutumika taa za kuongozea magari ambazo hufanya kazi kwa usahihi mkubwa.

Na shughuli za Bunge nazo zinahitaji umakini mkubwa zaidi ya taa ya kuongozea magari. Sio sehemu ya majaribio ya uongozi (trial and error). Kwa misingi misingi hiyo Chama chako kimekuchagua kikijua kuwa una siza za utendaji na sio majaribio:
Kwa msingi huu itapendeza sana kwa jamii ya watanzania kama utakuwa:
  • Spika ambaye utaaminiwa na kutegemewa wa watu wote
  • Spika ambaye utaweza kujichanganya na tayari kujifunza kutoka kwa wengine ( ndani ya chama chako na Nje ya chama chako (wapinzani)
  • Spika ambaye utaweza kutumia elimu yako na uzoefu katika katabiri usahihi wa majadiliano yatakayo iletea tija mbadala  Taifa letu kwa ustawi wa watu wake na demokrasia yake.
  • Kutoa uamuzi ambao utakuwa unafuata kanuni za uendeshaji wa Bunge bila upendeleo au kuwafurahisha wachache,
  • Kufanya maamuzi mazito kwa faida ya wengi ambao ni masikini bila kujali kuwa unapoteza umaarufu ndani ya chama chako au vyama vya upinzani.

Yakumbuke sana maneno haya:God grant me the serenity to accept the things I cannot change; courage to change the things I can; and wisdom to know the difference”.

Nakupongeza sana kwa kuchaguliwa, Mwenyezi Mungu akujalie Afya njema na Busara katika kutenda kazi yako kwa uadilifu, upendo na kwa Kumwogopa Muumba wako ili kujijengea uadilifu AMIN

“A warrior must learn to make every act count, since he is going to be here in this world for only a short while, in fact, too short for witnessing all the marvels of it.” By Carlos Castaneda  


“The challenges of change are always hard. It is important that we begin to unpack those challenges that confront this nation and realize that we each have a role that requires us to change and become more responsible for shaping our own future”. By Hillary Rodham Clinton