Mheshimiwa
Majaliwa Kassim Majaliwa ni waziri mkuu wa
awamu ya Tano ambaye anaendana na kasi ya utendaji wa kazi wa Rais wa awamu ya
tano Mheshimiwa Dr. Magufuli katika kurudisha uwajibikaji na matumizi mazuri ya
fedha za watanzania katika idara za serikali na mashirika ya
umma.
Katika
hiki kipindi kifupi akiwa kama waziri mkuu ameweza kuonyesha nia dhabiti ya
kuwatumikia watanzania wanyonge ambao kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa masikini
katika taifa lao ambalo lina utajiri mkubwa ambao ulikuwa ukiishia amikanoni
mwa wachache.
Ameanza
kazi kwa kutembelea au kufanya ziara za ghafla katika idara nyeti za serikali
ambazo ni nguvu ya uchumi wa Taifa na daraja pekee katika kuondoa umasikini wa
watanzania wanyonge . kauli ya ambayo alitoa hivi karibuni kuwa amekuja tu
kujifunza bila kuhitaji maelezo zaidi ilikuwa ni nzito ambayo kwa kweli
watendaji wa serikali na idara zake wanatakiwa kuizingatia na kuwa tayari
kuwajibika mara moja.
Mheshimiwa Majaliwa ameonyesha ujasiri wake wa
kujifunza nini kinaendelea katika utendaji wa watumishi wa serikali na uma na
tayari ameanza kuyapa mgongo mazoea ya kale. Kwa mhesjimiwa majaliwa ambaye hakuwa maarufu
sana katika siasa za Tanzania sasa kwa kushirikiana na mhemishimiwa Rais
Magufuli kwa pamoja wameamua kuhakikisha wanabadilisha mifumo ambayo ilikuwa
inawanyima watanzania kaktika kuyafikia maendeleo kammili, Lengo kubwa la
serikali ya tano chini ya Rais, Magufui, Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan na
Waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ni kuona kuwa wanabadilisha mifumo yote
mibovu ili kuifanya Tanzmi kuifanya inakuwa
bora zaidi kwenye masuala ya uchumi, utawala na maisha ya watanzania masikini.
Waziri Mkuu kwa kushirikia na Uongozi wa awamu ya Tano
chini ya Rais John Magufuli wana kila nafasi sasa ya kuandika historia kwa
kutumia kauli mbio ya hapa kazi tu na kuhakikisha wanabadilisha mifumo yote
mibovu ya kuendesha nchi kwa fiada ya watanzania
Tukubali kuwa Tanzania ya leo inaweza kuwa tofauti
sana na ya jana, na ya kesho ikawashangaza hata watu wa dunia. Kama Mheshimiwa Majaliwa katika nafasi yake
ataweza kuhakikisha kuwa anajenga mfumo ambao, hata kama yeye hatakuwepo
madarakani, bado Tanzania na Watanzania watafuata na kuheshimu mifumo mipya
itakayowekwa. Ndio maana kauli yake “ nimekuja kujifunza tu ni muhimu sana kwa
taifa hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko. Kwa nchi kama ya kwetu, lililo
muhimu kwenye mifumo ni kwa wenye kukiuka sheria, kanuni na taratibu
zitakazowekwa kuadhibiwa, punde tu wanapokosea.
Je Mheshimiwa Majaliwa amejifunza nini? Na atakuja na
somo gani au fundisho gani kwa hao aliowatembelea? Je ataweka mifumo mipya,
yenye kutanguliza maslahi ya nchi na si ya watendaji binafsi ambao wameamua
kutumia pesa katika kujilipa wao wenyewe? Je hili litakuwa anguko jingine kwa
watendaji wabovu ambao wanajali sana masilahi yao na sio ya taifa?,
Kama wengi ambavyo wameseama kuwa kitendo
chochote cha kupunguza matumizi yasiyo na lazima, na kutumia fedha kwa ajili ya
maendeleo ya Watanzania lazima kiungwe mkono kwa hali na mali. Waziri Mkuu
Majaliwa anastahili sifa kwa hilo na tumwombee Mungu amlinde ampe nguvu na
aweze kutuletea mabadiliko ya kweli.
Kwangu mimi leo kauli ya
“nimekuja kujifunza” ina maana kubwa sana sisi kama taifa tunao wajibu wa
kujikomboa kimawazo ili tuweze kufikiri sisi wenyewe, katika kuyapa thamani maamuzi
yetu ya utendaji badala ya kusubiri ziara za ghafla za viongozi wetu ili
watufundishe jinsi ya kutumia nyazifa zetu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Haiingia
akili kwa watendaji wa mashirika ya umma pamoja na bozi zake kutumia pesa
nyingi ili walipane mishahara na malupulupu binafsi na kuliona shirika
linaendelea kudidimia na wafanyakaza na likishindwa kujiendesha. Tuwe na vichwa
timamu vya kutuwezesha kuyatafakari masuala sisi wenyewe. Tunapaswa tujijengee
huu msingi ili tuweze kuitathmini dhana ya maendeleo, tuweze kujiuliza
maendeleo ni nini?
Katika kufanya hivyo, tunapaswa
kuchukua jukumu na wajibu wa kujitungia vigezo vyetu na kuvitumia. Lazima
tujenge utashi wa kujiamini na kujiamulia mambo yetu wenyewe kwa manufaa ya taifa letu.
Ni uongo kudhani kuwa hakuna nchi ambayo imesimama tu na haibadiliki.
Kosa tunalofanya ni kutozingtia ukweli huo na badala yake kuziona nchi za Ulaya
na Marekani kama nchi zilizoendelea na sisi kutumia rasilimali zetu vibaya
tukiendelea kusaidiwa na nchi hizo kama sisi ni mataira wa kufikira na hatujui kutenda
kazi ipasavyo isipookuwa ni kufikira kuiba tu . Kwa mtindo tulio nao sasa tutabaki
na hii dhana ya kujidunisha, na watu wetu kuendelea kuwa masikini miaka yote. Kwa
kweli tunatakiwa Kujifunza ili tuweze badilisha huu msimamo tegemezi.
Mheshimiwa Majaliwa
anatuonyesha kuwa tuna takiwakuwajibika kujikomboa kifikra, tuweze kujiwekea
vigezo vyetu wenyewe. Pasipo kuwa na vigezo vinavyozingatia haki ya uwajibikaji. Uadilifu na kumwogopa Mungu dhana
ya mabadiliko na maendeleo itaendelea kuwa ndoto. Asante awamu ya Tano sasa mmeanza
kutoondolea dhana hii. Inatubidi
tubadili fikra; tukatae huu mkondo uliopo sasa wa kuitwa au kujiita sisi ni
masikini wakati watu wachache ambao wamepata nafasi serikalini katika mashirika
ya umma kwa sababu zao binafsi wanarudisha maendeleo yetu nyuma.
Dhana ya Maendeleo ni
mabadiliko katika kitu au hali yoyote, katika nyanja mbali mbali za maisha,
mabadiliko ya manufaa kwa mujibu wa mazingira husika. Katika jamii au nchi,
maendeleo yanaboresha maisha ya binadamu, yanahifadhi au kuboresha mazingira,
na yanaendana na heshima, utu, na haki. Maendeleo yanatokana na msukumo wa
jamii au nchi husika, kwa mujibu wa mahitaji yake halisi, na kwa mujibu wa
maamuzi na matakwa ya jamii hiyo, maamuzi yatokanayo na fikra huru na tambuzi,
zenye mwelekeo wauwajibikaji na uadilifu. Maendeleo hayatakiwi yalete matabaka
miongoni watanzania.
KWA KWELI NIMEKUJA KUJIFUNZA mimi imenifundisha kuwa tukitaka kufanikiwa katika hii safari ya
kuondoa umasikini wa Taifa letu tunatakiwa kuendelea kuitekeleza kauli mbiu ya
Ya Hapa Kazi Tu kwa vitendo katiaka kujiletea maendeleo yetu na sisi kama wazalendo wa taifa
hili lazima kwa umoja wetu tusiwaonee haya mafisadi, wla rushwa wazembe katika kusukuma
gurudumu la nchi yetu mbele , na tuondoe dhana ya kungojea misaada kutoka nchi
za nje hii haiwezi kusaidia maendeleo bali inatufanya tuendelee kuwa tegemezi
zaidi .
Tunaona mfano wa nchi
kama CUBA ile haifuati njia za uchumi kama nchi nyingi duniani ina uchumi wake
unaokuwa kila siku , angalia uchina na mipango yao na mao ni serikali ya
kikomunisti ndio lakini walikuwa na malengo ikazaa mikakati hii tunayoiona sasa
hivi ni dira ya china na kufikia mwaka 2030 iwe super power; au tuangalie nini
walifanya south Korea iaka ile ya 1960s.
Kwahiyo tuwekeze katika rasilimali ambayo tunajua inaweza kututoa hapa
tulipo kwenda hatua mbili au 3 zaidi mbele bila kutegemea msaada kutoka nje. ,
Tunaweza kuendeleza
mawazo ma-pya, na kuyakusanya, kuyachuja, kuyaangalia na kuyaunganisha. Hivyo,
maendeleo ni hatua ambayo husonga mbele na yenye mabadiliko. Maendeleo
yanajumu-isha utendaji ufuatao malengo. Viongozi
wetu wengi wanajiona wao pekee ndio wenye wajibu wa kufaidi utajiri wa
nchiyetu, kupitia hulka zao za RUSHWA NA UFISADI.
Sisi kama wananchi
wazalendo wa taifa letu tuko tayari kushirikiana na viongozi wa awamu ya tano
katika kuyachoma magugu ambayo mengine yalikuwa yameota sugu na kuwa msitu
mkubwa ambao umekuwa tishio kwa wachomaji na walulima ambao wako tayari
kulisafisha pori hili. Tumeamua kuwaunga Mkono Mheshimiwa Dr. Magufuli Rais
wetu na Mama Samia Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Majaliwa msitoke jasho peke
yenu katika kufyeka msitu huu. Nasi tjuko tayari kutoa ili shamba letu liweze
kutoa mazao bora na sio tene kuitwa shamb la BiBi. Tunafahamu kuwa Shamba la
Bibi ni letu sote kila mtu anamchango wa kulifanya listawi na kutoa mazao bora
kwa faida ya wajukuu na watoto wote wa Bibi.
Kwa kweli nimekuja
kujifunza na kugundua kuwa UFISADI NA RUSHWA unatengeneza kikundi cha watu...wenye kusimamia
maslahi yao kwa faida yao UFISADI NA RUSHWA Inaunda uwepo wa vikundi visivyo rasimi
kisheria kwa ajili ya kupinga/kuzuia/kufanya lobbing na kufanikisha mambo
ambayo wao walio kwenye kundi husika Watafaidika nayo;
UFISADI NA RUSHWA Inapanua wigo wa Rushwa kwenye jamii na kufanya baadhi ya watu
kwenye jami wasiweze kuguswa na sheria kwa sababu ya uwezo wao kwenye fedha. UFISADI
NA RUSHWA Inaleta usumbufu kwenye
utendaji wa Serikali kwa kuwa baadhi ya raia wanakuwa na nguvu ya fedha hivyo
umma wa raia wa kawaida unatengeneza hofu ya kuogopa watu wao wenye ukwasi.
UFISADI NA RUSHWA Inavunja na kuharibu mfumo wa HAKI kwa kuwa wenye UKWASI huo wa
kifisadi wanatumia ukwasi huo kuvulugu HAKI inapotafutwa. UFISADI
NA RUSHWA Uzalisha kiburi/Jeuri
za watu wenye ukwasi dhidi ya Watumishi wa Umma na kuwafanya waonekane si kitu
mbele ya sura za jamii UFISADI NA RUSHWA Uchochea kwa kasi kubwa ongezeko la kukosekana
kwa maadili ya umma na maadili ya Viongozi wa umma.Hivyo kuongeza mpasuko wa
kuwa Taifa lina mmomonyoko wa maadili.
UFISADI NA RUSHWA Usababisha woga wa kitaifa hata uwezo wa kitaifa kukemea mambo
yasiyostahiki utegemea ujasili wa mkemeaji. UFISADI NA RUSHWA Pia utengeneza ushawishi wa wageni kuona sehemu
za kupenyeza mambo yao kwa kuwa utafuta milango ya kuingia kwa namna ambayo wao
wanaona kuna njia ama upenyo. UFISADI NA RUSHWA Uchafua pia mfumo wa uendeshaji wa siasa na
Serikali kwa kujalibu kuweka mapandikizi yake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA KATIKA AWAMU HII YA TANO HAPA KAZI TU
No comments:
Post a Comment