Swali la msingi ambalo najiuliza sana hivi sasa hii dhana ya
utumbuaji wa majipu ambao umelipatia sana hasara taifa letu asili yake wapi na
kwa nini tumefikia hapa ambapo tumefika leo hii kama taifa tukiwa tumepoteza
mapato mengi sana ya taifa kwa muda mrefu na taifa kukosa mwelekeo.
Jambo la msingi ambalo halipingiki ni kuwa viongozi wa taifa letu
ambao walipewa dhamana ya kutuongoza walikuwa wakitekeleza dhana ya uongozi
bora kwa tafsiri binafsi. Dhana ya uongozi inatakiwa ianzie wapi?
Dhana ya uongozi wa namna yeyote ile unafaa uanzie nyumbani kwa
kila mtu uongozi ni uwezo wa kuweza kuyakabili kwanza matatizo yako mwenyewe na kufanya maamuzi sahihi bila
kushawishiwa na mtu mwingine yeyote yule.
kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kuyatawala maisha yako
kulingana utaratibu ambao wewe mwenyewe umejiwekea kuanzia ndani ya familia
yako; ukifanikiwa hili unakuwa umefaulu katika mtihani huu wa kwanza wa
uongozi ndipo jamii inapoanza kukuona kuwa hata ukipata nafasi ya
kuwaongoza wao pia utaweza kufanya maamuzi sahihi.
Kwa maneno mengine ni uwezo au njia ya kuweza kuwashawishi
watu ili waweze kufanya kitu au kufikia lengo fulani la kikundi kwa ridhaa yao
wenyewe. ili uongozi uwe bora ni lazima kuwe na kiongozi anayeongoza kundi
fulani la watu au jamii husika kwa usahihi na kufuata maaadili ya uongozi yanayozingatia
uaminifu, ukweli na uadilifu.
Katika kila jamii kuna umuhimu wa kuwa na kiongozi kunatokana na
ukweli kwamba watu wanapaswa kuwa na namna ya kuunganisha nguvu zao ili kufikia
malengo yao. Katika kila jamii, ni lazima kuwepo na mikakati ya
kuunganisha nguvu, vipaji, uwezo na stadi mbalimbali za wana jamii.
Wajibu wa msingi wa kiongozi yoyote ni kusaidia kuunganisha uwezo
wa watu, kuratibu, kusimamia shughuli za watu, na kila inapobidi aonyeshe njia
itakayosaidia kufikia lengo. Hii ndio dhana ya serikali ya awamu ya tano chini
ya Dr. John Magufuli ambaye ameonyesha utayari wa kufanya kazi na viongozi
ambao wataonyesha uadilifu katika kazi zao za kuwatumikia watanzania ili
kuwakwamua kutoka katika wimbi la
umasikini na kuwawajibisha viongozi wote wabadhilifu ambao wamehujumu uchumi wa
watanzania.
Kwa dhana ya Plato uongozi ni dhana au taaluma inayompa
muhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaoongozwa kuunganisha nguvu,
stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo ya Taifa lao ili
kujikwamua kutoka katika tabaka kandamizi ambalo linawasumbua. Kuongoza ni
kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi bora una mchango mkubwa sana katika uimara wa jamii.
Lakini tufahamu kuwa Ubora wa kiongozi unachangiwa na vitu vingi lakini
tusisahau kuwa vile vile uongozi au kiongozi bora hutoka kwa Mungu. Kama rais
wa awamu ya tano alivyowahi sema kuwa serikali yake ina kazi na dhamana nzito
wa kuwajengea uchumi wa kati jamii ya watanzania kwa kuelewa kuwa wakiwatendea watanzania ndivyo sivyo adhabu yao
itatoka pande mbili kwa Mungu na kwa jamii iliyowachagua.
Ikumbukwe kuwa viongozi wetu waelewe kuwa ni viongozi muhimu sana
ambao wataingia katika vitabu vya kumbukumbu ya Taifa hili kuhusu ubora au ubaya
kwa Taifa letu.
swali la kuwauliza Viongozi wetu wa awamu ya tano Je watendaji
wake watampa Kaisari yaliyo ya Kaisari ili kutimiza yale waliokuwa wamehaidi wakati
wa kampeni ili kubadilisha maisha ya watanzania?
Je Viongozi wa awamu ya Tano chini ya mwitikio wa Hapa Kazi Tu
chini ya DR. Magufuli wanafahamu ukubwa na umuhimu wa maamuzi yao
kwa jamii ya Tanzania?
Je viongozi wetu wa awamu ya tano wametawaliwa na maadili gani katika utendaji
wa kazi yaokuendesha serikali? Ni ukweli usio fichika kuwa ili waweze
kufanikiwa katika kutumiza maendeleo ya wananchi
ni lazima wazingatia maadili ya msingi ya
kufanikisha na kusimamia kwa weledi
mkubwa falfasa ya Mpe kaizari yaliyo ya kaizari hasa katika kipengele ya
ukusanyaji kodi ili kuimalisha mfuko wa serikali kwa maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Rais Dr Magufuli ameonyesha nia dhabiti katika
kutekeleza falfasa hii kwa kuanza kutumbua majipu na kupaisha makusanyo ya kodi
katika mwezi huu wa December 2015. Kama taifa tunafarijika kuwa timu nzima ya
serikali kwa nia nzuri sasa wanawajibika na kuwawajibisha wale wote ambao
walikuwa wanakwenda kinyume na falfasa hii ambayo Yesu aliwambia wafarisayo
kuhusu dhana ya kutoa kodi.
Tunaendelea kufarijika kila siku njisi watendaji wakuu wa serikali
wanavyowajibika sasa na kuruduisha imani kwa Watanzania masikini kuhusu
mabadiliko ya maisha yao na jamii nzima. Hivyo ni vyema waendelee kutimiza
wajibu badala ya kujali maslahi yao binafsi yatokanayo na itikadi au faida
ambayo wanafikiria wao tu watanufaika nayo na sio taifa;
Daima Rais wetu ameendelee kusisitiza kuwa Tanzania niyetu sote na
rasilimali ambazo tumejaliwa ni zetu sote na sio mali ya kikundi Fulani tu. Na ameendelea
kusisitiza kuwa anafafahamu wananchi
wanatamani nini; wanatamani watoto wao wapate elimu bora ndio maana sasa
serikali imerudisha tena elimu bure kwa watoto wetu;
Anajua watanzania wanataka umoja ndio maana anaendelea kuhubiri na kuwaomba wananchi kuendelea kudumisha amani iliyopo
katika pande zote mbili za jamuhuri ya Muungano;
Hebu tujikumbushe Busara za Baba wetu wa Taifa Mwalimu
Nyerere alipozungumzia dhana ya uongozi, Mwalimu Nyerere alisema, “uongozi ni
kuonyesha njia.” Kwa maana hiyo, viongozi shurti wafahamu vyema matokeo ya
uongozi wao. Wasome imani za wanaowaongoza na nyakati zilizopo ili kutambua
matumaini ya umma kimaisha.
VIONGOZI GANI TUNAWAHITAJI?
Amabao hawawezi jisahau wamepewa
dhamana ya kushika hatamu ya uongozi la
msingi hapa ni kuwa kiongozi amabye yuko tayari kuongoza na na ajuwe anabeba jukumu la kubadilisha hali za
watu kuwa nzuri. Atumie stadi za uongozi mwema kuonyesha njia. Mheshimiwa Dr.
Magufuli ameweza kulionyesha hili kuwa kiongozi ambaye anajali Taifa na sio
kukitumikia kikundi Fulani.
Wanaepuka kutumia stadi za
uongozi kusimamia haki za waliowa wafikisha hapo hasa wanyonge. Wajikumbushe
kuwa kupewa uongozi ni kuchukua ahadi ya kutenda kwa haki. Ukitaka kulitendea
haki jipu lazima ulikamue na ulikamue vizuri na kuhakikisha kuwa kiini kimetoka
ili kumpa nafuu mgonjwa. Ugonjwa ambao kama taifa tunao kwa sasa ni uchumi wetu
ambao hauendani na maisha ya wananishi wetu. Tunashkukuru majipu haya sasa
yanaendelea kutumbuliwa na mgojwa wetu uchumi anaendelea kuimarika.
Mwalimu Nyerere aliandika miongozo mizuri katika Azimio la Arusha
miongoni mwao akisema kwamba ili tuendelee tunahitaji Siasa Safi na
Uongozi Bora. Alitambua mchango wa mambo hayo katika maendeleo ya mwanadamu.
Kupitia siasa safi kila kitu cha kunufaisha wananchi hupatikana. Bali ni muhimu
viongozi wanaotarajiwa kufanikisha ustawi wa wanadamu, wapatikane kwa njia ya
haki. Watokane na ridhaa ya watu wenyewe wanaotaka kuongozwa. Na wakisha
chaguliwa anatende kazi kwa uadilifu na ustadi mkubwa. Waweze kukusimai uchumi
wetu kwa kuhakikisha kuwa yaliyo ya Kaizari anapewa Kaizari kwa faida ya Taifa
nzaima.
Watendaji wetu timizeni
wajibu wenu ili muweze kumsaidia rais wetu katika kufanikisha adhima ya
kulijenga taifa letu kiuchumi kwa faiada ya vizazi vyetu
Mungu ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment