A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people.John F. Kennedy
“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kamaraia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri,mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) nawanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii nakubadili mawazo na matumaini ya taifa.”Julius Kambarage Nyerere
mwaka 2015 kama taifa tumeshuhudia ajali nyingi sana zikiendelea kudhoofisha uchumi wa taifa letu kwa kuwapoteza watanzania wenzetu wengi ambao wamefarika katika ajali zilizosababishwa na ajali nyingi za barabarani kama makala ya hapo juu ilivyoelezea. umekuwa mwaka wa huzuni kubwa kwani kuna baadhi ya ajali tungeweza kuzizuia kama wahusika wangekuwa makini.
Katka mwaka wa 2015 Mheshimiwa Zitto aliaga rasmi kuachana na chama cha CHADEMA; lilikuwa ni tukio ambalo liligusa nyoyo za wapenzi wengi wa siasa wale wa upinzani na wa chama tawala pia.
Katika Mwaka huu wa 2015 Mheshimiwa Lowassa alikihama chama cha mapinduzi na kujiunga na chama cha Upinzani CHADEMA ili kuweza kuwania kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
DR. John Pombe Magufuli aliteuliwa na chama chake ili kuogombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi, kutoka kuwa hakuwa na makundi ndani ya chama hicho , uwajibikaji wake uadilifu wake ndivyo vilimfikisha hapo alipofika.
Katka Mwaka wa 2015 tulishuhudia Prof Ibrahim Lipumba akiamua kuacha na siasa kama mwenyekiti wa CUF na Mwenyekiti Pacha wa UKAWA, kwa kuto ridhika na taratibu ndani ya UKAWA katika harakati za kumpata mgombea urais kupitia muungano huo.
Dr Slaa pia katika mwaka huu wa 2015 aliamua kuachana na siasa akiwa kama katibu mkuu wa CHADEMA. hilo lilitoka na tofauti zilizojitokeza ndani ya UKAWA. lilikuwa ni tukio lililovuta hisia za wengi.
Tukio nyingine kubwa katika mwaka wa 2015 ni CCM kushinda uchaguzi Mkuu uliofanyika October 2015 ; ambapo mgombea wa urais wa CCM Dr. JPM na Makamu wa Kwanza Mwanamke katika historia ya Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan walikabidhiwa vyeti vya ushindi.
DR. JPM awashukuru wana CCM kwa kumchagua na kuanza kuwasha cheche kuhusu unafiki wa baadhi ya wanachama wa chama hicho
Tumeshuhudia Rais DR. JPM akianza kazi kwa ujasili wa kuwa tayari kutumbua majipu ambayo yamerudisha sana nyuma maendeleo ya watanzania.
katika mwaka huu 2015 tuliona wananchi kuguswa na hotuma ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alipofungua Bunge la 11 kwani ilikuwa imegusa kiu yao na matarajio yao ya muda mrefu. ilikuwa hotuba ambayo imeonyesha mwelekeo wa serikali yake kwa kipindi cha miaka 5 ya utumishi wake kwa umma wa watanzania hasa wanyonge.
Ilikuwa shangwe na vigelegele wakati DR.JPM alivyofanya ziara za kushitukiza na kugundua jinsi watanzania walivyokuwa wakikosa hudumu muhimu kwa uzembe wa wa watendaji, hivyo Katibu Mkuu Kiongozi alitoa mchumuisho wa ziara ya Mheshimiwa Rais na majumuisho ya uwajibikaji kwa wazembe.
Katika mwaka huu wa 2015 Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alifanya ziara ya Ghafla Bandarini Na TRA na kujionea njinsi Taifa lilivyokuwa likipoteza kiasi kukubwa cha mapato kwa Tamaa ya watendaji wachacche ambao walikuwa hawana maadili. ziara hiyo iliweza kubadilisha ukusanyaji wa mapato na serikali kuanza kupata mapato mengi zaidi.
Katika mwaka wa 2015 tumeshuhudia jinsi Rais Dr. JPM akishiriki kufanya usafi wa mazingira. Lilikuwa ni tukio ambalo liliweza kumjumuisha kila mtu kushiriki kufanya usafi ikiwa na sehemu ya kusherekea siku ya kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu.
Tunawatakieni sherehe njema za kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016 kwa amani na utulivu na tuendelee kumwombea Rais wetu ili katika mwaka huu wa 2016 aendelee kutekeleza majuku yake, kwa kasi kwa faida ya watanzania kama alivyoanza. Mwenyezi Mungu amjalie afya njema Amen
BADO TUNAHITAJI MCHANGO WA
UPINZANI KATIKA KUBORESHA DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA NA WA HAKI TUKIZINGATIA
KUWA:
“Siasa si mchezo mchafu, ila wachezaji wake ndiyo wachafu.”
Litakuwa ni jambo la kuheshimiwa ka viongozi wetu wetu watakuwa
wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya mioyo kwa faida ya wananchi wao.
Confucius aliwahi sema kuwa ‘Utajiri
na vyeo ndivyo vitu ambavyo kila bianadamu anavitamani; lakini ikiwa njia ya
kuvipata ni kwa kwenda kinyume na misingi yake, anapaswa ajiepushe navyo.’
Rudolph Giuliani
aliwahi sema kuwa ‘Kiongozi
huchaguliwa kwa kuwa yeyote anayemuweka pale huwa anaamini maamuzi, tabia na
uwezo wa maarifa yake – siyo ujuzi wa kufuata maoni. Ni wajibu wa kiongozi
kuchukua hatua kufuatana na sifa hizo.’
“kiongozi
ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi
Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi,
ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama
fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu za kuwafurahisha
viongozi wengine”
Demokrasia kama falsafa ya
Plato ambayo inahusiana na uendeshaji wa shughuli za kisiasa inalenga zaidi
katika utumishi kwa umma na uendeshaji
wa jamii na taifa. Wananchi wote hawawezi ongoza nchi kwa mara moja; Katika
msingi huu wananchi kutokana na wingi wao waliridhika itakuwa sio rahisi kwa
wao wote kukutana, kufanya maamuzi na kuyasimamia moja kwa moja maamuzi hayo
yanayowahusu wao kama jamii; dhana ya kuwachagua viongozi wachache huzaliwa kwa
chimbuko hili na kuruhusiwa kuunda serikali.
Tatizo kubwa tulilonalo
kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio
katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Kwani inatupasa kutambua
kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu. Lakini ridhaa hiyo
haitolewi hivi hivi tu, inaambatana na amana, kwamba waongozi watatekeleza
dhamana na wajibu wao kwa makubaliano na maelewano ya kufuata
barabara na kuheshimu ipasavyo kanuni na maadili fulani yanayoitambulisha
na kuiongoza jamii husika.
Hapa ndipo chimbuko la
demokrasia linapochimbuka na dhana ya Upinzani kwa masilahi ya wananchi
linapoanzia. Lengo la vyama nya upinzani ni kuleta ushindani wa kisiasa dhidi
ya chama kinachotawala katika nchi husika. Upinzani unasimama kama mbaadala wa
wananchi katika kukosoa shughuli za serikali ambazo huzitenda kinyume na utaratibu
ambao unafaida kwa taifa husika.
Pamoja na hamu kubwa ya
upinzani kushika hatamu lakini husaidia kuleta uwajibikaji na uadilifu kwa
viongozi ambao wameshika hatamu ya uongozi. ikumbukwe kuwa kiongozi muadilifu
hakubali kufuata au kutoa maamuzi bila
kufanya ukadirifu wa hoja na hali husika. Uongozi ni kujitolea na kuweka
matwakwa na maslahi ya wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na
kujinufaisha.
Marehemu John Kennedy rais
wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa. Tuchague viongozi si kwa
kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza, kuhamasisha na
kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama wanavyojinadi. Hii ndio
dhana ya upinzani inapoingia kwani hutupa sisi wananchi nafasi zaidi ya kupima
uwezo wa viongozi kupitia vyama vyao nani unafaa kuongoza nchi kwa kipindi Fulani
kulingana na mahitaji ya Taifa.
Tukumbuke kuwa, Serikali ni watu, inaundwa na
watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya
kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa
kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa
matakwa na utashi wa Wananchi wake.
Upinzani tunahitaji ni ule
ambao unatija kwa taifa, kwani taifa letu linahitaji utulivu, amani na upendo
miongoni mwa wananchi wake na kudumisha umoja wa kitaifa kupitia viongozi wake;
kiongozi muadilifu pia hufanya kila bidii kuhakikisha amani na utulivu wa kweli
katika nchi vinapatikana. Amani na utulivu ni chachu ya wananchi kwa
kushirikiana na Serikali yao kujiletea maendeleo. Maendeleo hayaji mahala penye
magomvi na huhasama. Lakini na amani na utulivu pia haviji mahala pasipo na
haki na uadilifu. Uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi hupelekea hasara ya
maisha na mali ya watu na hayo hayawi malengo ya uongozi muadilifu katika nchi
wala upinzani wa kweli ambao haujejaa uroho wa madaraka kwa nia binafsi.
Uadilifu wa uongozi unadai
kuheshimu nguvu ya hoja na fikra bora na hayo yanaweza kupatikana tu iwapo nchi
inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia. Hivyo, katika kutoa uongozi sahihi, kwa
kuzingatia maslahi bora ya nchi na watu wake, haki, uadilifu, umoja, amani na
utulivu, hapana budi kwa kiongozi kuiamini, kuiheshimu na kuifuata barabara
misingi ya kidemokrasia.
Bado binadamu si mkamilifu
na kwa vyovyote vile hufikia mahala akafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kama
yalifanywa kwa nia njema na kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana wakati
maamuzi hayo yanafanywa. Hayo yanaeleweka na kiongozi muadilifu anapaswa
kuyakubali na kuliomba radhi Taifa. Hiki ndiyo kilele na kigezo kikuu cha
uadilifu wa uongozi katika siasa. Kukubali kubeba dhamana kwa madhara
yaliyotokana na maamuzi yako au yaliyofanywa kwa jina lako.
Maamuzi ya kiongozi wa
kisiasa huathiri taifa zima, busara na hekima huzaa maamuzi yanayotokana na
tafakuri ya kina, yanayozingatia hali halisi ya mambo na maslahi na manufaa ya
muda mrefu. Kiongozi muadilifu anatakiwa ayaone haya na ayazigatie kwa kila
hatua anayochukua. Kama viongozi wetu wa bunge wakikiri kuwa walikurupuka
katika kufanya maamuzi hayo bila kuyafanyia kazi vizuri heshima na uwajibikaji
wa kuliendesha bunge letu itarudi. Tukubali tu kuwa njia ya kusonga mbele ni
kukubali kutofautiana katika fikra lakini tubaki kuwa wamoja.
Kama taifa bado tunahitaji
upinzani katika uendeshaji wa taifa letu ili kuweza kuikumbusha na kuibana
serikali pale ambapo hukiuka utekelezaji wa majukumu yake ya maendeleo kwa
wananchi wake; na pale inapokiuka utaratibu wa demokrasia na kukiuka haki za
binadamu na matumizi mabaya ya selikali.
Swali la msingi ambalo najiuliza sana hivi sasa hii dhana ya
utumbuaji wa majipu ambao umelipatia sana hasara taifa letu asili yake wapi na
kwa nini tumefikia hapa ambapo tumefika leo hii kama taifa tukiwa tumepoteza
mapato mengi sana ya taifa kwa muda mrefu na taifa kukosa mwelekeo.
Jambo la msingi ambalo halipingiki ni kuwa viongozi wa taifa letu
ambao walipewa dhamana ya kutuongoza walikuwa wakitekeleza dhana ya uongozi
bora kwa tafsiri binafsi. Dhana ya uongozi inatakiwa ianzie wapi?
Dhana ya uongozi wa namna yeyote ile unafaa uanzie nyumbani kwa
kila mtu uongozi ni uwezo wa kuweza kuyakabili kwanza matatizo yako mwenyewe na kufanya maamuzi sahihi bila
kushawishiwa na mtu mwingine yeyote yule.
kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kuyatawala maisha yako
kulingana utaratibu ambao wewe mwenyewe umejiwekea kuanzia ndani ya familia
yako; ukifanikiwa hili unakuwa umefaulu katika mtihani huu wa kwanza wa
uongozi ndipo jamii inapoanza kukuona kuwa hata ukipata nafasi ya
kuwaongoza wao pia utaweza kufanya maamuzi sahihi.
Kwa maneno mengine ni uwezo au njia ya kuweza kuwashawishi
watu ili waweze kufanya kitu au kufikia lengo fulani la kikundi kwa ridhaa yao
wenyewe. ili uongozi uwe bora ni lazima kuwe na kiongozi anayeongoza kundi
fulani la watu au jamii husika kwa usahihi na kufuata maaadili ya uongozi yanayozingatia
uaminifu, ukweli na uadilifu.
Katika kila jamii kuna umuhimu wa kuwa na kiongozi kunatokana na
ukweli kwamba watu wanapaswa kuwa na namna ya kuunganisha nguvu zao ili kufikia
malengo yao. Katika kila jamii, ni lazima kuwepo na mikakati ya
kuunganisha nguvu, vipaji, uwezo na stadi mbalimbali za wana jamii.
Wajibu wa msingi wa kiongozi yoyote ni kusaidia kuunganisha uwezo
wa watu, kuratibu, kusimamia shughuli za watu, na kila inapobidi aonyeshe njia
itakayosaidia kufikia lengo. Hii ndio dhana ya serikali ya awamu ya tano chini
ya Dr. John Magufuli ambaye ameonyesha utayari wa kufanya kazi na viongozi
ambao wataonyesha uadilifu katika kazi zao za kuwatumikia watanzania ili
kuwakwamua kutoka katika wimbi la
umasikini na kuwawajibisha viongozi wote wabadhilifu ambao wamehujumu uchumi wa
watanzania.
Kwa dhana ya Plato uongozi ni dhana au taaluma inayompa
muhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaoongozwa kuunganisha nguvu,
stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo ya Taifa lao ili
kujikwamua kutoka katika tabaka kandamizi ambalo linawasumbua. Kuongoza ni
kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi bora una mchango mkubwa sana katika uimara wa jamii.
Lakini tufahamu kuwa Ubora wa kiongozi unachangiwa na vitu vingi lakini
tusisahau kuwa vile vile uongozi au kiongozi bora hutoka kwa Mungu. Kama rais
wa awamu ya tano alivyowahi sema kuwa serikali yake ina kazi na dhamana nzito
wa kuwajengea uchumi wa kati jamii ya watanzania kwa kuelewa kuwa wakiwatendea watanzania ndivyo sivyo adhabu yao
itatoka pande mbili kwa Mungu na kwa jamii iliyowachagua.
Ikumbukwe kuwa viongozi wetu waelewe kuwa ni viongozi muhimu sana
ambao wataingia katika vitabu vya kumbukumbu ya Taifa hili kuhusu ubora au ubaya
kwa Taifa letu.
swali la kuwauliza Viongozi wetu wa awamu ya tano Je watendaji
wake watampa Kaisari yaliyo ya Kaisari ili kutimiza yale waliokuwa wamehaidi wakati
wa kampeni ili kubadilisha maisha ya watanzania?
Je Viongozi wa awamu ya Tano chini ya mwitikio wa Hapa Kazi Tu
chini ya DR. Magufuli wanafahamu ukubwa na umuhimu wa maamuzi yao
kwa jamii ya Tanzania?
Je viongozi wetu wa awamu ya tano wametawaliwa na maadili gani katika utendaji
wa kazi yaokuendesha serikali? Ni ukweli usio fichika kuwa ili waweze
kufanikiwa katika kutumiza maendeleo ya wananchi
ni lazima wazingatia maadili ya msingi ya
kufanikisha na kusimamia kwa weledi
mkubwa falfasa ya Mpe kaizari yaliyo ya kaizari hasa katika kipengele ya
ukusanyaji kodi ili kuimalisha mfuko wa serikali kwa maendeleo ya Taifa.
Mheshimiwa Rais Dr Magufuli ameonyesha nia dhabiti katika
kutekeleza falfasa hii kwa kuanza kutumbua majipu na kupaisha makusanyo ya kodi
katika mwezi huu wa December 2015. Kama taifa tunafarijika kuwa timu nzima ya
serikali kwa nia nzuri sasa wanawajibika na kuwawajibisha wale wote ambao
walikuwa wanakwenda kinyume na falfasa hii ambayo Yesu aliwambia wafarisayo
kuhusu dhana ya kutoa kodi.
Tunaendelea kufarijika kila siku njisi watendaji wakuu wa serikali
wanavyowajibika sasa na kuruduisha imani kwa Watanzania masikini kuhusu
mabadiliko ya maisha yao na jamii nzima. Hivyo ni vyema waendelee kutimiza
wajibu badala ya kujali maslahi yao binafsi yatokanayo na itikadi au faida
ambayo wanafikiria wao tu watanufaika nayo na sio taifa;
Daima Rais wetu ameendelee kusisitiza kuwa Tanzania niyetu sote na
rasilimali ambazo tumejaliwa ni zetu sote na sio mali ya kikundi Fulani tu. Na ameendelea
kusisitiza kuwa anafafahamu wananchi
wanatamani nini; wanatamani watoto wao wapate elimu bora ndio maana sasa
serikali imerudisha tena elimu bure kwa watoto wetu;
Anajua watanzania wanataka umoja ndio maana anaendelea kuhubiri na kuwaomba wananchi kuendelea kudumisha amani iliyopo
katika pande zote mbili za jamuhuri ya Muungano;
Hebu tujikumbushe Busara za Baba wetu wa Taifa Mwalimu
Nyerere alipozungumzia dhana ya uongozi, Mwalimu Nyerere alisema, “uongozi ni
kuonyesha njia.” Kwa maana hiyo, viongozi shurti wafahamu vyema matokeo ya
uongozi wao. Wasome imani za wanaowaongoza na nyakati zilizopo ili kutambua
matumaini ya umma kimaisha.
VIONGOZI GANI TUNAWAHITAJI?
Amabao hawawezi jisahau wamepewa
dhamana ya kushika hatamu ya uongozi la
msingi hapa ni kuwa kiongozi amabye yuko tayari kuongoza na na ajuwe anabeba jukumu la kubadilisha hali za
watu kuwa nzuri. Atumie stadi za uongozi mwema kuonyesha njia. Mheshimiwa Dr.
Magufuli ameweza kulionyesha hili kuwa kiongozi ambaye anajali Taifa na sio
kukitumikia kikundi Fulani.
Wanaepuka kutumia stadi za
uongozi kusimamia haki za waliowa wafikisha hapo hasa wanyonge. Wajikumbushe
kuwa kupewa uongozi ni kuchukua ahadi ya kutenda kwa haki. Ukitaka kulitendea
haki jipu lazima ulikamue na ulikamue vizuri na kuhakikisha kuwa kiini kimetoka
ili kumpa nafuu mgonjwa. Ugonjwa ambao kama taifa tunao kwa sasa ni uchumi wetu
ambao hauendani na maisha ya wananishi wetu. Tunashkukuru majipu haya sasa
yanaendelea kutumbuliwa na mgojwa wetu uchumi anaendelea kuimarika.
Mwalimu Nyerere aliandika miongozo mizuri katika Azimio la Arusha
miongoni mwao akisema kwamba ili tuendelee tunahitaji Siasa Safi na
Uongozi Bora. Alitambua mchango wa mambo hayo katika maendeleo ya mwanadamu.
Kupitia siasa safi kila kitu cha kunufaisha wananchi hupatikana. Bali ni muhimu
viongozi wanaotarajiwa kufanikisha ustawi wa wanadamu, wapatikane kwa njia ya
haki. Watokane na ridhaa ya watu wenyewe wanaotaka kuongozwa. Na wakisha
chaguliwa anatende kazi kwa uadilifu na ustadi mkubwa. Waweze kukusimai uchumi
wetu kwa kuhakikisha kuwa yaliyo ya Kaizari anapewa Kaizari kwa faida ya Taifa
nzaima.
Watendaji wetu timizeni
wajibu wenu ili muweze kumsaidia rais wetu katika kufanikisha adhima ya
kulijenga taifa letu kiuchumi kwa faiada ya vizazi vyetu
Mheshimiwa
Majaliwa Kassim Majaliwa ni waziri mkuu wa
awamu ya Tano ambaye anaendana na kasi ya utendaji wa kazi wa Rais wa awamu ya
tano Mheshimiwa Dr. Magufuli katika kurudisha uwajibikaji na matumizi mazuri ya
fedha za watanzania katika idara za serikali na mashirika ya
umma.
Katika
hiki kipindi kifupi akiwa kama waziri mkuu ameweza kuonyesha nia dhabiti ya
kuwatumikia watanzania wanyonge ambao kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa masikini
katika taifa lao ambalo lina utajiri mkubwa ambao ulikuwa ukiishia amikanoni
mwa wachache.
Ameanza
kazi kwa kutembelea au kufanya ziara za ghafla katika idara nyeti za serikali
ambazo ni nguvu ya uchumi wa Taifa na daraja pekee katika kuondoa umasikini wa
watanzania wanyonge . kauli ya ambayo alitoa hivi karibuni kuwa amekuja tu
kujifunza bila kuhitaji maelezo zaidi ilikuwa ni nzito ambayo kwa kweli
watendaji wa serikali na idara zake wanatakiwa kuizingatia na kuwa tayari
kuwajibika mara moja.
Mheshimiwa Majaliwa ameonyesha ujasiri wake wa
kujifunza nini kinaendelea katika utendaji wa watumishi wa serikali na uma na
tayari ameanza kuyapa mgongo mazoea ya kale. Kwa mhesjimiwa majaliwa ambaye hakuwa maarufu
sana katika siasa za Tanzania sasa kwa kushirikiana na mhemishimiwa Rais
Magufuli kwa pamoja wameamua kuhakikisha wanabadilisha mifumo ambayo ilikuwa
inawanyima watanzania kaktika kuyafikia maendeleo kammili, Lengo kubwa la
serikali ya tano chini ya Rais, Magufui, Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan na
Waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ni kuona kuwa wanabadilisha mifumo yote
mibovu ili kuifanya Tanzmi kuifanya inakuwa
bora zaidi kwenye masuala ya uchumi, utawala na maisha ya watanzania masikini.
Waziri Mkuu kwa kushirikia na Uongozi wa awamu ya Tano
chini ya Rais John Magufuli wana kila nafasi sasa ya kuandika historia kwa
kutumia kauli mbio ya hapa kazi tu na kuhakikisha wanabadilisha mifumo yote
mibovu ya kuendesha nchi kwa fiada ya watanzania
Tukubali kuwa Tanzania ya leo inaweza kuwa tofauti
sana na ya jana, na ya kesho ikawashangaza hata watu wa dunia. Kama Mheshimiwa Majaliwa katika nafasi yake
ataweza kuhakikisha kuwa anajenga mfumo ambao, hata kama yeye hatakuwepo
madarakani, bado Tanzania na Watanzania watafuata na kuheshimu mifumo mipya
itakayowekwa. Ndio maana kauli yake “ nimekuja kujifunza tu ni muhimu sana kwa
taifa hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko. Kwa nchi kama ya kwetu, lililo
muhimu kwenye mifumo ni kwa wenye kukiuka sheria, kanuni na taratibu
zitakazowekwa kuadhibiwa, punde tu wanapokosea.
Je Mheshimiwa Majaliwa amejifunza nini? Na atakuja na
somo gani au fundisho gani kwa hao aliowatembelea? Je ataweka mifumo mipya,
yenye kutanguliza maslahi ya nchi na si ya watendaji binafsi ambao wameamua
kutumia pesa katika kujilipa wao wenyewe? Je hili litakuwa anguko jingine kwa
watendaji wabovu ambao wanajali sana masilahi yao na sio ya taifa?,
Kama wengi ambavyo wameseama kuwa kitendo
chochote cha kupunguza matumizi yasiyo na lazima, na kutumia fedha kwa ajili ya
maendeleo ya Watanzania lazima kiungwe mkono kwa hali na mali. Waziri Mkuu
Majaliwa anastahili sifa kwa hilo na tumwombee Mungu amlinde ampe nguvu na
aweze kutuletea mabadiliko ya kweli.
Kwangu mimi leo kauli ya
“nimekuja kujifunza” ina maana kubwa sana sisi kama taifa tunao wajibu wa
kujikomboa kimawazo ili tuweze kufikiri sisi wenyewe, katika kuyapa thamani maamuzi
yetu ya utendaji badala ya kusubiri ziara za ghafla za viongozi wetu ili
watufundishe jinsi ya kutumia nyazifa zetu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Haiingia
akili kwa watendaji wa mashirika ya umma pamoja na bozi zake kutumia pesa
nyingi ili walipane mishahara na malupulupu binafsi na kuliona shirika
linaendelea kudidimia na wafanyakaza na likishindwa kujiendesha. Tuwe na vichwa
timamu vya kutuwezesha kuyatafakari masuala sisi wenyewe. Tunapaswa tujijengee
huu msingi ili tuweze kuitathmini dhana ya maendeleo, tuweze kujiuliza
maendeleo ni nini?
Katika kufanya hivyo, tunapaswa
kuchukua jukumu na wajibu wa kujitungia vigezo vyetu na kuvitumia. Lazima
tujenge utashi wa kujiamini na kujiamulia mambo yetu wenyewe kwa manufaa ya taifa letu.
Ni uongo kudhani kuwa hakuna nchi ambayo imesimama tu na haibadiliki.
Kosa tunalofanya ni kutozingtia ukweli huo na badala yake kuziona nchi za Ulaya
na Marekani kama nchi zilizoendelea na sisi kutumia rasilimali zetu vibaya
tukiendelea kusaidiwa na nchi hizo kama sisi ni mataira wa kufikira na hatujui kutenda
kazi ipasavyo isipookuwa ni kufikira kuiba tu . Kwa mtindo tulio nao sasa tutabaki
na hii dhana ya kujidunisha, na watu wetu kuendelea kuwa masikini miaka yote. Kwa
kweli tunatakiwa Kujifunza ili tuweze badilisha huu msimamo tegemezi.
Mheshimiwa Majaliwa
anatuonyesha kuwa tuna takiwakuwajibika kujikomboa kifikra, tuweze kujiwekea
vigezo vyetu wenyewe. Pasipo kuwa na vigezo vinavyozingatia haki ya uwajibikaji. Uadilifu na kumwogopa Mungu dhana
ya mabadiliko na maendeleo itaendelea kuwa ndoto. Asante awamu ya Tano sasa mmeanza
kutoondolea dhana hii. Inatubidi
tubadili fikra; tukatae huu mkondo uliopo sasa wa kuitwa au kujiita sisi ni
masikini wakati watu wachache ambao wamepata nafasi serikalini katika mashirika
ya umma kwa sababu zao binafsi wanarudisha maendeleo yetu nyuma.
Dhana ya Maendeleo ni
mabadiliko katika kitu au hali yoyote, katika nyanja mbali mbali za maisha,
mabadiliko ya manufaa kwa mujibu wa mazingira husika. Katika jamii au nchi,
maendeleo yanaboresha maisha ya binadamu, yanahifadhi au kuboresha mazingira,
na yanaendana na heshima, utu, na haki. Maendeleo yanatokana na msukumo wa
jamii au nchi husika, kwa mujibu wa mahitaji yake halisi, na kwa mujibu wa
maamuzi na matakwa ya jamii hiyo, maamuzi yatokanayo na fikra huru na tambuzi,
zenye mwelekeo wauwajibikaji na uadilifu. Maendeleo hayatakiwi yalete matabaka
miongoni watanzania.
KWA KWELI NIMEKUJA KUJIFUNZA mimi imenifundisha kuwa tukitaka kufanikiwa katika hii safari ya
kuondoa umasikini wa Taifa letu tunatakiwa kuendelea kuitekeleza kauli mbiu ya
Ya Hapa Kazi Tu kwa vitendo katiaka kujiletea maendeleo yetu na sisi kama wazalendo wa taifa
hili lazima kwa umoja wetu tusiwaonee haya mafisadi, wla rushwa wazembe katika kusukuma
gurudumu la nchi yetu mbele , na tuondoe dhana ya kungojea misaada kutoka nchi
za nje hii haiwezi kusaidia maendeleo bali inatufanya tuendelee kuwa tegemezi
zaidi .
Tunaona mfano wa nchi
kama CUBA ile haifuati njia za uchumi kama nchi nyingi duniani ina uchumi wake
unaokuwa kila siku , angalia uchina na mipango yao na mao ni serikali ya
kikomunisti ndio lakini walikuwa na malengo ikazaa mikakati hii tunayoiona sasa
hivi ni dira ya china na kufikia mwaka 2030 iwe super power; au tuangalie nini
walifanya south Korea iaka ile ya 1960s.
Kwahiyo tuwekeze katika rasilimali ambayo tunajua inaweza kututoa hapa
tulipo kwenda hatua mbili au 3 zaidi mbele bila kutegemea msaada kutoka nje. ,
Tunaweza kuendeleza
mawazo ma-pya, na kuyakusanya, kuyachuja, kuyaangalia na kuyaunganisha. Hivyo,
maendeleo ni hatua ambayo husonga mbele na yenye mabadiliko. Maendeleo
yanajumu-isha utendaji ufuatao malengo. Viongozi
wetu wengi wanajiona wao pekee ndio wenye wajibu wa kufaidi utajiri wa
nchiyetu, kupitia hulka zao za RUSHWA NA UFISADI.
Sisi kama wananchi
wazalendo wa taifa letu tuko tayari kushirikiana na viongozi wa awamu ya tano
katika kuyachoma magugu ambayo mengine yalikuwa yameota sugu na kuwa msitu
mkubwa ambao umekuwa tishio kwa wachomaji na walulima ambao wako tayari
kulisafisha pori hili. Tumeamua kuwaunga Mkono Mheshimiwa Dr. Magufuli Rais
wetu na Mama Samia Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Majaliwa msitoke jasho peke
yenu katika kufyeka msitu huu. Nasi tjuko tayari kutoa ili shamba letu liweze
kutoa mazao bora na sio tene kuitwa shamb la BiBi. Tunafahamu kuwa Shamba la
Bibi ni letu sote kila mtu anamchango wa kulifanya listawi na kutoa mazao bora
kwa faida ya wajukuu na watoto wote wa Bibi.
Kwa kweli nimekuja
kujifunza na kugundua kuwa UFISADI NA RUSHWA unatengeneza kikundi cha watu...wenye kusimamia
maslahi yao kwa faida yao UFISADI NA RUSHWA Inaunda uwepo wa vikundi visivyo rasimi
kisheria kwa ajili ya kupinga/kuzuia/kufanya lobbing na kufanikisha mambo
ambayo wao walio kwenye kundi husika Watafaidika nayo;
UFISADI NA RUSHWA Inapanua wigo wa Rushwa kwenye jamii na kufanya baadhi ya watu
kwenye jami wasiweze kuguswa na sheria kwa sababu ya uwezo wao kwenye fedha. UFISADI
NA RUSHWA Inaleta usumbufu kwenye
utendaji wa Serikali kwa kuwa baadhi ya raia wanakuwa na nguvu ya fedha hivyo
umma wa raia wa kawaida unatengeneza hofu ya kuogopa watu wao wenye ukwasi.
UFISADI NA RUSHWA Inavunja na kuharibu mfumo wa HAKI kwa kuwa wenye UKWASI huo wa
kifisadi wanatumia ukwasi huo kuvulugu HAKI inapotafutwa. UFISADI
NA RUSHWA Uzalisha kiburi/Jeuri
za watu wenye ukwasi dhidi ya Watumishi wa Umma na kuwafanya waonekane si kitu
mbele ya sura za jamii UFISADI NA RUSHWA Uchochea kwa kasi kubwa ongezeko la kukosekana
kwa maadili ya umma na maadili ya Viongozi wa umma.Hivyo kuongeza mpasuko wa
kuwa Taifa lina mmomonyoko wa maadili.
UFISADI NA RUSHWA Usababisha woga wa kitaifa hata uwezo wa kitaifa kukemea mambo
yasiyostahiki utegemea ujasili wa mkemeaji. UFISADI NA RUSHWA Pia utengeneza ushawishi wa wageni kuona sehemu
za kupenyeza mambo yao kwa kuwa utafuta milango ya kuingia kwa namna ambayo wao
wanaona kuna njia ama upenyo. UFISADI NA RUSHWA Uchafua pia mfumo wa uendeshaji wa siasa na
Serikali kwa kujalibu kuweka mapandikizi yake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA KATIKA AWAMU HII YA TANO HAPA KAZI TU
Katika kipindi chote cha Kampeni Mheshimiwa Dr. Magufuli daima
alionyesha upendo, maumivu na haja ya
kuibadilisha Tanzania kuwa kweli ya watanznaia na sio Tanzania ya wachache
katika kufurahia matunda yatokanayo na rasilimali la taifa letu. Mfuatiliaji
mzuri aliweza kugundua kuwa Magufuli aliamua kwa hiari yake kuwatumikia
watanzania kuwa kiongozi mzuri kufuatia kwa ajili ya watanzania wote bila
ubaguzi wowote.
Rekodi zake za utendaji kwa falfasa ya kuwa atakuwa kiongozi
ambaye hataficha chochote kwa wananchi; hatasema uongo, na
atafichua uongo kila unapoibuka. hatakuwa mtu wa kuficha matatizo, makosa,
mapungufu na kushindwa kuyatafutia suluhu na kamwe sio mtu wa makundi au wa
kujijengea sifa nyepesi nyepes binafsi.
Mchakamchaka ambao anaendlea kuufanya Magufuli sasa ndicho haswa
kinachotakiwa kufanyika katika kipindi kirefu nyuma. Kwa kufanya hivyo,
Magufuli anaonyesha wazi kuwa anajua matatizo na mapungufu yaliyopo na badala
ya kuyafunika na kuyapaka rangi anayaweka wazi kwa maendeleo ya watanzania wote.
Bahati nzuri Magufuli amekuwa akielezea namna atakavyoshughulikia hayo matatizo
na mapungufu. Bahati nzuri tabia hii ya Magufuli siyo mpya. Watanzania
watakumbuka kuwa hulka hii ya Magufuli ilijionyesha wakati hata alipokuwa
waziri chini ya Rais Benjamin Mkapa alipoikosoa Ofisi yake hadharani kwa baadhi
ya watumishi wa ofisi hiyo kujimilikishia magari ya umma isivyo halali. Tukumbuke
hata Katika kipindi cha kampeni, Magufuli amekuwa akitoa mapungufu ya serikali
hata pale ambapo Rais Kikwete yupo.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuandika kitabu mwaka
1962 kiitwacho "Tujisahihishe" akitaka Watanzania na hasa viongozi
wawe tayari muda wote kujisahihisha. Katika kitabu hicho Baba wa Taifa, alisema
kuwa “makosa ni makosa bila kujali ni nani ameyafanya. Muhimu ni kuyajua makosa
hayo na kujisahihisha.” Katika kitabu hicho, Mwalimu Nyerere aliendelea kusema;
“Kujielimisha ni kujua ukweli wa mambo na kuwa na ujuzi wa sababu
mbalimbali za mambo; na kama mambo hayo ni mabaya ni kujua jinsi ya kuyaondoa;
na kama ni mema, jinsi ya kuyadumisha. Mpumbavu ni yule anayeyapa mambo sababu
zisizo za kweli na kushauri dawa isiyo ya kweli katika kutafuta sababu za
matatizo na jinsi ya kuyaondoa(Nyerere, 1962, 5).”
Kwa maelezo hayo ya Baba wa Taifa, ni wazi kuwa Magufuli ameamua kuwa mkweli
katika utendaji wake kama Rais wa wamu ya tano na ameepuka kuwa mpumbavu kama
alivyobainisha Baba wa Taifa. Magufuli anaamini dhana hii kiongozi mkweli
na aliye na uthubutu wa kujikosoa anaonyesha kuwa ana uwezo wa kutafuta
suluhisho la kweli la matatizo yaliyopo, na tumejionea katika kipindi kifupi
sana akiwa ameanza kutumbua majipu kama alivyohaidi.
kama mwandishi Maggid alivyowahi andika kuwa Sehemu kubwa ya
matatizo ya nchi zetu hizi yanatokana na ubinafsi huo. Na bahati mbaya kabisa,
baadhi ya viongozi tuliowapa dhamana za uongozi ndio wenye kuongoza kwa matendo
yenye kutanguliza maslahi yao binafsi. Kwetu sisi Watanzania hali yetu ya
kiuchumi bado duni mno. Ufisadi unalitafuna taifa letu. Tuna lazima ya
kukumbushana ukweli huu, maana, tukifanya masihara taifa letu liko katika
hatari ya kuingia katika hali ya machafuko makubwa. Ili kuunusuru uchumi wetu
usiyumbe zaidi tuna lazima ya kutumia fedha na rasilimali zetu kwa busara
kubwa. Kuna busara ya kutomuiga tembo kwa lolote lile
Sokoine alionyesha moyo wa kujitoa kuwatumikia wananchi mara tu
baada ya kuteuliwa katika wadhifa wa waziri mkuu wakati huo akiwa mbunge wa
Monduli mkoani Arusha. Katika utawala wake, kama waziri mkuu, aliendesha na
kusimamia mwenyewe vita dhidi ya dhuluma iliyokuwa inaendeshwa na wachache
wenye nacho dhidi ya wengi wasionacho. Vita dhidi ya walanguzi na wahujumu
uchumi ni miongoni mwa mambo ambayo yaliinua jina la Sokoine kila pembe ya nchi
hii na katika medani za kisiasa.
Sokoine alipenda haki, aliona ni kitu cha kushangaza kwamba wananchi
walio wengi walikuwa wanaishi maisha ya dhiki, hawakusikilizwa na watendaji.
Alishangaa kuona kwamba urasimu umezama kwenye rushwa za nipe-nikupe na
kuporomoka kwa maadili hasa upungufu mkubwa katika kutoa huduma na haki.
Sokoine alitumia uwezo kama waziri mkuu kujaribu kurejesha nidhamu katika sekta
ya utawala kwa kuwajibisha viongozi na watendaji wabovu. Kwa upande mwingine,
alijitahidi kuvunja ushirikiano kati ya viongozi warasimu na wafanyabiashara
ambao kwa pamoja waligeuza sekta ya umma kama shamba la bibi. Hili ndilo
analolifanya Magufuli na watendaji wake katika mwezi huu wa kwanza wa awamu
yake ya Tano ya kuliongoza Taifa hili.
Dr.
Magufuli tuko alipopendekezwa na chama chake cha mapinduzi kupeperusha bendera
ya kuwania urais wa awamu ya tano alisema wazi kabisa kuwa wananchi
wategemee utumishi uliotukuka toka
kwake, watarajie uadilifu wa khali ya juu,watarajie uchapakazi, watarajie
serikali itakayo kuwa imara: itakayo simamia maslahi ya uma; na wategemee
nidhamu sio tu kwa watumishi wa serikali bali kwa watanzania wote; wasitegemee
propaganda za ujanja ujanja; balo ukweli wakati wote; na alihaidi kufuatilia
mambo mengi kwa kina mimi mwenyewe;
wasitarajie sherehe na hafla nyingi toka kwangu. Na watarajie kuwa nitalinda
umoja amani na usalama wan chi yetu kwa nguvu yetu zote. Nitakuwa kiongozi wa
wote bila kubagua mkoa kanda dini kabila wala vyama.
Kama mwandishi Mmoja alivyowahi
andika “Dr John Pombe Magufuli raisi wa awamu ya tano anataka kuwaonyesha
watanzania kwa ujumla wake kuwa atakaye aliyethubutu kuchezea shilingi ya
Serikali atajitutia yeye mwenyewe; ni kweli ilikuwa inasikitisha kila siku
kusoma magazeti yenye vichwa vya habari, Mamilioni yametafunwa yayeyuka na
kuunda kamati ambazo zilikuwa vile vile zikitumia pesa katika kutafuta suluhu
na suluhu haipatikani. Kama mwandishi Maggid alivyowahi andika Maana, kuna walioishi wakiamini, kuwa ng'ombe
wa Serikali huzikwa na ngozi yake. Ni nani anayejali? Maana, kama ng'ombe ni wa
mtu binafsi, basi, akifa, atahakikisha walau anachuna ngozi yake, ili walau
aambulie senti kidogo! Utamaduni huu wa kudhibiti mapato ya hazina ni utamaduni
mwema utakaomsaidia mwananchi wa kawaida”.
Hatua ambazo ampaka sasa rais Dr
Magufuli, ameshchukua ni funzo tosha kwa watu wengine; tunafahamu kuwa kuteuliwa
na hatimaye kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa awamu ya tono kulitokana sana na record
yake ya uchapakazi, uadilifu, kutoyumbishwa hovyo hovyo kwa sababu ya kusimamia
kile anachokiamini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla, Hiyo
imejidhihirisha zaidi katika wizara zote alizowahi kuziongoza mfano Ujenzi na
Miundombinu pamoja na Kilimo na ufugaji. Ni kweli kuwa fundisho tunalopata hapa
ni kwamba usingoje mpaka upewe nafasi kubwa ya utumishi ndio uanze kuonyesha namna
ya kuwatumikia wananchi.
Dr Magufuli ni visionary leader ambaye anaamini katika jambo
moja kuwa mabadiliko ya maisha bora yanawezekana katika Tanzania yetu. Tatizo ambalo analijua
linalokwamisha maisha bora kwa watanzania ni Usimamizi mbovu sekta
zote kutokana na ubinafsi, udugu, rushwa. Katika kampeni yake alipotembelea
kaburi la hayati sokoine alisifu weledi wa hayati sokoine ambaye alikuwa
mkweli, mchukia rushwa, na alikuwa na uthubutu bila kumwogopa kiongozi yeyote Edward
Moringe Sokoine alikuwa kiongozi mwenye uthubutu wa dhahiri katika kupigania na
hata kufia maslahi ya raia, hasa maskini. Tunamkumbuka Moringe alivyowasha moto
bungeni kabla ya kuondoka, hasa
alipozungumza kuhusu kubana matumizi ya serikali, ambako kuliambatana na hoja
juu ya ukubwa wa serikali na hasa mantiki ya kuwa na mawaziri wasiokuwa na
wizara maalum, lakini wakipatiwa haki zote sawa na mawaziri wenye wizara. Nyota
yake ilizidi kung'ara na kuwa chachu ya kupendwa miongoni mwa walio wengi;
akaonekana mwiba kwa walafi na wadokozi wa keki ya taifa.
Ingawa
kwa upande mmoja Sokoine alionyesha kupata mafanikio kwa kuungwa mkono na
wananchi, kwa upande mwingine alijikuta akipoteza marafiki na kujijengea maadui
lukuki kutokana na mfumo wa utendaji uliokuwepo kabla yake. Katika utendaji
wake mara zote, Sokoine aliamini katika siasa za uwazi. Alizungumza kile
alichoamini ndicho na alisimamia na alionyesha mfano katika utekelezaji wa kila
jambo alilotaka lifanyike. Mambo mengi aliyojaribu kufanya Sokoine yalitokana
na uthubutu wake binafsi. Alitumia mfano wake kama kiongozi ambaye alikuwa na
uadilifu mkubwa na hakuwa na ubinafsi.
Rekodi
ya utendaji kazi wa kiongozi huyu ambaye alibahatika kushika wadhifa wa waziri
mkuu katika vipindi viwili tofauti, haijafikiwa na kiongozi yeyote katika ngazi
hiyo, miongo mitatu tangu kifo chake. Inasemekana ni katika kipindi chake cha
uongozi, Mwalimu Nyerere alipata ahueni, alinenepa.
Na katika awamu hii ya Magufuli watanzania wanyonge ni zamu yao kunenepa; na kuanza kufurahia matunda ya nchi yao tumejionea wenyewe muhimbili wagonjwa wakiwa wamelala katika vitanda na sio katika sakafu.
Kama
ilivyokuwa kwa marehemu Sokoine Mheshimiwa
Dr. Magufuli ameanza kuonyesha kuwa atakuwa kiongozi mkuu ambaye ataweza
kuisimamia kusimamia serikali kwani ameonyesha kwa moyo mkunjufu kuwa
anamainisha kila ambacho anakiongelea na kukiishi. Tunafahamu kuwa viongozi wa
aina ya Mwalimu Nyerere na Sokoine hawazaliwi kila mara. Kama taifa tumepata
bahati ya ajabu kwani sasa tumempata kiongozi wa aina hii ndio mheshimiwa Dr.John
Pombe Joseph Magufuli. Amekuwa kiongozi mwenye ujasiri wa
kuchukua maamuzi katika mazingira magumu ambayo yanawagusa hata vigogo wa
serikali ili nguvu kubwa zielekezwe kuwasaidia maskini,.
Dr. Magufuri ameonyesha awajibike
wa ukweli, kuwa muwazi katika utendaji wake kubana matumizia ya serikali.
Maswali
ambayo najiuliza leo
Uwajibikaji ulipotelea wapi kwa viongozi wetu?
Nini maana ya kuwa kiongozi wa umma?
Je wengi wa viongozi wetu
wanaelewa dhana hii nzima ya kuutumikia umma au jamii?
Je walioko madarakani na wanaoongozwa wanaonyesha na kufahamu
wajibu wao kwa jamii na kuwa viongozi bora wa kuigwa na kizazi chetu cha
baadae?
Ninachofurahia
mimi katika awamu hii ya tano, misamiati kama kula nchi kwa watendaji wa
serikali na mashirika ya umma; dhana ya umungu mtu kwa watendaji wengi sasa
inapotea katika kamusi ya utumishi wa umma.
Ni
wakati umefika sasa kwa watendaji wetu kujua nini maana ya uongozi; na
wakumbuke kuwa uongozi sio maana yake kulindana katika utendaji wa maovu. Imefika
wakati wa kuwaambia viongozi wote wabovu umekosea ondoka: Mheshimiwa Magufuli ameweza kuonyesha hili
katika kipindi kifupi sasa cha uongozi wake kama Rais Magufuli ameonyesha kwa
dhati Moyo wa kuwatumikia hao waliomchagua na sio kujali maisha yake na familia
yake tu kama ambavyo hali ilivyo sasa. Hivi sasa Dr. Magufuli anaifufua dhana yaw
a kuwatumikia wanachi ambayo ilikuwa imeshakufa na kupitwa na wakati. Hapa
nchini kwetu kila aingiaye madarakani anafikiria kujinufaisha binafsi na
waliomzunguka.
Uongozi
na kuwa kiongozi Tanzania ilikuwa ni mradi wa kutajirika na wala hakuna
anaeuliza mara baada ya kiongozi kuwa madarakani maisha yake kwa ujumla
yanabadilika na kuwa ni mtu wa juu kupita wote ndani ya jamii husika.
Inashangaza lakini hii ndio hali halisi kwa Tanzania yetu. Hatukatai mabadiliko lakini hali iliyoko sasa
inakatisha tamaa kwa wanaojua maana ya kuwa kiongozi wa umma.
Nimefurahi
kwa ujasili wa Dr. Magufuli wa kuondoa utamaduni uliojengeka wa kusifia makosa na
pale mmoja miongoni mwetu anapotaka kusema ukweli huambiwa ni msaliti wakati
anachotaka kukisema au alichosema ni cha haki na ukweli kabisa. Asante Mheshimiwa
Magufuli kwa kuanza kuibadili dhana hii na kuwabadili na wananchi kwa ujumla
huu sio wakati tena wa kuwaachia watu wachache wakitupeleka peleka katika lindi
la umasikini na matatizo kutokana na ubinafsi na ulafi wao tu.
Mheshimiwa
Magufuli amesema kuwa kazi iliyo mbele
yake ni kubwa na ngumu lakini amekubali kuwa yeye ndiye atakuwa anatumbua haya
majipu; hivyo Kama Mwandishi mmoja aliandika kuwa “ Uzalendo wetu kama
Watanzania tunaoipenda nchi hii ni kubainisha yale machafu ya viongozi na sio
kuwa wanafiki. Ilishasemwa zamani kuwa Ukweli ni mchungu, hatuna budi kuusema
japo unauma tuseme ukweli bila ya hivyo matatizo yetu hayawezi kwisha kwa kutegemea
wanafiki na walioingia madarakani kwa maslahi binafsi”
Maendeleo
ya kweli ya watanzania yatatoka na watanzania wenyewe; Hata siku moja
hatotokea mtu toka nje ya nchii hii kuja kutuletea maendeleo ila ni sisi
wenyewe tunapaswa kujiletea hayo maendeleo, nayo ni kuwajibika kutokana na
dhamana tulizopewa na sio kuipelekea kuzimu nchi yetu kama hali ilivyo sasa.
Mfano mdogo tu hebu angalia uozo wa Bandari na TRA na hasara ambayo Taifa
limepata.
Mheshimiwa
Rais Magufuli ameliona wazi kuwa Kiongozi wa umma anawajibika kwa umma
uliomuweka madarakani na sio kufanya safari nyingi za nje na kusema kuwa hana
nafasi na kwenda vivijini kuona shida za
watanzania Hongera Dr. Magufuli kwa kuliona hilo. Uamuzi wa hivi karibuni wa kufuta safari za nje ni wa kishujaa na
utapunguza matumizi makubwa ya pesa za wananchi. Hii inaonyesha jinsi ya ukubwa wa tatizo la
viongozi kutowajibika kutokana na nafasi zao ndani ya nchi hii lilivyo.
Ni
wakati umefika sasa wa kuanza upya kuanza kujitawala tukaanza kujenga Taifa la
viongozi na wananchi wanaowajibika kutokana na nafasi zao kwa maendeleo ya
Taifa hili kama ilivyokuwa kwa viongozi waadilifu kama Mwalimu Nyerere na
Edward Moringe Sokoine; Unapowajibika kutokana na nafasi ya uongozi inaonesha
ni jinsi gani ulivyokuwa kimaadili na kuwa tayari kulitumikia Taifa la
wanyonge.
Tukumbuke
kuwa zao la viongozi wabovu limezalisha taifa la Watanzania walio wengi sasa
wamejikita katika mazingira ya udanganyifu, rushwa na uzembe. Tukumbuke kuwa Watumishi wa umma
wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, uwajibikaji, weledi na ushirikiano ili
kuuiwezesha Serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake na taifa kwa
ujumla.
MHESHIMIWA RAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI WATANZANIA TUNAKUOMBEA
KATIKA SAFARI HII YA UTUMBUAJI MAJIPU KWA AJILI YA MAENDELEO YA WANYONGE:
TANZANIA SIO MASIKINI ILA VIONGOZI WACHACHE AMBAO TULIWAKABIDHI NAFASI
MBALIMBALI WALIKIUKA MAADILI YA UONGOZI NA KULILETEA TAIFA HASARA KUBWA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI RAIS WETU MAGUFULI AENDELEE
KUWAHUDUMIA WANYONGE NA MASIKINI -TANZANIA