Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika harakati za kusaka urais, wamechukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge kupitia chama hicho.
Kabla ya hapo, kulikuwa na uvumi kuwa wabunge hao hawatachukua fomu kutokana na kukatwa kwa Lowassa katika kinyang’anyiro cha urais.
Baadhi ya wabunge hao ambao wamechukua fomu hizo na kuzirejesha jana ni pamoja na Kangi Lugola (Mwibara), Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), Philipo Mulugo (Songwe).
TANGA
Mkoani Tanga, wabunge watatu waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa nao wamechukua na kurudisha fomu za kuomba kutetea majimbo yao.
Wabunge hao ni Stephen Ngonyani maarufu kama Majimarefu ambaye ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Beatrice Shelukindo (Kilindi) na Henry Shekifu wa Lushoto.
NIPASHE imefuatilia mchakato wa uchukuaji na urudishaji fomu ndani ya CCM ambao ulihitimishwa jana saa 10:00 jioni na kubaini kuwa wabunge hao wameshachukua na kurudisha fomu za kutetea nafasi zao licha ya kuwapo kwenye ushindani mkali kutokana na idadi ya wagombea kuongezeka kwenye majimbo yao.
Katika majimbo yote 11 ya Mkoa wa Tanga, wabunge wote waliokuwapo katika awamu inayomalizika, wamejitosa tena na kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo.
Kwa sasa Mkoa wa Tanga una jumla ya majimbo 12 baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuongeza jimbo moja la Handeni Vijijini.
KILIMANJARO
Vigogo watano wa CCM mkoani Kilimanjaro wakiwamo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango-Malecela na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, ni miongoni mwa mawaziri `waliokabwa koo' kwa kupata upinzani mkali ndani ya majimbo yao.
Wengine ni Waziri wa zamani wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Mathayo David Mathayo, ambaye anakabiliwa na upinzani mkali baada ya makada wenzake 13 kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti hicho katika Jimbo la Same Mashariki.
Waliojitosa kutaka kumng’oa Dk. Mathayo David ni John Chaggama, Daniel Mkemi, Alfred Ngelula, David Mawa, Amon Shahidi, Gerald William, Katery Daniel, Yusuph Singo, Michael Mrindoko, Ahadi Kakore, Jordan Mmbaga na Mwalimu John Singo.
Anne Kilango naye anakabiliwa na upinzani baada ya makada wanane akiwamo Dk. Michael Kadeghe, Dk. Eliji Kibacha, Semi Kiondo, Abraham Shakuri, Nyangasu Werema, Daudi Mambo na Ombeni Mfariji kujitosa kuwania kiti cha ubunge wa jimbo hilo.
Kigogo mwingine aliyepata upinzani, ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwanri, ambaye jimboni kwake, wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimasai wamelazimika kumwangukia, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (Nec), Meijo Laizer, kujitoa katika orodha ya makada watatu waliotangaza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti hicho.
Kwa upande wa Jimbo Moshi Mjini ambalo kwa muda mrefu limekuwa ngome ya Chadema, makada 12 wamejitokeza kuwania kiti hicho.
Makada hao ni Patrick Boisafi, David Mosha, Buni Ramole, Priscus Tarimo, Edmund Utaraka, Shaniel Ngindu, Innocent Siriwa, Amani Ngowi, Omari Mwariko, Michael Mwita, Daudi Mrindoko na Khalifa Kiwango.
Katika Jimbo la Moshi Vijijini, Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, amekutana na kikwazo baada makada watano kujitokeza kutaka kuteuliwa kugombea kiti hicho, huku Jimbo la Vunjo likiwa na watia nia wanane ambao wanakabana koo kutaka kuteuliwa kugombea kiti hicho.
DODOMA
Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, Livingstone Lusinde (Mtera), Gregory Teu (Mpwapwa), Omari Badwel (Bahi) na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai (Kongwa), ni miongoni mwa makada waliochukua fomu kutetea nafasi zao.
BAHI:
Mbunge wa sasa Badwel atapambana na Pascal Mwaja, Levison Chilewa, Donald Mejitii, Hebron Kipiko, Anthony Lyamunda, Salum Kanyika na Kondo Chaurembo.
MPWAPWA:
Mbunge wa sasa Teu, amepata wapinzani ambao ni George Lubeleje, June Fusi, Nyange Mtoro, Charles Kuziganika, Rehema Halahala, Emmanuel Mbeho na Gabriel Hango.
KIBAKWE:
Simbachawene atapambana na Amani Bendera, Gabriel Mwikola, Sabas Chambas, Shahel Gayesh, Aclay Mnyang’ali na Solomoni Ngiliule.
KONGWA:
Ndugui amepata wapinzani wake ambao ni Samwel Chimanyni, Dk. Elieza Chilongani, Epafra Mtango, Pascal Mahinyila, Hussein Madeni, Simon Katunga na Joseph Palingo.
MTERA:
Lusinde atapambana na Richard Masimba, Samwel Malecela, Essan Mzuri, Lameck Lubote na Dk. Michael Msendekwa.
CHILONWA:
Waliojitokeza kutaka kuwania jimbo hilo ni Peter Nasoni Mlugu (Mwalimu wa Shule ya Msingi Chilonwa), Kusakula Amosi (mfanyabiashara jijini Dar es Salaam), Chibutii Masagasi, Charles Ulang, (Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Chamwino) na Vincent Chomol.Wenslous Mazanda (Mwalimu wa Shule ya sekondari Mpunguzi), Joel Mwaka (Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi, Wilaya ya Chamwino), Daniel Robina Logoha, Palolet K. Mgema (Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea), Deo Ndejembi, Godrick Ngoli, Anderson Kusenha Magolola na Kk. David Mapana.
KYELA
WANACHAMA 10 wamejitokeza kuchukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kyela mkoani Mbeya kupambana na Mbunge wa sasa, Dk. Harrison Mwakyembe.
Dk.Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alichukuliwa fomu na baadhi ya wananchi ambao walijichangisha fedha na kumkabidhi jana mjini Kyela ambaye alizirudisha Makao Makuu ya CCM Kyela.
Wengine waliochukua fomu na kurejesha katika jimbo hilo ni Gabriel Kipija, ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, John Mwaipopo, Profesa Leonard Mwaikambo, Gwakisa Mwandembwa, Vincent Mwamakingula, George Mwakalinga, Benjamin Richard, Asajile Mwambambale na Ackim Jackison.
MBEYA VIJIJINI
Waliochukua fomu Jimbo la Mbeya Vijijini ni Mbunge wa sasa, Luckison Mwanjale, Oran Njera, Godon Kalulunga (Mwandishi wa Habari),Japhet Mwanasenga, Anderson Kabenga, Walimu Sikwembe, Kassim Chakachaka.
ILEJE
Aliko Kibona (Mbunge wa sasa) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janneth Mbene.
MBEYA MJINI
Nwaka Mwakisu, Aman Kajuna, Charles Mwakipesile
VWAWA
Mchungaji Tito Nduka, Japhet Hasunga na Mtella Mwampamba.
MASWA MAGHARIBI
Waliochukua fomu ni Michael Bukwimba, Mashimba Ndaki, Benjamin Rungu, Aaron Mbojo (Mjumbe wa Nec) na Henry Mbichi.
MASWA MASHARIKI
Waliojitokeza kuwania ubunge Jimbo la Maswi Mashariki ni George Nangale (Mbunge wa Afrika Mashariki), Peter Bunyongole (Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswi), George Lugomela, Ali Ntegwa, Stanslaus Nyongo na Jonathan Mnyela.
Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Emmanuel Lengwa, Lulu George, Godfrey Mushi, Editha Majura, Jacqueline Massano, Ibrahim Joseph na Peter Mkwavila, Dodoma.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment