Na Mwinyi Sadallah
Zanzibar. Chama cha Wananchi CUF kimempitisha katibu mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa mara ya tano.
Pia, CUF imewarudisha baadhi ya wagombea wa nafasi za ubunge na uwakilishi walioanguka katika kura za maoni za majimboni.
Maalim Seif amepitishwa na CUF kuwania nafasi hiyo
kwa mara tano tangu kurejeshwa kwa mfumo wa siasa za ushindani na mara
moja akiwa CCM mwaka 1984 wakati alipochuana na Marehemu Idirisa
Abdulwakili.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Vuga mjini
hapa, mkurugenzi wa mipango na uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe alisema
kwamba, Maalim Seif amechaguliwa baada ya kupata ushindi wa asilimia 100
kwa kuzoa kura zote 56 za wajumbe wa Baraza Kuu.
Alisema wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa
walilazimika kupiga kura ya “Ndiyo” na “Hapana” kutokana na kuwa na
mgombea mmoja na kura zote zilimuunga mkono mwanasiasa huyo mkongwe na
hakuna kura iliyoharibika.
Shehe aliwataja wagombea waliorudishwa kuwa ni
mbunge wa Mtambile, Masoud Abdalla Salim na mwakilishi wa Jimbo la
Kojani, Hassan Hamad Omar huku kukiwa hakujapatikana kwa wagombea kwenye
majimbo ya Raha Leo, Makunduchi na Mtambwe kutokana na sababu
mbalimbali ikiwamo ya kukatiwa rufaa pamoja na Baraza kuu kutoridhika.
Wagombea waliopitishwa kugombea ubunge na
uwakilishi ni Ismail Jussa Ladhu (uwakilishi) na Ali Saleh Abdalla
(ubunge) wa Jimbo la Jangombe, Ali Haki Mwadini (uwakilishi) na Mohamed
Yussuf Maalim (uwakilishi).
Katika Jimbo la Kikwajuni, Moh’d Khalfan Sultani (uwakilishi) na nafasi ya ubunge imeachiwa Chadema.
Jimbo la Chumbuni ni Maulid Suleiman Juma
(uwakilishi) na Omar Ali Khamis (ubunge), Jimbo la Kwamtipura Amina
Rashid Salum (uwakilisihi) na Abdi Seif Hamad (ubunge), Jimbo la
Magomeni Yussuf Idrisa Mudu (uwakilishi ) na Ahmed Khamis Hamad
(ubunge).
Jimbo la Mpendae ni Ali Hamad Ali (uwakilishi) na
Omar Moh’d Omar (ubunge), Jimbo la Amani ni Khamis Rashid Abeid
(uwakilishi) na Khamis Silima Ame (ubunge) . Jimbo la Kwahani Hassan
Juma Hassan (uwakilishi) na Khamis Mussa Haji (ubunge) Magomeni,
Abdilahi Jihad Hassan (uwakilishi) na Saleh Mohamed Saleh (ubunge).
Jimbo la Bububu, Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano, Juma Duni Haji (uwakilishi) na Juma Khamis Juma (ubunge).
Jimbo la Mfenesini ni Saleh Khamis Omar (uwakilishi) na Hassan Othman
Makame (ubunge) huku Jimbo la Mtoni ni Waziri wa Biashara na Masoko,
Nassor Ahmed Mazrui (uwakilishi) na Ali Ame Ali (ubunge).
Katika jimbo la Dole amepitishwa Yussuf Omar
Muhine (uwakilishi) na Khamis Msabah Mzee (ubunge) Jimbo la Dimani ni
Mohamed Hashim Ismail (uwakilishi) na Khalid Said Suleiman (ubunge) na
Jimbo Kiembesamaki ni Waziri wa zamani SMZ Mansour Yussuf Himid
(uwakilishi) na Mohamed Nassor Mohammed (ubunge), Mwanakwerekwe ni Ussi
Juma Hassan (uwakilishi) na Ali Salum Khamis (ubunge). wakati Jimbo la
Fuoni Suleiman Simai Pandu (Uwakilishi) na Mohamed Juma Aminia (Ubunge)
na jimbo la Nungwi Hassan Jani Masoud (Uwakilishi) na Yussuf Haji Khamis
(Ubunge).
Wengine ni Nahoda Khamis Haji (Uwakilishi) jimbo la Matemwe na
Dunia Haji Pandu (Ubunge ) Jimbo la Mkwajuni Haji Kesi Haji (Uwakilishi)
na Khamis Masoud Nasor (Ubunge).
Katika jimbo la Chaani Khamis Amour Vuai
(Uwakilishi) na Khatib Ali Juma (Ubunge) wakati jimbo la Tumbatu Makame
Haji Makame (Uwakilishi) na Rashid Khamis Rashid (Ubunge) pamoja na
jimbo la Donge Suleiman Ahmed Sleiman (Uwakilishi) na Kombo Mohamed
Kombo (Ubunge)
Wagombea wengine waliteuliwa ni Zahran Juma
Mshamba (Uwakilishi) Jimbo la Bubwini na Mohamed Amour Mohamed (Ubunge)
Jimbo la Kitope Hassan Khatib Kheir (Uwakilishi) na Mwinshaha Shehe
Abdalla (Ubunge).
Jimbo la Uzini Asha Simai Issa (Uwakilishi)
na Adam Ali Wazir (Ubunge) Khamis Malik Khamis (Uwakilishi) Jimbo Koani
Shaaban Iddi Ame (Ubunge)na jimbo la Chwaka Arafa Shauri Mjaka
(Uwakilishi ) pamoja na Ali Khamis Ame (Ubunge).
Wagombea wengine Asha Abdu Haji (Uwakilishi) Jimbo
la Muyuni na Baswira Hassan Suleiman (Ubunge) wakati nJimbo la Tumbe
Mohamed Hemed (Uwakilishi) na Rashid Ali Abdalla (Ubunge) pamoja na
Jimbo la Micheweni Subeit Khamis Faki (Uwakilishi) na Haji Khatib Kai
(Ubunge).
Wengine Issa Said Juma Jimbo la Konde (Uwakilishi)
na Khatib Said Haji (Ubunge) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria
Abubakar Khamis Bakar Jimbo la Mgogoni (Uwakilishi) na Juma Kombo Hamad
(Ubunge) wakati Jimbo la Wete DK Suleiman Ali Yussuf (Uwakilishi) na
Mbarouk Salum Ali (Ubunge).
Hamad Masoud Hamad Jimbo la Ole (Uwakilishi) na
Rajab Mbarouk Mohamed (Ubunge) pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni,
Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk Jimbo la Gando (Uwakilishi) na Othman
Omar Haji (Ubunge).
Katika jimbo la Mtambwe Mwakilishi
hajapatikana kutokana na matokeo ya kura ya maoni kukatiwa rufaa lakini
Khalifa Mohamed amepitishwa nafasi ya (Ubunge) na Jimbo la Kojani Hassan
Hamad Omar (Uwakilishi) na Hamad Salum Maalim (Ubunge).
Jimbo la Chake Chake Omar Ali Shehe
(Uwakilishi) na Yussuf Kaiza Makame (Ubunge) wakati Jimbo la Chonga
Khamis Faki Marango (Uwakilishi) na Moh’d Juma Khatib (Ubunge) Jimbo la
Ziwani Mohamed Ali Salum (Uwakilishi) na Ahmed Juma Ngwali (Ubunge)
Wengine Khalifa Abdalla Ali Jimbo la Wawi
(Uwakilishi) na Waziri wa zamani wa Utalii katika Serikali ya Jamhuri ya
Muungano Juma Hamad Omar (Ubunge) na jimbo la Chamabani Mohamed Mbwana
Hamad (Uwakilishi) Yussuf Salim Husein (Ubunge) wakati Jimbo la Kiwani
Hija Hassan Hija (Uwakilishi) na Abdalla Haji Ali (Ubunge).
Katika Jimbo la mkanyageni Tahir Aweis Mohamed
(Uwakilishi) na . Mohamed Habibu Juma Mnyaa (Ubunge) na Seif Khamis
Mohamed Jimbo la Mkoani (Uwakilishi) na Ali Khamis Seif (Ubunge) wakati
Jimbo la Mtambile Abdalla Bakar Hassan (Uwakilishi) na Masoud Abdalla
Salim (Ubunge)
Wagombea hao kwa tiketi ya Chama cha wananchi CUF
ndiyo wanatarajia kuchuana na vyama vingine vitakavyosimamisha wagombea
katika uchaguzi wa mwaka huu.
chanzo: mwananchi
chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment