WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, July 22, 2013

MIILI YA WANAJESHI WA ZANZIBAR WALIOFARIK​I DAAFUR YAWASILI ZANZIBAR


02 bcd22
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza la Sajent Shaibu Shehe Othman aliyeuawa Daafur katika harakati za kulinda amani chini ya Kikosi cha Umoja wa Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar
hdg
01 ad2b1
Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
02 6fdd8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam
03 1edf7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla
7 b6b52
8 654fbBaadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo. hdg

source: mjengwa blog

Sunday, July 21, 2013

Mugabe ni giza, Mandela ni nuru - Maggid Mjengwa

 


DAIMA Mzee Nelson Mandela atabaki kuwa nuru kwa Wana wa Afrika na hata watu wa dunia. Hata siku atakapotutoka duniani, basi, itakuwa kimeondoka kiwiliwili chake tu, lakini, fikra za Mandela zitabaki nasi, hivyo Mandela ataishi milelele.

Mandela atabaki kuwa nuru yenye kutuangazia na kutupa matumaini. Mwanga wake hautafifia, bali, nuru yake itaambukiza wengine, hivyo, nuru nyingine zitachomoza. Mandela ni matumaini. Ni matumaini ya uwezekano wa uwepo wa jamii yenye kuishi pamoja bila ubaguzi wa rangi, dini, kabila. Na pia, jamii isiyo na ubaguzi wa kisiasa. Mandela ametufundisha, kuwa jamii kama hiyo inawezekana kuwepo.

Lakini ona mfano wa  viongozi wenye kuleta giza badala ya nuru ya matumaini; Robert Mugabe ni
mfano wa viongozi hao. Tunaona , kuwa Mugabe amedhamiria kufia madarakani. Na anafanya yote kuhakikisha hilo linawezekana, bila kujali Wazimbabwe wengine.

Mugabe amevidhibiti vyombo vya habari na anawaandama wote wenye kupingana nae. Kuna Wazimbabwe waliopoteza na wanaoendelea kupoteza maisha yao kwa kupingana na Mugabe. Kuna wengi pia walioikimbia nchi yao.

Mugabe kama ilivyokuwa kwa Mobutu wa Zaire na madikteta wengine wa Afrika, naye  anataka na anapenda, Wazimbabwe wamuimbe yeye. Wampigie makofi hata kwa kauli za kipumbavu. Mugabe anashindwa kuelewa, kuwa unaweza kumpeleka punda mtoni, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji. Kwamba unaweza kumlazimisha mwanadamu kukupigia makofi, lakini kamwe si kutabasamu. Hilo la mwisho hutoka moyoni.

Mara kadhaa Mugabe na kundi lake wameshiriki kuendesha chaguzi za kihuni. Kuna kila dalili,  kuwa mwanzo wa mwisho wa Mugabe umefikia. Mugabe amewatumbukiza Wazimbabwe kwenye shimo refu na lenye giza nene. Hakika, Mugabe amewapeleka Wazimbabwe wengi motoni wangali bado duniani.  Ndipo hapa unajiuliza busara za kutamka kuwa mtawala ni chaguo la Mungu! Hivi Mugabe nae ni chaguo la Mungu? Mobutu na  Idi Amin nao walikuwa chaguo la Mungu?

Hakika, Zimbabwe ni mfano wa kutia majonzi. Nilibahatika kufika Zimbabwe kwa mara ya kwanza mwezi Desemba mwaka 1987. Ni miaka 26 iliyopita. Niliyoiona wakati huo ni nchi ilionyesha dalili zote za kunawiri kiuchumi. Niliiona Zimbabwe yenye umri wa miaka 7 tangu ipate uhuru wake. Kama ni mtoto , basi ulikuwa ni umri wa kwenda shule. Ndio, nchi ilinawiri, kwa dola moja ya Zimbabwe mfukoni niliweza kula mlo mmoja wa mchana na chenji ikabaki.

Miaka 26 iliyopita sikuishia Harare tu, nilifika mji wa Bulawayo pia katika Zimbabwe hiyo hiyo. Huko  nikaona dalili hizo hizo za matumaini. Nikaenda hadi vijijini, sehemu za Mberengwa karibu na mpaka wa Msumbiji. Huko nikaona pia dalili za matumaini. Watoto walikwenda kwenye shule zenye kutoa elimu bora kuanzia ngazi ya msingi. Huduma za afya nazo zilikuwa bora. Kwa wakati huo, Mugabe na chama chake ZANU walijitahidi kuhakikisha Wazimbabwe wanapata elimu bora na huduma nyingine kama vile afya.

Miaka kumi baadae, mwaka 1997 nikafika tena Zimbabwe. Nikaanza kuona dalili za treni inayoacha njia. Niliyaona hayo Harare, Bulawayo na kule Nyanga, mbali sana na mjini. Ikawa ni tofauti kubwa na 1987. Kinachomtokea Mugabe leo ni kile alichokipanda mwenyewe lakini anaogopa mavuno yake. Watoto wale niliowaona kule kijijini Mberengwa miaka 26 iliyopita ndio "Wanaomsumbua" Mugabe sasa. Wamepata elimu bora, sasa wanayaona mapungufu pia. wanataka kushiriki siasa za nchi yao kupitia vyama vingi. Mugabe ameshindwa kusoma alama za nyakati. Wengi wa vijana wale aliowasomesha wakaja kuwa manesi bora barani Afrika, walimu bora pia. Leo wengi wao wamekimbilia ughaibuni,  Mugabe hawataki tena. Kwa Mugabe, hao "wameelimika sana!" Lakini, waliokimbia Zimbabwe nao wanawaamsha wenzao walio nyumbani, vuguvugu la kutaka mabadiliko linaendelea.

Mugabe nae anakikimbia kivuli chake. Hata kama amedhamiria kufia madarakani, kifo chake kitabaki kuwa ni cha aibu. Mugabe wa sasa anarudisha nyumba mshale wa saa ya kuelekea kwenye maendeleo ya Zimbabwe na watu wake. Huu ni wakati wa Wazimbabwe kuongeza ari ya mapambano yao dhidi ya utawala dhalimu wa Mugame na kundi lake. Ni wakati wa kufanya mabadiliko.

Na somo kubwa tunalojifunza hapa, ni namna gani mtu mmoja au kikundi cha watu kinavyoweza kuiingiza nchi shimoni kwa sababu za kifisadi. Ni imani yetu, kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho. Nuru ya Mzee wetu Mandela inatuangazia, na tunauona sasa  mwanzo wa mwisho wa Mugabe. Si mwisho wa mwanzo wa Zimbabwe.

Naam, Mugabe ni giza, Mandela ni nuru.

Mungu Ibariki Afrika.
0754 678 252
MjengwaBlog.com

Kilio kwa makamanda waliokufa Darfur

 

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza moja kati ya saba ya miili ya askari wa Tanzania waliokuwa katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Jeshi (Airwing) Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix 
 

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji kupokea miili saba ya wanajeshi wa Tanzania waliouawa Darfur, Sudan, Julai 13, mwaka huu.

Miili ya wanajeshi hao saba iliyowasili jana ni SajIni Shaibu Sheha Othman, Koplo Osward Paulo Chaula, Koplo Mohamed Juma Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Peter Werema na Private Fortunatus Msofe.

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), kusini mwa Darfur na walitoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma, Songea, 44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa wanajeshi hao waliuawa na kikundi cha waasi cha Janjaweed kinachoungwa mkono na serikali ya Sudan, huku wengine 19 wakijeruhiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yametekwa na kundi hilo.

Hali ilivyokuwa
Baada ya miili hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi saa 10:40 jioni na ndege ya Antlantis iliyotolewa na Umoja wa Mataifa(UN), mamia ya watu waliokuwapo uwanjani hapo walionekana kuingiwa na huzuni baada ya kuona miili ya marafiki, ndugu na jamaa zao ikishushwa kwenye ndege hiyo.

Baada ya ndege hiyo kuwasili, viongozi wakuu wa Serikali pamoja na wambolezaji wengine waliisogelea ndege hiyo kwa ajili ya kupokea miili ya wanajeshi hao.

Miili hiyo ilishushwa na kuingizwa kwenye magari saba ya jeshi, na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi la Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Wanajeshi hao wanatarajiwa kuagwa kesho Jumatatu katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi Upanga, baadaye miili hiyo itasafirishwa kwenda kuzikwa katika maeneo yaliyotengwa na familia zao.

Waombolezaji
Baadhi ya ndugu wa marehemu waliofika kwenye viwanja hivyo walisema kuwa walikuwa wakiwategemea sana ndugu zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema mara baada ya kupata taarifa za vifo hivyo, walishtuka na kutoamini kilichotokea huku wakieleza kuwa walikuwa wanawasiliana nao mara kwa mara wakati wakiwa Darfur.

“Tuliwasiliana na baba (Koplo Mohamed Chukilizo wa kikosi cha 41KJ, Majimaji, Nachingwea), siku chache kabla ya kifo chake, aliniambia anarudi hivi karibuni na kunitaka niendelee vizuri na masomo,” alisema Amina mtoto wa marehemu Chukilizo.

Aliongeza, “Baada ya wiki mmoja tulipewa taarifa za kifo chake, jambo hili lilitustua sana na hatukuamini kabisa.”

Amina ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Nachingwea alisema mpaka sasa hajui hatima yake katika elimu kwa sababu alikuwa akimtegemea baba yake kwa kila kitu.

Binti huyo aliyekuwa ameongozana na mama yake, hawakuwa na ndugu yeyote wa familia ya baba yake waliomsindikiza.

Chukilizo atazikwa mkoani Kigoma mara baada ya kukamilika kwa taratibu za mazishi.

Naye Msemaji wa familia wa marehemu, Sajini Shaibu Othman kutoka Makao Makuu ya Jeshi Upanga (MMJ) jijini Dar es Salaam, Mohamed Sadiki alisema kuwa marehemu ameacha mjane na watoto watatu.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, walishtuka na kutoamini kilichotokea.

“Tumeshtushwa sana na tukio hilo, hatukuamini kabisa kwa sababu tulikuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa, na ameacha mama yake mzazi, mjane na watoto watatu,”alisema Sadiki.

Aliongeza, marehemu alikuwa anaishi Kigamboni, kwamba atazikwa Zanzibar kwa maelezo kuwa ndiko familia ilikopendekeza kumzika.

Naye mke wa marehemu, Oswald Chaula kutoka kikosi 42KJ Chabruma, Songea, Maria Chaula alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walipatwa na mshangao na walikusanyika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kupanga taratibu za mazishi.

“Nilipopata taarifa za msiba huu wa mume wangu nilihisi kuchanganyikiwa. Mume wangu tegemeo langu niliomba arudi salama ili tuweze kupanga maisha yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema kwa uchungu Maria.

Hata hivyo, waombolezaji wengine walishindwa kuongeza chochote katika eneo hilo, huku wakionekana kulia wakati wote tangu walipofika kwenye eneo la uwanja huo hadi miili ya wapiganaji hao ilipowasili.

Hata hivyo, Kaimu Msemaji Mkuu wa JWTZ, Meja Joseph Masanja alisema kuwa, miili ya wapiganaji hao imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi kwa ajili ya kusubiri utaratibu wa kuagwa ifikapo Jumatatu ili iweze kusafirishwa vijijini kwao.

“Ratiba iliyopo ni kupokea miili ya marehemu na kwenda kuihifadhi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, na ifikapo Jumatatu majira ya saa 2:30 asubuhi itapelekwa kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi kwa ajili ya kuaga,”alisema Meja Masanja.

Dk Bilal aliongozana na mke wa Rais, Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)Said Mwema.

source: Patricia Kimelemeta  Mwananchi VIA Mjengwa blog

Saturday, July 20, 2013

Nyerere: Serikali corrupt haikusanyi kodi - Sehemu ya hotuba “Nyufa”


Nguvu ya kudai kodi kwa Wamachinga, Wenye magenge, SIMCard, Wafanyakazi n.k. VERSUS nguvu ya kudai kodi kwa mfano:
  1. Raia wa kigeni akwepa kulipa kodi kwa miaka 8 - Habarileo Julai 20, 2013
  2. Serikali imewekwa mfukoni na Said na Ghalib Saad wa Home Shopping Center? - Rai 2010
  3. Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center - JamiiForums, 2012.

'All animals are equal, but some animals are more equal than others,' Animal Farm, book by George Orwell.
Nazungumza habari za kutokusanya kodi. Kutokusanya kodi ni sifa moja ya viserikali corrupt popote pale. Popote, wala usifikiri ni Tanzania peke yake, au Kenya peke yake... Italy pale. Italy, serikali iliyotoka hii wana mzigo wa madeni. Serikali corrupt popote pale, haitozi kodi. Serikali corrupt inatumwa na wenye mali. Inawafanyia kazi wenye mali. Serikali corrupt itamwambieje mwenye mali, kwamba “utalipa, uspolipa utakiona!" Atacheka tu huyu. Atakwambia “unaniambia hivyo wewe? kesho siji basi!”

Serikali ya wala rushwa haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi basi. 

Nukuu ya sehemu ya alichokisema hayati Mwl. Julius K. Nyerere, kuanzia dakika ya 16:32. 
Hotuba nzima imepachikwa hapo chini (youtube video).
Miiko ya Uongozi — Zamani tulikuwa na kitu kinaitwa miiko ya uongozi wakati wa TANU, zilikuwa zinaitwa Kanuni za TANU. Na kanuni moja ya TANU, ambayo baadaye tukarithi katika CCM au tukairithisha CCM, inasema; “Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa”.

Usije ukadhani kwamba wakati wa awamu ya kwanza palikuwa hapana rushwa; ilikuwapo, lakini tulikuwa wakali sana. Siku za mwanzo kabisa, tulitaka watu wajue hivyo. Tulitaka watu watu wajue kwamba tutakuwa wakali sana na wala rushwa ndani ya serikali na wale wanaotoa rushwa. Mwanzo kabisa wakujitawala tulitaka kila mtu ajue. Tukapitisha sheria kwamba mtu akila rushwa, eh! Kiongozi wetu anakula rushwa: anayetoa, aliyepokea, Wazanaki wanasema manzi ga nyanza yaani, wote wanapata msukosuko.

Rushwa! Sasa Tanzania inanuka kwa rushwa. Ufa mwingine tulioupata. Tunataka kiongozi anayejua hivyo ambaye atasema “rushwa kwangu ni mwiko.” Mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa na wanamjua watoa rushwa: watamjua hivyo. Lakini hatutaki aishie hapo tu. Maana haitoshi wewe mwenyewe uwe mwaminifu. Mambo haya yana matatizo. Unaweza ukawa wewe mwenyewe mwaminifu kabisa, safi kabisa, lakini una presha za ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako. Kwa hiyo, sio kwamba inatosha wewe uwe mwaminifu tu, bali uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa na rafiki zako kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena, IKULU NI MAHALI PATAKATIFU. Unawaambia ngu zako na jamaa zako na marafiki zako firmly kabisa kabisa ‛Ikulu ni mahali patakatifu. Mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi.” Ukishakuwaambia hivyo ndugu na rafiki zako na ikajulikana hivyo, mtu wala hakusogelei. Nafsi yake haimtumi kukusogelea.

source: wavuti.com

Thursday, July 18, 2013

Sherehe ya Mandela hospitalini Medclinic


 
Raia wa Afrika Kusini akiwa na bango la kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Mstaafu wa nchi hiyo, mjini Polokwane nchini humo.

Johannesburg: “Happy birthday Mzee Madiba.” Rais wa kwanza na mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, leo anatimiza umri wa miaka 95, pia anatimiza siku ya 40 tangu alipolazwa katika Hospitali ya Medclinic, Pretoria kwa ajili ya matibabu.

Nelson Rolihlahla Mandela, alizaliwa Julai 18, 1918 katika Kijiji cha Mvezo, eneo la Mthatha, Transkei Mkoa wa Eastern Cape na ametumia zaidi ya asilimia 70 ya maisha yake akipigania haki na usawa wa wananchi wa Afrika Kusini.

Maadhimisho ya miaka 95 tangu kuzaliwa kwa Mandela yanabeba uzito mkubwa kuliko maadhimisho mengine yaliyotangulia kwani kwa siku 40, wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa katika wasiwasi mkubwa hasa kutokana na kuzorota kwa afya ya kiongozi huyo.

Mandela alilazwa katika hospitali hiyo Juni 8, mwaka huu akiugua magonjwa ya figo na afya yake imeelezwa kuwa ni mbaya.

Leo, Rais Jacob Zuma atawaongoza mamilioni ya wananchi wa Afrika Kusini katika maadhimisho ya nne ya kimataifa ya ‘Siku ya Mandela’ ambayo yanakwenda sambamba na siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Tangu kulazwa kwa Mandela huko Pretoria, Rais Zuma amekuwa akiwahimiza wananchi wake wajiandae kusherehekea miaka 95 ya Mandela akiwatia moyo wale waliokuwa na wasiwasi kwamba Madiba asingeweza kuifikia leo kutokana na matatizo ya kiafya.

Siku ya Mandela huadhimishwa kuenzi kazi za kiongozi huyo alizozifanya kwa miaka 67 akiutumikia umma wa wananchi wa Afrika Kusini, zikiwamo vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na hatimaye kuwa Rais wa kwanza mzalendo kwa miaka mitano, kisha kustaafu.
Pia ‘Mandela Day’ hutumika kukumbuka kampeni yake dhidi ya ubaguzi wa rangi na utetezi wa haki za binadamu maarufu kwa jina la “46664”, ambayo ni namba ya utambulisho aliyoitumia alipokuwa mfungwa katika Gereza la Visiwa vya Robben.
Dakika 67 za Mandela

Kwa maana ya Siku ya Mandela ambayo pia imeidhinishwa na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, wananchi wa Afrika Kusini wanatumia dakika 67 kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni hatua ya kuenzi kile wanachokiita ‘kazi za mtu aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kupigania haki na utu’.

Dakika hizo 67 zinawakilisha idadi kama hiyo ya miaka ambayo Mandela alitumika, hivyo Waafrika Kusini watakuwa wakitoa msaada na huduma kwa jamii iwe ni kwa watoto yatima au watu wengine ambao ni wahitaji katika jamii.

Kituo cha Kumbukumbu ya Mandela kimewataka wananchi kuungana na kuonyesha ushirikiano wao kwa Mandela kwa kutumia dakika 67 za muda wao kuzisaidia jamii zao ili kumuenzi kiongozi huyo ambaye ni alama ya dunia.

Kumbukumbu za kihistoria zinaonyesha kuwa alianza kampeni na harakati za kutetea haki za binadamu mwaka 1942 na baadaye mwaka 1964 alikamatwa na kuwekwa gerezani alikokaa miaka 27 lakini alipotoka aliwatumikia Waafrika Kusini akiwa rais wao wa kwanza mzalendo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho, Sello Hatang aliwataka Waafrika Kusini kufanya shughuli yeyote ile au msaada ambao utakuwa ni mchango kwa jamii yao.

“Watu wafanye kile wanachoona kinawapendeza, watumie dakika 67 za kumuenzi Mandela. Ni vyema wakafanya kitu ambacho kinawafurahisha ili waendelee kukifanya kila mwaka katika maisha yao”, alisema Hatang.

Alisema Waafrika Kusini wanaweza kumuenzi Mandela kwa kuwasaidia wazee na watoto yatima katika vituo mbalimbali, kufanya usafi au kuwatazama na kuwapa chochote wagonjwa.
Miaka 15 ya ndoa

Siku hii pia inakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 15 ya ndoa yake na mke wake wa tatu; Graca Machel ambaye walifunga naye ndoa Julai 18, 1998 wakati wa kumbukumbu ya miaka 80 ya kuzaliwa kwake.

Pia siku hii inaadhimishwa siku tatu baada ya kutimia miaka 69 tangu Mandela alipofunga ndoa na mkewe wa kwanza Evelyn Mase Julai 15, 1944. Evelyn ambaye sasa ni marehemu alikuwa muuguzi, pia binamu wa aliyekuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini, Walter Sisulu.

Graca ndiye mtu wa karibu zaidi na Mandela kwa sasa na kwa siku 40 amekuwa akiishi hospitalini Medclinic akimuuguza mumewe na mchana kutwa amekuwa akikaa pembezoni mwa kitanda cha Mandela na pale anapochoka hasa usiku, hulala kwenye chumba kinachopakana na kile alicholazwa mumewe.

Ndugu wengine kutoka familia ya Mandela wamekuwa wakifika hospitalini mara kwa mara kumjulia hali kisha kuondoka. Miongoni mwao ni pamoja na mtalaka wake, Winnie Madikizela-Mandela pamoja na binti yake mkubwa, Makaziwe ambaye ni binti pekee wa Mandela aliye hai aliyemzaa kwa Evelyn miaka 60 iliyopita.

Nje ya Medclinic, kuta za uzio unaozunguka hospitali hiyo zimeendelea kupambwa kwa kadi, michoro, picha, maua na ujumbe ambao unamtakia heri ya kupona haraka Mzee Mandela. Hata hivyo, leo pengine na siku chache zijazo kuta hizi zitageuzwa kuwa mahali pa salamu za pongezi kwa Mandela kufikisha umri wa miaka 95.

Mbali na hayo, kwenye kuta za Medclinic, katika lango la kuingilia hospitalini hapo, nyimbo na sala vimeendelea kusikika kutoka makundi mbalimbali kumwomba Mungu ampe maisha marefu zaidi.

Miongoni mwa vikundi vilivyokuwapo hapo vikipaza sauti zao ni kwaya ya Shule ya Sekondari ya Juu ya Wasichana ya Oranje ambao ni siku chache tu ilirejea kutoka katika tamasha la muziki la vijana huko Slovakia na kupata ushindi dhidi ya vikundi vingine 22.
Mandela ni nani?

Kwa jumla, Mandela unaweza kumwita utakavyo kwa maana ya ukombozi na Afrika Kusini ya sasa. Kwa maana hiyo ni mwanasiasa, mpigania uhuru, mwanasheria, mfungwa wa uhaini, Baba wa Taifa la Afrika Kusini, Chifu wa Wathembu na zaidi ya yote, Rais wa Kwanza Mzalendo wa Afrika Kusini.

Nelson Rolihlahla Mandela ni mtoto wa Mama Nonqaphi Nosekeni na Mzee Henry Mgadla Mandela ambaye alikuwa Kiongozi wa Kimila (Chifu) katika jamii ya Wathembu.

Awali, kabla ya kuitwa Nelson, alijulikana kwa jina lake la kati, Rolihlahla ambalo maana yake ni ‘kungo’a tawi kutoka kwenye mti’ au kwa maana isiyo rasmi ‘mtu mkorofi’. Jina la Nelson alipewa na mwalimu wake alipojiunga na shule ya wamisionari.

Mandela aliishi na baba yake kwa miaka 12 tu kwani mzazi wake huyo alifariki dunia mwaka 1930 na kuanzia hapo alilelewa na mpwa wa baba yake, David Dalindyebo ambaye pia alikaimu uongozi wa katika jamii ya Wathembu.

Mwaka 1944, Mandela alioana na Evelyn ambaye alijaliwa kupata mtoto wa kiume mwaka 1945 na kumwita Madiba Thembekile (Thembi kwa kifupi). Hata hivyo, mtoto huyo alifariki katika ajali ya gari mwaka 1969 wakati Mandela akiwa jela.

Mandela na Evelyn walijaliwa kupata watoto wengine watatu; Makaziwe mkubwa ambaye hata hivyo, alifariki dunia akiwa mchanga 1948, Makgatho Mandela aliyezaliwa 1950 na kufariki 2005 na Makaziwe mdogo mwaka 1953 ambaye kwa jumla ndiye anayesimamia shughuli na mali katika familia hivi sasa.

Desemba 1956 alikuwa mmoja wa washtakiwa wa kesi ya uhaini na wakati kesi hiyo ikiendelea alioana na Nomzamo Winifred Madikizela mwaka 1958. Alibahatika kupata naye watoto wawili wa kike.
Kijijini Qunu

Kumekuwa na harakati nyingi za maadhimisho ya Siku ya Mandela na mojawapo ni tukio la Waafrika Kusini wawili waliopanda Mlima Kilimanjaro kumuenzi.
Katika Kijiji cha Qunu, vijana wamejipanga kusafisha mitaa, kupaka rangi shule, huku wanasiasa wakitumia kila mmoja dakika 67 kuzindua au kukamilisha mradi wowote wa kitaifa.

Watoto wote katika shule za msingi na sekondari wametakiwa kuanza vipindi vyao vya masomo kwa kuimba ‘happy birthday’ Mandela.

Msemaji wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, huko Port Elizabeth, Jean Makasiwe alisema kila mhadhiri, mwanafunzi na mfanyakazi wa chuo hicho atashiriki kwa namna moja au nyigine kumuenzi Mandela.

“Natumaini kuwa kila mmoja atashiriki, ingawa yeye Mandela hataifurahia siku hiyo muhimu kwake, lakini tuna hakika atafanya hivyo wakati akiadhimisha miaka 96 hapo mwakani,” alisema Makasiwe.

Alisema chuo hicho kilijengwa kwa kumbukumbu ya Mandela, hivyo ni lazima kila mmoja ajitoe kumuenzi baba huyo wa taifa.

Rais Zuma leo atakabidhi nyumba 300 kwa wazungu wa eneo la Bethlehemu huko Pretoria ambao wanaishi katika makazi duni.
Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon amewataka watu wote duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya kazi nzuri kwa watu na kwa dunia.
“Hii ndiyo namna pekee ambayo tunaweza kumlipa mtu huyu wa kipekee ambaye alijitoa kwa namna ya pekee kuwasaidia watu wa taifa lake,” alisema Ban na kuongeza:

“Mandela alitumia miaka 67 kupigania haki za binadamu, usawa na umoja. Katika kuadhimisha siku hii, UN inashiriki kwa kuwataka watu ulimwenguni kutoa dakika 67 za muda wao kwa ajili ya kuadhimisha.”

Watu tisa kati ya 10 Afrika Kusini, wapo tayari kushiriki kikamilifu kusherehekea na kutoa muda wao kumuenzi Mandela.

Asilimia 89 ya watu 16,046 waliofanyiwa uchunguzi wamekubali kutoa dakika 67 za muda wao kwa ajili ya kufuata njia ya kujitoa kwa jamii kama Mandela alivyofanya.

Utafiti huo uliotolewa jana na Kampuni ya Pondering Panda ulionyesha kuwa karibu Waafrika Kusini wote wapo tayari kusherehekea Sikukuu ya Mandela kwa kujitoa kusaidia, kuchangisha fedha, kufanya usafi, kuhudumia wagonjwa na yatima.

“Idadi hii inaonyesha kuwa tutafanya mambo makubwa hapa nchini kupitia siku hii, hapo kesho (leo), tunataka kila mtu aonyeshe kuijali siku hii kama Mandela alivyosema,” alisema Msemaji wa Pondering Panda, Shirley Wakefield.

Alisema Siku ya Mandela iliundwa maalumu kwa ajili ya kuwaunganisha Waafrika Kusini wote wenye mapenzi mema kwa nchi yao na duniani kote.

Katika eneo la Upington, kundi la wazee linamuenzi na kumshukuru Madiba kwa kuwapa eneo la makazi na wanasema pasipo jitihada zake za 1998, wasingeweza kupata eneo hilo.

Huko Eastern Cape alikozaliwa Mandela, baadhi ya shule za msingi zilinufaika na Wiki ya Mandela baada ya kupata ufadhili wa seti zote muhimu za vifaa vya kompyuta ambavyo awali hawakuwa navyo.

source: mwananchi

Wednesday, July 17, 2013

Nyuma ya ushujaa wa huyu Mandela yupo Kambarage!




UKIZUNGUMZIA mashujaa wa Afrika ni lazima kutaja majina ya Kwame Nkrumah wa Ghana, Patrice Lumumba wa Kongo, Benjamin Nnamdi Azikiwe na Abubakar Tafawa Balewa wa Nigeria, na wengine wengi, orodha inaweza kuwa ndefu lakini si ndefu kiasi hicho, na bila shaka juu ya orodha hiyo yuko Nelson Rolihlahla Mandela na Julius Kambarage Nyerere.

Katika orodha hiyo ndefu, dunia na hata baadhi ya Watanzania wanamjua au kumsikia zaidi Mzee Mandela au Madiba kama wanavyopenda kumuita watu wake. Mzee Madiba yuko taabani hospitalini, bila shaka si rahisi tena kuona tabasamu lake, haitakuwa kazi rahisi kuona macho yaliyobeba uchungu wa mateso makali ya serikali ya kibaguzi lakini yanayohubiri amani na msamaha, walau  kitu kimoja kiko dhahiri popote na kwa yeyote anayetaka kukiona, ni jinsi historia ilivyomuandika, maandishi yako wazi kwa kila mwenye macho ya kuona, na akili ya kuelewa, yu aelekea kuvikwa taji ya haki.

Ni vigumu kweli kuandika au kumzungumzia mtu wa kiwango cha Madiba,  lakini inaweza kuswihi kuanza na mchapuo huu. Mapema mwaka  2005 wakati huo akiwa Seneta, Barack Obama, alipata fursa kuhudhuria kipindi cha television cha Oprah Winfrey na katika mazungumzo, Oprah alimpatia fursa  Obama ya kumpa ujumbe wowote anaotaka ampelekee Mzee Nelson Mandela.

Obama aliingia chumba cha nyuma ya studio ya Oprah kuandika ujumbe huo kwa Mandela, ilipoonekana amechukua zaidi ya muda uliotarajiwa katika kuandika ujumbe huo, msemaji wake Roberts Gibbs alimfutata kumwangalia ni kitu gani kimemchukulia muda namna hiyo.

Akiwa bado anatafakari nini kuandika, Obama alimwambia msemaji wake; "Ni lazima mnipe muda wa kutosha, huwezi ukaandika ujumbe mwepesi mwepesi tu kwa Nelson Mandela". Anaandika  mwandishi Michael D. Shear wa New York Times, toleo la Juni 27, mwaka 2013.

Hakuna ubishi juu ya ushujaa wa Nelson Mandela na heshima anayopata duniani, yeye ni ishara ya amani na maridhiano, ni alama ya ushirikiano dhidi ya chuki na visasi. Ni Mwafrika pekee mwenye sanamu katika eneo maarufu jijini London la Parliament Square, sanamu yake ikiwa sambamba na sanamu za watu maarufu duniani kama Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln, Waziri Mkuu Uingereza Winston Churchill.

Lakini huyu Mandela amefikaje hapo? kama Waswahili wasemavyo ukiona vyaelea ujue vimeundwa, bila shaka Nelson Mandela wa leo asingekuwa Mandela huyu tunayemfahamu bila kuwepo juhudi za watu waliokuwa na fikra na misimamo thabiti ya kupambana dhidi ya ubaguzi rangi wakati akiwa gerezani kwa miaka yote 27 na hata kabla ya hapo.

Miongoni mwa watu muhimu waliomfanya Mandela huyu awe hivi alivyo leo, anayeweza kuchukua nafasi ya kwanza ni Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza Tanganyika na Tanzania, msimamo wa dhati na usioyumba wa Nyerere dhidi ya aina zote za dhuluma ndiyo umejenga msingi ushujaa wa Mandela unaojulikana duniani leo.

Kwa maneno yake mwenyewe, Nelson Mandela, katika dhifa aliyoandaa kwa heshima ya Mwalimu Nyerere, Oktoba 17 mwaka 1997, alimwelezea Mwalimu kama mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Jumuiya ya Madola kuitenga Afrika Kusini ya kibaguzi, baada ya mauaji ya Sharpville.

"Huyu ni mpigania Uhuru ambaye aliitika wito wa Chifu Luthuli kuungana na Trevor Huddleston kuanzisha vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi nchini Uingereza mwaka 1959, kiongozi ambaye juhudi zake katika mkutano wa Jumuiya ya Madola zilisababisha Afrika Kusini ya kibaguzi kutengwa, baada ya mauaji ya Sharpville.
Nilipata bahati kukutana naye miaka mingi iliyopita, mwaka 1962, nilipozuru Tanzania kutafuta msaada tulipoanzisha mapambano ya silaha. Wakati huo, kama ilivyo sasa, nilishangazwa na msimamo wake, hamu yake ya kutaka haki na usawa popote, na dhamira yake kwa maslahi ya Afrika"

Wakati tukielekea kupata Uhuru, Mwalimu pamoja na kuwa kiongozi wa taifa changa hakusita kuweka wazi msimamo wake ambao bila kuwa na ujasiri wa kipekee, viongozi wachache sana wangeweza kuwa na msimamo wa namna hiyo hasa msimamo wenyewe unapowawekea wale wanaotarajiwa kuwa wahisani wako.
Mei mwaka 1961 kuelekea mkutano wa mawaziri wakuu wa Jumuiya ya Madola, huku Waziri Mkuu wa Afrika Kusini akitarajiwa kuhudhuria mkutano huo, Mwalimu aliandika makala kwenye gazeti la London Observer ikiweka wazi msimamo wa Tanganyika akisisitiza kuwa Tanganyika haitajiunga Jumuiya ya Madola kama Afrika Kusini wataendelea kuwa wanachama.

Makala hiyo iliyohitimishwa kwa maneno mazito yenye msisitizo; "To vote South African in, is to vote us out" kwamba kuwakubalia Afrika Kusini uanachama ni kutukataa sisi, iliamsha hamasa kubwa dhidi ya sera za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Mwandishi nguli wa masuala ya Jumuiya ya Madola ambaye pia ni mwasisi mwenza wa Umoja wa Waandishi wa Habari wa Jumuiya ya Madola (CJA), Derek Ingram, anazungumzia hatua hiyo ya Mwalimu kuwa ilisababisha shinikizo kubwa kwa Afrika Kusini mpaka ikajitoa; "His move stepped up the pressure on South Africa and led to its withdrawal a few days later."

Mchango wa Mwalimu katika harakati za ubaguzi hauishii hapo, Juni 26, 1959 Kamati ya Jumuiya za Kiafrika (CAO) iliitisha kikao katika ukumbi wa Holbourne jijini London, kuwataka Waingereza wasusie bidhaa za Afrika Kusini, hasa matunda yaliyokuwa yanauzwa kwa wingi katika miji mbalimbali ya Uingereza katika vuguvugu lililoitwa Boycott Movement, Askofu Mkuu Trevor Huddleston, Mwalimu Nyerere na Kanyama Chiume wa Malawi ndiyo walikuwa wasemaji wakuu katika hadhara hiyo na waasisi wa vuguvugu hilo lililokuja kujulikana baadaye kama Ant - Apartheid Movement (AAM).

Tangu mwanzo wa miaka ya 1960 mchango wa AAM katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi ulikuwa hauna kifani, lakini pia ikumbukwe kuwa vuguvugu hilo halikuwahi kuwafurahisha wakubwa kwa sababu ya maslahi yao Afrika Kusini.

Pamoja na Chama cha Labour cha Uingereza, kuahidi kuacha kuiuzia silaha Afrika Kusini kama kingeshinda uchaguzi lakini hata baada ya kuingia madarakani kwa Waziri Mkuu wake, Harold McMillan, ahadi hiyo ilishindwa kutekelezwa kwa vitendo.

Hata alipozuru Afrika Kusini na kutoa hotuba yake maarufu katika Bunge la Afrika Kusini; “The wind of change is sweeping across Africa,” pamoja na kuona huo upepo wa mabadiliko uliokuwa unalikumba Bara la Afrika wakati huo, McMillan siyo tu hakuunga mkono shughuli za AAM lakini alilaani harakati hizo.

Hili halishangazi kwa vile kwa mujibu wa mtandao wa South African History on line (SAHO), katika miaka hiyo ya 1950 Uingereza ilikuwa mshirika mzuri wa biashara wa Afrika Kusini, zaidi ya asilimia 30 ya bidhaa zilizoingizwa Afrika Kusini zilitoka Uingereza, asilimia 28 ya mauzo ya bidhaa za nje za Afrika Kusini ziliuzwa Uingereza. Ukiondoa uhusiano huo wa kiuchumi, kati ya mwaka 1946 na 1959 kulikuwa na Raia wa Uingereza zaidi ya 113, 000 waliokuwa wakiishi Afrika Kusini.

Hizi ndizo juhudi zilizoweka msingi wa mapambano ya dhati dhidi ya aina zote za dhuluma ambazo kwa hakika zisingeweza kufika mbali au kufanikiwa kwa kiwango hicho bila kuwa na nguvu ya Mwalimu Nyerere ambaye, msimamo wake dhidi ukandamizaji wa aina yoyote ile ulikuwa dhahiri hata kwa wasiokubaliana naye.

Kujitolea kwake kulikoifanya Tanganyika na kisha Tanzania kuwa kimbilio na ngome ya kutumainiwa na wapigania uhuru wa Kusini mwa Afrika katika mazingira hatari kama vita baridi vya wakati huo, kwa kiwango cha juu kabisa pamoja na mambo mengine yamechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Afrika Kusini ya Mandela na hata Madiba mwenyewe kuwa jinsi walivyo leo. Na ni uungwana tu kusema kuwa nyuma ya fahari aliyonayo Mandela leo, yuko Julius Kambarage Nyerere aliyeongoza kuwapinga makuburu si kwa sababu ya rangi yao bali matendo yao.

Tuesday, July 16, 2013

WANAJESHI WALIOUWAWA DAFUR WAAAGWA,KUREJESHWA NCHINI


  Mojawap0 ya magari ya askari hao likiwa limeharibika vibaya kutokana na shambulio hilo.
 Miili ya wanajeshi saba wa JWTZ waliouawa katika machafuko nchini Sudani, Darfur.  Askari hao walifariki wakiwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini humo.  Majina yao ni (1)Sajenti Shaibu Othuman, (2)Koplo Oswald Chaula, (3)Koplo Mohamed Juma, (4)Koplo Mohamed Chikilizo, (5)Pte. Rodney Ndunguru, (6)Pte. Peter Werema na (7)Pte. Fortunatus Msofe
Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania wanaolinda amani nchini Darfur
 On 14 July 2013, following a 13 July attack in which seven military peacekeepers of the African Union - United Nations Mission in Darfur (UNAMID) were killed and 17 military and Police personnel wounded, among them two female Police Advisers, Joint Special Representative Mohamed Ibn Chambas visited the wounded peacekeepers at UNAMID’s hospital in Nyala to provide encouragement and support.
Picha juu na chini Askari wa Tanzania wa Kikosi cha Kulinda Amani Darfur wakiwa wamelazwa mjini Khor Abeche, Sudan juzi baada ya kunusurika kuuawa katika shambulizi lililofanywa na waasi na kusababisha wenzao saba kuuawa na wengine 14 kujeruhiwa.
Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony

He wished quick recovery for the injured soldiers, saying: “I don’t have a lot of words to express my shock and sadness on the soldiers who died while on a very important mission of United Nations, on keeping peace in an area where thousands of people have been killed…” Mr. Kikwete said in a statement issued by the Directorate of Presidential Communications yesterday, adding; “since the fallen servicemen and women were deployed in Darfur in February this year and since Tanzania  started deploying troops in 2007, they have done a good work and the country is proud of them”.
Top Sector leadership led by Mr. Hussain (3rd R) -
UNAMID JSR Dr. Mohamed Ibn Chambas along with Acting Force Commander Lt. Gen. Wynjones Kisamba and Police Commissioner Ms. Hester Adriana Paneras visited the other 17 injured peacekeepers at the same Hospital yesterday. The Mission leadership and the UNSG Ban Ki-moon have condemned the act and called for the Government of Sudan to bring the perpetrators of the “heinous” act to justice.Meanwhile, according to press reports, Tanzanian President JakayaKikwete expressed his deep shock following the incident and he sent condolences to the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF) and the bereaved families.
Maj. Elinami Moshi reads brief CVs of the deceased to the top brass

 Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers
 Prayers from another  chaplain
 Prayers from a chaplain
Military salute as the 'Last Post'  rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes

  The African Union – United Nations Mission in Darfur (UNAMID), held a memorial ceremony, in Nyala, the capital of South Darfur, to honor the seven fallen peacekeepers who lost their lives in the 13 July attack in South Darfur. The bodies are scheduled to be repatriated to Tanzania, the home country of the fallen peacekeepers. In addition to the seven killed, 17 military and police personnel were wounded, among them two female Police Advisors, all of whom are recovering from their injuries in UNAMID’s hospital in Nyala, South Darfur. Photo by Saidi Msonda, UNAMID.
 A section of the top brass
 A portion of  staff members at the ceremony

The TPDF Spokesperson, Lt. Col. KapambalaMgawe, said during a press conference yesterday that a special delegation has been sent to Khartoum and Darfur to talk with the authorities over the incident. Tanzania has a battalion of about 850 peacekeepers in Darfur located at Khor Abeche and Menawashi, South Darfur State.
 Miili ikiweka kwenye gari maaalum tayari kwa safari ya kurejea nchi Tanzania
Start of the last journey home.Photos by Albert González Farran, UNAMID.
 
source: Haki Ngowi