WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, July 9, 2011

WAMACHINGA VS SERIKALI TANZANIA

Wamachinga na Harakati za Kujikomboa au ni harakati za kuwakomesha wengine?

Maswali haya wameulizwa na waandishi wengi sana wa habari kuhusu wamamchinga zidi ya Serikali

·        Je ni nini chimbuko la wamachinga?
·        kwanini 'wamachinga' wanakuwa ni tatizo ?
·        je huduma wanayoitoa inatakiwa na wananchi au haitakiwi ?
·        Ni njia gani zinazoweza kufanyika ili tatizo ligeuzwe ni fursa ya kiuchumi kwa manufaa ya wote? 
·        Je wa wafanyabiashara hao ni wa rika gani wanafikia wangapi hivi sasa?

Ni ukweli kuwa wamachinga ni wachuuzi waliozagaa katika maeneo tofauti wakifanya shughuli zao kiholela ambao waiibuka kwa wingi miaka ya 1980s wakati wa sera za Ruksa. Ni ajira ambayo inaweza kusemwa sio rasmi kama hawalipi kodi lakini kama wanalipa Kodi ni ajira Rasmi kwani taifa linafaidika na kodi yao na kwa msingi huo, na kwa upande mwingine na wao wnafanikiwa kupata riziki inayowasaidia kuendesha maisha yao

Idadi ya Wamachinga “nifikiri” ni  zadi ya wafanya biashara milioni moja: kwa upande mwingine kama ajira zaidi ya Milioni moja zimetengenezwa hapa, taifa limepunguziwa mzigo wa kuwatafutia ajira vijana hao.

Kwa nini wamamchinga wengi wanazagaa sana?
Nafikiri tuyaangalie maeneo ambayo pengine serikali wamewapangia hawa wamamchinga; je Maeneo  hayo yanajitosheleza?  Je yanavutia kibiashara, je kuna usafiri wa kuweza kuwaunganisha wafanya biashara hawa na wateja?

Je wakifukuzwa na wakakosa kuingiza ridhiki hata ya shilling mia moja nini kitatokea?
 Serikali inatakiw akuwa makini kwani, Nafikiri wamachiga wengi kama watafukuwza bila kupewa msaada woote, na kubaki kuwa hawana kazi,watagueka vibaka na kuliletea taifa  na raia wake.

Je serikali kuwafukuza wamamchinga ni suluhisho la tatizo?
Kuwaondoa wamachinga kabla ya kuwaandalia maeneo mbadala ya kufanyia biashashara zao ni mfumo mbaya wa namna serikali isivyojali maisha ya watu wake. Hakuna ustaarabu ulio bora zaidi duniani zaidi ya ule wa kujali uhai wa mtu kwanza kabal ya kumpokonya rizika yake. Wenzetu walioendelea wana progam kama kuwalipa raia wao ambao kwa namna moja au nyingine wameshindwa kufanya kazi “ unemployment Payments” au msaada wa chakula kwa familia za kipato kidogo “ food stamps” hata nyumba za watu wenye vipato vidogo “ low income Housing” sasa tunapowafukuza wamamchinga tunawapa msaada gani? Zaidi ya askari Mgambo kuwapora Mali zao

Tunaiomba serikali pamoja na kufanya maamuzi ya kuwaondoa wamachinga bila utaratibu makini, bado ina nafasi ya kuhakikisha inaboresha mazingira ya machinga hao kufanya biashara huko walikopelekwa, malalamiko ya machinga yanayoendelea hadi sasa kuwa huko walikopelekwa palikuwa tayari pamenunuliwa na baadhi ya watu ambao si wafanyabiashara ni mfano mbaya wa utekelezaji wa zoezi hili na serikali inapaswa kuwajibika katika hilo mapema iwezekanavyo.

Je mfumo wete wa elimu ya msingi inatusaidia katika kutatua tatizo la wamamchinga kuzagaa zagaa?
Nafikiri tunahitaji (innovative education system) mwanafunzi anayehitimu elimu ya msingi au sekondari asiwe tegemezi na badala yake awe mbunifu kwa maendeleo yake binafsi na kwa  Taifa. Zama hizi  zinahitaji hat kam ni mmachinga  inapaswa kuwa mbunifu. Tusitegemee wachinga bila ubunifu katika hizi zama za sayansi na teknolojia.

Kama taifa tutaweza kuuwezesha mfumo wetu wa elimu ukawafundisha vijana wetu Sayansi na teknolojia hii itakuwa ndiyo njia pekee ya kuokoa nguvu kazi inayoendelea kupotea kwa kujiunga na mfumo maisha wa machinga nchini Tanzania.

Je yanayotokea sasa sehemu mbali mbali za wamachinga kupigana na polisi na kuharibu mali za watu wengine hata kuiba ni sahii?
Katika jamii ambayo mambo yake mengi yako shaghalabadhala saa zingine inaonekana ni uonevu na dhuluma kuanza kukamata wavunja sheria wadogo wadogo wanaokidhi haja zao kila siku za. Tatizo hakuna  hakuna mipango madhubuti na mibadala ya kusaidia na kuwafanya wamachinga wajisikie kuwa wanatakiwa kubadilika na kufanya biashara zao kwa taratibu zinazoeleweka; kinachotokea kila tatizo likijitokeza na mapigano kuumizwa na mali kuharibiwa;


Serikali inatakiwa ifanye nini?
Ni ukweli ambao haukwepeki kuwa nchi imeshindwa kutoa ajira kwa vijana na vijana wameamua kujiajiri wenyewe kwa kuuza chochote kile wakipatacho mitaani.

Nakubali kabisa kwamba kitendo cha wafanyabiashara ndogondogo kuamua kufanya biashara zao sehemu yoyote wanayotaka na kujenga vibanda vyao vya biashara sehemu yoyote bila kuzingatia mipango miji ni ukiukaji wa sheria na taratibu za nchi kuhusiana mipango miji.

Kwa hali hiyo suala la biashara ndogondogo ni suala la maisha.
Kwa mtazamo huo tatizo la Wamachinga ni pana kuliko kuwavunjia vibanda vyao na kuwahamishia sehemu maalumu. Ni suala ambalo linatoa wito wa kurekebisha mfumo mzima wa kiuchumi na kijamii tulionao.

Ni suala ambalo linaitaka Serilaki kusimamia utekelezaji wa sheria na kutumia mbinu zote ili kuepusha hasara kwa raia wake. Ni bora kukinga kwa kutumia busara kuliko kuboboa kwa sababu za siasa;
Kwa nini tusiwe tekeleze sherai ya kuwazuia kujenga vibanda sehemu ambazo sio stahili?, tukiweza kuzuia ujenzi ni utu kuliko kuliko kumbomolea hata kama anastahili kubomolewa kwa kukiuka taratibu.

ACCOUNTABILITY:



I cannot give you the formula for success, but I can give you the formula for failure: which is: Try to please everybody.
Herbert B. Swope

Friday, July 8, 2011

LEADERS THINK ABOUT



It is every man's obligation to put back into the world at least the equivalent of what he takes out of it. ~Albert Einstein

JE STAILI YA KUJICHANGANYA YA NAPE ITASAIDIA KUREJESHA UHAI WA CCM?

Huyu ndie KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye



Je nafasi hiyo ambayo chama chake imemkabidhi inamfaa au hapana?

Je staili zake za utendaji zitasaidia kurudisha imani ya wananchama wake hasa wale ambao wamehama au wako wako tu ?





Je kujichanganya kwake na ndani ya maisha ya wanachama wake na wapenda siasa kutasaidia kukiimarisha na kukijengea chama chake  imani? kama ndio je anahitaji watendaji kama yeye amabao ni vijana ambao wana hitaji nguvu ya hoja na sio porojo;












Nape Nnauye kweli ataweza kuokoa Chama kilichofanya vibaya wakati wa uchaguzi kwa kupata kura ambazo hazikutarajiwa; Kijana anayedhani anaweza kuokoa CCM kwa kubadilishana hoja dhidi ya upinzani.


Kabla ya kupata nafasi hiyo alishawahi sema, “Wenzetu wamepiga hatua sana katika ‘accountability’, uongozi si jambo watu wanapigania, maana tunahitaji maadili makubwa na mara nyingi ku-sacrifice kwa mengi, hivyo anayekwenda hata kama si wote, anakuwa kaamua kweli kuwatumikia watu... Tulikuwa nayo hii kwenye Azimio la Arusha na nadhani sasa ni muhimu sana kuliko mwaka 1967 lilipoanzishwa,” alisema Nnauye.



Alisema kwa siasa za Tanzania, bado kuna safari ndefu ya kwenda tunakotaka japo kuwa yapo mazuri, lakini pia yapo mapungufu yanayopaswa kufanyiwa kazi na vyama vya siasa ili kuweza kujenga demokrasia ya kweli.


Je kauli zake hizi ndizo anazozifanyia kazi sasa au naye anarudi kule kule nyuma akifuata mapigo ya Gitaa ambalo pengine ni bovu au nyuzi zake zimelegea, au mpigaji hajui au hana uzoefu au tatizo la uelewa au ni woga hajelizoea hilo gitaa, au anaogopa vitisho vya wasikilizaji.

Kila la kheri Bwana Nape wana CCM wameonyesha kukusikiliza

Sunday, June 26, 2011

KWA NINI TUNASHINDWA KUTEKELEZA SHERIA ?



Kwa nini sheria hazifuatwi katika maisha ya kila siku ya mtanzania  tatizo liko wapi? Sheria hazieleweki au sheria zimejaa mianya mingi inayoruhusu kutofuatwa katika utekeleji wake?

Tunapaswa kufanya nini ili kuhakikisha kuwa harakati za kutetea na kuona kuwa sheria zinafuatwa, zinafanikiwa bila kuvunja misingi ya utawala bora na wa sheria?

Je "Watu wote ni sawa mbele ya sheria, au wengine wanayo haki zaidi kutokana na umaarufu wao?.

Je utekelezaji wa sheria unafanyika bila ubaguzi wowote, na kumwezesha kila raia keheshimiwa na kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria"?


Ni kwa namna gani tunaweza kujenga mfumo wa utawala wa sheria usioipa nafasi dola kutumia kiujanja mianya ya kisheria na kupata nafasi ya kutotekeleza kanuni za sheria na kama itatekelezwa kuchukua muda mrefu ili kupunguza nguvu ya kosa katika kuleta haki inayotakiwa kwa jamii?

Je Migomo, maandamano, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali unaofanywa kutoka na matukio haya ni sababu ya kwisha kwa uvumilivu kutoka na uzembeaji katika kutekeleza sheria au ni mazoea tu yaliyojengeka mbele ya raia au jamii?

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa miaka takribani 50 ya uhuru wa  nchi hii wananchi wameweza kuona ni kwa jinsi gani matatizo yanayoikumba nchi Tanzania yanazidi kuongeza licha ya kuwepo utawala wa sheria. Na wakati huo huo kuna vyombo na taasisi mbalimbali za kisheria zenye nguvu na mamlaka ya kushughulikia zikiwa zimepewa nyenzo na nguvu za kisheria katika kutekeleza majukumu yao, cha kushangaza ni kuwa taasisi au idara hizo zipo na pengine zinaangalia tu bila kuwajibika. Je zinaogopa au hazioni umuhimu wa kuwajibika kwa sababu za masilahi zaidi?

Je hii inatokana na ukweli kuwa pengine sheria pamoja na kupitishwa na vyombo husika lakini utekelezaji wake lazima ubarikiwe na kikundi kidogo cha wenye mali Mafisadi ili itekelezwe kwa matakwa yao.

Kama ni hivyo basi sheria iko kwa ajili na kwa manufaa ya nani? Je sheria zinatungwa na matajiri kuwazuia maskini kuwasogelea matajiri na kuhakikisha matajiri wanaendelea kutumia utekelezaji wa sheria kuwakandamiza maskini; je sheria zinatungwa kuwafurahisha matajiri na kuwaridhisha maskini lakini wakati wote kuwanufaisha watawala!

Ni aibu kama vyombo vya dola vinaweza kumfunga Mmachinga katika siku mbili kwa kosa na kuuza vitu katika sehemu ambayo haijeruhusiwa na wakati huo huo inashindwa kumfunga Fisadi aliyethibitika kuliibia taifa mabilioni ya shilling kwa vile tu eti kwa sababu ya pesa zake anaweza kushinda kesi na kuisababishia serikali hasara zaidi; lo hii ni hatari.

Swali la msingi hapa sheria zetu ni kwa ajili na manufaa ya nani? Kwa nini utekelezaji wake unakuwa na kigugumizi. Nafikiri uzaifu huu wa sheria zetu ndio unaotuletea kila ambacho wananchi kuhukumu na kuchukua hatua ambazo wakati mwingine zinakiuka utaratibu wa utawala bora;

je ni busara haki hata kama iko ndani ya sheria haitatekelezwa mpaka kwa maandamano na migomo;

Haki ya ya matibabu bora haitapatikana mpaka kwa utoaji rushwa;
Haki yangu ya kosa lolote la barabarani haitaeleweka mbele ya askari wa usalama wa barabarani bila ya hongo;

Wananchi wanatakiwa kuelimisha kwa upole na upendo pale wanapokosea na ikibidi adhabu ifanywe kulingana na sheria; mkosa alipe faini yake kihalali ili iwe ni fundisho na pesa hiyo isadie maendeleo ya nchi;

Kwa kufanya hivyo taifa litaweza kuimarisha utawala bora, amabao ni utawala wa sheria, na hapo itakuwa rahisi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa, dawa za kulevya, matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma. Mhalifu anaweza na anapaswa kuadhibiwa kwa sababu amehalifu sheria kwa matakwa/ridhaa yake.  kwani inamaanisha kuwa mara mtu anapotiwa hatiani na kuonekana kuwa alitenda kwa ridhaa yake na akijua anachotenda hapo hapo uhuru wake unabadilishana na faini halali ambayo inampasa kulipa. tukiweza kujenga mazingira ya kulipa faini halali kwa makosa halali;tutafanikiwa vile vile kwashinda wale ambao wanatumia mamlaka au madaraka waliyopewa vibaya kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi. 


Nafikiri itakuwa ni busara kama wasimamizi wa sheria watakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao katika kupinga matumizi mabaya ya sheria hizo kwa mtu yeyote bila kujali cheo chake na pesa zake na anamfahamu nani;

Hilo likiwezekana tutaondoa dhana ya kukimbilia kuhukumu wakati hatuna vithibitisho “Prejudice” ni ukweli ambao haupingiki kuwa watu hawajezaliwa na hali ya kupinga kutotaka kutekeleza sheria bali tatizo na utaratibu mzima wa usimamiaji wa sheria ndio unaopelekea watu kuvunja sheria.
Wazo la leo nini kifanyike kuondoa hali hii ambayo imetawala vichwa vyetu kwa muda mrefu sasa?
·        Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu haki zao za msingi za     sheria na wanatakiwa wasiinunue haki yao kwa rushwa.
·        Tunahitaji wasimamiaji wa sheria ambao watakuwa tayari kutekeleza majukumu yao bila kuogopa na vile vile kuwaelimisha jamii kuhusu haki yao ya msingi.
·        Inatupasa kujenga uhusiano mzuri kati ya raia na watekelezaji wote wa sheria mfano polisi wawe ni msaada mzuri kwa madereva pale madereva wanapokosea na wawaadhibu bila ya kuwaonea haya hata kidogo na hii itatusaidia kupunguza ajali nyingi;
·        Viongozi wetu wakuu waonyeshe mfano mzuri katika kutekeleza majukumu yao bila upendeleo wowote ule;

Tukifanya hivyo huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuirudisha nchi yetu katika dira ya utawala bora na wa sheria.

Pamoja tukisimama hatutashindwa jambo lolote

Saturday, June 11, 2011

SEMINA ELEKEZI VS MAADILI YA UTENDAJI KAZI

UKOSEKANAJI WA MAADILI KATIKA UTENDAJI WA KAZI NDANI YA SERIKALI;



Siku za hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya semina iliyoitwa”Elekezi” kwa watendaji wakuu wa serikali; lengo la semina hiyo ilikuwa ni kujaribu kuwakumbusha watendaji hao kuhusu wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika utendaji wao;

Je lengo la jumla la semina hiyo ilikuwa nini?

Kuwakumbusha watendaji juu ya utendaji wao ambao hauna tija?

Kujisafisha mbele ya wananchi wa Tanzania kuhusu kushindwa kwa serikali kufikia malengo ya mipango yao ya utendaji?

Kwa nini Rais  amewataka wateule wake katika ngazi zote za uongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa; wawe watu wa kupigiwa mfano, wasinyooshewe kidole kwa ulevi, uchelewaji kazini na kuwahi kuondoka, kwa uzembe, wizi, kutumia ofisi kujinufaisha, kwa uzinzi na ubabe?.

Je watendaji wake wengi ni mzigo kwa serikali?
Nani amewachagua kushika wadhifa huo mkubwa na kama ni mzigo kwa nini wasitemwe?

Kwa nini Rais amewashauri kujielimisha kuhusu kusoma na kujua zaidi kuhusu katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi katika sehemu zao za kazi.
Kwanini amewataka watendaji hao kuacha umangimeza, badala yake watoke ofisini kujionea matatizo ya wananchi. Mawaziri na makatibu wakuu lazima mtoke. Hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujua mambo yahusuyo wizara zenu na ndiyo njia bora ya kuongoza: kuona wenyewe na kutenda?

Nani aliwachagua kushika nafasi hizo, je ni vigezo gani vilitumika kuwachagua watendaji hao, je ni watendaji ambao hawana uzoefu au elimu yao inatia mashaka, au wamejikita zaidi katika rushwa?

je kwa nini baraza la mawaziri halifanyi kazi kupitia utaratibu wa  “uwajibikaji wa pamoja? Kwani walipochaguliwa hawakueleza utendaji wao ni wa pamoja? Nani kavuruga uwajibikaji huu wa pamoja? Hata miswada ya sheria bungeni ni ya mawaziri wote; Ni kinyume cha maadili Waziri kupinga muswada wa Waziri mwenzake?
Kwa nini wanapingana wao kwa wao? Who is behind the scene?

Lakini nafikiri sio sahihi kwa mheshimiwa Rais kuwapa nafasi ya kujiondoa kama hawafai; nafikiri wanatakiwa waondolewe kama hawafai? Tusiogope kuharibu urafiki kwa kuwaacha watendaji wabovu katika nafasi zao za kazi waendelee kuharibu na kutowajibika.

Je watendaji wetu wanafanya kazi kulingana na kiapo wanachoapa wanapokabidhiwa madaraka? Kama wanafanya ndivyo sivyo kwa nini tuwaachie muda wajiondoe, tuwaondoe.

Semina hii yote ililenga katika kuwakumbusha watendaji wetu umuhimu wa kufuata maadili ya uadilifu na utawala bora;

Kwa hiyo nasema tena hapa tatizo letu kuu ni maadili. Maadili yamemomonyoka kabisa. Watu wanafanya kazi kwa mazoea mno. Hakuna umakini na wala ufanisi. Watendaji hawaguswi na hali mbaya za wanaowahudumia. Rushwa ufisadi na kutojali mahitaji ya wanaohudumiwa ni kigezo kikuu cha kushindwa kutatua matatizo.

Friday, June 10, 2011

SERIKALI VS VIONGOZI WA DINI -

JE KAULI YA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE IKO SAHII DHIDI YA VIONGOZI WA DINI NA BIASHARA YA MADAWAYA KULEVYA?


‘RAIS Jakaya Kikwete, amewaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya na badala yake washirikiane na viongozi wa serikali kuidhibiti biashara hiyo haramu’.

Mheshimiwa Rais alisema ‘Inasikitisha sana na kutisha, biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili kwani baadhi yenu tumewakamata. Kwa kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususan vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa hizi,’ mmmmm

Je kuna utata gani katika taarifa hii ya mheshimiwa Rais ambayo , imewapandisha mumkari maskofu (CCT) na kumpa kiongozi wa nchi masaa 48 ya kuwataja wahusika?
Je Maaskofu wamekurupuka katika kumpa kiongozi wa Nchi amri ya kutekeleza matakwa yao?

Je kama Mheshimiwa Rais asipotekeleza matakwa yao jamii ya watanzania inajifuanza nini katika swala hili nzima?

Je wale ambao serikali imesema imewakamata tayari  wameshafikishwa katika vyombo vya sheria kama bado kwa nini?

Je sheria na haki ya kushitakiwa kwa kosa la kujihusishwa na madawa ya kulevya “ambalo ni kosa la  jinai” inatekelezwa tofauti kulingana na hadhi na heshima, cheo cha mtu?

Tunafahamu kuwa serikali sio mtu ni taasisi ambayo kiongozi wake mkuu ni Rais wa nchi; na kiongozi huyo ili atekeleze majukumu yake hafanyi kazi peke yake ana timu nzima abayo inamsaidia ili aweze kufanikisha adhima yake ya kuongoza nchi na watu wake ili kufikia maendeleo ambayo jamii ina tegemea kufikia;

Katika siku za karibuni kumekuwako na vitendo ambavyo hufanywa na baadhi ya watu au kikundi cha watu au mtu mmoja moja ili kudhoufisha nguvu za maendeleo au hata kuharibu nguvu kazi ya jamii yetu; kwa kujihusisha na mambo kama;

·        Rushwa,
·        Uingizaji wa madawa ya kulevya,
·        Ufisadi wa rasilimali za umma na kadhalika


Mshangao wa watanzania wengi kwa nini Mheshimiwa Rais Kikwete pamoja na timu yake ya usalama wasiwafikishe kwenye vyombo vya sheria wahusika ili wachukuliwe hatua baada ya kuendelea kuyaeleza haya katika majukwao ya mikutano na makongamano? Inafahamika wazi kuwa Biashara ya madawa ya kulevya ni kosa, na kama hivyo sheria zipo? Sasa kama wamekamatwa kwa nini serikali inaendelea kuwabembeleza bembeleza waache hiyo biashara?

Nafikiri ni vyema kuikumbusha serikali kuwa kama washauri wa usalama hawana uhakika na taarifa sio vyema kumshauri mshemihwa Rais kutozisema kwani swala la madawa ya kulevya sio la kuendelea kulikemea kama wahusika wanajulikana; serikali itaendelea kuwakemea mpaka lini na ni nini? Hivi kisheria mtu ukiwa na taarifa za uhalifu lakini mwenye taarifa au uthibitisho akaendelea kukaa kimya bila kuzichukulia hatua ni kosa kisheria kwani ni namna ya kuendelea kuruhusu uhalifu huo, kuendelea na kama ni uhalifu wa   madawa ya kulevya taifa linazidi kuangamia kwa faida ya wachache.

nakubalia na kauli ya Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyosema ”Katika kupambana na tatizo hili la madawa ya kulevya, hatuna budi kutofumba macho ili kutowaonea haya watakaobainika kuwa chanzo cha usambazaji madawa ya kulevya, kwa sababu hili ni janga la kitaifa na tayari limeshawaathiri vijana wetu wengi sana” matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya yana madhara makubwa kwa Taifa, kiuchumi, kiafya na kijamii. Alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa ni vyema kushirikiana na jamii na kuwa waaminifu katika utekelezaji wake kwani wasambazaji kutokana na ushawishi na uwezo mkubwa wa kifedha walionao wamiliki na waingizaji madawa ya kulevya bado ni tishio kwa usalama wa jamii.

Lakini pamoja na  utata wa serikali katika kulikabili jambo hili sio busara kwa baraza la maaskofu  kumpa mheshimiwa Rais masaa ili kuwataja wahusika;  ni vyema Baraza hilo lingetumia njia mbadala yenye hekima katika kuiomba Serikali kuwafichua wahusika na sio kutoa muda wa kumshinikiza rais katika utendaji wake; kwa kumweleza rais kuwa asipofanya hivyo yeye atakuwa Mwongo na Mzushi; Ni kweli kuwa maneno haya yamesemwa na   watu wenye heshima kabwa ndani ya jamii. 

“Tunampa saa 48 rais awataje kwa majina viongozi hao ambao yeye anadai wanajihusisha na kuuza dawa na kama atashindwa kufanya hivyo tunamtafsiri ni mwongo na mzushi... Tunasikitishwa na kushangazwa kwa kauli hiyo na tunamheshimu kama kiongozi wa nchi, hivyo tunampa masaa hayo awataje kwa majina” 

Nafikiri umefika wakati kwa viongozi wa dini nchini Tanzania kukaa pamoja na Serikali kupembua kwa dhati mambo yanayopelekea uwepo wa mkanganyiko huu wa kutofautiana na kutokukubaliana 


Ni kweli  kuna tatizo ambalo linahitaji kulitafutiwa suluhu ya haraka; ama sivyo linaweza hatarisha misingi ya haki, amani na utulivu. Lazima tukubali kuwa sheria inapovunjwa haiangalii huyu ni kiongozi wa dini au la, inatakiwa chukua mkondo wake dhidi ya watu hao

Serikali ikiwaogopa vigogo na viongozi wa dini katika biashara hii, serikali itakuwa inakimbia jukumu lake la msingi la kulinda raia wake; hivyo jukumu la serikali kulinda maisha ya watanzania  hasa vijana dhidi ya madawa ya kulevya itakuwa ni ndoto tu.


Kwa hiyo serikali lazima isimamie kwa dhati kabisa  katika kulinda heshima ya Tanzania kama nchi isiyovumilia siyo tu biashara bali pia matumizi haramu ya dawa za kulevyawa. Kwa msingi huu hata watu wa Mungu kama wamo katika biashara hii ni busara kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria na kukamata mali zao na pasi zao za kusafiria ili haki itendeke.