JE FALSAFA YA MHESHIMIWA MAGUFULI YA HAPA NI KAZI TU
NI SAWA NA SEMI HIZI?
Kumpa mtu samaki
utakuwa umemlisha katika siku ya leo; ukiweza Kumfundisha mtu namna
ya kuvua samaki utakuwa umeweza kumsaidia kumlisha katika maisha yake
yote.
Ukiweza kumfundisha
mtu namna ya kutengeneza na kusafirisha na kuweza kuuza samaki katika masoko ya
nje; utakuwa umefanikiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi
Raisi Magufuli toka aliposhika nafasi ya kuliongoza Taifa la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea kuwa gumzo la utendaji uliotukuka hasa akipigania maendeleo ya wananchi Masikini. Amekuwa na maono ya uzalendo wake kwa kujitoa kwa kusimamia vizuri rasilimalia za taifa letu. Ameweza kuonyesha umahili katika kusimamia nidhamu ya utendaji katika Wizara na idara zote za serikali, huku akibana matumizi ili kuelekeza nguvu zaidi katika miradi ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja.
Raisi magufuli katika
kipindi hiki kifupi amweza kujijengea sifa ya kuwa "unforgettable"
miongoni mwa viongozi wa juu wa Tanzania na amekuwa kipenzi cha wanyonge ambao
wanamwona kama mkombozi wao katika shida na umasikini wao. Mfano maauzi yake ya
haraka ya kuwanusuru wagonjwa waliokuwa wanalala chini katika hospitali zetu; vitendo
kama hivyo wananchi wananwmona Dr. Magufuli kama Kiongozi mwenye maono ya
maendeleo ya nchi yake:
Katika kipindi hiki kifupi
ameweza kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali ambayo yameongezeka sana na
kusaidia katika kupunguza utengemezi hasa katika bajeti ya maendeleo ambayo
tulikuwa tunategemea sana ufadhili na kukwamisha shughuli za msingi za
maendeleo ya Taifa letu. Amekuwa kiongozi ambaye ameonyesha uwezo wa
Kujenga na kuboresha uchumi, wetu katika siku zijazo mbele; Ameweza pia kukuza
mifumo ya kiutawala na sera zinazolenga zaidi katika kusimamia maisha na ukuaji
wa uchumi wa nchi ili tuweze kuondokana na tatizo kubwa la umasikini wa Taifa
letu.
Nimejaribu kueleza hayo
yote ili kuonyesha kuwa bila kuwa na uongozi wenye maono usiotafuta faida
yake wenyewe, usiokuwa tayari kuwawajibisha watendaji wabovu na wanaokiuka
maadili na uvunja sheria hatuwezi kutoka hapa tulipo, tutaendelea
kufurahia kauli mbiu ambazo hazina maana wala msingi mkubwa kwa maendeleo
ya Taifa.
Kwa sasa Taifa linamwitaji
kiongozi mwadilifu, mkweli ambaye anaweza kupambana na matatizo ya rushwa na
ufisadi bila kuyaonea aibu. Ili kulivusha Taifa la Tanzania katika mabadiliko
ya maendeleo ambayo kama taifa tunayahitaji kwa sasa; tunahitaji Kiongozi
ambaye anauchungu sana na nchi yake hasa katika kuwasaidia wananchi ambao ni
wanyonge ambao wanahitaji mkate wao wa kila siku na watoto wao waweze kwenda
shule; Tumeliona hili kwa Raisi wetu Dr. Magufuli amekuwa msimamizi wa khali ya
juu wa utekelezaji wa mpango wa mabadiliko ambayo kama taifa tunayahitaji kwa
sasa; katika kampeni alituhahidi kuwa hana
mchezo hata kidogo katika hili na
hatakuwa na msamaha kwa wale wote ambao hawatafikia malengo ambayo serikali
yake imeainisha kutekeleza.
Ameshatoa onyo kwa
viongozi na wafanyakazi kuwa hayuko tayari kuona kuwa rasilimali ya taifa zinachezewa
na wajanja wachache, ikibainika serikali yake itawafukuza kazi bila huruma; Kwa Dr, Magufuli ufanisi utakuwa unapimwa
kwa uwajibikaji na uadilifu na sio propaganda za kisiasa.
Mheshimiwa Magufuli
amepania kurudisha kwenye kamusi maneno uwajibikaji na uwajibishaji kwa watendaji
wa serikali katika taasisi zake na idara zake, na ameamua kuondoa kabisa kwenye kamusi maneno
kama utashi wa kisiasa urafiki na undugu na michakato
katika kutekeleza wajibu katika majukumu yako ya kikazi.
Mheshimiwa Magufuli anaamini kuwa hakuna maendeleo ya kweli kama tutaendelea kuendekeza utashi wa kisiasa; ni dhahiri kuwa tuwe tayari kuhesabu kuwa hakuna maendeleo ya haraka yatapatika katika nchi yetu bado tukiwa tunatawala na michezo michafu ya siasa; tukumbuke kuwa majukumu ya kiserikali yanatakiwa kuzingatia zaidi, misingi yake ya utendaji, na utaalamu, nidhamu na ukweli na sio kuendekeza urafiki na undugu.
Mheshimiwa Magufuli
amethubutu na amejitangazia wazi kuwa yeye ni sadaka ya watanzania katika
kupambana na ufisadi na yuko tayari kujitoa Muhanga ili tu watanznaia wanyonge
waweze kunufaika na rasilimali za taifa lao.
Mheshimiwa Magufuli utendaji
wake unaongozwa na kauli mbiu ya sitawaangusha:
Hapa Ni Kazi Tu; katika imani kuwa
ameona umasikini na tabu ya Taifa letu hivyo kama watanznia walivyojenga imani
kwake hivyo naye ameweka juhudi zote katika kusimamia kwa dhati kabisa
rasilimali za Taifa ili kurudisha matumaini makubwa kwa serikali yake anayoiongoza
kwa wananchi kwa maendeleo yao.
Binafsi kama mtanzania na
mfuatiliaaji wa utendaji wa kazi Dr. John Pombe Magufuri, pamoja na
mapungufu yake kama binadamu amekuwa miongoni mwa viongozi
wachache ; kama
kiongozi wa juu kabisa hataki kuona watendaji ambao wako chini
yake wanatenda kazi kwa mazoea; daima ameonyesha kuthubutu katika kutekeleza
sheria na kuwashugulikia watendaji wabovu
huku akiwa tayari kufuata sheria na kujielimisha ili aweze kuzielewa zaidi sheria za nchi na wizara husika;
kwa keli ni
ni msimamiaji mzuri wa sheria katika utendaji
hata kama wakati mwingine maamuzi yake yanakuwa
kero kwa kwa watendaji wenzake wanaomzunguka lakini bado yanafaida
kubwa kwa jamii ya Kitanzania. Kimsingi
kama nilivyoainisha hapo
juu inawezekana magufuli akawa na madhaifu yake
lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa katika kipindi
hiki kifupi cha uongozi wake amekuwa kiongozi mzuri wa Juu aliyeweza kufanya vizuri katika kazi ya kusimamia hata kuchukua hatua kali kwa wakati
dhidi ya wale wote ambao wamekuwa na hawafuati maadili ya kazi na vinara wote
wa Rushwa na Ufisadi. Hilo hata wananchi wa kawaida wameliona hilo nao
wamempa tano.
Ni ukweli ni wazi
kuwa Magufuli ni kiongozi mchapakazi na msimamizi
mzuri “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,
wengi tunamtambua Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya,
tunakuomba uendelee kufanya hivyo hivyo na Serikali yake ya awamu ya tano iendelee
kujiepusha kufanya kazi na watendaji wabovu:
Watanzania
wamemchagua mheshimiwa Magufuli kwa sababu utendaji wake kazi mzuri na kuwa
kiongozi ambaye ameonyesha kiwango cha juu cha maadili; na ameonyesha katika
kampeni zake kuwa yuko tayari kuwavusha wananchi kuelekea katika bandari ya salama na
yenye amani na maisha bora.
Magufuli
ameonyesha upendo wa juu kabisa sio tu kwa watanzania wote bila kujali itikadi
zao au dini zao au makabila yao. Ni kiongozi ambaye anaonyesha upendo kwa wananchi wote; kwake uongozi ni kwa
ajili ya wote na sio watu wachahce tu.
Tukumbuke
kuwa kuwa uongozi ni dhana nzito ya kuaminiwa ambayo unakabiziwa na watu;
lakini na kwa kuwa uongozi
wa kweli ni matokeo ya kuwa na maadili mazuri. Tukumbuke kuwa kuweza kutekeleza
majukumu yako vizuri, Lazima kuwe na uhuisano wa karibu kati ya uongozi na
mwongozo.
Mheshimiwa
Magufuli tunaweza sema kuwa amejitambua mwenyewe
kuwa kazi moja ambayo anakabiliwa nayo ni kuwaletea mabadiliko wananchi wa
Tanzania hivyo amejiaamini YeYe mwenywe kuwa anaweza kufanya hivyo hivyo anayo
mizizi ya huruma na uvumilivu ndani na
ni mtu ambaye haogopi kushindwa
Kiongozi
bora atahangaika kuhakikisha kuwa maisha ya wananchi wake yanasonga mbele na
kuwa na misha bora. Ukiwa mnyonyaji wewe ni kiongozi mbovu; viongozi ni
viashiria vya mabadiliko katika jamii, na kuendeleza mafanikio tukumbuke kuwa
sio vigumu kumtawala mtu ila jukumu ni kumwendeleza mtu.
Viongozi
wanaishi kwa kuelewa mazingira na tabia za watu; kiongozi lazima awe tayari
kuyapokea mabadiliko kila kitu kinaendelea kubadilika; kiongozi lazima ajue
kuwa haitakiwi kuogopa awe tayari kujifunza na kamwe ahitimu shule ya
mabadiliko, kiongozi lazima awe tayari kuishi na mabadiliko ya tamaduni. kiongozi
mzuri anajua mapungufu ya watu wake, mapungufu yetu yanakamilishwa na wengine
ambao wanautaalamu zaidi.
uvumilivu
ni nguzo muhimu kwa viongozi wazuri ( role model). kiongozi mzuri lazima ajue
kuwa kushindwa ni sehemu ya uongozi bora kwani inakupa nguvu ya kuanza upya,
unawapenda watu wako kama huwapendi basi usiwe kiongozi hata kama watu
hawakupendi bali kama kiongozi bado unatakiwa kuwajali.
kiongozi
lazima ujifunze kutokuona wivu wa mafanikio ya watu wengine sio kukosoa kila
kitu hata kama mwenzako amefanya vitu vizuri tabia ya kupongezana ni nzuri sana
kwa kiongozi mwenzake. viongozi ni wabunifu ambao wanatakiwa kuleta mabadiliko
na kuleta utamaduni wa kazi na kudumisha utamaduni wa mafanikio ni wajibu wa
kiongozi mzuri, kwa hiyo viongozi wanatakiwa kuwa viashiria wa mabadiliko ya
kweli kwa taifa.
kiongozi
wanatakiwa kuwa na mawazo mazuri ya kimaendeleo na kujua namna ya kuyatumia kwa
ajili ya maendeleo ya watu wao na kwa faida ya watu wao, mgonagano wa mawazo ni
sehemu tu ya uongozai mzuri. kiongozi hatakiwi kuhangaika wakati kunatokea
matatizo ndani ya uongozi kila kitu kipo kwenye mpito. kiongozi lazima uelewe
kuwa yale uliyojifunza shuleni wakati mwingine hayafnayi kazi wakati wote na
tayari kufahamu kuwa kufanyia utafiti mabadiliko ya tamaduni za uongozi wako.
VIVA
MAGUFULI TUNAKUJUA WEWE NI:
Ni Jembe:
Ni
Tingatinga
Ni
Mtumishi wa watanzania wote
Unayajua
mapungufu yako.
Unaongoza
kwa usemi wa sisi sisi.
Ni Mnyenyekevu
na mtumishi wa watu wote.
Ni
mwadilifu
Mtu wa
watu hasa wanyonge
Ni Mwogopa Mungu
VIVA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI RAISI WA AWAMU YA TANO
MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU YA KULIVUSHA SALAMA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MIAKA
HII MITANO KATIKA MAENDELEO AMBAYO SISI
WATANZANIA TUMEYASUBIRI KWA MIAKA MINGI SANA;
UKADIRIFU INAKUTAKIA
UONGOZI BORA MIEZI HII MINNE YA UONGOZI WAKO KAMA RAISI WA AWAMU YA TANO
No comments:
Post a Comment