AZAM FC
imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC jioni hii Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi
huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25,
nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.
Simba SC
ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na hata ikishinda mechi yake ya
mwisho itafikisha 47, hivyo kwa mwaka wa tatu mfululizo Wekundu wa
Msimbazi watakosa michuano ya Afrika.
Azam FC
ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia
kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya
14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.
Kikosi
cha azam kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Gadiel Michael, Shomary
Kapombe, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Brison Raphael, Frank Domayo,
Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche na Brian Majwega.
YangaFC;
Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Pato
Ngonyani, Saum Telela, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Amissi Tambwe,
Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho
No comments:
Post a Comment