Ndugu zangu,
Kwenye moja ya picha za magazetini
leo, kuna hii inayomwonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Iddi akimpa pole Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mazishi ya baba
mzazi wa mkewe, Marehemu Mzee Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye
makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam,Aprili4, 2015.
Kwa hakika, hii ndio Tanzania tunayoijua. Kwamba Watanzania ni ndugu na tumechanganyika. Hata hivyo, Wahenga walisema; " Kamba hukatikia pabovu.
Kwa hakika, hii ndio Tanzania tunayoijua. Kwamba Watanzania ni ndugu na tumechanganyika. Hata hivyo, Wahenga walisema; " Kamba hukatikia pabovu.
Siku zote, uzoefu ni mwalimu mzuri
sana. Mathalan, uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi
sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.
Ona, moto ulioanza kwenye nyumba moja
ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza kijiji
kizima. Na tangu utotoni tumetahadharishwa hatari ya kucheza na moto.
Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.
Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.
Jumapili hii ya leo ningependa sana
tuyakumbuke maneno ya busara na hekima nyingi kutoka kwa Bi. Joy
Mukanyange. Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa Rwanda nchini Tanzania.
Mama huyu aliyatamka maneno haya miaka 16 iliyopita, takribani miezi
sita kabla ya kifo cha Baba wa Taifa. Bi. Joy Mukanyange ( Pichani juu)
alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona. Ni kama vile alikuwa
mtabiri, maana, alichokisema mama yule leo ndio tunaanza kukiona. Siku
ile ya Aprili 6, 1999, katika iliyokuwa Kilimanjaro Hotel, Bi Joy
Mukanyanga aliyatamka haya;
" Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili
zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la
Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha maauji ya halaiki kama
yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994." Alisema Balozi yule wa Rwanda
kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio
yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ndio, Bi Joy
Mukanyange alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona.
Na tutafanya makosa makubwa, kama hata sasa, tutajifanya kuwa hatukioni kile ambacho Balozi Joy Mukanyange alikiona . Kwamba hatukioni pia kile kilichotokea westgate na garissa.
Na tutafanya makosa makubwa, kama hata sasa, tutajifanya kuwa hatukioni kile ambacho Balozi Joy Mukanyange alikiona . Kwamba hatukioni pia kile kilichotokea westgate na garissa.
Watanzania tukubali sasa kuwa
tumepatwa na bahati mbaya sana ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza
kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze
kubaguana kwa misingi ya kidini. Tunayashuhudia yakifanywa na baadhi ya
viongozi wa kidini, makanisani na misikitini. Ni hao, ambao sasa
wameamua kuchanganya dini na siasa huku waumini wao wakiwa ni wafuasi wa
vyama tofauti tofauti vya kisiasa.
Hili ni jambo la hatari sana.
Hili ni jambo la hatari sana.
Ni hulka ya mwanadamu, anapokuwa
matatizoni kumtafuta kondoo wa kafara. Mtu mwingine wa kummyooshea
kidole kwa matatizo yake. Hali duni ya uchumi wa nchi, hali duni za
maisha na umasikini wa watu wetu isiwe chachu ya kuanzisha vurugu za
kijamii kwa kuegemea kwenye mitazamo ya kidini.
Maana, taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwapo na WAO.

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la
wengi wetu kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya
zaidi, ufahamu mdogo wa historia yetu. Hivyo basi, kupelekea hali ya
kutojitambua kama taifa. Ndio, uelewa wa historia ya jamii husika ni
jambo muhimu sana. Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa
kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na
unakokwenda. Historia ni kama maji ya mto, kamwe haijirudii. Historia ni
wakati, ni muda. Kihistoria jana ni sawa na zamani.
Karne nyingi zilizopita wahenga wetu
walitafsiri muda kama mkusanyiko wa matukio ya zamani na sasa. Waliamini
kuwa yaliyotokea zamani na yanayotokea sasa ndiyo yenye kusaidia
kubashiri yatakayotea kesho, yataamua mustakabali wetu.
Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini na maeneo tunakotoka si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa. Tuliopata bahati ya kutumia kalamu zetu hatuna budi kuliweka hili hadharani.
Hii ni nchi yetu. Ni Nchi yetu sote. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu ambao hawana nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda heshima na hadhi ya nchi yetu.

Mengine yanayofanyika sasa sio tu
yanaitia doa nchi yetu, bali, yanaiaibisha nchi yetu. Hatukupata
kufikiri, kuwa atatokea anayejiita kiongozi kwa kiimani, akasimama
hadharani na kumtukana kiongozi mwingine wa kiimani. yanatokea sasa, na
tusiyaone ni ya kawaida. Tuyakemee kwa nguvu zote.
Watanzania hatuna haja wala sababu za kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe. Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz.

Na dini hizi za kimapokeo
zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na kuzikuta dini zetu za asili,
na bado tunazo. Na hakika, Afrika hatugombanii matambiko. Afrika kila
ukoo una tambiko lake, hivyo basi, dini yake. Kamwe hutasikia Waafrika
wanagombania matambiko. Hutasikia Waafrika wakigombana kwa tofauti za
matambiko yao.
Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.
Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.
Naam; kamba hukatikia pabovu, wanasema
wahenga.Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba
inayotuunganisha Watanzania. Tusifike mahali tukagombana kutokana na
tofauti za imani ama dini ambazo wala si za asili yetu. Imani au dini
ambazo, kama ilivyo dini zetu za asili, nazo zinatutaka wanadamu tuishi
kwa amani, upendo na maelewano.
Maggid Mjengwa,
Iringa
Iringa
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment