Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maaalim Seif Sharif Hamad akizungumza na bolozi wa Uingereza nchini Tanzania Diane Loise Corner ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar. (Picha, Salmin Said, OMKR)
Na Hassan Hamad (OMKR).
Zanzibar na Uingereza zinakusudia kuendeleza mahusiano katika nyanja mbali mbali za kiuchumi kwa maslahi ya pande hizo mbili.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo huko Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania bibi Diane Loise Corner.
Amesema katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Uingereza Maalim Seif amesema Zanzibar imeweza kugundua maeneo tofauti ambayo nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana katika kukuza uchumi wake.
Amesema ziara yake hiyo imempa matumaini makubwa kwamba Zanzibar inaweza kunufaika kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Uingereza.
Kwa upande wake balozi wa Uingereza nchini Tanzania bibi Diane Corner amesema nchi yake imefurahishwa na hali ya amani inayoendelea Zanzibar , na kwamba iko tayari kutoa mashirikiano katika kuendeleza uchumi wa Zanzibar .
Ameahidi kuwa Uingereza ambayo ni rafiki wa muda mrefu wa Zanzibar itaendelea kukuza mahusiano hayo kwa lengo la kuisaidia Zanzabar kuendeleza uchumi wake.
No comments:
Post a Comment