TATIZO LA AJALI ZINAZOENDELEA NA KUPOTEZA MAISHA YA WATANZANIA WENGI;
NI UBUTU WA SHERIA?
UBOVU NA UFINYU WA BARABARA ZETU
KIBURI CHA MADEREVA?
UBOVU WA MAGARI NA UBABE WA WAMILIKI?
Taifa la Tanzania limeendelea kushuhudia mwendelezo wa ajali nyingi za barabarani ambazo zimeendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa hili. Kwa ujumla ajali hizi zimekuwa zikitokea kila kona wakati mamlaka za kisheria zikiendelea kuhimiza kuwa zitahakikisha kuwa zitakomesha vifo vinavyoyokana na ajali hizo.husika kutekeleza yafuatayo;.
· Kuimarisha doria katika njia kuu,
· Askari wa Usalama Barabarani kuimarisha shughuli za ukaguzi wa magari mabovu,
· Kuimarisha elimu kwa wananchi na wadau wengine juu ya umuhimu wa kuisaidia Serikali kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kuhusu madereva walezi, wanaoendesha mabasi yao kwa kasi, madereva wanaotiliwa mashaka kuhusu ujuzi wao wa kuendesha, na pia kukataa kupanda magari mabovu au yaliyojaa kupita kiwango kinachohitajika,
· Kuendelea kuboresha sheria za Usalama Barabarani ili zichangie katika kudhibiti shughuli za usafiri na usafirishaji,. Kutoa elimu kwa madereva ili wazingatie sheria za kanuni za kazi zao,
· Kukagua leseni za madereva ili kuhakikisha kuwa ni za halali,
· Kuwashirikisha wenye magari ili washiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wanaajiri wadereva waaminifu na wenye kuwajibika.
Pengine swali ambalo daima ninajiuliza pamoja na malengo mazuri yaliyoainishwa hapo juu, kwa nini serikali imeshindwa kabisa kisimamia utekelezaji wa sheria na sera zake za usalama barabarani kwa raia wake kwa muda mrefu?
Je serikali haina askari wa usalama barabarni wa kutosha kukabiliana na tatizo hili?
Je ni tatizo ni la wamiliki wa biashara hii wamefanikiwa kuiteka idara nzima ya usalama barabarani?
Je madereva wanaoendesha magari hayo wanafahamu fika maadili ambayo wanapaswa kuyafuata kulingana na sheria za usalama barabarani wakati wa kuendesha magari hayo?
Tathimini ya muda mrefu kutoka vyanzo mbalimbali inabaini kuwa licha askari hawa kuwapo na tunaambiwa kwa kiasi kikubwa ajali zinazotokea zinasababishwa na madereva wazembe ambao wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani.
Tunajua, kwamba madereva wengi wa mabasi ya abiria wanaendesha wamelewa. Je hakuna sheria inayowabana kama katika nchi nyingine kuhusu kilevi? Je, dereva huyu aliyekunywa pombe kabla ya kuanza kuendesha nap engine wakati wa safari ataweza kuendelea kuwa na maarifa yake ya kawaida na uwezo wake wa kawaida kumudu gari na mazingira ya barabara yanayomkabili?
Inafahamika wazi mara nyingi askari wa usalama barabarani wanabariki mwendo kasi wa madereva kwa kupokea rushwa; je taifa linakubaliana na tabia hii izidi kuendelea? Tunawaacha wakimbize magari wanavyotaka mpaka lini?. Je tumeshindwa kabisa kusimamia “Speed Limit” ni ukweli ambao huupingiki kuwa Madereva wa mabasi wengi wanakimbia kupita speed waliyopangiwa. Je ni kweli kuwa serikali kupitia wizara yake kweli imeshindwa kuwadhibiti hawa madereva ambao ambao tunaweza kuwaita wahuni na wenye viburi kwani wamekuwa wakiendesha vyombo hivi vya moto kwa mwendo kasi, usiofuata taratibu za usalama barabarani na matokeo yake kusababisha ajali mbaya ambazo matokeo yake ni vifo vingi vya watu. Lo imefila wakati sasa serikali iamke na kusema basi inatosha kwa sasa hasa kwa kuanzaia na askari wake wa usalama barabarani wanaelezwa kuchangia uwepo wa ajali kwani wamekuwa wakiruhusu makosa kutendeka kwa sababu tu ya kuchukua rushwa ndogondogo.
Kwa nini serikali imeshindwa kusimamia sheria ya kutowaruhusu madereva matumizi ya simu za mikononi wanapokuwa wakiwaendesha raia; ni vigumu sana kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja uwe makini barabarani na hapo hapo utumie simu kuongea na mtu mwingine; Ni busara ya kawaida tu dhamana ambayo umebeba kama dereva ni zaidi ya Kuongea kwenye simu za mikononi kwa hiyo tabia hii haifai kabisa kwa dereva wa gari la abiria aendeshapo gari. Hii ni hatari kwa abiria na watu wengine watembeao kwa miguu. Matokeo yake baada ya kujenga madereva wanaleta kilio na hasara kubwa kwa taifa taifa letu na familia zetu kwa mambo tunayonaweza kuyazuia bila gharama yoyote
Je serikali kupitia wizara inakubali kuwaona askari wake wakikwepa maadili na kiapo chao cha kazi kwa kujihusisha na rushwa na kuhatarisha usalama wa watu wake; Tumke sasa kwa usalama wa watu wetu na kupinga kwa kauli moja mwendo kasi unaoendana na kutojali sheria na alama za barabarani
Ni ukweli ambao haufichiki kuwa hata sheria zetu zinatoa mwanya mkubwa kwa mahakama kuwatoza faini ndogo badala ya kifungo au adhabu kubwa ambayo itakuwa pigo kwa dereva mna mmiliki wa biashara hiyo. Wote ni mashahidi wa jinsi ambayo watu ambao wamesababisha ajali kwa uzembe wa kujitakia, tena ajali ambayo imesababisha vifo vingi , lakini wamekuwa wakipigwa faini ya Sh50,000 na kuachiwa huru. Je nchi nyingine wamefanikiwa namna gani kudhibiti ajali hizo za uzembe? Kwa nini tusijifunze kutoka huko?
Pamoja na kwamba ajali haziwezi kuzuilika jumla,lakini tuzipunguze.Ajali ya gari inapotokea sio dereva tu ndiye wakulaumiwa,ang alia hali za barabara zetu zilivyo,hali ya hewa,abiria nao je wanaelewa sheria za barabarani ili kumkemea dereva anapovunja sheria hizo.Jambo la msingi ni kuelimisha watanzania wote wajue sheria za barabarani.
Tuangalie sheria Namba 30 ya Mwaka1973 na marekebisho yake ya mwaka 1996 inayohusu ni jinsi gani magari yanatakiwa yawe yakiwa barabarani. Pamoja na tatizo la madereva tuzinagatie vile vile tatizo la ubovu wa magari amabayo vile viel huwa ni chanzo cha ajali nyingi;
je wamiliki wanatoa kipaumbele gani katika kuhakikisha kuwa magari yao yako katika hali nzuri ya kusafirisha abiria kwa usalama?
Kwani nini gari bovu ambalo halina break nzuri linaruhusiwa kusafiri? Kama dereva ambaye anajali akatae kuendesha mpaka litengenezwe; uungwana wa wamiliki utaweza kuepusha ajali nyingi ambazo zinaweza kuzuilika kwa kutumia muda wa ziada kutengeneza gari na kuhakikisha kuwa liko salama kwa matumizi ya wananchi; kama wamamiliki watalazimisha matumizi ya gari bovu hatulidanganyi jeshi la polisi bali tunajidanganya sisi wenyewe na hatimaye kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Pamoja na tatizo kubwa la uchakavu wa miundombinu, ikizingatiwa kuwa barabara nyingi haziko katika hali nzuri sana au nyingine pamoja na kutengenezwa hivi karibuni bado hazijeweza kusaidia kupunguza vifo kutokana na pengine kuwa chini ya kiwango na kusababisha ajali haraka.
Tunaomba serikali ikishauriana na wataalamu wake kuangalia namna ya kuepusha janga hili kwa kuwa na usimamizi ulio bora na kurekebisha mapungufu yatokanayo na:
Barabara mbovu; Magari mabovu; Mwendo wa kasi; Udereva mbaya; Usimamizi dhaifu wa sheria; na Watembea kwa miguu wasiojali. Rushwa katika utoaji leseni za udereva umetajwa katika orodha ya sababu za ajali chini ya kifungu cha Usimamizi dhaifu wa sheria. Kuruhusiwa kwa magari mabovu.
Safari bila ajali zinawezekana kabisa
No comments:
Post a Comment