WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, June 26, 2011

KWA NINI TUNASHINDWA KUTEKELEZA SHERIA ?



Kwa nini sheria hazifuatwi katika maisha ya kila siku ya mtanzania  tatizo liko wapi? Sheria hazieleweki au sheria zimejaa mianya mingi inayoruhusu kutofuatwa katika utekeleji wake?

Tunapaswa kufanya nini ili kuhakikisha kuwa harakati za kutetea na kuona kuwa sheria zinafuatwa, zinafanikiwa bila kuvunja misingi ya utawala bora na wa sheria?

Je "Watu wote ni sawa mbele ya sheria, au wengine wanayo haki zaidi kutokana na umaarufu wao?.

Je utekelezaji wa sheria unafanyika bila ubaguzi wowote, na kumwezesha kila raia keheshimiwa na kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria"?


Ni kwa namna gani tunaweza kujenga mfumo wa utawala wa sheria usioipa nafasi dola kutumia kiujanja mianya ya kisheria na kupata nafasi ya kutotekeleza kanuni za sheria na kama itatekelezwa kuchukua muda mrefu ili kupunguza nguvu ya kosa katika kuleta haki inayotakiwa kwa jamii?

Je Migomo, maandamano, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali unaofanywa kutoka na matukio haya ni sababu ya kwisha kwa uvumilivu kutoka na uzembeaji katika kutekeleza sheria au ni mazoea tu yaliyojengeka mbele ya raia au jamii?

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa miaka takribani 50 ya uhuru wa  nchi hii wananchi wameweza kuona ni kwa jinsi gani matatizo yanayoikumba nchi Tanzania yanazidi kuongeza licha ya kuwepo utawala wa sheria. Na wakati huo huo kuna vyombo na taasisi mbalimbali za kisheria zenye nguvu na mamlaka ya kushughulikia zikiwa zimepewa nyenzo na nguvu za kisheria katika kutekeleza majukumu yao, cha kushangaza ni kuwa taasisi au idara hizo zipo na pengine zinaangalia tu bila kuwajibika. Je zinaogopa au hazioni umuhimu wa kuwajibika kwa sababu za masilahi zaidi?

Je hii inatokana na ukweli kuwa pengine sheria pamoja na kupitishwa na vyombo husika lakini utekelezaji wake lazima ubarikiwe na kikundi kidogo cha wenye mali Mafisadi ili itekelezwe kwa matakwa yao.

Kama ni hivyo basi sheria iko kwa ajili na kwa manufaa ya nani? Je sheria zinatungwa na matajiri kuwazuia maskini kuwasogelea matajiri na kuhakikisha matajiri wanaendelea kutumia utekelezaji wa sheria kuwakandamiza maskini; je sheria zinatungwa kuwafurahisha matajiri na kuwaridhisha maskini lakini wakati wote kuwanufaisha watawala!

Ni aibu kama vyombo vya dola vinaweza kumfunga Mmachinga katika siku mbili kwa kosa na kuuza vitu katika sehemu ambayo haijeruhusiwa na wakati huo huo inashindwa kumfunga Fisadi aliyethibitika kuliibia taifa mabilioni ya shilling kwa vile tu eti kwa sababu ya pesa zake anaweza kushinda kesi na kuisababishia serikali hasara zaidi; lo hii ni hatari.

Swali la msingi hapa sheria zetu ni kwa ajili na manufaa ya nani? Kwa nini utekelezaji wake unakuwa na kigugumizi. Nafikiri uzaifu huu wa sheria zetu ndio unaotuletea kila ambacho wananchi kuhukumu na kuchukua hatua ambazo wakati mwingine zinakiuka utaratibu wa utawala bora;

je ni busara haki hata kama iko ndani ya sheria haitatekelezwa mpaka kwa maandamano na migomo;

Haki ya ya matibabu bora haitapatikana mpaka kwa utoaji rushwa;
Haki yangu ya kosa lolote la barabarani haitaeleweka mbele ya askari wa usalama wa barabarani bila ya hongo;

Wananchi wanatakiwa kuelimisha kwa upole na upendo pale wanapokosea na ikibidi adhabu ifanywe kulingana na sheria; mkosa alipe faini yake kihalali ili iwe ni fundisho na pesa hiyo isadie maendeleo ya nchi;

Kwa kufanya hivyo taifa litaweza kuimarisha utawala bora, amabao ni utawala wa sheria, na hapo itakuwa rahisi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa, dawa za kulevya, matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma. Mhalifu anaweza na anapaswa kuadhibiwa kwa sababu amehalifu sheria kwa matakwa/ridhaa yake.  kwani inamaanisha kuwa mara mtu anapotiwa hatiani na kuonekana kuwa alitenda kwa ridhaa yake na akijua anachotenda hapo hapo uhuru wake unabadilishana na faini halali ambayo inampasa kulipa. tukiweza kujenga mazingira ya kulipa faini halali kwa makosa halali;tutafanikiwa vile vile kwashinda wale ambao wanatumia mamlaka au madaraka waliyopewa vibaya kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi. 


Nafikiri itakuwa ni busara kama wasimamizi wa sheria watakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao katika kupinga matumizi mabaya ya sheria hizo kwa mtu yeyote bila kujali cheo chake na pesa zake na anamfahamu nani;

Hilo likiwezekana tutaondoa dhana ya kukimbilia kuhukumu wakati hatuna vithibitisho “Prejudice” ni ukweli ambao haupingiki kuwa watu hawajezaliwa na hali ya kupinga kutotaka kutekeleza sheria bali tatizo na utaratibu mzima wa usimamiaji wa sheria ndio unaopelekea watu kuvunja sheria.
Wazo la leo nini kifanyike kuondoa hali hii ambayo imetawala vichwa vyetu kwa muda mrefu sasa?
·        Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu haki zao za msingi za     sheria na wanatakiwa wasiinunue haki yao kwa rushwa.
·        Tunahitaji wasimamiaji wa sheria ambao watakuwa tayari kutekeleza majukumu yao bila kuogopa na vile vile kuwaelimisha jamii kuhusu haki yao ya msingi.
·        Inatupasa kujenga uhusiano mzuri kati ya raia na watekelezaji wote wa sheria mfano polisi wawe ni msaada mzuri kwa madereva pale madereva wanapokosea na wawaadhibu bila ya kuwaonea haya hata kidogo na hii itatusaidia kupunguza ajali nyingi;
·        Viongozi wetu wakuu waonyeshe mfano mzuri katika kutekeleza majukumu yao bila upendeleo wowote ule;

Tukifanya hivyo huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuirudisha nchi yetu katika dira ya utawala bora na wa sheria.

Pamoja tukisimama hatutashindwa jambo lolote

Saturday, June 11, 2011

SEMINA ELEKEZI VS MAADILI YA UTENDAJI KAZI

UKOSEKANAJI WA MAADILI KATIKA UTENDAJI WA KAZI NDANI YA SERIKALI;



Siku za hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya semina iliyoitwa”Elekezi” kwa watendaji wakuu wa serikali; lengo la semina hiyo ilikuwa ni kujaribu kuwakumbusha watendaji hao kuhusu wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika utendaji wao;

Je lengo la jumla la semina hiyo ilikuwa nini?

Kuwakumbusha watendaji juu ya utendaji wao ambao hauna tija?

Kujisafisha mbele ya wananchi wa Tanzania kuhusu kushindwa kwa serikali kufikia malengo ya mipango yao ya utendaji?

Kwa nini Rais  amewataka wateule wake katika ngazi zote za uongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa; wawe watu wa kupigiwa mfano, wasinyooshewe kidole kwa ulevi, uchelewaji kazini na kuwahi kuondoka, kwa uzembe, wizi, kutumia ofisi kujinufaisha, kwa uzinzi na ubabe?.

Je watendaji wake wengi ni mzigo kwa serikali?
Nani amewachagua kushika wadhifa huo mkubwa na kama ni mzigo kwa nini wasitemwe?

Kwa nini Rais amewashauri kujielimisha kuhusu kusoma na kujua zaidi kuhusu katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi katika sehemu zao za kazi.
Kwanini amewataka watendaji hao kuacha umangimeza, badala yake watoke ofisini kujionea matatizo ya wananchi. Mawaziri na makatibu wakuu lazima mtoke. Hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujua mambo yahusuyo wizara zenu na ndiyo njia bora ya kuongoza: kuona wenyewe na kutenda?

Nani aliwachagua kushika nafasi hizo, je ni vigezo gani vilitumika kuwachagua watendaji hao, je ni watendaji ambao hawana uzoefu au elimu yao inatia mashaka, au wamejikita zaidi katika rushwa?

je kwa nini baraza la mawaziri halifanyi kazi kupitia utaratibu wa  “uwajibikaji wa pamoja? Kwani walipochaguliwa hawakueleza utendaji wao ni wa pamoja? Nani kavuruga uwajibikaji huu wa pamoja? Hata miswada ya sheria bungeni ni ya mawaziri wote; Ni kinyume cha maadili Waziri kupinga muswada wa Waziri mwenzake?
Kwa nini wanapingana wao kwa wao? Who is behind the scene?

Lakini nafikiri sio sahihi kwa mheshimiwa Rais kuwapa nafasi ya kujiondoa kama hawafai; nafikiri wanatakiwa waondolewe kama hawafai? Tusiogope kuharibu urafiki kwa kuwaacha watendaji wabovu katika nafasi zao za kazi waendelee kuharibu na kutowajibika.

Je watendaji wetu wanafanya kazi kulingana na kiapo wanachoapa wanapokabidhiwa madaraka? Kama wanafanya ndivyo sivyo kwa nini tuwaachie muda wajiondoe, tuwaondoe.

Semina hii yote ililenga katika kuwakumbusha watendaji wetu umuhimu wa kufuata maadili ya uadilifu na utawala bora;

Kwa hiyo nasema tena hapa tatizo letu kuu ni maadili. Maadili yamemomonyoka kabisa. Watu wanafanya kazi kwa mazoea mno. Hakuna umakini na wala ufanisi. Watendaji hawaguswi na hali mbaya za wanaowahudumia. Rushwa ufisadi na kutojali mahitaji ya wanaohudumiwa ni kigezo kikuu cha kushindwa kutatua matatizo.

Friday, June 10, 2011

SERIKALI VS VIONGOZI WA DINI -

JE KAULI YA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE IKO SAHII DHIDI YA VIONGOZI WA DINI NA BIASHARA YA MADAWAYA KULEVYA?


‘RAIS Jakaya Kikwete, amewaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya na badala yake washirikiane na viongozi wa serikali kuidhibiti biashara hiyo haramu’.

Mheshimiwa Rais alisema ‘Inasikitisha sana na kutisha, biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili kwani baadhi yenu tumewakamata. Kwa kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususan vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa hizi,’ mmmmm

Je kuna utata gani katika taarifa hii ya mheshimiwa Rais ambayo , imewapandisha mumkari maskofu (CCT) na kumpa kiongozi wa nchi masaa 48 ya kuwataja wahusika?
Je Maaskofu wamekurupuka katika kumpa kiongozi wa Nchi amri ya kutekeleza matakwa yao?

Je kama Mheshimiwa Rais asipotekeleza matakwa yao jamii ya watanzania inajifuanza nini katika swala hili nzima?

Je wale ambao serikali imesema imewakamata tayari  wameshafikishwa katika vyombo vya sheria kama bado kwa nini?

Je sheria na haki ya kushitakiwa kwa kosa la kujihusishwa na madawa ya kulevya “ambalo ni kosa la  jinai” inatekelezwa tofauti kulingana na hadhi na heshima, cheo cha mtu?

Tunafahamu kuwa serikali sio mtu ni taasisi ambayo kiongozi wake mkuu ni Rais wa nchi; na kiongozi huyo ili atekeleze majukumu yake hafanyi kazi peke yake ana timu nzima abayo inamsaidia ili aweze kufanikisha adhima yake ya kuongoza nchi na watu wake ili kufikia maendeleo ambayo jamii ina tegemea kufikia;

Katika siku za karibuni kumekuwako na vitendo ambavyo hufanywa na baadhi ya watu au kikundi cha watu au mtu mmoja moja ili kudhoufisha nguvu za maendeleo au hata kuharibu nguvu kazi ya jamii yetu; kwa kujihusisha na mambo kama;

·        Rushwa,
·        Uingizaji wa madawa ya kulevya,
·        Ufisadi wa rasilimali za umma na kadhalika


Mshangao wa watanzania wengi kwa nini Mheshimiwa Rais Kikwete pamoja na timu yake ya usalama wasiwafikishe kwenye vyombo vya sheria wahusika ili wachukuliwe hatua baada ya kuendelea kuyaeleza haya katika majukwao ya mikutano na makongamano? Inafahamika wazi kuwa Biashara ya madawa ya kulevya ni kosa, na kama hivyo sheria zipo? Sasa kama wamekamatwa kwa nini serikali inaendelea kuwabembeleza bembeleza waache hiyo biashara?

Nafikiri ni vyema kuikumbusha serikali kuwa kama washauri wa usalama hawana uhakika na taarifa sio vyema kumshauri mshemihwa Rais kutozisema kwani swala la madawa ya kulevya sio la kuendelea kulikemea kama wahusika wanajulikana; serikali itaendelea kuwakemea mpaka lini na ni nini? Hivi kisheria mtu ukiwa na taarifa za uhalifu lakini mwenye taarifa au uthibitisho akaendelea kukaa kimya bila kuzichukulia hatua ni kosa kisheria kwani ni namna ya kuendelea kuruhusu uhalifu huo, kuendelea na kama ni uhalifu wa   madawa ya kulevya taifa linazidi kuangamia kwa faida ya wachache.

nakubalia na kauli ya Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyosema ”Katika kupambana na tatizo hili la madawa ya kulevya, hatuna budi kutofumba macho ili kutowaonea haya watakaobainika kuwa chanzo cha usambazaji madawa ya kulevya, kwa sababu hili ni janga la kitaifa na tayari limeshawaathiri vijana wetu wengi sana” matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya yana madhara makubwa kwa Taifa, kiuchumi, kiafya na kijamii. Alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa ni vyema kushirikiana na jamii na kuwa waaminifu katika utekelezaji wake kwani wasambazaji kutokana na ushawishi na uwezo mkubwa wa kifedha walionao wamiliki na waingizaji madawa ya kulevya bado ni tishio kwa usalama wa jamii.

Lakini pamoja na  utata wa serikali katika kulikabili jambo hili sio busara kwa baraza la maaskofu  kumpa mheshimiwa Rais masaa ili kuwataja wahusika;  ni vyema Baraza hilo lingetumia njia mbadala yenye hekima katika kuiomba Serikali kuwafichua wahusika na sio kutoa muda wa kumshinikiza rais katika utendaji wake; kwa kumweleza rais kuwa asipofanya hivyo yeye atakuwa Mwongo na Mzushi; Ni kweli kuwa maneno haya yamesemwa na   watu wenye heshima kabwa ndani ya jamii. 

“Tunampa saa 48 rais awataje kwa majina viongozi hao ambao yeye anadai wanajihusisha na kuuza dawa na kama atashindwa kufanya hivyo tunamtafsiri ni mwongo na mzushi... Tunasikitishwa na kushangazwa kwa kauli hiyo na tunamheshimu kama kiongozi wa nchi, hivyo tunampa masaa hayo awataje kwa majina” 

Nafikiri umefika wakati kwa viongozi wa dini nchini Tanzania kukaa pamoja na Serikali kupembua kwa dhati mambo yanayopelekea uwepo wa mkanganyiko huu wa kutofautiana na kutokukubaliana 


Ni kweli  kuna tatizo ambalo linahitaji kulitafutiwa suluhu ya haraka; ama sivyo linaweza hatarisha misingi ya haki, amani na utulivu. Lazima tukubali kuwa sheria inapovunjwa haiangalii huyu ni kiongozi wa dini au la, inatakiwa chukua mkondo wake dhidi ya watu hao

Serikali ikiwaogopa vigogo na viongozi wa dini katika biashara hii, serikali itakuwa inakimbia jukumu lake la msingi la kulinda raia wake; hivyo jukumu la serikali kulinda maisha ya watanzania  hasa vijana dhidi ya madawa ya kulevya itakuwa ni ndoto tu.


Kwa hiyo serikali lazima isimamie kwa dhati kabisa  katika kulinda heshima ya Tanzania kama nchi isiyovumilia siyo tu biashara bali pia matumizi haramu ya dawa za kulevyawa. Kwa msingi huu hata watu wa Mungu kama wamo katika biashara hii ni busara kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria na kukamata mali zao na pasi zao za kusafiria ili haki itendeke. 

Thursday, June 9, 2011

NINI KIFANYIKE KUEPUSHA AJALI ZA BARABARANI TANZANIA?


TATIZO LA AJALI ZINAZOENDELEA NA KUPOTEZA MAISHA YA WATANZANIA WENGI;


NI UBUTU WA SHERIA?


UBOVU NA UFINYU WA BARABARA ZETU


KIBURI CHA MADEREVA?

UBOVU WA MAGARI NA UBABE WA WAMILIKI?

Taifa la Tanzania limeendelea kushuhudia  mwendelezo wa ajali nyingi za barabarani ambazo zimeendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa hili.  Kwa ujumla ajali hizi zimekuwa zikitokea kila kona wakati mamlaka za kisheria  zikiendelea kuhimiza kuwa zitahakikisha kuwa zitakomesha vifo vinavyoyokana na ajali hizo.husika kutekeleza yafuatayo;.
·         Kuimarisha doria katika njia kuu,
·         Askari wa Usalama Barabarani kuimarisha shughuli za ukaguzi wa magari mabovu,
·         Kuimarisha elimu kwa wananchi na wadau wengine juu ya umuhimu wa kuisaidia Serikali kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kuhusu madereva walezi, wanaoendesha mabasi yao kwa kasi, madereva wanaotiliwa mashaka kuhusu ujuzi wao wa kuendesha, na pia kukataa kupanda magari mabovu au yaliyojaa kupita kiwango kinachohitajika,
·         Kuendelea kuboresha sheria za Usalama Barabarani ili zichangie katika kudhibiti shughuli za usafiri na usafirishaji,. Kutoa elimu kwa madereva ili wazingatie sheria za kanuni za kazi zao,
·         Kukagua leseni za madereva ili kuhakikisha kuwa ni za halali,
·         Kuwashirikisha wenye magari ili washiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wanaajiri wadereva waaminifu na wenye kuwajibika. 

Pengine swali ambalo daima ninajiuliza pamoja na malengo mazuri yaliyoainishwa hapo juu, kwa nini serikali imeshindwa kabisa kisimamia utekelezaji wa sheria na sera zake za usalama barabarani kwa raia wake kwa muda mrefu?

Je serikali haina askari wa usalama barabarni wa kutosha kukabiliana na tatizo hili?

Je ni tatizo ni la wamiliki wa biashara hii wamefanikiwa kuiteka idara nzima ya usalama barabarani?

Je madereva wanaoendesha magari hayo wanafahamu fika maadili ambayo wanapaswa kuyafuata kulingana na sheria za usalama  barabarani wakati wa kuendesha magari hayo?

Tathimini ya muda mrefu kutoka  vyanzo mbalimbali inabaini kuwa licha askari hawa kuwapo na tunaambiwa kwa  kiasi kikubwa ajali zinazotokea zinasababishwa na madereva wazembe ambao wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani.

Tunajua, kwamba madereva wengi wa mabasi ya abiria  wanaendesha wamelewa. Je hakuna sheria inayowabana kama katika nchi nyingine kuhusu kilevi? Je, dereva huyu aliyekunywa pombe kabla ya kuanza kuendesha nap engine wakati wa safari  ataweza kuendelea kuwa na maarifa yake ya kawaida na uwezo wake wa kawaida kumudu gari na mazingira ya barabara yanayomkabili?

Inafahamika wazi mara nyingi  askari wa usalama barabarani wanabariki mwendo kasi wa madereva  kwa kupokea rushwa; je taifa linakubaliana na tabia hii izidi kuendelea? Tunawaacha wakimbize magari wanavyotaka mpaka lini?. Je tumeshindwa kabisa kusimamia “Speed Limit” ni ukweli ambao huupingiki kuwa Madereva wa mabasi wengi wanakimbia kupita speed waliyopangiwa. Je ni kweli kuwa serikali kupitia wizara yake kweli imeshindwa kuwadhibiti hawa madereva ambao ambao tunaweza kuwaita  wahuni  na wenye viburi kwani wamekuwa wakiendesha vyombo hivi vya moto kwa mwendo kasi, usiofuata taratibu za usalama barabarani na matokeo yake kusababisha ajali mbaya ambazo matokeo yake ni vifo vingi vya watu. Lo imefila wakati sasa serikali iamke na kusema basi inatosha kwa sasa hasa kwa kuanzaia na askari wake wa usalama barabarani wanaelezwa kuchangia uwepo wa ajali kwani wamekuwa wakiruhusu makosa kutendeka kwa sababu tu ya kuchukua rushwa ndogondogo.



Kwa nini serikali imeshindwa kusimamia sheria ya kutowaruhusu madereva matumizi ya simu za mikononi wanapokuwa wakiwaendesha raia;  ni vigumu sana kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja uwe makini barabarani na hapo hapo utumie simu kuongea na mtu mwingine;  Ni busara ya kawaida tu dhamana ambayo umebeba kama dereva ni zaidi ya Kuongea kwenye simu za mikononi kwa hiyo tabia hii  haifai kabisa kwa dereva wa gari la abiria aendeshapo gari. Hii ni hatari kwa abiria na watu wengine watembeao kwa miguu. Matokeo yake baada ya kujenga   madereva wanaleta kilio na hasara kubwa kwa taifa taifa letu na familia zetu kwa mambo tunayonaweza kuyazuia bila gharama yoyote


Je serikali kupitia wizara inakubali kuwaona askari wake wakikwepa maadili na kiapo chao cha kazi kwa kujihusisha na rushwa na kuhatarisha usalama wa watu wake; Tumke sasa kwa usalama wa watu wetu na kupinga kwa kauli moja mwendo kasi unaoendana na kutojali sheria na alama za barabarani

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa hata sheria zetu zinatoa mwanya mkubwa kwa mahakama kuwatoza faini ndogo badala ya kifungo au adhabu kubwa ambayo itakuwa pigo kwa dereva mna mmiliki wa biashara hiyo. Wote ni mashahidi wa jinsi ambayo watu ambao wamesababisha ajali kwa uzembe wa kujitakia, tena ajali ambayo imesababisha vifo vingi , lakini wamekuwa wakipigwa faini ya Sh50,000 na kuachiwa huru.  Je nchi nyingine wamefanikiwa namna gani kudhibiti ajali hizo za uzembe? Kwa nini tusijifunze kutoka huko?  



Pamoja na kwamba ajali haziwezi kuzuilika jumla,lakini tuzipunguze.Ajali ya gari inapotokea sio dereva tu ndiye wakulaumiwa,ang alia hali za barabara zetu zilivyo,hali ya hewa,abiria nao je wanaelewa sheria za barabarani ili kumkemea dereva anapovunja sheria hizo.Jambo la msingi ni kuelimisha watanzania wote wajue sheria za barabarani.

Tuangalie sheria Namba 30 ya Mwaka1973 na marekebisho yake ya mwaka 1996 inayohusu ni jinsi gani magari yanatakiwa yawe yakiwa barabarani.  Pamoja na tatizo la madereva  tuzinagatie vile vile tatizo la ubovu wa magari amabayo vile viel huwa ni chanzo cha ajali nyingi;


je wamiliki wanatoa kipaumbele gani katika kuhakikisha kuwa magari yao yako katika hali nzuri ya kusafirisha abiria kwa usalama?



Kwani nini gari bovu ambalo halina break nzuri linaruhusiwa kusafiri? Kama dereva ambaye anajali akatae kuendesha mpaka litengenezwe; uungwana wa wamiliki utaweza kuepusha ajali nyingi ambazo zinaweza kuzuilika kwa kutumia muda wa ziada kutengeneza gari na kuhakikisha kuwa liko salama kwa matumizi ya wananchi;  kama wamamiliki watalazimisha matumizi ya gari bovu  hatulidanganyi jeshi la polisi bali tunajidanganya sisi wenyewe na hatimaye kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Pamoja na tatizo kubwa la uchakavu wa miundombinu, ikizingatiwa kuwa   barabara nyingi haziko katika hali nzuri sana au nyingine pamoja na kutengenezwa hivi karibuni bado hazijeweza kusaidia kupunguza vifo kutokana na pengine kuwa chini ya kiwango  na kusababisha ajali haraka.  



Tunaomba serikali ikishauriana na wataalamu wake kuangalia  namna ya  kuepusha janga hili kwa kuwa na usimamizi ulio bora na kurekebisha mapungufu yatokanayo na:

Barabara mbovu; Magari mabovu; Mwendo wa kasi; Udereva mbaya; Usimamizi dhaifu wa sheria; na Watembea kwa miguu wasiojali. Rushwa katika utoaji leseni za udereva umetajwa katika orodha ya sababu za ajali chini ya kifungu cha Usimamizi dhaifu wa sheria. Kuruhusiwa kwa magari mabovu.

Safari bila ajali zinawezekana kabisa