WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 29, 2012

Jengo La Jumuiya Ya Afika Mashariki Lazinduliwa



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
 Mfano wa  jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia  kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki

PICHA NA IKULU 

Ziara ya Maalim Seif Sharif Hamad


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikaguzwa ujenzi wa shule ya ghorofa ya Sekondari Mpendae, alipotembelea ujenzi huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimpongeza mkandarasi wa ujenzi wa shuleya ghorofa ya Sekondari Mpendae bwana Liu Dao Xing kutoka China, alipotembelea ujenzi huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitembelea Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kampas ya Tunguu wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi za sekta ya elimu Zanzibar.
Mkandarasi wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari Tunguu kutoka Kampuni ya Electrics Intarenational ya Dar es Salaam Bibi Consolata Ngimbwa akitoa maelezo ya ujenzi huo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipotembelea ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi za sekta ya elimu Zanzibar.

Na Hassan Hamad-Zanzibar
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeitupia lawama Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai ya kutoishirikisha ipasavyo wakati inapofanya mabadiliko hasa yale yanayohusiana na mitihani ya Taifa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamuhuna ametoa malalamiko hayo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko makao makuu ya wizara hiyo Mazizini, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika sekta ya elimu.
Mhe. Shamuhuna amefahamisha kuwa Wizara ya Elimu Tanzania kupitia Baraza la Mitihani la Taifa, mara nyingi imekuwa ikafanya maamuzi bila ya kuishirikisha Wizara ya Elimu Zanzibar, jambo ambalo linawapa ugumu wa kuetekeleza mipango yao ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi kuweza kuyafahamu mabadiliko yanayofanywa na baraza la mitihani.

Ametoa mfano wa maamuzi yaliyofanywa hivi karibuni na baraza la mitihani ya kuwazuia baadhi ya wanafunzi kutofanya mitihani yao ya kidato cha sita hapo Februari mwakani kwa madai ya kutotimiza masharti ya kufanya mtihani huo, kwamba Wizara yake haikuarifiwa mapema juu ya masharti mapya ya sifa za kufanya mtihani wa kidato cha sita.

Amesema Wizara hiyo imekuwa ikikwepa kuiarifu Wizara yake juu ya mabadiliko yanayofanywa na Baraza la Mitihani la Taifa, na badala yake imekuwa ikiziarifu Skuli binafsi, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Amesema hali hiyo imekuwa ikichangia kutoa matokeo mabaya kwa wanafunzi wa Zanzibar kutokana na kutoarifiwa mapema juu ya mabadiliko yanayofanywa ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa ratiba za mitihani pamoja na muongozo wa kufundishia “Syllabus” kwa baadhi ya masomo.

Akizungumzia suala hilo Makamu wa Kwanza wa Rais amezishauri Wizara hizo kukaa pamoja na kujadiliana juu ya hatua bora za kuchukuliwa katika kuondosha tofauti hizo, na kuelezea haja ya kuwepo kwa mashirikiano ya karibu baina ya Wizara hizo mbili.

Baada ya kupokea taarifa ya Wizara hiyo iliyowasilishwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Abdalla Mzee, Maalim Seif alihoji juu ya uhaba wa madarasa ya kusomea pamoja na vikalio katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba.

Pia ameelezea haja ya kurejeshwa kwa huduma za dakhalia ili kuwaondoshea usumbufu wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali, hoja ambayo imeungwa mkono na uongozi wa Wizara hiyo kwamba wamelifikiria kwa muda mrefu suala hilo lakini bado wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mwanaidi Saleh amesema Wizara hiyo ina dhamira ya kurejesha huduma hiyo kwa wanafunzi wakati wowote hali ya bajeti itakaporuhusu.

Katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) huko Tunguu, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idrisa Ahmada Rai, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais juu ya mipango ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kukifanya kuwa kituo bora zaidi cha elimu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Profesa Rai amesema miongoni mwa dhamira kuu za chuo hicho ni kutoa wahitimu wa ngazi mbali mbali ambao wataweza kukabiliana na changamoto za karne ya 21 ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameupongeza uongozi wa Chuo kicho kutokana na mafanikio makubwa yaliyofikiwa pamoja na mipango imara ya kukiendeleza.

Hata hivyo ameutaka uongozi wa SUZA kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa malengo yake ili kuweza kukamilisha malengo hayo kwa wakati muafaka.

Katika ziara hiyo Maalim Seif pia alitembelea ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Sekondari Mpendae pamoja na ujenzi wa skuli ya sekondari Tunguu, ambapo amewataka wakandarasi wa ujenzi huo kukamilisha kazi zao kwa wakati.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais amefanya mazungumzo na ujumbe wa serikali ya Uturuki ukiongozwa na Waziri wa Chakula, Kilimo na Mifugo wa nchi hiyo Bwana Mehmet Mehdi Eker.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea haja ya kukuza mashirikiano katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi zikiwemo biashara na utalii.

Bwana Aker amesema Uturuki imepata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita baada ya kufanya mabadiliko ya sera yake ya kilimo, jambo ambalo limeongeza uzalishaji hasa katika kilimo cha mpunga.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ameiomba Uturuki kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Zanzibar katika kilimo cha umwagiliaji ikizingatiwa kuwa nchi hizo zina uhusiano wa muda mrefu

source: Hassan Hamad-Zanzibar

Ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga


sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River
Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania




Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania
Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki Jumatano Novemba 28, 2012 wamefungua rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga kwa upande wa Tanzania, na Namanga– Athi River kwa upande wa Kenya, kama sehemu ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi unaofanyika Nairobi, Kenya.
Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya shughuli za uzinduzi rasmi wa Makao Makuu Mapya za Jumuiya uliofanyika mapema siku hiyo hiyo jijini Arusha, kabla ya viongozi hao kuelekea Athi River kwa ufunguzi wa barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Tanga–Horohoro, yenye urefu wa kilomita 66 pia nao umekamilika na tayari imeanza kurahishisha usafiri na usafirishaji baina ya Tanzania na Kenya na nchi nyingine wanachama.
Barabara nyingine zilizopo katika mtandao wa barabara wa Jumuiya zinazoendelea kujengwa kwa upande wa Tanzania, ni pamoja na zile za mtandao wa Dar es Salaam-Isaka-Lusahunga na Mutukula hadi Masaka; Lusahunga-Nyakasanza hadi Rusumo, na Rusumo-Kigali hadi Gisenyi.
Nyingine ni Biharamulo - Mwanza - Musoma - Sirari - Lodwar – Lokichogio; Tunduma - Sumbawanga - Kigoma - Manyovu (Mugina) - Rumonge - Bujumbura - Ruhwa (Bugarama) – Karongi hadi Gisenyi, pamoja na ile ya Tunduma - Iringa – Dodoma - Arusha - Namanga hadi Moyale.
Ujenzi wa barabara hizi utarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na huduma baina ya nchi wanachama, na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na vilevile gharama za kufanya biashara katika nchi za Jumuiya na hivyo kuvutia uwekezaji.

source: vijimambo blog

KILI STARS YALALA CHALI I - O KWA BURUNDI


Kocha wa Tanzania, Mdenmark, Kim Poulsen akihamaki wakati dakika zikiyoyoma, huku timu yake ikiwa imelala 1-0 katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Burundi, Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0
Mbunge wa Kondoa, Juma Nkamia (kushoto) akiwa na Mjumbe wa TFF, Wallace Karia wakifuatilia mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kati ya Tanzania na Burundi Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0
Kikosi cha Stars leo
Mshambuliaji wa Tanzania, Simon Msuva akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa Tanzania, Simon Msuva akijaribu bila mafanikio kumfunga kipa wa Burundi,Arthur Arakaza katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa Tanzania, Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0
Mshambuliaji wa Tanzania, Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Kiungo wa Tanzania, Frank Domayo akimdhibiti kiungo wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Kiungo wa Tanzania, Frank Domayo akimdhibiti kiungo wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa Tanzania, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa Tanzania, John Bocco akiruka juu lupiga mpira kichwa mbele ya mabeki wa Burundi katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. Burundi ilishinda 1-0.
Mashabiki wa Tanzania wakishangilia bila kukata tamaa

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
BAO pekee la mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Suleiman Ndikumana dakika ya 52, leo limeizamisha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, usiku huu. 
Nahodha huyo wa Burundi, anayechezea Inter Stars ya nyumbani kwao kwa sasa, alifunga bao hilo kwa penalti, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari na Shomary Kapombe.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Burundi walifanya mashambulizi mawili ya hatari zaidi, lakini sifa zimuendee ‘TZ One’, Juma Kaseja aliyeokoa hatari hizo.
Stars hawakucheza soka yao ya chini kutokana na hali mbaya ya Uwanja, kujaa matope, kuwa wenye kuteleza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya leo.
Kipindi cha pili Stars walijitahidi kutaka kusawazisha mabao hilo, lakini bahati haikuwa yao na zaidi waliishia kukosa mabao mawili ya wazi.
Kwa matokeo hayo, Burundi imeendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zao sita, mabao sita ya kufunga na moja la kufungwa, wakati Bara inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, Sudan ya tatu ikiwa na pointi tatu na Somalia yenye pointi moja inashika mkia.
Kikosi cha Tanzania Bara leo kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe/Issa Rashid, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco, Mwinyi Kazimoto/Shaaban Nditi na Simon Msuva/Amri Kiemba.
Burundi; Arthur Arakaza, Gilbert Kaze, Haruna Manirakiza, Hassan Hakizimana, Emery Nimubona, Yussuf Ndikumana, Steve Nzigamasabo, Chris Nduwarugira, Suleiman NdikumanaChris Ndayishimiye na Amisi Tambwe.
source: vijimambo.blog

Neno Fupi La Usiku Huu: Chagua Vita Vyako...



Ndugu zangu, 

 Maishani kuna kushinda na kushindwa. Hata hivyo, ushindi una gharama. Siku zote, mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Mana, ushindi waweza kuwa ghali mno. Ndio, unaweza kupambana ukashinda, lakini, gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako. Yawezekana watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu. 

Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine, ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui. 

Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi". Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu! Ndio, kama unapigana vita ya muhimu. Na kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda (winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani. Na kama la, basi, tafuta suluhu, au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat). 

 Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la? Miaka mingi iliyopita alitokea Mfalme wa Epilus aliyeitwa Pyrrhic. 

Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi. Ni jeshi la Warumi. Lakini, kabla ya Mfalme kuingia baharini na vikosi vyake ili kuitafuta Italia ya Warumi, msaidizi wake wa karibu, Cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na Mfalme. Alitaka kumwuliza maswali na kumshauri. Cineas alimtamkia Mfalme; “ E bwana Mfalme, Warumi wanasadikika kuwa na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana wameteka nchi nyingi. 

Je, Mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda Warumi, tutafanya nini na ushindi wetu? Mfalme akajibu: “ Mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara ile tukiwashinda Warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa Italia litakaloweza kupambana nasi.” Cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza Mfalme: 

“ Tukishaikamata Italia ya Warumi, kipi kitafuatia?” Mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa, itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho.” Cineas aliendelea kuuliza:

 “ Bwana Mfalme, unaongea juu ya mambo ya kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha Sicily kutakuwa na maana ya kukoma kwa vita?” Mfalme akajibu: “Hapo tutakuwa tumeikaribia Afrika. 

Na tukishaikamata Afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita?” “Hakuna” Alijibu Cineas, kisha akauliza; “ Na baada ya hapo tutafanya nini?” Mpaka hapo Mfalme hakujua Cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya kifikra. Mfalme akajibu: “Baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa. Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima.

” Kama ni hivyo, alisema Cineas; “ Ni kitu gani kinachotuzuia kufanya hayo yote sasa bila kwenda vitani? Mfalme hakuielewa mantiki ya Cineas. Akakaidi ushauri. Akavipeleka vikosi vyake kupambana na Warumi. 

Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme liliwashinda Warumi. Hata hivyo, lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu kuitwaa Sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye akakakamatwa kama kuku. Akauawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya Argos. 

Naam, chagua vita vyako, 

Na hilo Ni Neno fupi la usiku huu. 

 Maggid,

Safari Ya Mwisho Ya Sharo Milionea



                                                                
MAELFU ya waombolezaji jana walijitokeza kushiriki mazishi ya msanii Hussein Ramadhan maarufu kwa jina la Sharo Milionea, huku mamia wakizirai baada ya kushindwa kujizuia wakati mwili wake unawekwa kaburini.


Mwili wa msanii huyo ulizikwa jana kijijini kwake Lusanga wilayani Muheza saa 7 mchana, katika tukio lililomshirikisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.


Waombolezaji walianza kumiminika kijijini Lusanga tangu juzi jioni na idadi yao iliongezeka zaidi jana asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi.Sala ya mazishi iliongozwa na Sheikh Twaha Juma ambaye baadaye aliamuru jeneza hilo kupelekwa makaburini, ambako waombolezaji kadhaa walipoteza fahamu.

20 wapelekwa hospitali
Miongoni mwa matukio yaliyojitokeza katika msiba huo ni baadhi ya waombolezaji kupoteza fahamu msibani.Matukio tofauti ya watu kuzirai yalitokea wakati mwili wa msanii huyo ulipokuwa unapelekwa nyumbani kwao kijijini Lusanga ukitokea Hospitali Teule ya Wilaya ambako ulihifadhiwa tangu alipopata ajali Jumatatu usiku na wakati wa mazishi.

Miongoni mwa waliopoteza fahamu katika msiba huo ni wasanii na waigizaji wa filamu waliokuwa wakiigiza na Sharo Milionea wakati akiwa katika kundi la AL Riyam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MC wa shughuli hiyo, Steve Nyerere, zaidi ya watu 20 walipoteza fahamu katika msiba huo na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza.


DC Mgalu aliwaomba waombolezaji kutokuwa na shaka juu ya waliopoteza fahamu kwa kuwa madaktari maalumu walikuwa wameandaliwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuwapa huduma.
Mwananchi lilifika katika hospitali Teule na kukuta waliokuwa wamepoteza fahamu, wengi wao wakiwa ni wasichana, wakipata huduma huku wengine wakiomba kupewa ruhusa ili wakahudhurie maziko.

JK atuma rambirambi
Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kutokana na vifo vya wasanii watatu vilivyotokea hivi karibuni, kikiwamo cha Sharo Milionea.


Taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema kuwa Rais Kikwete ameshtushwa na vifo hivyo vya ghafla.
Wasanii hao ambao walifariki dunia katika mazingira tofauti ni Mwigizaji wa Kundi la Kaole, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu

Soma zaidi:  http://www.mwananchi.co.tz/habari



Mkuu Wa Wilaya Na Nape Wamzika Sharobaro

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nauye, akitupa mchanga kaburini, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama  Anna Mkapa, kwenye msiba huo. Pamoja naye ni Nape

 (Picha na Bashir Nkoromo).


Wednesday, November 28, 2012

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Arejea Ziarani Nchi Veitinam



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein, alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akivishwa shada la maua
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimuelezea jambo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akitokea ziarani nchi Vietinam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Serekali waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Abdalla Mwinyi Khamis na Meya wa Mji wa Zanzibar Khatib Abrahaman, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Zanzibar.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumzia ziara yake Nchini Vietinam na mafanikio ya ziara hiyo kwa Zanzibar na Wananchi wakev katika sekta ya Biashara na Uvuvi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amamaan Karume. akirejea katika ziara yake ya Kiserekali Nchini Vietinam.