"Wananchi wanatakiwa wasiiogope Serikali; bali Serikali inatakiwa iwaogope Wananchi wake"
WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;
A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy
“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere
Sunday, December 26, 2010
Monday, December 20, 2010
Politics Corner "Debate on Constitution"
The discussion of change of Constitution let remember Hillary Rodham Clinton once said:
"The challenges of change are always hard. It is important that we begin to unpack those challenges that confront this nation and realize that we each have a role that requires us to change and become more responsible for shaping our own future."
Philip Crosby reminded us that;
Philip Crosby reminded us that;
"If anything is certain, it is that change is certain. The world we are planning for today will not exist in this form tomorrow."
Leadership advise:
- Theodore Roosevelt
Leadership advise:
People ask the difference between a leader and a boss. . . The leader works in the open, and the boss in covert. The leader leads, and the boss drives.
- Theodore Roosevelt
Think of managing change as an adventure. It tests your skills and abilities. It brings forth talent that may have been dormant. Change is also a training ground for leadership. When we think of leaders, we remember times of change, innovation and conflict. Leadership is often about shaping a new way of life. To do that, you must advance change, take risks and accept responsibility for making change happen.
§ Charles E. Rice, CEO of Barnett BankSunday, December 19, 2010
Politics Corner
The fight for justice against corruption is never easy. It never has been and never will be. It exacts a toll on our self, our families, our friends, and especially our children. In the end, I believe, as in my case, the price we pay is well worth holding on to our dignity.
Frank Serpico
Frank Serpico
Thursday, December 16, 2010
BURIANI DOCTOR REMMY ONGALA
NINI TUMEJIFUNZA TOKA KWA HAYATI REMMY ONGALA aka DOCTOR?
Wapenzi wa muziki wa dansi na Muziki wa Injili tumepokea kwa masikitiko habari za kifo cha mkongwe wa muziki/Injili doctor Remmy Ongala ambacho kimetokea tarehe 13/12/2010.
Swali la msingi kwa nini kifo chake kimewagusa wengi? Majibu ya swali hili ni mengi sana kulingana na kila mtu na mtazamo wake na kwa namna ambavyo alikuwa anamfahamu na Doctor Remmy kupitia nyimbo na maisha yake mengine ya kawaida na kwa namna ambavyo aligusa hisia zetu.
Kwa upande wangu nitazungumzia hasa URITHI gani ambao Remmy ametuachia sisi kama wananchi wa Tanzania. Marehemu Remmy ametuachia jambo moja kubwa la kuwa wakweli katika katika kutekeleza majukumu yetu bila kumwogomba mtu yeyote Yule; ni Mwenyezi Mungu tu wa kuogopewa. Remmy alikuwa mkweli, muungwana na mwelimishaji wa aina yake.
Aliweza kukitumia kipaji chake katika kuwatetea wanyonge kwa kupitia musiki wake, alikuwa anajitahidi sana kutoimba sana nyimbo za mapenzi na badala yake kuimba zaidi nyimbo zilizokuwa zinagusa na kueleza matatizo ya wanyonge watu wa kipato cha chini, ambao hawana sauti amabyo wakiitumia inaweza kuwasaidia kutatua mataizo yao.
Aliwahi kusema huko nyuma kuwa dunia hii ni gereza wanyonge ambao hawana uwezo wa kuyafurahia maisha kwa vile hawana uwezo hivyo wao ni wakuamuriwa tu nini wafanye ni sawa na wafungwa. Mafanikio ya wanyonge lazima yatokane na furaha ya matajiri ambao furaha yao ndio nafuu ya wanyonge na hasira yao ni kiyama kwa wanyonge.
Doctor Remmy kwa kweli Alifanikiwa sana kueleza ukweli wa maisha wa wanyonge kama umasikini, tatizo la ukimwi na namna ya kujikinga na maambukizo, ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu, rushwa mapenzi na uvumilivu kwa kupitia muziki wake; ndio maana kumbi zake zilikuwa zinawapenzi wengi wa Muziki.
Nakumbuka sana ule wimbo wake wa Mambo kwa soksi ambao ulikuwa unahamasisha sana watu watumie kondom katika swala la mapenzi ili kujikinga na maambukizo ya ukimwi; wimbo huu ulionekana kupingana na maadili kwa wakati huu, lakini ukweli Doctor Remmy ulikuwa miongoni mwa elimishaji wa ngono salama kwa jamii. Aliitumia sanaa yake kuwa kweli ni kioo cha jamii katika kutatua tatizo. Hatukuwa tayari kuukubali ukweli huu, tukitumia kigezo ujumbe huu ulikuwa umewasilishwa kunyume na utamaduni wetu. Bila kuogopa ukweli huu Remmy aliuweka bayana, je leo hii Jamii yetu tunaielimisha vipi? Tukubali au tukatae myonge myongee lakini haki yake mpe Remmy alikuwa ameona mbali na alikuwa anawaonyesha wanyonge haki hiyo ya gharama nafuu kwa usalama wa maisha yao;
Yako mengi ya kusema la msingi tu muziki ambao ulikuwa ukipigwa na kutungwa na Doctor Remmy ulikuwa na hisia kali za kuelimisha kulingana na mazingira; tutamkumbuka sana kupitia nyimbo zake; tutamkosa kwa sababu hatutapata tena mashairi na na uimbaji wa hisia kwama wake;
Mwenyezi Mungu amempa Baraka za maisha yake kwa kazi kubwa ambayo ametufanyia kwa kumuwezesha kutumia muda wake wa kutosha kabla ya kifo chake kumwimbia yeye; na kwa kulisoma neno lake kwa utulivu zaidi na kwa makini ampaka pale alipowita kwake katika mapumziko ya milele; kama wengi walivyosema tumempenda sana mpendwa wetu Remmy lakini Mungu amempenda zaidi; Yeye alitoa na Yeye Ametwaa, jina lake na lihimidiwe milele Amin
Thursday, December 9, 2010
KWA NINI BADO TUNAHITAJI ELIMU YA URAIA KWA WATANZANIA HASA WAISHIO VIJIJINI?
Demokrasia ina gharama kubwa sana, ambayo pengine haionekani kwa haraka sana, kwa wananchi wa kawaida; mfumo huu wa maisha unawahusisha wananchi katika kutekeleza sehemu hii kubwa ya uchaguaji wa viongozi wao. Wananchi wengi hawapendi sana kujihusisha na swala hili kwa vile wanaamini kuwa sio lazima sana wao wahusike wakati kuna wengine wengi wanaweza fanya hivyo. Hivyo kila mmoja humsukumia mwenzake swala la upigaji wa kura. Kuchagua kiongozi mzuri kwao hakuna maana yeyote kwao na haina manufaa kwao mimi naungana na kundi hili kwa sababu ambazo nitazieleza hapo baadae.
Leo nitazungumzia kwa nini wananchi wengi hawajitokezi wakati wa zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge wake: Tumeshuhudia katika uchaguzi huu uliomalizika October 2010 kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuto kujitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, swali ni kwa nini?
Mtazamo wangu unalenga zaidi katika ukosekanaji wa elimu ya uraia;
Kwa nini tunahitaji elimu ya uraia? Je hatuna kabisa mashirika au idara za serikali au za watu binafsi au Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanajishughulisha na ufundishaji wa elimu hiyo? Kama tunayo kwa nini hakuna mabadiliko ya msingi ya uelewa huu kwa wananchi kwa ujumla hasa wale wanaoishi vijijini? Je idara na mashirika hayo yamelenga zaidi katika ufundishaji wa elimu gani kwa ustawi wa demokrasia?
Lengo kubwa la elimu ya uraia ni kuleta na kuimarisha uelewa wa wananchi katika kuzielewa na haki zao zitokanazo na upigaji wa kura; Elimu ya uraia vile vile husaidia sana katika kuondoa fikra tofauti ambazo zinaweza kuletwa na chama au vyama katika kujinadi hasa wakati wa kampeni za uchaguzi, kama tu wananchi wameiva katika kuelewa haki zao. Wananchi hawajui hata kama wao ndio wafanyanyi wa maamuzi makubwa sana ya maendeleo yao;
Kwa nchi kama Tanzania kwa hivi sana umasikini ndio umekuwa kielelezo cha kuwachagua viongozi, ukizingatia kuwa kutokana na ugumu huo pesa utumika kununua kura, ambazo huwachagua wawakilishi wa watanzania walio wengi ambao wanakuwa hawana sauti katika kujua hatima ya maendeleo yao. Wananchi walio wengi hawana elimu kabisa ya uraia na hawajui namna gani kura zao zina thamani kwa maendeleo ya nchi. Kwa mfano katika wananchi takribani karibu million 19 waliojiandikisha kupiga kura ni ni pungufu ya nusu ndio waliopiga kura. Je hii inamaanisha nini?
Inaelekea kuwa elimu kama inatolewa haitolewi kwa ukamilifu hasa kwa wananchi wa vijijini, ndio maana hata leo katika nchi ya Tanzania bado kuna wananchi ambo wanafahamu fika kuwa Mwalimu J. Nyerere bado ni rais wa Tanzania; je REDET wako wapi? Serikali na mashirika yake pamoja na NGOS wako wapi katika kueleimisha hili? Ifahamike kuwa kuto kumpa mwananchi elimu ya uraia ni kumnyanyasa kifikra na kimaendeleo. Kwa ufupi kukosekana kwa elimu ya uraia kumesababisha :
· wananchi wasione umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa kujua kuwa kupiga kwao kura ama sivyo hakuwezi kubadilisha chochote.
· Wananchi hawajioni ni kama wanaweza kudai haki yao kwa njia sahihi ya kupiga kura
Wakati umefika wa kuwauliza wote wanaohusika na utoaji huo wa elimu je kipimo cha ufanisi au ubora wa kazi yao ni nini? Kwa mwanafunzi kipimo cha elimu aliyepewa ni kuelewa alichofundishwa, kufanya tathimini na hatimaye kuweza kufaulu mitihani yake, je kwa vikundi vyote vinavyojihusisha na utoaji wa elimu hii kipimo chao ni nini. Je wanaweza kuwapimaje wale wananchi hasa wa vijijini ambao wanahitaji sana elimu hiyo je wako;
· Chini ya kiwango (below Basic) hawa ni wale wenye elimu kidogo au hawana kabisa.
· Wastani(basic) wana elimu ya kutosha kuhusu mada nzima
· Juu ya kiwango (advanced) wamebobea katika elimu ya uraia wanaijua nini wanataka na watapata vipi.
Bado tunasafari ndefu lakini inahitaji umakini mkubwa sana; ambao unahitaji wannanchi makini ambao ndio wanaweza kutuletea viongozi makini, maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe na sio mtu mwingine yeyote Yule? Tukumbuke kuwa kama hatutachukua hatua ya haraka katika kuwaelimisha watu wetu kuhusu elimu ya uraia tunaemdelea kuwajaza wananchi wetu na ujinga hivyo na tutaendelea kuwajaza hofu katika kufanya maamuzi, hivyo hakuna namna yeyote wataweza kumchagua mtu sahihi kwa namna wao wanavyoona; watamchagua mtu kupitia ulipaji wa fadhila kwa vile ulinipa hiki name nakupa hiki. elimu ya uraia ikifundishwa vyema ni rada ya kuongozea demokrasia katika nchi kwani huipeleka nchi katika njia sahihi kwa faida ya taifa na sio tija binafsi wa wanjanja wachache.
Wananchi wazuri ambao wanaelewa taarifa kuhusu mwelekeo wa serikali na siasa katika nchi yao hawajezaliwa hivyo bali wamepikwa kutokana na elimu ya uraia.
Thursday, December 2, 2010
JE NI KWELI KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU? ( IS IT TRUE THAT POLITICS IS A DIRTY GAME?)
Siasa ni mfumo ambao unahusisha zaidi uongozi wa watu kwa kufuata kanuni, sheria, sera, uwajibikaji, uwazi na ugawaji wa rasilimali sawa kwa wnanchi wake;katika kuwaleta maendeleo wadau wakuu ambao ni wananchi.
Kwa msingi wa utashi huu, wananchi wanakichagua kikundi cha watu ambao wanawaamini na kuwapa uwezo wa kuunda serikali ili iwaongoze kwa niaba yao. Kwa hivyo hakuna nchi yeyote hapa duniani ambayo haina serikali. Tofauti inayoweza kujitokeza ni namna serikali hiyo inavyoundwa katika misingi ipi? Na inatekeleza vipi kanuni na taratibu zake? Je kuna uwazi katika shughuli zake? Viongozi wanabebe dhamana ya watu katika utendaji wao na wawajibikaje kwa wananchi ambao ndio waliowaweka ofisini; na viongozi wanatakiwa wawajibike na kuwaletea maendeleo wananchi wao.
Siasa kama siasa sio mchezo mchafu;siasa inageuka kuwa mchezo mchafu pale tu serilali ambayo imekabidhiwa dhamana na wananchi inaanza kwenda kinyume na utaratibu na kanuni sahihi, na kuto fuata maadili ya uongozi (code of conduct) ndipo tafsiri ya siasa inaanza kugeuka na kuwa mchezo mchafu. Amin Dada
Misingi ya siasa chafu imechochewa sana na mwanasalsafa Machiavelli ambaye aliandika katika maandishi yeke kuhusu viongozi na madaraka; kitabu chake kinawanufaisha sana viongozi katika kuimarisha nafasi zao za uongozi, amewafundisha viongozi namna ya kuwa waongo (liar), wakatili, wanafiki, kuwa na uchu wa mali, na hata ikibidi kuua ili kupata madaraka na kuudumisha adhima yao ya kuendelea kunyonya na kujitajirisha. mwongozo huu wa Machiavelli unatumiwa sana na watawala wa mabavu (dictators), kutoka nchi mbalimbali ambao waliongoza au wanaongoza nchi zao kwa manufaa binafsi na sio kuwaletea maendeleo wananchi bali huwajengea hofu na kuwasababishia wananchi wao maisha magumu, watawala kama; Idd Amin Dada, Mabuto, na kadhalika. Katika mlengo huu hakuna kuwajibishana, kinachofanyika hapa wananchi ni kusikiliza na kutii tu
Uchafu wa siasa ni pale tunapoilinganisha siasa kama wapiganaji katika mchezo wa mieleka ule ambao hauna kanuni yeyote ili ushinde, unaweza kumchezee au kumpiga au kumwangusha mpinzani wako kwa namna yeyote ile uwezayo ili mradi tu wewe uwe mshindi; hapa hakuna kanuni yeyote inayohitajika refarii yuko pale kutangaza mshindi tu kwani hana kanuni yeyote ambayo anafuata; hapo ndipo tafsiri ya mchezo mchafu inapoanza.je nini kazi ya wanasheria wetu? Utetezi au uonevu? Tatizo la mchezo huu ukiuanza huwezi kuuacha. Ushauri kama huuwezi kamwe usiucheze waache wanaouweza waucheze, watu wenye kiburi na wasiojali utu hata mara moja. Na ukiamua kuucheza kamwe usiuache au usiwasaliti wenzako ukifanya hivyo safari yako yakuendelea kufurahia maisha ya siasa yataishia kaburini.
Je siasa zetu zinalenga wapi tunaoutaratibu ambao tunaweza kumwajibisha hata kiongozi wa juu wa nchi anapokiuka maadili ya uongozi? mkumbuke Nixon na “Watergate scandal” kwa kosa lolote lile ambalo alifanya akiwa kama kiongozi mkuu wan nchi alikiuka maadili ya uongozi kulingana na taratibu za serikali ya Marekani kilichofuata ni kumpigia kura ya kutomwamini na kumwondoa ofisini kama Raisi; alikwenda kwenye ziara kama Raisi wa Marekani ndani ya "Airforce One" lakini alirudi nyumbani kama raia wa kawaida kwa kutumia ndege ya kawaida ya abiria.
Je siasa zetu zinalenga wapi tunaoutaratibu ambao tunaweza kumwajibisha hata kiongozi wa juu wa nchi anapokiuka maadili ya uongozi? mkumbuke Nixon na “Watergate scandal” kwa kosa lolote lile ambalo alifanya akiwa kama kiongozi mkuu wan nchi alikiuka maadili ya uongozi kulingana na taratibu za serikali ya Marekani kilichofuata ni kumpigia kura ya kutomwamini na kumwondoa ofisini kama Raisi; alikwenda kwenye ziara kama Raisi wa Marekani ndani ya "Airforce One" lakini alirudi nyumbani kama raia wa kawaida kwa kutumia ndege ya kawaida ya abiria.
Nixon
Siasa sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneykevu na wenye huruma ya kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi nyingine?
Tukumbuke kwa wale ambao wamesoma kitabu cha sharkespear nini alikifanya Macbeth kwa kusababisha umwagaji wa damu ambao ulikuwa hauna sababu kwa sababu tu ya siasa za ubinafsi na hatimaye kutekeleza mwonekano wa siasa kuwa mchezo mchafu ambao mwisho wa siku ulimgeukia mwenyewe na kuuwawa. Tatizo la uchafu wa siasa pengine huanzia kwa serikali kuona kuwa ofisi zao ndio biashara yao hivyo hata ile mishahara ambayo wamewekewa kisheria haiwatoshi na huanza kujiingiza katiak rushwa, mikataba mibovu ambayo inawapa masilahi wao binafsi, na kuwaongezea nguvu ya kipesa na uwezo wa kuongoza kwa masilahi ya watu wachache.
Katika nchi zetu ambazo umasikini umekidhiri, tatizo la kukosekana kwa ajira, kupeana kazi na vyeo kwa kufuata undugu na urafiki na sio sifa za elimu, kuwanunua watu kwa kuwapa zawadi wakati wa kampeni na hatimaye wakati wa upigaji wa kura, kwa misingi hiyo sio rahisi baada ya uchaguzi kwa wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Siasa taalumu nzuri sana na muhimu kwa jamii ikiwa itawapata viungozi wazuri na waungwana ambao wamewaeka wananchi mbele ya maendeleo yao, lakini siasa ikiwapata viongozi wabovu wala rushwa nchi imekwisha na wanyonge hawana chao ndipo hapo siasa inapokuwa ni mchezo mchafu. Kwa msingi huu ni kuwa siasa sio mchezo mchafu ni mchafu tu ikipata watu wala rushwa na sio waaminifu, walafi wa madaraka,
Ni mchezo mchafu tu kama utaratibu wote wa uchaguzi haukwenda vizuri na matokeo yake baada ya hapo ni chuki binafsi baina ya vyama na hiyo mwisho wa siku itamaanisha kuwa chama tawala na chama cha upinzani ni maadui na hakuna wa umuhimu wa chama kingine kuwapo, vyama vya siasa katika nchi vinaweza kuiongoza kwa kupokezana ni kama huko Marekani wakati wananchi wanapoona kuwa nchi iko amani yao ina mashaka wanakipigia Republican lakini wakiona uchumi wao unayumba wanakipigia Democratic;
Tukumbuke maneno ya Raisi JF Kennedy wa Marekani alivyosema” hakuna mtu ambaye atanishawishi mimi kufanya kitu ambacho nafikiri sio kwa masilahi ya nchi yangu, kama wewe au mtu mwingine anafikiri kuwa ndiye, basi huyo ni Mwendawazimu” Hii ndio tofauti ya kiongozi ambaye kwake siasa ni mchezo mzuri kwa masilahi ya wananchi wake na taifa lake, ambaye ni mkweli mwadilifu na ambaye anaweza kutoa maamuzi mazito kwa faida ya nchi yake, LAKINI pale tunapokosa maadili ya uiongozi tunakaribisha sana urafiki, undugu na kugeuza ofisi zetu ambazo zimewekwa kwa masilahi ya Taifa kuwa sehemu za biashara na kuwakaribisha zaidi wenye fedha kututawala kwa kutoa mwongozo nini kifanyike hapo ndipo tunabadilisha tafsiri sahii ya siasa kuwa mchezo mchafu. Pengine bora hata kiongozi ambaye ni mbabe wa maendeleo ya taifa ambaye anapinga uzembe na hana rafiki wala ndugu ndugu yake ni maendeleo ya nchi yake. Je tunao viongozi wa namna hii hasa barani Afrika. tumkumbuke Mzee wetu, Mandela Nyerere na wengine wa namna kama yao
Nukuu:
Politics is the gentle art of getting votes from the poor and campaign funds from the rich, by promising to protect each from the other.
Oscar Ameringer
Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason.
Author Unknown
Blessed are the young, for they shall inherit the National Debt."
Herbert Hoover
Richard Nixon is a no good, lying bastard. He can lie out of both sides of his mouth at the same time, and if he ever caught himself telling the truth, he'd lie just to keep his hand in."
Harry S. Truman.
Subscribe to:
Posts (Atom)









