Demokrasia ina gharama kubwa sana, ambayo pengine haionekani kwa haraka sana, kwa wananchi wa kawaida; mfumo huu wa maisha unawahusisha wananchi katika kutekeleza sehemu hii kubwa ya uchaguaji wa viongozi wao. Wananchi wengi hawapendi sana kujihusisha na swala hili kwa vile wanaamini kuwa sio lazima sana wao wahusike wakati kuna wengine wengi wanaweza fanya hivyo. Hivyo kila mmoja humsukumia mwenzake swala la upigaji wa kura. Kuchagua kiongozi mzuri kwao hakuna maana yeyote kwao na haina manufaa kwao mimi naungana na kundi hili kwa sababu ambazo nitazieleza hapo baadae.
Leo nitazungumzia kwa nini wananchi wengi hawajitokezi wakati wa zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge wake: Tumeshuhudia katika uchaguzi huu uliomalizika October 2010 kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuto kujitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, swali ni kwa nini?
Mtazamo wangu unalenga zaidi katika ukosekanaji wa elimu ya uraia;
Kwa nini tunahitaji elimu ya uraia? Je hatuna kabisa mashirika au idara za serikali au za watu binafsi au Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanajishughulisha na ufundishaji wa elimu hiyo? Kama tunayo kwa nini hakuna mabadiliko ya msingi ya uelewa huu kwa wananchi kwa ujumla hasa wale wanaoishi vijijini? Je idara na mashirika hayo yamelenga zaidi katika ufundishaji wa elimu gani kwa ustawi wa demokrasia?
Lengo kubwa la elimu ya uraia ni kuleta na kuimarisha uelewa wa wananchi katika kuzielewa na haki zao zitokanazo na upigaji wa kura; Elimu ya uraia vile vile husaidia sana katika kuondoa fikra tofauti ambazo zinaweza kuletwa na chama au vyama katika kujinadi hasa wakati wa kampeni za uchaguzi, kama tu wananchi wameiva katika kuelewa haki zao. Wananchi hawajui hata kama wao ndio wafanyanyi wa maamuzi makubwa sana ya maendeleo yao;
Kwa nchi kama Tanzania kwa hivi sana umasikini ndio umekuwa kielelezo cha kuwachagua viongozi, ukizingatia kuwa kutokana na ugumu huo pesa utumika kununua kura, ambazo huwachagua wawakilishi wa watanzania walio wengi ambao wanakuwa hawana sauti katika kujua hatima ya maendeleo yao. Wananchi walio wengi hawana elimu kabisa ya uraia na hawajui namna gani kura zao zina thamani kwa maendeleo ya nchi. Kwa mfano katika wananchi takribani karibu million 19 waliojiandikisha kupiga kura ni ni pungufu ya nusu ndio waliopiga kura. Je hii inamaanisha nini?
Inaelekea kuwa elimu kama inatolewa haitolewi kwa ukamilifu hasa kwa wananchi wa vijijini, ndio maana hata leo katika nchi ya Tanzania bado kuna wananchi ambo wanafahamu fika kuwa Mwalimu J. Nyerere bado ni rais wa Tanzania; je REDET wako wapi? Serikali na mashirika yake pamoja na NGOS wako wapi katika kueleimisha hili? Ifahamike kuwa kuto kumpa mwananchi elimu ya uraia ni kumnyanyasa kifikra na kimaendeleo. Kwa ufupi kukosekana kwa elimu ya uraia kumesababisha :
· wananchi wasione umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa kujua kuwa kupiga kwao kura ama sivyo hakuwezi kubadilisha chochote.
· Wananchi hawajioni ni kama wanaweza kudai haki yao kwa njia sahihi ya kupiga kura
Wakati umefika wa kuwauliza wote wanaohusika na utoaji huo wa elimu je kipimo cha ufanisi au ubora wa kazi yao ni nini? Kwa mwanafunzi kipimo cha elimu aliyepewa ni kuelewa alichofundishwa, kufanya tathimini na hatimaye kuweza kufaulu mitihani yake, je kwa vikundi vyote vinavyojihusisha na utoaji wa elimu hii kipimo chao ni nini. Je wanaweza kuwapimaje wale wananchi hasa wa vijijini ambao wanahitaji sana elimu hiyo je wako;
· Chini ya kiwango (below Basic) hawa ni wale wenye elimu kidogo au hawana kabisa.
· Wastani(basic) wana elimu ya kutosha kuhusu mada nzima
· Juu ya kiwango (advanced) wamebobea katika elimu ya uraia wanaijua nini wanataka na watapata vipi.
Bado tunasafari ndefu lakini inahitaji umakini mkubwa sana; ambao unahitaji wannanchi makini ambao ndio wanaweza kutuletea viongozi makini, maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe na sio mtu mwingine yeyote Yule? Tukumbuke kuwa kama hatutachukua hatua ya haraka katika kuwaelimisha watu wetu kuhusu elimu ya uraia tunaemdelea kuwajaza wananchi wetu na ujinga hivyo na tutaendelea kuwajaza hofu katika kufanya maamuzi, hivyo hakuna namna yeyote wataweza kumchagua mtu sahihi kwa namna wao wanavyoona; watamchagua mtu kupitia ulipaji wa fadhila kwa vile ulinipa hiki name nakupa hiki. elimu ya uraia ikifundishwa vyema ni rada ya kuongozea demokrasia katika nchi kwani huipeleka nchi katika njia sahihi kwa faida ya taifa na sio tija binafsi wa wanjanja wachache.
Wananchi wazuri ambao wanaelewa taarifa kuhusu mwelekeo wa serikali na siasa katika nchi yao hawajezaliwa hivyo bali wamepikwa kutokana na elimu ya uraia.
No comments:
Post a Comment